Ukweli kuhusu tukio la walimu waliompiga mwanafunzi Mbeya

hhhhj

Member
Oct 5, 2016
41
68
NI KWELI WALIMU WAMEMPIGA MWANAFUNZI KINYAMA HUKO MKOANI MBEYA LAKINI KIJUE CHANZO KILICHOSABABISHA KUPIGWA KWAKE

Na Mathias Canal

Majira ya asubuhi hapo jana nilianza kuiona kanda ya sekunde 38, ambayo tangu nilipoiona kabla ya kujua serikali itafanya maamuzi gani kwa Walimu waliofanya unyama huo mimi niliwatazama takribani watu hao watano wakiwa wanaonekana kumshambulia mvulana mmoja ambaye ni Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya kutwa ya Mbeya ambaye baadaye alianguka chini kwa kupigwa ngumi pamoja na mateke.

Hakika tangu jana nimekuwa nikihangaika kujua chanzo cha Walimu kuwa na hasira za aina hiyo kama Chui Mwenye njaa, Machache haya nimebaini.

KISA CHA KUPIGWA...!

Mwanafunzi huyo kabla ya kuonekana kwenye kanda hiyo alikataa kuchapwa wala kuchuchumaa pamoja na kwamba wenzake wote ambao hawakufanya zoezi darasani.

Aliipohojiwa akamjibu vibaya mwalimu ambapo Mwalimu yule alitaka kumuadhibu kwa kumchapa viboko kama adhamu ya kuimarisha nidhamu yake.

Mwalimu alipojaribu kutaka kumchapa ghafla mwanafunzi huyo alirusha ngumi nzito ambayo ilituama kwenye mdomo wa Mwalimu huyo.

Baada ya kadhia hiyo ambayo haikumaliza hata sekunde moja walimu wengine walioshuhudia tukio hilo waliamua kumchukua mwanafunzi huyo ili kumpelekea ofisini huku Mwalimu aliyepigwa ngumi akiwa ameamua kurudi darasani kutuliza wanafunzi wengine ambao walitaka kufanya vurugu kwa sababu ya kukerwa na Matukio ya ubabe yanayofanywa na Mwanafunzi huyo na Alipoona wanafunzi hao wametulia alianza kurudi ofisini.

Baada ya Mwanafunzi huyo kufikishwa ofisini akaona Walimu wamebaki wawili tu aliwapiga ngumi kiasi kwamba Walimu hawakuwa na namna ya kumkabili.

Mwanafunzi huyo baada ya kuwamudu Walimu wale wawili Akaanza kutoka nje ya ofisi huku akiwa anakimbia yule mwalimu ambaye alipigwa ngumi ya mdomo na akaenda kuwatuliza wanafunzi darasani akamuona mwanafunzi huyo akiwa ametoka anakimbia ndio alipomuwahi kukawa na majibizano ya ngumi na mateke kidogo.

Mwalimu alifanikiwa kumudu majibizano ya kipigo na hatimaye akafanikiwa kumrudisha ofisini kwa walimu wengine hapo ndio kila mmoja akajikuta anahitaji kumaliza hasira zake. Kumbuka Walimu walikuwa na hasira za Kupigwa tena na mwanafunzi wao...! Na kubaki wakiwa wanaugulia maumivu.

TAARIFA NYINGINE MPENYEZO

Mwanafunzi huyu yeye aliridhia kichapo alichopewa na walimu hao baada ya kufanikiwa kummudu akiwa kwenye ofisi ya walimu ndio maana siku 11 toka tukio limetokea hakwenda kuripoti mahala popote, yaaani Hata nyumbani kwao hakwenda kusema kwakuwa anakesi tatu nzito na aliwahi kumjibu hovyo baba yake mbele ya walimu alipokuwa ameenda kutetea asifukuzwe shule.

Achilia mbali hayo Mwanafunzi huyo alishawahi kuvunja TV ya baba yake nyumbani kwao kama wiki mbili zilizopita.

Pamoja na mambo yote hayo Wiki hili amekamatwa na walimu akiwa anavuta bangi shuleni na wenzake. baba yake mzazi hamtaki huyo Mwanafunzi lakini hana namna ya kumkabili.

