Ukweli kuhusu tukio la walimu waliompiga mwanafunzi Mbeya

Ukweli kuhusu tukio la walimu waliompiga mwanafunzi Mbeya

Hahahaha

Leo alikuwa NMB ilala anachimba Mfereji wa Ruzuku kuelekea Buguruni na kuuziba ule Mfereji wa kupeleka Ruzuku Pemba!

Mtatiro kahamia kwa Scorpion kumfariji Mtolewa macho kaona Mziki wa Prof sio wa Mchezo mchezo
😀 😀 😀 😀 😀 😀 😀 😀 siasa za bongo hizoo mkuuu kama muvi za india vileeeee
 
NI KWELI WALIMU WAMEMPIGA MWANAFUNZI KINYAMA HUKO MKOANI MBEYA LAKINI KIJUE CHANZO KILICHOSABABISHA KUPIGWA KWAKE

Na Mathias Canal

Majira ya asubuhi hapo jana nilianza kuiona kanda ya sekunde 38, ambayo tangu nilipoiona kabla ya kujua serikali itafanya maamuzi gani kwa Walimu waliofanya unyama huo mimi niliwatazama takribani watu hao watano wakiwa wanaonekana kumshambulia mvulana mmoja ambaye ni Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya kutwa ya Mbeya ambaye baadaye alianguka chini kwa kupigwa ngumi pamoja na mateke.

Hakika tangu jana nimekuwa nikihangaika kujua chanzo cha Walimu kuwa na hasira za aina hiyo kama Chui Mwenye njaa, Machache haya nimebaini.

KISA CHA KUPIGWA...!

Mwanafunzi huyo kabla ya kuonekana kwenye kanda hiyo alikataa kuchapwa wala kuchuchumaa pamoja na kwamba wenzake wote ambao hawakufanya zoezi darasani.

Aliipohojiwa akamjibu vibaya mwalimu ambapo Mwalimu yule alitaka kumuadhibu kwa kumchapa viboko kama adhamu ya kuimarisha nidhamu yake.

Mwalimu alipojaribu kutaka kumchapa ghafla mwanafunzi huyo alirusha ngumi nzito ambayo ilituama kwenye mdomo wa Mwalimu huyo.

Baada ya kadhia hiyo ambayo haikumaliza hata sekunde moja walimu wengine walioshuhudia tukio hilo waliamua kumchukua mwanafunzi huyo ili kumpelekea ofisini huku Mwalimu aliyepigwa ngumi akiwa ameamua kurudi darasani kutuliza wanafunzi wengine ambao walitaka kufanya vurugu kwa sababu ya kukerwa na Matukio ya ubabe yanayofanywa na Mwanafunzi huyo na Alipoona wanafunzi hao wametulia alianza kurudi ofisini.

Baada ya Mwanafunzi huyo kufikishwa ofisini akaona Walimu wamebaki wawili tu aliwapiga ngumi kiasi kwamba Walimu hawakuwa na namna ya kumkabili.

Mwanafunzi huyo baada ya kuwamudu Walimu wale wawili Akaanza kutoka nje ya ofisi huku akiwa anakimbia yule mwalimu ambaye alipigwa ngumi ya mdomo na akaenda kuwatuliza wanafunzi darasani akamuona mwanafunzi huyo akiwa ametoka anakimbia ndio alipomuwahi kukawa na majibizano ya ngumi na mateke kidogo.

Mwalimu alifanikiwa kumudu majibizano ya kipigo na hatimaye akafanikiwa kumrudisha ofisini kwa walimu wengine hapo ndio kila mmoja akajikuta anahitaji kumaliza hasira zake. Kumbuka Walimu walikuwa na hasira za Kupigwa tena na mwanafunzi wao...! Na kubaki wakiwa wanaugulia maumivu.

