Ukweli kuhusu tukio la walimu waliompiga mwanafunzi Mbeya

Ukweli kuhusu tukio la walimu waliompiga mwanafunzi Mbeya

Toa ujinga wako hapa, huyo mtoto ndo wa kupiga ngumi majibaba mazima yale eti mawili yazidiwe na yule mtoto? Hebu wacha hizo kiongozi! Huyo mtoto hawezi kupiga ngumi ya kumfanya mwalimu asalimu amri!!


Huna sababu ya kutumia neno 'ujinga' katika mjadala huu...Huyo jamaa ametoa upande mwingine wa habari...na wako watakaotoa maelezo mengine...Kijana kuwapiga ngumi 'waalimu' hao kwa ngumi za 'kuvizia' inawezekana na baadaye akatimua mbio...Lakini kilichopo hapa kwa wengi wetu ni kuwa hata kama ni kweli kijana yule aliwapiga 'waalimu' hao hiyo haitoshi au siyo sababu tosha kuwafanya waalimu kumpa kipigo kile mithili ya jambazi....Mimi binafsi nataka kuufahamu ukweli wa suala Zima...je, ni kitu kilichowafanya 'waalimu' wale kupanda mori/hasira na kuanza 'kumsulubu' dogo yule???
 
NI KWELI WALIMU WAMEMPIGA MWANAFUNZI KINYAMA HUKO MKOANI MBEYA LAKINI KIJUE CHANZO KILICHOSABABISHA KUPIGWA KWAKE

Na Mathias Canal

Majira ya asubuhi hapo jana nilianza kuiona kanda ya sekunde 38, ambayo tangu nilipoiona kabla ya kujua serikali itafanya maamuzi gani kwa Walimu waliofanya unyama huo mimi niliwatazama takribani watu hao watano wakiwa wanaonekana kumshambulia mvulana mmoja ambaye ni Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya kutwa ya Mbeya ambaye baadaye alianguka chini kwa kupigwa ngumi pamoja na mateke.

Hakika tangu jana nimekuwa nikihangaika kujua chanzo cha Walimu kuwa na hasira za aina hiyo kama Chui Mwenye njaa, Machache haya nimebaini.

KISA CHA KUPIGWA...!

Mwanafunzi huyo kabla ya kuonekana kwenye kanda hiyo alikataa kuchapwa wala kuchuchumaa pamoja na kwamba wenzake wote ambao hawakufanya zoezi darasani.

Aliipohojiwa akamjibu vibaya mwalimu ambapo Mwalimu yule alitaka kumuadhibu kwa kumchapa viboko kama adhamu ya kuimarisha nidhamu yake.

Mwalimu alipojaribu kutaka kumchapa ghafla mwanafunzi huyo alirusha ngumi nzito ambayo ilituama kwenye mdomo wa Mwalimu huyo.

Baada ya kadhia hiyo ambayo haikumaliza hata sekunde moja walimu wengine walioshuhudia tukio hilo waliamua kumchukua mwanafunzi huyo ili kumpelekea ofisini huku Mwalimu aliyepigwa ngumi akiwa ameamua kurudi darasani kutuliza wanafunzi wengine ambao walitaka kufanya vurugu kwa sababu ya kukerwa na Matukio ya ubabe yanayofanywa na Mwanafunzi huyo na Alipoona wanafunzi hao wametulia alianza kurudi ofisini.

Baada ya Mwanafunzi huyo kufikishwa ofisini akaona Walimu wamebaki wawili tu aliwapiga ngumi kiasi kwamba Walimu hawakuwa na namna ya kumkabili.

Mwanafunzi huyo baada ya kuwamudu Walimu wale wawili Akaanza kutoka nje ya ofisi huku akiwa anakimbia yule mwalimu ambaye alipigwa ngumi ya mdomo na akaenda kuwatuliza wanafunzi darasani akamuona mwanafunzi huyo akiwa ametoka anakimbia ndio alipomuwahi kukawa na majibizano ya ngumi na mateke kidogo.

Mwalimu alifanikiwa kumudu majibizano ya kipigo na hatimaye akafanikiwa kumrudisha ofisini kwa walimu wengine hapo ndio kila mmoja akajikuta anahitaji kumaliza hasira zake. Kumbuka Walimu walikuwa na hasira za Kupigwa tena na mwanafunzi wao...! Na kubaki wakiwa wanaugulia maumivu.

TAARIFA NYINGINE MPENYEZO

Mwanafunzi huyu yeye aliridhia kichapo alichopewa na walimu hao baada ya kufanikiwa kummudu akiwa kwenye ofisi ya walimu ndio maana siku 11 toka tukio limetokea hakwenda kuripoti mahala popote, yaaani Hata nyumbani kwao hakwenda kusema kwakuwa anakesi tatu nzito na aliwahi kumjibu hovyo baba yake mbele ya walimu alipokuwa ameenda kutetea asifukuzwe shule.