MTAZAMO YAKINIFU

Serikali umefanya Kazi Mkubwa kwanza kubaini hiyo video imerekodiwa katika shule gani na Walimu hao ni kina nani, hakika ni jambo la kupongezwa sana lakini imesahau kwamba maamuzi yote yaliyofanyika dhidi ya Walimu yameshindwa kuzingatia chanzo Chake Bali imejikita kukabili matokeo, Wahenga walisema Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo lakini wakaenda mbali zaidi kwa kusema Samaki mkunje angali mbichi. Mwanafunzi huyu ni samaki aayetaka kukunjwa akiwa amekauka Kamwe haiwezekani.

Watanzania, Wanafunzi, jamii kwa ujumla itambue kuwa binafsi nimesikitishwa sana na kadhia hiyo iliyofanywa na walimu karibu wa tano kwa mujibu wa Video iliyosambaa mtaani tena imenikera mno mno lakini vyema zaidi kama tutajikita kuhangaika na chanzo cha tatizo ili kumaliza mzizi wake kuliko kukabili matokeo huku tukiacha mambo hayo yaendelee kukutikana mitaani.

Kuteleza si kuanguka lazima tukiri kwa pamoja kwamba hapo tumeteleza kabla hatujaanguka basi vyema tukatazama mahala pa Kushika ili kuhakikisha hatuanguki Tunapotoa maamuzi ni vyema sana tuangalie mambo kwa ujumla wake tusitazame tu wapi kumesisimua Jamii...?

Tutambue kuwa tukio hilo la Mbeya ni la wanafunzi wa Chuo kumchangia na kumpiga mwanafunzi wa shule ya kutwa ya Sekondari Mbeya tukiwaita Walimu maana yake tutajadili pia Chama Cha Walimu Mkoa wa Mbeya (CWT) kinafanya Kazi gani...?

Kuna mwandishi mmoja huwa anasema hawezi kuwa adui kwa kusema Ukweli nami sitarajii hilo.

Naaam, Ni Neno La Wakati Mwema
Mathias Canal (Sauti ya Wanyonge)
0756413465
Igunga-Tabora
 
Toa ujinga wako hapa, huyo mtoto ndo wa kupiga ngumi majibaba mazima yale eti mawili yazidiwe na yule mtoto? Hebu wacha hizo kiongozi! Huyo mtoto hawezi kupiga ngumi ya kumfanya mwalimu asalimu amri!!
 
Hakuna neno au tukio lolote linaloweza kuhalalisha unyama aliofanyiwa Yule Kijana japo nae anaonekana ni Nunda Mkorofi. Hata Kama angemtia Dole Mwalimu nini konde bado haikuwa sahihi kushambuliwa ( ile sio kuadhibiwa).
Story ya kusema alivunja TV ni ya Uongo kwa kuwa kwa Mujibu wa Nipashe ya Leo Baba Mzazi wa Yule Kijana anasema Nyumbani kwake bado hajafanikiwa kuweka Umeme sasa hiyo TV alikuwa anatumia Mkaa au Power bank?

Pamoja na Yote hayo adhabu ya kuwafukuza Chuo wale Vjana ni kubwa mno kwao na familia zao na Taifa kwa Jumla, ingeangaliwa namna ya kuwaadhibu hao Walimu wa Field sio kuwakomoa Kama wao walivyomkomoa Yule Mwanafunzi
 
taifa limehamaki upepo hauwez kubadilika tena nakumbuka nlivyokuwa nasoma shule flan hapo mbeya kama ningekuwa narecord video ya matukio tang 4m1 hadi 4m4 nadhani hakna mwalimu ambaye angebaki salama
 
Naona braza anajiita mtetezi wa wanyonge... Wanyonge wanaokunja ngumi na kumchangia mtoto wa form three... You see, baya ni baya hata likiwa limelipiza baya.
 
Mkuu umesema alimjibu yule mwalimu vbaya je ni jibu gani hilo alilojibiwa?
Pili,kwenye hilo darasa kulikua na walimu wangapi kwasababu umesema walimu wengine walimchukua uyo mwanafunzi na kumpeleka ofisini.
Tatu,kama kweli uyo mwanafunzi ni mkorofi na ni tabia yake kupiga walimu kwanini mwalimu wa nidhamu au mwalimu mkuu ajamchululia hatua kipindi chote kabla ya hao walimu wa mafunzo kuja?

