Ukweli kuhusu tunaoishi nje ya Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli kuhusu tunaoishi nje ya Tanzania

Discussion in 'International Forum' started by rosemarie, Jun 16, 2011.

 1. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa nikifuatilia jamii forum ambayo sio maarufu sana hapa Africa kusini,
  Nitakayoyasema hapa naomba nieleweke nimeshawishika sana baada ya kufatilia sana
  Hii thread inayoendelea hapa jamvini kuhusu watanzania waishio nje ya nchi,
  Nimeishi nchi kumi na moja za kiafrica pekee, sijawahi kutoka nje ya Africa japo nina visa ya china ambayo niliamua kutokusafiri kwa sababu zangu binafsi zikiwemo mahesabu ya kibiashara.
  Nimeishi hapa ni miaka 15 sasa,nimeishi miji yote mikubwa hapa ikiwemo Pretoria,Johannesburg,na capetown.
  Kwanza kabla sijatoa yaliyo moyoni naomba niwarudishe nyuma kama wiki zilizopita kuna mtu alitoa thread hapa akisema watanzania tunafanya biashara ndogondogo kama za saloon na bar,aliongezea eti watanzania hawawezi biashara kubwa,
  Naomba kumweleza huyo member ya kwamba anajidanganya,hapa south Africa kuna watanzania wengi sana wenye biashara kubwa kama za business consultant, building construction, super market kubwa,hospital,ict na nyingine nyingi,
  Sio kweli kwamba watanzania hawawezi biashara kubwa,inawezekana huyo jamaa hajasafiri ,nafikiri kusafiri ni jambo la muhimu sana kwa sababu unapata kitu kinaitwa “exposure”ambayo inakufungua macho na kuona mbali sana.
  Sipendi kueleza mengi hapa kuhusu maisha lakini ndugu zangu kama unaona mtu kashindwa kurudi ujue mambo sio mazuri,
  Watanzania tuna kitu kinaitwa home sick,kama mtu mambo mazuri anakimbilia home chapchap,
  Kuna watu wako hapa miaka mingi na niliwakuta lakini hawajarudi home kwa sababu mambo sio mambo na wamekataa tamaa kabisa
  Wengine wamebadili majina kwa sababu hali ni mbaya kwelikweli,
  Mlio hapo Tanzania naomba msidanganyike kukimbilia nchi nyingine,bora ukomae hapo,
  Nikiwaona jamaa zangu niliowaacha hapo miaka ya 90 wako mbali sana,wana vinyumba vyao vizuri,wanajiamini katika maisha,kikubwa zaidi wana familia,
  Tunaoishi nje wengi asilimia kubwa maisha mabovu,naomba msidanganyike!
  Tutaonana.
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Jun 16, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Post yako ina contradiction. Unasema kuna watanzania hapo South Africa wana biashara kubwa kubwa, halafu tena unasema watanzania hapo South Afrika mambo yao siyo mazuri na unadiscourage wengine wasikimbile nje wakati wewe mwenyewe unaish nje. Ni ujumbe gani unaojaribu kutuma.

  Kumbuka kuwa kila mtu ana njia yake ya maisha. Ingawa kuna uliowaacha Tanzania wana maisha mazuri leo, vile vile kuna uliowaacha ambao wana maisha mabaya sana. Equally well, kuna waliokimbilia nje ambao maisha yao ni mazuri sana, wakati kuna waliokimbia nje ambao maisha yao siyo mazuri. Acha watu wajiamulie wenyewe kuhusu maisha yao.
   
 3. YoungCorporate

  YoungCorporate JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2011
  Joined: Apr 30, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mhhh unazungumzia wazamiaji, illegal immigrant ambao waliacha shule toka bongo au unazungumzia watu wenye legal status na ambao wanakajishule na wako huru kutumia majina yao halisi maana hawakimbii kukamatwa na polisi??
   
 4. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  du!mzee lakini mbona watu hapa warudi na marcedes benzi kali kabisa
   
 5. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  piga box kaka usijali
   
 6. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  mkuu kwa mtaji huo basi kichwa cha habari kilitakiwa kuwa " UKWELI KUHUSU TUNAOISHI SOUTH AFRICA"...manake umeshasema hujatoka nje ya Africa
   
 7. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mbona wewe umechemka sasa? Kama unataka kurekebisha kichwa cha habari kwanini usimshawishi aseme, ukweli kuhusu tunaoishi Africa? Jamani maisha ni popote iwe Tanzania au nchi nyingine.
   