Achilia mbali hayo Mwanafunzi huyo alishawahi kuvunja TV ya baba yake nyumbani kwao kama wiki mbili zilizopita.

Pamoja na mambo yote hayo Wiki hili amekamatwa na walimu akiwa anavuta bangi shuleni na wenzake. baba yake mzazi hamtaki huyo Mwanafunzi lakini hana namna ya kumkabili.

MTAZAMO YAKINIFU

Serikali umefanya Kazi Mkubwa kwanza kubaini hiyo video imerekodiwa katika shule gani na Walimu hao ni kina nani, hakika ni jambo la kupongezwa sana lakini imesahau kwamba maamuzi yote yaliyofanyika dhidi ya Walimu yameshindwa kuzingatia chanzo Chake Bali imejikita kukabili matokeo, Wahenga walisema Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo lakini wakaenda mbali zaidi kwa kusema Samaki mkunje angali mbichi. Mwanafunzi huyu ni samaki aayetaka kukunjwa akiwa amekauka Kamwe haiwezekani.

Watanzania, Wanafunzi, jamii kwa ujumla itambue kuwa binafsi nimesikitishwa sana na kadhia hiyo iliyofanywa na walimu karibu wa tano kwa mujibu wa Video iliyosambaa mtaani tena imenikera mno mno lakini vyema zaidi kama tutajikita kuhangaika na chanzo cha tatizo ili kumaliza mzizi wake kuliko kukabili matokeo huku tukiacha mambo hayo yaendelee kukutikana mitaani.

Kuteleza si kuanguka lazima tukiri kwa pamoja kwamba hapo tumeteleza kabla hatujaanguka basi vyema tukatazama mahala pa Kushika ili kuhakikisha hatuanguki Tunapotoa maamuzi ni vyema sana tuangalie mambo kwa ujumla wake tusitazame tu wapi kumesisimua Jamii...?

Tutambue kuwa tukio hilo la Mbeya ni la wanafunzi wa Chuo kumchangia na kumpiga mwanafunzi wa shule ya kutwa ya Sekondari Mbeya tukiwaita Walimu maana yake tutajadili pia Chama Cha Walimu Mkoa wa Mbeya (CWT) kinafanya Kazi gani...?

Kuna mwandishi mmoja huwa anasema hawezi kuwa adui kwa kusema Ukweli nami sitarajii hilo.

Naaam, Ni Neno La Wakati Mwema
Mathias Canal (Sauti ya Wanyonge)
0756413465
Igunga-Tabora
Tatizo ni chanzo cha hizi taarifa maana wewe uko Igunga, tukio limetokea Mbeya, halafu maelezo ya wanafunzi wenzake walioshudia sakata hilo ambao walihojiwa na kurekodiwa yanaonesha kwa 100% mwanafunzi alionewa!

Maana chanzo ilikuwa ni kitofanya test, na hakufanya test kwa sababu mwanafunzi huyo hakuwa shuleni siku ya test kwani alikuwa anaumwa,mwl alielezwa sababu hiyo lkn hakutaka kumsikiliza mwanafunzi.

Sasa ndugu haya ya kwako umeyapata wapi,? Yaani chanzo chake. Ili tipate kuyaamini kama ni ya kweli au uzushi tu. Kwani kuna jamaa mwingine majuzi alipotosha umma kwa kueleza kuwa "yule kijana aliyepigwa na walimu hakuwa mwanafunzi bali mwananchi kajifanya mwanafunzi kwa lengo la kuwapata wasichana shuleni hapo," watu wengi waliaminishwa maneno hayo kumbe ni ya uongo!!!!
 
Toa ujinga wako hapa, huyo mtoto ndo wa kupiga ngumi majibaba mazima yale eti mawili yazidiwe na yule mtoto? Hebu wacha hizo kiongozi! Huyo mtoto hawezi kupiga ngumi ya kumfanya mwalimu asalimu amri!!
Huwajui wanafunz
 
Mtaongea mengi mwaka huu na kila mnavyohangaika ku-justify ndo kwanza mnazidi kumbe walimu wengi ni majipu ndo maana mmekazana ku-justify ule unyama wa wenzenu!
 
Tukio limetokea mbeya we upo huko igunga haya umeyajulia wapi??

