Ukweli kuhusu tunaoishi nje ya Tanzania

Maisha magumu ni popote na maisha mazuri ni kote kote. Hapa hapa tz kuna watu wanamaisha ya kusikitisha. Watu na madigrii zao wanakosa kazi. Wengine wanafanya kazi 14hrs kwa siku, mshahara laki 2. But, but but... kuna wanao ishi maisha mazuri sana, shopping ya mbwa millioni 6 in china etc.
Wanao amua kwenda SA kutafuta maisha siwalaumu, siwa-encourage pia. My advise ni kila mtu awr na vision na benchmarks. Realistic and hardworking.
 
kuna traffic hapa nyumbani wanakuuliza wewe kabila gani
Chamoto..I have no problem if I meet someone; and after having few minutes of chat the question about my country of origin arise....That's ok... However, in most cases, things aren't the same. You just pop in car, and immediately someone ask..where are you from..or you just order food in a restaurant and the waiter ask the same. Or in a meeting.. immediately after greetings ..the question pops up.. At the airport.. Customs officers seldom ask same question to those people with the colour other than black, But it is a common question to those blacks...I don't like it at all...You can read the face of them..they are curious to know the reason of you being there..Yes, I am black and definitely have roots in Africa.. I am not running from myself.. I am proudly African..why you need to prove that?...That's why I love home.. no one ask that question...
 
Hamna swali linalonikera kama unaenda wapi? Utadhani anataka kukuongezea wese, serukamba kabisa! Trafic siwapendi manake hawako kwa ajili ya kumsaidia wala kumlinda yeyote.

Hahahahaaa eti kama vile anataka kukuongezea wese, labda anataka akupe ulinzi
 
Wapendwa nitatoa maoni yangu binafsi. Wazo la kuwa nje ya nchi au kusettle nyumbani linachangiwa sehemu kubwa na uchumi. Ni sawa na yule aliye-relocate toka Nchinga-Mtwara kuja Dar es Salaam. Lakini pia kuna suala la feeling za ki-binadamu; hebu fikiri.. umeamua kurudi home baada ya kuangaika sana..na hela zako umeweza pata kagari kako kamtumba...umepiga kiyoyozi unapita pale kituoni..watu wamejaa ile mbaya hakuna usafiri..roho inakuuma ..Ok,,, unarudi nyumbani ambako umeweka Kagenerator pale nyumbani..baada ya Tanesco kuishiwa umeme..wakati kagenerator kanaunguruma na unapata mwanga..Nyumba ya jirani hakuna umeme..watoto wachanga wa majirani wanalia unasikia huruma ..dhamira inakusuta.unaangalia utawaze kusaidia jirani..lakini masikini kagenerator kenyewe kadogo..Anyway... una kajumba kako umeweka uzio mzuri..lakini kila siku vibaka wanakusumbua.Unaamua kuchukua wamasai..kesho yake wamasai wanafanya nyumba yako ndio Ngome..wanawaleta wenzao kushinda..Unaona karaha unawatimua..Ok.. Unaanza na ka Investment..uanpata kahela ambako kanakuwezesha kubadili mboga .lakini extended family kuna watoto wanataka shule, ndugu wengi maisha magumu..unajitahidi kusaidia unashindwa... Anayway...Unajaribu kujiliwaza kwa kuangalia TV ..au kusikiliza Taarifa ya habari ..unasikia utumbo wa wanasiasa wanaoshindwa kuwathamini wananchi...wanagombana wenyewe kwa wenyewe chama A and B..Mafisadi na walalahoi..Unaudhika kwani kuna ka chama kanajaribu kuwatetea walalahoi na kuna kachama kanajaribu kuwatumia walahoi hao hao kuwatetea maslahi ya matumbo yao na mafisadi..unakasirika na kuzima TV....Unaamua kuondoka.. unatoka kidogo traffic anakukamata..huna tatizo..lolote..kwani Maisha uliyoishi nje yamekunja ki-discipline..Huyu Traffic anazunguka gari.. ..anajenga hoja,,Fire Extinguisher ni ndogo kwa ukubwa wa gari ..Mnabishana sana..anaishia kukwambia ukweli anataka kahela akapate supu..unakasirika unampa unaondoka huku Moyo ukidunda kama unataka kutoka kwa hasira....Mbele kidogo unasimama ..umeshaamua ku - postpone kurudi settle..home ..Unaandika kwenye Face-book..kwa marafiki zako.. "Aluta -kontinua..Narudi ughaibuni" Binafsi unajipa moyo..wacha nikaangaike kidogo kama miaka miwili au mitatu nitarudi home..Well, ni -round nyingine umeshindwa ku-settle --ingawa ulikuwa na nia ya kweli..