TAARIFA NYINGINE MPENYEZO

Mwanafunzi huyu yeye aliridhia kichapo alichopewa na walimu hao baada ya kufanikiwa kummudu akiwa kwenye ofisi ya walimu ndio maana siku 11 toka tukio limetokea hakwenda kuripoti mahala popote, yaaani Hata nyumbani kwao hakwenda kusema kwakuwa anakesi tatu nzito na aliwahi kumjibu hovyo baba yake mbele ya walimu alipokuwa ameenda kutetea asifukuzwe shule.

Achilia mbali hayo Mwanafunzi huyo alishawahi kuvunja TV ya baba yake nyumbani kwao kama wiki mbili zilizopita.

Pamoja na mambo yote hayo Wiki hili amekamatwa na walimu akiwa anavuta bangi shuleni na wenzake. baba yake mzazi hamtaki huyo Mwanafunzi lakini hana namna ya kumkabili.

MTAZAMO YAKINIFU

Serikali umefanya Kazi Mkubwa kwanza kubaini hiyo video imerekodiwa katika shule gani na Walimu hao ni kina nani, hakika ni jambo la kupongezwa sana lakini imesahau kwamba maamuzi yote yaliyofanyika dhidi ya Walimu yameshindwa kuzingatia chanzo Chake Bali imejikita kukabili matokeo, Wahenga walisema Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo lakini wakaenda mbali zaidi kwa kusema Samaki mkunje angali mbichi. Mwanafunzi huyu ni samaki aayetaka kukunjwa akiwa amekauka Kamwe haiwezekani.

Watanzania, Wanafunzi, jamii kwa ujumla itambue kuwa binafsi nimesikitishwa sana na kadhia hiyo iliyofanywa na walimu karibu wa tano kwa mujibu wa Video iliyosambaa mtaani tena imenikera mno mno lakini vyema zaidi kama tutajikita kuhangaika na chanzo cha tatizo ili kumaliza mzizi wake kuliko kukabili matokeo huku tukiacha mambo hayo yaendelee kukutikana mitaani.

Kuteleza si kuanguka lazima tukiri kwa pamoja kwamba hapo tumeteleza kabla hatujaanguka basi vyema tukatazama mahala pa Kushika ili kuhakikisha hatuanguki Tunapotoa maamuzi ni vyema sana tuangalie mambo kwa ujumla wake tusitazame tu wapi kumesisimua Jamii...?

Tutambue kuwa tukio hilo la Mbeya ni la wanafunzi wa Chuo kumchangia na kumpiga mwanafunzi wa shule ya kutwa ya Sekondari Mbeya tukiwaita Walimu maana yake tutajadili pia Chama Cha Walimu Mkoa wa Mbeya (CWT) kinafanya Kazi gani...?

Kuna mwandishi mmoja huwa anasema hawezi kuwa adui kwa kusema Ukweli nami sitarajii hilo.

Naaam, Ni Neno La Wakati Mwema
Mathias Canal (Sauti ya Wanyonge)
0756413465
Igunga-Tabora

Adhabu ya viboko kwa mwanafunzi ni lazima iwe kwa kibali cha mwalimu mkuu au mkuu wa shule.Na mwanafunzi akikataa adhabu yoyote hufukuzwa shule. Hao waalimu ni kama wahuni wa sokoni na hawajui sheria za shule. Kama alikutwa anavuta bangi wangeripoti polisi au kwa mtendaji sheria ichukue mkondo wake. Tuko karne ya 21 mambo ya kupigana hata kwenye baa hayapo tena.
 
"...Hata Kama angemtia Dole
Mwalimu nini konde
bado haikuwa sahihi
kushambuliwa ( ile
sio kuadhibiwa)..."

mkuu Pohamba umekutwa na nini kwenye ufahamu wako mbona umeropoka upuuzi usiovumilika? samahani kama ntakua nimekuuliza kwa style isiyopendeza, ila vipi kama ni wewe ukatiwa dole na mwanafunzi wako mbele ya wanafunzi darasani, ungevumilia? duh hii kali kuliko zote.
 
