Ramani hizi ni kabla ya mwaka 1993
kwa mawazo yangu ziwa hili lipo malawi watanzania tuache ubabe.hii vita inayo lazimishwa ni kwa maslahi ya watu flani watanzania tuamke tusikabithi akili zetu kwa benard membe na lowasa hawa wanajua watakachokipata katika vita hii ndiyo maana wanaikazania.
Naomba kutokukubaliana na hoja yako si kwa kukipendelea chama chochote wala serikali. Kwa misingi ya sheria ya kimataifa (International Law) kwa ziwa lililo mpakani mwa nchi zaidi ya moja haliwezi kuwa mali ya mojawapo ya nchi hizo. Kisheria (International Law) mpaka unapita katikati ya ziwa. Kwa maana hii, wale wananchi wa nchi zote mbili wanaoishi kando kando ya lile ziwa, wanapoingia ziwani kuoga, kuvua, kuchota maji n.k wanakuwa hawajavuka mipaka ya nchi yao. Watavuka mpaka tu pale ambapo wataenda zaidi ya nusu (katikati) ya ziwa husika. Hii ina maana wanavijiji wa upande wa Tanzania na vitongoji vyake kama Mbamba Bay na kwingineko wana ruhusa kwa sheria ya kimataifa (sio ya Tanzania wala Malawi) kutumia rasilmali zilizopo kwenye maeneo yao bila kubugudhiwa na yeyote.
Kwa kuwa maziwa na nchi zetu hayako sawa (mfano sio duara, pembetatu au pembenne) mipaka inabidi sasa iangaliwe wapi ni kati ya nchi hizo mbili. Mfano ziwa Nyanza au Victoria, tuna nchi tatu hususan Kenya, Uganda na Tanzania na mipaka imewekwa kutokana na ukubwa wa eneo linalopakana na ziwa. Mfano watanzania tuna eneo kubwa la ziwa Victoria kuliko Uganda au Kenya, lakini hakuna mtu atakayeweza kusema mpaka upite Kisumu (Kenya), Jinja (uganda) au Mwanza na kuwanyima watumiaji wengine wa ziwa hilo haki yao.
Sasa kwa ziwa Nyasa, kwa kuwa mpaka wa kusini wa Tanzania unakwenda sambamba na mto Ruvuma kwa kiasi kikubwa, mpaka huo umenyooshwa kiasi kuelekea magharibi mpaka unapoingia ziwani. Unapoingia ziwani unaendelea mpaka kufika nusu ya ziwa (kwa upana wake, sio kwa urefu wake) halafu unapinda kuelekea kaskazini ya ziwa katikati. Ukiangalia ramani ya tatu, mpaka wa Tanzania unaunganisha hapo unapoishia mpaka wa Mozambique na Malawi kuelekea kaskazini. Kwa maana hiyo sehemu ya Tanzania ya ziwa Nyasa ni ndogo kuliko sehemu ya Malawi, ni karibu eneo sawa kabisa na eneo la ziwa lililoko Mozambique, lakini kisheria bado sehemu hiyo ni haki na ni mali ya wananchi wa Tanzania.
Hata mto Ruvuma unaogawa Tanzania na Mozambique ni hivyo hivyo, hatuwezi kusema mto huo uko Tanzania wala Mozambique. Kila upande wana haki na mto huo mpaka nusu ya mto (katikati). Hali kadhalika kwenye bahari pia kuna vipimo vilivyowekwa kwa sheris ya kimataifa inayowalinda wananchi wa nchi inayopakana na bahari kuweza kutumia rasilmali zao ndani ya mipaka yao. Bahati mbaya hizi sheria nilizisoma zamani, huenda kuna mabadiliko, na pia sikumbuki ni kilometa ngapi, lakini mpaka wa nchi kama Tanzania, Kenya, Somalia, Mozambique n.k hauko kwenye ufukwe wa Coco Beach.
Mtu yeyote anayepotosha watu kuhusu ukweli huu hawatakii mema watu wake. Viongozi wa Malawi wanalijua hilo, na wa Tanzania wanapodai kuingiliwa anga yao na eneo lao wana haki ya kupiga kelele. Binafsi sipendelei vita ya aina yoyote, lakini kwa hili wale wanaopiga kelele wana haki ya kusema.
Suala la chokochoko kuhusu Ziwa Nyasa sio la leo, lilikuwepo tangu wakati wa Rais Hastings Kamuzu Banda wa Malawi na Mwalimu, miaka ya 1960. Nadhani sasa lazima lipatiwe ufumbuzi wa kudumu, na wananchi wa pande zote mbili hawana budi kuelimishwa. Isije miaka ijayo likaleta tena mivutano.