"

Duh! Mkuu, yaani ulivyoweka huu mtitiriko umenifanya nicheke... yote ni kweli yapo na maisha ni magimu lakini nafuu yake ni kwamba huwezi kukutana na yote haya yote kwa siku moja unless ni siku ya mkosi

mlioko nje kaeni huko huko, enjoy huduma bora za jamii na mishahara minono (kwa walioipata) na mjitahidi kunyoosha mambo huko huko, ila tu msisahau kujenga nyumbani ili mkizeeka mrudi huku mpate walao shikamoo zenu na mkifa wajukuu wawazike...sio baada ya miaka 60 ya kufanya kazi na kulipa kodi mzee mzima wa miaka 85 unaulizwa "where are you from"

Mlio ndani ya bongo, enjoy maisha ya kibongobongo-ni raha sana kukaa na ndugu, jamaa au marafiki wa tangu utotoni mkila kuku wa kuchoma kwenye mkaa na vinywaji baridi mkipigaa gumzo wikiend au kuishi na jirani kama ndugu.... endeleeni kujitafutia maisha bora pia kwani inawezekana kabisa
 
Mzizimkavu unanishangaza mkubwa wangu kwenye thread nyingine ulikuwa unahamasisha watu kusafiri nje na utawasaidia kupata visa na kazi! Hii thread unaonyesha na wewe unataabika na kushauri watu kubaki nyumbani! Which side are you? Nafikiri maisha ya nje yanataka umakini zaidi Kama unaishi kihalali, Kama umeshindwa east Europe njoo japan Kama umesoma engineering ila itakubidi ukasome kijapan miaka 3, kazi za kumwaga karibu.
 
Dunia ya leo bila elimu hakuna utakalo fanya, japo wapo wachache sana wanaofanikiwa bila elimu. Kuvuta kumleta dunguyo kama si kwa ajili ya shule, yani shule ya ukweli basi utakuwa unampoteza.

ukiangalia wengi wanaovutana mfano wavietnam, wachina, wahidi nk, hawa wanapoletana wanakuwa tiyari wana biashara zao ambazo mtu akifika tu tayari anaiingizwa dukani kuuza ama kufanya kazi anatafutiwa makaratasi. Ni rahisi tu mfano kama wewe una duka lako na unataka kuajili ndugu yako unatangaza kazi harafu qualification zake unaweka awe anajua kuongea na kuandika kiswahili sanifu.

Mnigeria na wacongo, japo huwa kuna sehem naona tunajaribu kuwadharau lakini wanatuacha mbali sana na ndio maana utakuta wengi wanafanikiwa kuliko wabongo.

Kitu nyingine, mfano wachina, kuna nchi wananchi wanapewa makusudi loan na serikali zao kwenda kuwekeza ktk nchi zingine, na ndio maana wanafanikisha hata kuvutana pia kukuza uchumi wa nchi. Mfano kwa bei ya kahawa kwa wakulima wa tz ni kiduchu, basi serikali inatafuta wazaliwa wa tz na wenye makaratasi tuseme ya EU, basi hawa watz-EU wanafungua vijimaduka kwa kama local. Na wanakuwa wanatoa bidhaa moja kwa moja bongo na kuiuza hapa kwa bei nzuri kabisa. Hii inakuwa biashara virtually ya serikali kwa kupitia wazawa.

Mfano kule Tabora kuna asali nyingi kweli wakati ndani ya EU, asali bei yake si haba. Serikali si lazima iingize pesa kwa kutengeneza maviwanda makubwa. Kwa hiyo kwa mtaji huo, ukiwa na vijisehem vya namna hiyo ulaya kote, kinachofuata unahakikisha fedha haipotei kwa kuwalipa watu wa nje mshahara, basi unawavuta watz wafanyakazi, kwa namna moja ama nyingine unakuwa na uhakika hizo pesa lazima atamtumia shangazi , binamu yake nk.
Ushauri mzuri kwa serikali huu
 
Post yako ina contradiction. Unasema kuna watanzania hapo South Africa wana biashara kubwa kubwa, halafu tena unasema watanzania hapo South Afrika mambo yao siyo mazuri na unadiscourage wengine wasikimbile nje wakati wewe mwenyewe unaish nje. Ni ujumbe gani unaojaribu kutuma.

Kumbuka kuwa kila mtu ana njia yake ya maisha. Ingawa kuna uliowaacha Tanzania wana maisha mazuri leo, vile vile kuna uliowaacha ambao wana maisha mabaya sana. Equally well, kuna waliokimbilia nje ambao maisha yao ni mazuri sana, wakati kuna waliokimbia nje ambao maisha yao siyo mazuri. Acha watu wajiamulie wenyewe kuhusu maisha yao.
Kichuguu usituchanganye. Jamaa kaongea vizuri SANA. Kwamba kuna Wa-Tanzania wachache wana biashara kubwa. Hii ilikuwa ni kuondoa dhana kuwa WaTanzania wote huko South ni CHINGA!