 8. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu kuna jamaa nipo nao wana elimu nzuri lakini kupata kazi hapa sa ni shughuli
   
 9. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #9
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  maisha ya tanzania ni bora kwa sababu ukishindwa mjini utarudi kijijini na maisha yanaendelea,tumeona mifano mingi
   
 10. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #10
  Jun 16, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Hongera sana kwa kuishi nchi 11 za kiafrika. Ongelea maswala ya SA usichanganye na maswala ya nje ya Afrika. BTW M k w e r e amekuwa akitembea kila nchi hapa ulimwenguni je amefanikiwa vipi kugeuza maisha ya Watanzania? Usiseme ameuza magenerator yake kwa symbion power khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee baada ya kuadhirika na Dowans, Richmond etc.
   
 11. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #11
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280

  nashukuru kunipongeza,huyu unayemtaja mkweree ni waziri au ni nani?
   
 12. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #12
  Jun 16, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kama humjui ****** natilia wasiwasi utanzania wako na umember wako wewe ni UWT. SIDANGANYIKI. Hata hivyo ****** ni rais ***** wa nhi yako amechakachua kura kutawala. Wewe wa wapi?
   
 13. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #13
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  ukiandika ****** linafutika,andika mkweree,mods hawajashtukia hilo
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Maisha ni popte pale Mungu alipokupangia ili mradi upate kutia mkono kinywaji. Maisha ya nje ya nchi ni magumu ukizingatia Asilimia ya watu wengine wanaosafiri kisomo chao ni Darasa la saba au Darasa la kumi na 12. Na wengi wao hao wasafiri wanaishi kinyume cha sheria (illegal) kwa

  hiyo kupata kazi inakuwa Tabu sana matokeo yake wanakuwa ni wezi,majambazi, Wauza unga, kuna watu wengine wanalal nje kwa sababu hawana pesa za kulipa kodi ya nyumba na kodi ya nyumba kwa mwezi ni dola 300 au Dola 500 kwa mwezi ,na mengineyo mengi tu. Kwa hiyo kwa Ushauri wangu kama una kazi nyumbani na hali yako nzuri bora usisafiri, kuliko kuja huku kuteseka bure huna ndugu huna jamaa wa kukusaidia sisi tupo

  nje lakini hakuna kitu chochote kile maisha ya tabu tunateseka huku jamani baridi kali hakuna faida watu tupo huku zaidi ya miaka 20 ukirudi nyumbani utafika kwa nani? Baba na Mama na ndugu wote wamekwisha fariki! jamani huku nje maisha magumu jamani tupo Pembeni mwa shimo ukianguka ( ukiumwa) unalichungulia Kaburi. kwa ushauri wangu bora nyumbani Waarabu Husema ( NYUMBANI NI NYUMBANI HATA KAMA KUKIWA NI JUU YA MLIMA NI NYUMBANI) Msije huku jamani Endelezeeni maisha yenu huko huko nyumbani Home is Best.
   
 15. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #15
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mzizi mkavu umetoa mawazo mazuri sana!mimi binafsi simshauri ndugu yangu yeyote kuja hapa! upo nchi gani?
   
 16. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #16
  Jun 16, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Nimechemka wapi wakati yeye amesema anaishi S.Africa? na hajatoka nje ya Africa. Please read my point b4 hujacomment
   
 17. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #17
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Sipo South Africa nipo East Europe
   
 18. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #18
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 654
  Trophy Points: 280
  Huku niipo kuna watu wengine tunaishi kimazabe,wengine tunaishi kihalali,kuna watu wenye maisha mazuri na wengine wana struggle kama ambavyo ilivyo tanzania.
  Ila,nimekaa miaka mingi hapa US na nimetembelea states karibu 35,sijaona mtanzania homeless! acheni kudangany'a watu! but to some of us life is so tough compared to my college mates back home.
  But for some reasons of my own....I JUST LOOVE WALKING ON THESE STREETS.
   
 19. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #19
  Jun 16, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Eastern Europe! Ni bora ungebaki bongo manake wenyewe hao Eastern Europeans njaa kali na maisha yao magumu sana
   
 20. Kingvictor87

  Kingvictor87 Member

  #20
  Jun 16, 2011
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 25
  Nikimuona kocha wa taifa starz ama the vice president himself daaah nachoka hata mawazo ya kurudi böngo yanatoweka!nimewataja wachache 2 sema kuna vizee kibao kila sector wanang'ang'ana kama kupe!!ful uchawi!itabaki historia tu kwamba nilizaliwa tanzania!inatia sana uchungu hadi landlockd country rwanda,malawi,burundi,uganda zambia wana2acha kila kitu,sio tu kiuchumi!
   
Loading...