Taarifa yako ina maswali mengi kuliko majibu ya ulichotaka kutuaminisha
 
Hakuna neno au tukio lolote linaloweza kuhalalisha unyama aliofanyiwa Yule Kijana japo nae anaonekana ni Nunda Mkorofi. Hata Kama angemtia Dole Mwalimu nini konde bado haikuwa sahihi kushambuliwa ( ile sio kuadhibiwa).
Story ya kusema alivunja TV ni ya Uongo kwa kuwa kwa Mujibu wa Nipashe ya Leo Baba Mzazi wa Yule Kijana anasema Nyumbani kwake bado hajafanikiwa kuweka Umeme sasa hiyo TV alikuwa anatumia Mkaa au Power bank?

Pamoja na Yote hayo adhabu ya kuwafukuza Chuo wale Vjana ni kubwa mno kwao na familia zao na Taifa kwa Jumla, ingeangaliwa namna ya kuwaadhibu hao Walimu wa Field sio kuwakomoa Kama wao walivyomkomoa Yule Mwanafunzi

Yani watu wametunga habari za uongo ili kuficha maovu ya hap walimu.
Adhabu ya kuwafukuza chuo ni ndogo sana,wanatakiwa kufungwa kifungo cha zaidi ya miaka mi3.
 
bila kujali adhabu aliyopewa dogo,mimi hainiingii akilini kwamba hao walimu walikuwa vichaa kumpiga dogo kiasi hicho,me naona bado wametumia busara sana kwa simulizi hiyo aaaaah dogo anilushie ngumi tena mbele ya wanafunzi hahaha ndo maana sijawa mwalimu busara hizo sina
 
Kile kilichoonekana kikatengeneza mashitaka chenyewe, hakiwezi kupuuzwa kwa hoja za utetezi wa wahalifu na washirika wao, huko siiti kuongea, nakuita kubwabwaja
 
NI KWELI WALIMU WAMEMPIGA MWANAFUNZI KINYAMA HUKO MKOANI MBEYA LAKINI KIJUE CHANZO KILICHOSABABISHA KUPIGWA KWAKE

Na Mathias Canal

Majira ya asubuhi hapo jana nilianza kuiona kanda ya sekunde 38, ambayo tangu nilipoiona kabla ya kujua serikali itafanya maamuzi gani kwa Walimu waliofanya unyama huo mimi niliwatazama takribani watu hao watano wakiwa wanaonekana kumshambulia mvulana mmoja ambaye ni Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya kutwa ya Mbeya ambaye baadaye alianguka chini kwa kupigwa ngumi pamoja na mateke.

Hakika tangu jana nimekuwa nikihangaika kujua chanzo cha Walimu kuwa na hasira za aina hiyo kama Chui Mwenye njaa, Machache haya nimebaini.

KISA CHA KUPIGWA...!

Mwanafunzi huyo kabla ya kuonekana kwenye kanda hiyo alikataa kuchapwa wala kuchuchumaa pamoja na kwamba wenzake wote ambao hawakufanya zoezi darasani.

Aliipohojiwa akamjibu vibaya mwalimu ambapo Mwalimu yule alitaka kumuadhibu kwa kumchapa viboko kama adhamu ya kuimarisha nidhamu yake.

Mwalimu alipojaribu kutaka kumchapa ghafla mwanafunzi huyo alirusha ngumi nzito ambayo ilituama kwenye mdomo wa Mwalimu huyo.

Baada ya kadhia hiyo ambayo haikumaliza hata sekunde moja walimu wengine walioshuhudia tukio hilo waliamua kumchukua mwanafunzi huyo ili kumpelekea ofisini huku Mwalimu aliyepigwa ngumi akiwa ameamua kurudi darasani kutuliza wanafunzi wengine ambao walitaka kufanya vurugu kwa sababu ya kukerwa na Matukio ya ubabe yanayofanywa na Mwanafunzi huyo na Alipoona wanafunzi hao wametulia alianza kurudi ofisini.

Baada ya Mwanafunzi huyo kufikishwa ofisini akaona Walimu wamebaki wawili tu aliwapiga ngumi kiasi kwamba Walimu hawakuwa na namna ya kumkabili.