Ukiondoa hao wachache, wengi ni CHINGA na hali mbaya sana kiasi kwamba hawawezi hata kurudi home. Shida kubwa.

Wiki mbili zilizopita BBC ilirusha vipindi maalum vya wakaazi wa Afrika Mashariki wanaoishi Africa ya Kusini. Karibu wote walikiri kuwa kwenda kule ilikuwa ni MAKOSA na walituomba sisi wengine tusiende huko.

Kwa ujumla maisha ya South ni magumu maana wengi huenda huko bila elimu wala ujuzi wowote. Utapata mafanikio gani kama huna elimu wala ujuzi? Bora ubaki Bongo kama umachinga ufanyie hapa. Mungu Ibariki Tanzania
 
Duh! Mkuu, yaani ulivyoweka huu mtitiriko umenifanya nicheke... yote ni kweli yapo na maisha ni magimu lakini nafuu yake ni kwamba huwezi kukutana na yote haya yote kwa siku moja unless ni siku ya mkosi

mlioko nje kaeni huko huko, enjoy huduma bora za jamii na mishahara minono (kwa walioipata) na mjitahidi kunyoosha mambo huko huko, ila tu msisahau kujenga nyumbani ili mkizeeka mrudi huku mpate walao shikamoo zenu na mkifa wajukuu wawazike...sio baada ya miaka 60 ya kufanya kazi na kulipa kodi mzee mzima wa miaka 85 unaulizwa "where are you from"

Mlio ndani ya bongo, enjoy maisha ya kibongobongo-ni raha sana kukaa na ndugu, jamaa au marafiki wa tangu utotoni mkila kuku wa kuchoma kwenye mkaa na vinywaji baridi mkipigaa gumzo wikiend au kuishi na jirani kama ndugu.... endeleeni kujitafutia maisha bora pia kwani inawezekana kabisa


Aisee...nimependa sana fikra zako mkuu Tai Ngwilizi ..Saafi sana!
 
Last edited by a moderator:
mzizi mkavu umetoa mawazo mazuri sana!mimi binafsi simshauri ndugu yangu yeyote kuja hapa! upo nchi gani?

Humshauri mtu wa aina gani kuja South Africa au nchi yeyote ya nje? Kuna watu wana elimu zao ambazo zinahitajika sana duniani kwa nini wasiende wanakotaka kuishi? Tanzania ni kuzuri lakini kunachefua sana. Uchafu(hasa DSM), rushwa, watu kutokufuata sheria, matatizo ya kupata matibabu mazuri, n.k
 
nimebeba boksi sio kwa kutaka kwavile shule nilikimbia ndio niliona umuhimu wake lakini pia ningelikuwa nimeenda shule bahati niliyokuwa niliyoipata nisingeliipata kwani niliipata kwa kuchakarika na boksi aliyesoma asingeliikubali.
Maisha ni maisha popote unaweza kuyapata nje kuna raha zake na ugumu wake na nyumbani ndio hivyo hivyo
Lakini nyumbani Wanasiasa wanayachakachua zaidi ili sie tuwachumie wao zaidi ndio maisha yangu yote sitoweza kupiga kura na wala sitopiga kura kuwachagulia maisha wanasiasa
 
Iran, Saudiarabia, na falme za kiarabu ndio pa kuishi, Japan na Australia pa ukweli kama una elimu yako na ukiwa mchapakazi huto tamani kurudi bongo
 
Watanzania tulio wengi ni WAOGA KUJARIBU....hata pale ambapo tuna opportunities kibao....siwezi kuacha nafasi/mapande yanayonijia......nitakuwa mjinga nisipotumia mwanya huo kufunga goli!....Mwenyezi Mungu kanipa akili namshukuru na ninamshukuru pia kwa opportunities zinazonijia......who knows ningekuwa Tz hivi sasa pengine ningeuwa kwenye msoto!!??...
...however..tusidanganyane...nyumbani ni kuzuri sana kwani ni nyumbani....lakini maisha ni popote.....na sitaweza kubadilisha kuwa kwetu ni Ushiwa-Marangu...na wanangu wanalifahamu hilo na wao wanajitambua kama ninavyojitambua......kwa sababu from time to time tunatembelea nyumbani......na maisha yanaendelea.....

Shida zipo popote.....ni kupambana nazo...na hiondoi ukweli kuwa maisha ni popote.....nipo mbali na nyumbani lakini naongea na wazee/ndugu wangu kijijini na kuonana nao pia na marafiki zangu niliowaacha bongo.......wapo ndugu zangu huko bongo hata mawasiliano ni magumu kwa wazee/ndugu wetu kijijini...achilia mbali kuonana
 
Back
Top Bottom