Ukweli kuhusu maisha ya watanzania walioko ughaibuni

Ukweli kuhusu maisha ya watanzania walioko ughaibuni

mkuu mimi naona hapo ndiyo unapata connection sahihi za watu ambao watakusaidia kufanya maisha yako sehemu fulani yanakuwa afadhali, maisha kote siyo marahisi kabisa.....kikubwa kujipanga tu uishi sehemu kihalali ili na ww upate huduma wanazopewa wengine huko....

Ni kweli unayosema, tatizo watu wakianza kuelezea mambo ya abroad wanaeleza utasema ni pepo. Muda niliokua masomoni huko nimejifunza mengi, mtu akileta stori za huko hata hanitishi
 
Duh kwa uhandishi nahisi unatoka maeneo ya mpakani wa Tanzania na uganda
 
Walioko nje ya nchi kama professional migrants hao wana kitu cha kusema, wanafanya kazi za maana zenye ujira mzuri na wako kwenye position ya kuwekeza nyumbani, ila wale wa vibarua kwakweli wana hustle kusogeza siku.
 
Kwelii kabisaaaa yaan bongo ni shidaaaa,maji machafu,hospitali huduma mbovu,ajira hamna,,bora huko aiseee wanawaponda wabeba box huku wanatamanii waende na wao huko,,ughaibunii unafundishwa kutokua mvivu,kujitegemeaaaa
Sie wengine tunaishi kwaajili ya pesa za wabeba box, wabongo unafiki umetujaaaaaa
Waambieeeeee
 
Bravo kwa kujieleza vizuri na kutoa insight. Na hongera pia kwa kujitambua na kujipanga upya ukafaidika kwa kwenda majuu
 
kuna watu wanajifanyaga kama hawana shida huku zimewajaa hadi hadi hazina pa kukaa!

mi kwenda huko had niwe nafagia mabanda ya kuku, as long as napata satsfaction ya moyo wangu na target zangu zinaenda nakwenda, eti ughaibun maisha ovyo so tanaznia ndo mazuri!

sema kwa wanaoishi ya maisha ya kurishina vyeo ni ngumu sana kuelewa maisha ya mbambabay huko ambaye hajui hata nini maana ya sokon
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kuna jamaa yangu aliamua kurudi nchini miaka ya karibuni. Yeye tayari alikuwa na uraia wa huko alikokuwa anaishi. Kurudi kwake nchini ilikuwa ni kuanzisha biashara ambayo wageni hawaruhusiwi kuifanya bali Watanzania tu. Sasa alikuwa na mikakati mbali mbali ya kuhakikisha anaingia nchini kama mbongo. Na mikakati hiyo ilikuwemo pia kusaidiwa na kingunge mmoja mkubwa kuja kumpokea JKNIA na kumsaidia kuingia nchni kama "mbongo" na mikakati mingine pia. Kupata passport ya Tanzania alisema haikuwa tatizo. Na aliingia nchini salama salmini kama mbongo.

Wapo wabongo wengi wenye uraia wa nchi za nje ambao wanaishi nchini. Kama hupigipigi kelele kuhusu uraia uliokuwa nao wa nje basi hakuna atakayekufahamu ila ukipiga piga mayowe kila siku kuhusu uraia wako wa nje basi unaweza kuchomewa na ukapewa 24 hours kuondoka nchini.


Ha ha ha mkuu nimecheka Sana

binafsi nina ndugu na marafiki walopata uraia w ng'ambo wamerudi nchini maisha yanaendelea bughza coz hapa ukishajichanganya uraiani baaasi hakuna anaefwatilia wala kujali..


nimechukua point hapo kwenye mayowe ha ha ha unajua mkuu kuna watu hupenda waonekane wanajua hao ndo kinawapata...


Vinginevyo watu wanaishi na maisha yanaendelea hao wanaotafuta icon wacha wahangaike...
 
Abroad uwe umeenda kwa mpango maalum na njia zinazojulikana. Sehemu nyingi maisha yapo ghali sana hasa kwenye accommodation. Unaweza kupata kibarua pesa yote ukawa unalipa bills. Ukiwa na umeenda kihalali unaweza kupataa msaada kutoka ustawi wa jamiii kuweza kujikimu. Mlioko nje zungumzeni ukweli abroad maisha sio rahisi kama unavyoweza kudhani. Ni kweli social services kama maji na usafiri viko poa ukilinganisha na hapa nyumbani. Miji ni misafi na security sio kama hapa kwetu
Mkuu nitasema ukweli kama unavyotaka.Nitaongelea Scandinavia nilikoishi.Ni hivi,ni kweli maisha yako juu ila sio kweli kwamba yako juu kias kwamba kipato chote kiishie kwenye bills,sio kweli kabisaaa,mm nilikua natumia kama asilimia 20 d rest nasave.
Pia ughaibuni haijalish umefikaje,kufanikiwa akili zako tu.Pia hata ambao hawana makaratasi/vibali bado wanaingiza pesa nzuri tu.Wanafanya kaz zinaitwa black jobs.Wasio na vibali kuingiza pesa wanaingiza sema tu kuna vitu kama kuwa na appartment yenye jina lako hawawez kuwa nazo,ila haimaanishi hawana pa kuish,wanapanga nyumba kwa majina ya watu wengine.Kuna watu hawana vibal ila wanapesa kuliko wenye vibal wavivu.
 