Wale wote ni wanafunzi yaani watoto! Ushauri kama ww ni mwl mwanafunzi anaonyesha ubabe mbele ya wanafunzi wengine kweli hiyo huleta hasira mwanafunzi anakudindia na kurusha ngumi kwa walimu hiyo ni hatari sana kwani kazi yyt ni ushirikiano na walimu nao wananyongo ni sawa na polisi amekukamata unamtushia ngumi kwa kweli lazima zoezi la kukukamata linasitishwa kwa mda kwanza ule mkong'onto kwanza wakishakuweka sawa do wanakubeba, hivyo wanafunzi wengine akiangalia umri wa mwalimu wake umri haupishani lazima mwanafunzi alete jeuri kwa Mwalimu, ushauri wangu kwa serikali hasa waziri wa elimu au wa tamisemi fanyeni uchunguzi mbona majibu yapo shuleni hapo hapo tena hamtachukua mda kuipata picha yote, walimu nao wananyongo!
Ukitolea mfabo Polisi, wanaitwa "Police Force"
Kwa hiyo walimu waitwe "Teacher Force"
Matokeo ya kidato cha nne ya uyo mwanafunzi yatadhirisha kama alionewa ama laah, tutaona kama atabebwa na wanao mtetea.
 
Kaswali kadogo
Je huyo mwalim aliye pigwa ngumi ya mdomo alitoa taarifa kwa mkuu wa shule ?
Swali lako ni tete sana... Ni sawa na mimi nizabwe vibao na wife afu nikamshtaki kwa balozi wa nyumba kumi.

Sipendagi ujinga wala madharau mimi...
 
"...Hata Kama angemtia Dole
Mwalimu nini konde
bado haikuwa sahihi
kushambuliwa ( ile
sio kuadhibiwa)..."

mkuu Pohamba umekutwa na nini kwenye ufahamu wako mbona umeropoka upuuzi usiovumilika? samahani kama ntakua nimekuuliza kwa style isiyopendeza, ila vipi kama ni wewe ukatiwa dole na mwanafunzi wako mbele ya wanafunzi darasani, ungevumilia? duh hii kali kuliko zote.
Inawezekana kwa wengine kutiwa dole ni sehemu ya burudani....
 
Kuna namna na taratibu za kumuadhibu mwanafunzi mkorofi shuleni
Hata hao walimu wa field naamini walifundishwa vyuoni jinsi ya kuwadhibiti, lakini sio kwa kipigo kile jamani
Hivi yule mtoto si amekuja shule ili afute ujinga na kufundishwa maadili? Sasa matokeo yake badala ya waalimu kumfundisha wao ndio wanakua wa kwanza kupambana nae.
Hata sisi enzi hizo tumesoma na wanafunzi wakorofi, tena zaidi ya huyo dogo lkn hawakufanyiwa km alivyofanyiwa huyo mwanafunzi.
Kama mwanafunzi ni mkorofi sana si kuna mwalimu wa nidhamu shuleni yeye ndiye anajua jinsi ya kuwafundisha adabu vizuri hao wakorofi, akimshindwa anampeleka kwa mkuu wa shule napo akishindikana anafukuzwa shule au anaamishwa shule au kusimamishwa shule kwa muda.

Tatizo ninaloliona hapa ni wengi wa walimu wapya wa sasa hivi hawafati taratibu za kiualimu. Angalia rate ya wanafunzi kupewa mimba na walimu wapya. Sasa sijui kama huwa hawa walimu huwa wanasikiliza kwa umakini wanvyofundishwa vyuoni au ndio km kawaida Facebook kwa sana na whatsapp.
 
Yani watu wametunga habari za uongo ili kuficha maovu ya hap walimu.
Adhabu ya kuwafukuza chuo ni ndogo sana,wanatakiwa kufungwa kifungo cha zaidi ya miaka mi3.
Kwa vile vikofi vitatu? Tuliosoma enzi hizo tunashangaa kwanini mnashupalia kaadhabu kadogo namna ile.... Sie tulikuwa tumatandikwa kwelikweli... afu ole wako ukamwambie mzee nyumbani... unaangushiwa tsunami nyingine ya kiwango cha tetemeko la Kagera.