Mwanafunzi huyo baada ya kuwamudu Walimu wale wawili Akaanza kutoka nje ya ofisi huku akiwa anakimbia yule mwalimu ambaye alipigwa ngumi ya mdomo na akaenda kuwatuliza wanafunzi darasani akamuona mwanafunzi huyo akiwa ametoka anakimbia ndio alipomuwahi kukawa na majibizano ya ngumi na mateke kidogo.

Mwalimu alifanikiwa kumudu majibizano ya kipigo na hatimaye akafanikiwa kumrudisha ofisini kwa walimu wengine hapo ndio kila mmoja akajikuta anahitaji kumaliza hasira zake. Kumbuka Walimu walikuwa na hasira za Kupigwa tena na mwanafunzi wao...! Na kubaki wakiwa wanaugulia maumivu.

TAARIFA NYINGINE MPENYEZO

Mwanafunzi huyu yeye aliridhia kichapo alichopewa na walimu hao baada ya kufanikiwa kummudu akiwa kwenye ofisi ya walimu ndio maana siku 11 toka tukio limetokea hakwenda kuripoti mahala popote, yaaani Hata nyumbani kwao hakwenda kusema kwakuwa anakesi tatu nzito na aliwahi kumjibu hovyo baba yake mbele ya walimu alipokuwa ameenda kutetea asifukuzwe shule.

Achilia mbali hayo Mwanafunzi huyo alishawahi kuvunja TV ya baba yake nyumbani kwao kama wiki mbili zilizopita.

Pamoja na mambo yote hayo Wiki hili amekamatwa na walimu akiwa anavuta bangi shuleni na wenzake. baba yake mzazi hamtaki huyo Mwanafunzi lakini hana namna ya kumkabili.

MTAZAMO YAKINIFU

Serikali umefanya Kazi Mkubwa kwanza kubaini hiyo video imerekodiwa katika shule gani na Walimu hao ni kina nani, hakika ni jambo la kupongezwa sana lakini imesahau kwamba maamuzi yote yaliyofanyika dhidi ya Walimu yameshindwa kuzingatia chanzo Chake Bali imejikita kukabili matokeo, Wahenga walisema Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo lakini wakaenda mbali zaidi kwa kusema Samaki mkunje angali mbichi. Mwanafunzi huyu ni samaki aayetaka kukunjwa akiwa amekauka Kamwe haiwezekani.

Watanzania, Wanafunzi, jamii kwa ujumla itambue kuwa binafsi nimesikitishwa sana na kadhia hiyo iliyofanywa na walimu karibu wa tano kwa mujibu wa Video iliyosambaa mtaani tena imenikera mno mno lakini vyema zaidi kama tutajikita kuhangaika na chanzo cha tatizo ili kumaliza mzizi wake kuliko kukabili matokeo huku tukiacha mambo hayo yaendelee kukutikana mitaani.

Kuteleza si kuanguka lazima tukiri kwa pamoja kwamba hapo tumeteleza kabla hatujaanguka basi vyema tukatazama mahala pa Kushika ili kuhakikisha hatuanguki Tunapotoa maamuzi ni vyema sana tuangalie mambo kwa ujumla wake tusitazame tu wapi kumesisimua Jamii...?

Tutambue kuwa tukio hilo la Mbeya ni la wanafunzi wa Chuo kumchangia na kumpiga mwanafunzi wa shule ya kutwa ya Sekondari Mbeya tukiwaita Walimu maana yake tutajadili pia Chama Cha Walimu Mkoa wa Mbeya (CWT) kinafanya Kazi gani...?

Kuna mwandishi mmoja huwa anasema hawezi kuwa adui kwa kusema Ukweli nami sitarajii hilo.

Naaam, Ni Neno La Wakati Mwema
Mathias Canal (Sauti ya Wanyonge)
0756413465
Igunga-Tabora
Jamaa kamkamata mgoni wake akamla kiboga. Baada ya hapo akasambaza picha kalamba jela maisha. Tafakari naujuwe nikweli umekosea ila hupaswi kuvunja sheria.
 
Unaonekana wewe ni member mzoefu humu JF lakini umeamua kufungua hii ID mpya ili kuweka hili bandiko, je unaficha nini Mkuu? Kwanini ujifiche kwa kufungua ID mpya?
 
Back
Top Bottom