Kyatile
JF-Expert Member
- Feb 5, 2017
- 1,551
- 1,366
Wakuu,
Kuna imani kuwa Watanzania hawatuwezi kujiendeleza wenyewe na ni viongozi wetu wanatuaminisha hivyo. Matokeo yake mama anatumia muda mwingi nchi za nje kuliko kuifahamu nchi yake. Kinachoendelea ofisi za uma ni vituko na hizo taarifa hawawezi kumpelekea.
Ukweli ni kuwa hao wazungu na waarabu wamejenga nchi zao kwa akili zao, mioyo yao, na nguvu zao. Hawakuendekeza ujinga wa kutokufanya kazi, hawakuzururazurura nchi za wengine kuomba misaada, hawakuendekeza siasa za maji taka, hawakuvumilia kila mtu kula kwa urefu wa kamba yake wala ufisadi huu unaofanyika sasa.
Kama taifa maskini hatuwezi kumudu kubeba mzigo wa wabunge wale wote 400+ bungeni alafu unawalipa posho na mishahara kibao wakati ufanisi wa wengi wao ni sawa na bure.
Hutuwezi kama taifa maskini kumudu kuwa na mawizara yote haya yaliyopo na ukaweza kuwahudumia.
Hutuwezi kumudu gharama na magari ya starehe yanayonunuliwa na serikali kila mwaka kwa ajili ya viongozi.
Hutuwezi kama taifa maskini kuafford rundo la ziara nje ya nchi kwa ajili ya kwenda kuomba misaada.
Ombi langu raisi afute mawazo finyu ya kuwa wazungu na waarabu watatusaidia kuleta maendeleo. Aelewe kuwa misaada tunayopewa ni short term fixes na haziwezi kujenga maendeleo ya kweli.
Ndiyo maani husikii maziara ya ovyo kwa viongozi wa nchi zinazojielewa.
Aanze program za kuhamasisha kilimo ili tuzalishe chakula kinachotosheleza mahitaji kuanzia nafaka, mafuta pamoja na mazao ya biashara. Tuwe na akiba ya chakula na tuanze kulisha majirani na Afrika yote mpaka Ulaya na Asia.
Tujenge miundo mbinu yetu kwa kasi.
Tuzalishe umeme wa kutosha kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya umeme vinavyopatikana nchini.
Tuanze kusomeshe vijana vyuo vya nchi zilizoendelea huko Ulaya na Asia katika fani za kimkakati na tuwatumie katika maeneo ya hayo.
Baneni matumizi na kuzuia mianya yote ya rushwa. Tungeni sheria kali za kudhibiti rushwa na zifuatwe.
Wastaafu ambao wameshindwa kututoa katika umasikini achaneni nao. Msiwaendekeze. Waacheni wapumzike. Leteni watu wapya wenye ari mpya. Hizi sura tulizozizoea hazina jipya. Zinafiria tu kupata utajiri na mamlaka zaidi. Hivi Wasira, au Mwigulu au Januari au Nape wana lipi jipya la kuleta katika nchi hii?
Tumieni wachache wanaostahili kutumika ila wengi wao hawafai. Achana nao. Achaneni na mambo ya kulipa wenza wa viongozi wakuu. Nafasi hizo zinakuja na manufaa mengi. Kama mtu hawezi kutumika na haridhiki na manufaa yaliyopo sasa asiombe nafasi hizo za uraisi, nk. Acheni upumbavu.
Hamasisheni uzalendo na nyie muwe mfano wa huo uzalendo. Tufanye kazi, tulipe kodi lakini kikubwa zaidi tuone manufaa ya hizo kodi.
Miaka 60 haiendani na maendeleo tuliyo nayo na sababu kubwa ni kuwa na viongozi wengi wabovu wenye uono hafifu na wasio na akili ya kutumia rasilimali tulizo nazo. Huwezi kujenga nchi kwa kuangalia kuwafurahisha watu ndani ya miaka mitano ili wakupe kura. Tujue kuwa wengi wa watu kwenye hii nchi hawaoni mbali.
Tungeni sheria kwa ustawi wa taifa. Ingieni mikataba yenye masilahi ya muda mrefu kwa taifa.
Mama umetembelea nchi nyingi lakini kikubwa tunachokiona sisi huku ni deni la taifa kukua tu na hatuwaoni hao wawekezaji tulio wategemea kuja kuwekeza hasa ukilinganisha na gharama mnazotumia huko mfano kutengeneza sinema ya Royal tour, kusafirisha viongozi katika wingi tunaouona mkiambatana na wasanii akina Steve Nyerere nk
Hii inatuumiza sana kama taifa.