Watoto wa siku hizi wqnadekezwa sana
 
Mleta uzi usanii waachie wenye usanii wao wewe sifuri kabisa peleka huko MAUONGO yako
 
Kuna namna na taratibu za kumuadhibu mwanafunzi mkorofi shuleni
Hata hao walimu wa field naamini walifundishwa vyuoni jinsi ya kuwadhibiti, lakini sio kwa kipigo kile jamani
Hivi yule mtoto si amekuja shule ili afute ujinga na kufundishwa maadili? Sasa matokeo yake badala ya waalimu kumfundisha wao ndio wanakua wa kwanza kupambana nae.
Hata sisi enzi hizo tumesoma na wanafunzi wakorofi, tena zaidi ya huyo dogo lkn hawakufanyiwa km alivyofanyiwa huyo mwanafunzi.
Kama mwanafunzi ni mkorofi sana si kuna mwalimu wa nidhamu shuleni yeye ndiye anajua jinsi ya kuwafundisha adabu vizuri hao wakorofi, akimshindwa anampeleka kwa mkuu wa shule napo akishindikana anafukuzwa shule au anaamishwa shule au kusimamishwa shule kwa muda.

Tatizo ninaloliona hapa ni wengi wa walimu wapya wa sasa hivi hawafati taratibu za kiualimu. Angalia rate ya wanafunzi kupewa mimba na walimu wapya. Sasa sijui kama huwa hawa walimu huwa wanasikiliza kwa umakini wanvyofundishwa vyuoni au ndio km kawaida Facebook kwa sana na whatsapp.
Ni kweli walimu wengi hawa wa field na wanaoajiriwa hivi karibuni wanakuwa hawana maadili kabisa. Nahisi hata darasani hawatilii maanani. Kuna mwl mmoja wa fielld kule Mwanza imepita kama miezii miwili/mitatu hivi alitembea na wasichana wa Sekondari wapatao15 kwa nyakati tofauti tofauti, hali iliyopelekea wazazi wa wasichana hao kuandamana hadi shuleni. Mwl huyo baada ya hapo alifikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Sasa hapo yuko field tu, je akiajiriwa si atatembea na wasichana wote kwa kutumia madaraka yake vibaya!?
 
Toa ujinga wako hapa, huyo mtoto ndo wa kupiga ngumi majibaba mazima yale eti mawili yazidiwe na yule mtoto? Hebu wacha hizo kiongozi! Huyo mtoto hawezi kupiga ngumi ya kumfanya mwalimu asalimu amri!!
Nyie hamuwajui watoto wa shule nyie.ni kweli kile kitendo ni cha kinyama ila nakuambieni kuna siku nilienda shule anayosoma mtoto wangu kufatilia maendeleo yake na nikakuta vijana watatu wakipewa adhabu ya kutokufanya usafi,wale vijana jamani nilichoona nikaamini waalimu nao wana kazi
 
Hawa walimu wapya wamekua ni majanga kwakweli. Sasa mwalimu anafanya vitu kama hvo unategemea wanafunzi wataelewa nini hapo kama sio kuzidi kujazwa ujinga? Huku kuna baadhi ya shule unakuta mpaka mwalimu anaongea kishkaji kabisa na wanafunzi kisa tu mwalimu anajiona bado kijana. Ni upuuzi huu. Zamani kulikua na wale wakaguzi wanapita mashuleni sijajua kama siku hizi bado wanapita
 
Toa ujinga wako hapa, huyo mtoto ndo wa kupiga ngumi majibaba mazima yale eti mawili yazidiwe na yule mtoto? Hebu wacha hizo kiongozi! Huyo mtoto hawezi kupiga ngumi ya kumfanya mwalimu asalimu amri!!
Tena anavyojikanganya ,walimu watatu walishindwa kumdhibiti halafu mwalimu mmoja aliyeko nje ndio akamdhibiti na kumrudisha ili ale kipondo!
Hoja hapq yule mtoto ni mshenzi na hakufaa kuwepo shuleni na pia haobwalimu ni washenzi zaid kwa kutotambua nafasi zao na kuwajibika! Haiwezekani wao kucheza tune za mtoto mshenzi halafu wasiadhibiwe vikali !hatuhitaji wanafumzi wa aina hiyo kama tusivyohitaji walumu wa aina ile kqtikq mashule yetu!
 