Kwelii kabisaaaa yaan bongo ni shidaaaa,maji machafu,hospitali huduma mbovu,ajira hamna,,bora huko aiseee wanawaponda wabeba box huku wanatamanii waende na wao huko,,ughaibunii unafundishwa kutokua mvivu,kujitegemeaaaa
Sie wengine tunaishi kwaajili ya pesa za wabeba box, wabongo unafiki umetujaaaaaa
Waambieeeeee


CC: Karucee
 
Last edited by a moderator:
Walioko nje ya nchi kama professional migrants hao wana kitu cha kusema, wanafanya kazi za maana zenye ujira mzuri na wako kwenye position ya kuwekeza nyumbani, ila wale wa vibarua kwakweli wana hustle kusogeza siku.

usikariri bro....kuna unskilled/semi skilled jobs zinalipa kuliko baadhi ya pro jobs kuna truck driver/plant drivers/builders/carers tena unskilled au semi skilled ni msuli wa muhusika tu....ni sawa na bank teller hapa bongo analipwa tzs 700,000 wakati kuna dereva wa daladala anapata posho si chini 40,000 per day!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Ni kweli unayosema, tatizo watu wakianza kuelezea mambo ya abroad wanaeleza utasema ni pepo. Muda niliokua masomoni huko nimejifunza mengi, mtu akileta stori za huko hata hanitishi
Tueleze hayo uliyojifunza basi na sisi tujifunze.
Kwa upande wangu nitapasifia ughaibuni hadi siku nakufa.
Nisingeenda ughaibuni sijui hta ningrkua wapi leo.
Sijui ningeshakua kibaka wamenichoma moto,sijui ningeshakufa kwa kushindwa kujitibu malaria,wazee wangu sijui wangekua wamechoka kias gani.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mkuu nitasema ukweli kama unavyotaka.Nitaongelea Scandinavia nilikoishi.Ni hivi,ni kweli maisha yako juu ila sio kweli kwamba yako juu kias kwamba kipato chote kiishie kwenye bills,sio kweli kabisaaa,mm nilikua natumia kama asilimia 20 d rest nasave.
Pia ughaibuni haijalish umefikaje,kufanikiwa akili zako tu.Pia hata ambao hawana makaratasi/vibali bado wanaingiza pesa nzuri tu.Wanafanya kaz zinaitwa black jobs.Wasio na vibali kuingiza pesa wanaingiza sema tu kuna vitu kama kuwa na appartment yenye jina lako hawawez kuwa nazo,ila haimaanishi hawana pa kuish,wanapanga nyumba kwa majina ya watu wengine.Kuna watu hawana vibal ila wanapesa kuliko wenye vibal wavivu.

Tena kama huna documents utaishia kufanya casual labors tu, kufagia nakuosha vyombo vya hotel. Mi sipendi kuwapa watu taswira tofauti. Ni kweli life standard iko juu kuliko huku nyumbani, hata niliporudi nilipata shida sana kubre-adjust. Miji michafu na dampo hadi kwenye makazi ya watu mambo ambayo nchi niliyokua hayakuwepo. Ila kwenye ukweli si tuseme tuuu
 
usikariri bro....kuna unskilled/semi skilled jobs zinalipa kuliko baadhi ya pro jobs kuna truck driver/plant drivers/builders/carers tena unskilled au semi skilled ni msuli wa muhusika tu....ni sawa na bank teller hapa bongo analipwa tzs 700,000 wakati kuna dereva wa daladala anapata posho si chini 40,000 per day!

Ukifanya comparison ya currency utakua una compare apples with mangoes. Hizo currency 2 zina value tofauti, ndio maana kuna nchi mkate unauzwa dola 5 karibu Tsh 7000
 
Tueleze hayo uliyojifunza basi na sisi tujifunze.
Kwa upande wangu nitapasifia ughaibuni hadi siku nakufa.
Nisingeenda ughaibuni sijui hta ningrkua wapi leo.
Sijui ningeshakua kibaka wamenichoma moto,sijui ningeshakufa kwa kushindwa kujitibu malaria,wazee wangu sijui wangekua wamechoka kias gani.