Sisi tuna judge kwa kile tulichokiona sio hizo habar za kusikia, kama nae alipiga ngumi basi hao walimu watuoneshe nao hyo video ili tuwaamini
 
Wale wote ni wanafunzi yaani watoto! Ushauri kama ww ni mwl mwanafunzi anaonyesha ubabe mbele ya wanafunzi wengine kweli hiyo huleta hasira mwanafunzi anakudindia na kurusha ngumi kwa walimu hiyo ni hatari sana kwani kazi yyt ni ushirikiano na walimu nao wananyongo ni sawa na polisi amekukamata unamtushia ngumi kwa kweli lazima zoezi la kukukamata linasitishwa kwa mda kwanza ule mkong'onto kwanza wakishakuweka sawa do wanakubeba, hivyo wanafunzi wengine akiangalia umri wa mwalimu wake umri haupishani lazima mwanafunzi alete jeuri kwa Mwalimu, ushauri wangu kwa serikali hasa waziri wa elimu au wa tamisemi fanyeni uchunguzi mbona majibu yapo shuleni hapo hapo tena hamtachukua mda kuipata picha yote, walimu nao wananyongo!
 
Matokeo ya kidato cha nne ya uyo mwanafunzi yatadhirisha kama alionewa ama laah, tutaona kama atabebwa na wanao mtetea.
 
Walimu wamevunja sheria ya nchi, period, chochote alichofanya huyo kijana kabla ya tukio hakihalalishi ukatili uliofanywa na walimu
 
Yani ndo ningekuwa mimi ndo mwalimu alafu mwanafunzi anipige ngumi ,duh ningekuwa jela
 
Wanaume na wanawake wa dar bhana acheni kutetea ujinga, ndomana dar kuna mashoga wengi ni kutokana na mnavowalea watoto wenu kishoga shoga, mtu kapigwa tu kdogo vile ndio kulalamika utadhan wale waalimu wamemchinja bhana, mimi kama mimi nasema ivii nakubaliana na naunga mkono kichapo alichopewa yule dogo, vichapo kama vile ndio vitaleta nidhamu kwa watoto wetu na kuwanyoosha, kama sio media kumpa kichwa uyo dogo angekua na heshima na asingefanya tena makosa kwa kuogopa kichapo kama kile tena, eeeh mlidhan neno hapa kazi tu linamaanisha nn?
 
Bwana wee japo serikali imefanya maamuz yaharaka kwa ilichokiona ni unyanyasaji dogo, serikali imefanya gafla kwanza kupunguza jazba ya watz wote ili kuonyesha hawaungi mkonyo dogo kushambuliwa. Pili unaonekana unapenda kutetea sekta yetu ya ualimu kwakusema aliwapiga walimu wawili sio kweli . tatu serikali imefanya hivo iwe fundisho kwa wengine.
Angalizo na Ombi walimu wenzangu fundisheni tuu watt masuala yakufatilia sana kama Mtt ni wako muache . akifeli au afaulu atajua yeye na mzazi wake. Nawasilisha hoja. Mbunge mtalajiwa
 
Simulizi ya kijinga kabisa! Kila ninapoona simulizi za kipuuzi kama hizi napata nguvu kwamba kumbe Ndalichako kafanya uamuzi mujarab kabisa kutimua wale watu! Kama una confidence na unachokiandika kwanini hujatumia I'D yako ya kawaida?! Jana hapa mlikuja na story kwamba yule dogo kashindikana hadi kwao! Baba ake anahojiwa anasema hayo ya ujeuri kwake ni mapya lakini anachojua dogo darasani hazipandi!

Hivi hamuoni aibu wazima kutunga story za kumchafua mtoto mdogo?! Halafu unaweza kukuta miongoni mwenu ni walimu!!
 
Walimu wale wa kike wanapaswa kuthibitisha kama huyo dogo aliwapiga ngumi wale walimu wawili kabla ya kukimbilia nje, maana inaonekana tukio zima la ofisini walikuwepo.
 
Toa ujinga wako hapa, huyo mtoto ndo wa kupiga ngumi majibaba mazima yale eti mawili yazidiwe na yule mtoto? Hebu wacha hizo kiongozi! Huyo mtoto hawezi kupiga ngumi ya kumfanya mwalimu asalimu amri!!

kaka huo ndiyo ukweli wa mambo aliwachapa ngumi walimu wawili ofisini ukiachilia mbali aliyepigwa mbele ya wanafunzi
 
Toa ujinga wako hapa, huyo mtoto ndo wa kupiga ngumi majibaba mazima yale eti mawili yazidiwe na yule mtoto? Hebu wacha hizo kiongozi! Huyo mtoto hawezi kupiga ngumi ya kumfanya mwalimu asalimu amri!!

Ww ambae huns ujinga embu tengeneza u:zi wako tuusome
Au kama ulikuwepo tueleze kwa kina nyuma ya pazia y kile kichapo
Kile kichapo na hizo tetesi zinawiana kbs..hakuna mtu anaependa kudhAlilishwa ww...
 
Back
Top Bottom