Nyie hamuwajui watoto wa shule nyie.ni kweli kile kitendo ni cha kinyama ila nakuambieni kuna siku nilienda shule anayosoma mtoto wangu kufatilia maendeleo yake na nikakuta vijana watatu wakipewa adhabu ya kutokufanya usafi,wale vijana jamani nilichoona nikaamini waalimu nao wana kazi
Tatizo hapa Tz kwenye Taasisi nyingi za Elimu unakuta mwl na mwanafunzi wanaishi kama maadui. Wakati wanatakiwa kuwa marafiki.
 
Hakuna neno au tukio lolote linaloweza kuhalalisha unyama aliofanyiwa Yule Kijana japo nae anaonekana ni Nunda Mkorofi. Hata Kama angemtia Dole Mwalimu nini konde bado haikuwa sahihi kushambuliwa ( ile sio kuadhibiwa).
Story ya kusema alivunja TV ni ya Uongo kwa kuwa kwa Mujibu wa Nipashe ya Leo Baba Mzazi wa Yule Kijana anasema Nyumbani kwake bado hajafanikiwa kuweka Umeme sasa hiyo TV alikuwa anatumia Mkaa au Power bank?

Pamoja na Yote hayo adhabu ya kuwafukuza Chuo wale Vjana ni kubwa mno kwao na familia zao na Taifa kwa Jumla, ingeangaliwa namna ya kuwaadhibu hao Walimu wa Field sio kuwakomoa Kama wao walivyomkomoa Yule Mwanafunzi
Unyama gani mwanafunzi anarushia ngumi waalimu wake, wangeng'oa meno kabisa
 
Unyama gani mwanafunzi anarushia ngumi waalimu wake, wangeng'oa meno kabisa

Basi Kama ni kupigana hao Walimu ni Kama Mashosti tu, Mtoto Kama Yule mpaka muungane Kama UKAWA Walimu watano kumkabili tena kwa nyenzo za kupigania ( fimbo) Kama sio uoga ni nini? Ingekuwa mmoja kwa mmoja wala isingekuwa ishu tungeona pambano la Denti na Mwalimu wake tu mkono kwa Mkono katika lugha rahisi ina maana mnakiri kuwa Mmoja mmoja walishachezea Vitasa vya kiwango cha lami!
 
Ni kweli viadhabu vidogo kama vile vya huyo mwanafunzi wa mbeya vikofi tu kila mtu anawalaumu walimu waliotoa ka adhabu! Wakati ile ni adhsbu ya kawaida sana kwani ki mantiki yule mwanafunzi alikuwa anapewa mazoezi ya ukomavu, walimu wasilaumiwe, swali la kizushi, hv kwa nn majeshini kuna nidhamu ya hali ya juu ukizingatia askari anamiliki silaha mda mwingi na akawa na nidhamu ya matumizi sahihi ya silaha yake! Hao walimu msiwavunje nguvu kwa kazi waliyoanza nayo, mwanafunzi jeuri lazima arekebishe mapema kabla kumaliza shule na kutuletea taabu mitaani!
 
Kwa vile vikofi vitatu? Tuliosoma enzi hizo tunashangaa kwanini mnashupalia kaadhabu kadogo namna ile.... Sie tulikuwa tumatandikwa kwelikweli... afu ole wako ukamwambie mzee nyumbani... unaangushiwa tsunami nyingine ya kiwango cha tetemeko la Kagera.

Watoto wa siku hizi wqnadekezwa sana

Kutandikwa kwako hakuhalalishi mwingine atandikwe.
 
Back
Top Bottom