Nilichojifunza maisha yanaweza kua magumu sehemu zote. Hata mimi mwanzo nilikua siamini mtu anaweza kupigika akiwa nchi za watu. Mi nilikwenda kusoma tena nilikua na scholarship, pia nilifanya vibarua. Nimerudi niko poa ila ni kwasababu scholarship yangu ilikua inanilipia kila kitu. Otherwise saving ni ngumu sana
 
Ukifanya comparison ya currency utakua una compare apples with mangoes. Hizo currency 2 zina value tofauti, ndio maana kuna nchi mkate unauzwa dola 5 karibu Tsh 7000

bro,nimekwambia kuna unskilled zinalipa kuliko pro jobs....kuhusu bank teller wa bongo namlinganisha na dereva wa daladala bongo hii hii....dereva anapata tzs 40,000 kwa siku bank teller wapo wanapata laki saba au chini kwa mwezi, dollar inaingiaje hapo!!!!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Naona kumekua na maneno meengi kuhusu watanzania waishio ughaibuni.
Mimi nimeishi Scandnavia kwa muda mrefu ila baada ya kutimiza malengo yangu nilirudi nyumbani for good.Kwa sasa huwa ninakwenda mara kwa mara kwa sababu ya kibiashara kisha ninarudi nyumbani.

Kusema ule ukweli wa Mungu,kwa watoto wa maskini kama mimi ulaya ni bora kuliko bongo.Hapa nitaiongelea ulaya kama ninavyoifahamu mimi.Mimi mzee wangu hakua tajiri kama mzee wa Le mutuz,Tanzania niliyozaliwa mimi na kukulia ni tofauti sana na Tanzania aliyozaliwa na kukulia kaka yangu Le Mutuz.Mim Mungu alinijalia sana akili za darasani lakini kutokana na umaskini wa wazee nilishindwa kuendelea na chuo.

Ikatokea zali nikaenda scandinavia,nilienda kule nikiwa na malengo mawili,kusoma na kutafuta mtaji wa maana wa kijiajiri.Mungu alinisaidia,nimesoma,nina masters yangu,nina nyumba sita nimepangisha,nyumba moja ninafanyia biashara zangu na moja ninaishi na wadogo zangu na moja iko mkoani wazee wamejisitiri.Nina viwanja na mashamba.Vyote hivi nisingekuwa navyo leo kama nisingeenda ughaibuni.

Pia Mungu alinisaidia nikakusanya pesa ambazo nilitumia kujiajiri.

Mimi niliajiriwa kwenye kampuni ya kutengeneza magari.Huko nilikua na waafrika wengine wengi tu.

Sio kweli kwamba sehemu pekee wabongo waliyo nayo ni kwenye birthday za sebuleni tu LOL.Ulaya kuna viwanja vya maana bana za kula bata bongo itasubiri sana tu.Kitu kinachofanya wabongo wakusanyike kwenye hivyo vipati hadi nadhani ni ile hali ya kufurahia kukutana na wabongo wengine.Pia sio kila mtu anapenda kuwa kwenye hiyo mikusanyiko ya wabongo,mimi ni mmoja wa watu ambao nilikua sipendi kujimix na wabongo wenzangu.

Suala la kwamba wabongo walioko ughaibuni wana maisha magumu sikubaliani nalo.Kwanza kabisa idadi ya watanzania walioko tanzania wenye access ya internet inayowawezesha kusema wabongo wa ughaibuni wanateseka ni ndogo sana ukilinganisha na watanzania walioko bongo wasiojua hata internet ni nini.

Mimi kwa sasa ninaishi Tanzania na ninafurahia maisha ya hapa sababu ughaibuni imenisaidia leo hii sihitaji kwenda kujambiana kwenye madaladala,leo hii nikipata ugonjwa usio na tiba ya kueleweka bongo naenda zangu kutibiwa Scandinavia,mm nina uraia wa scandinavia tayari.

Hakuna binadamu yeyote awe muafrika au mzungu au muarabu hata awe amechoka vipi financialy aliyeko scandinavia anayelala njaa eti kisa hana hela ya chakula.Kwa Tanzania kila jua linapokuchwa kuna mamilioni ya watoto na watu wazima wanalala njaa.

Scndinavia inaongoza kwa uchache wa vifo vya watoto na wazazi,kwa Tanzania hebu tuchukue sekunde tano kuwaombea R.I.P dada na mama zetu watakaokufa wakati wakijifungua usiku wa leo.Tanzania mama zetu wanajifungua huku wakitzabwa makofi na manesi.Dada zetu waliko ughaibuni wanajifungualia katika mazingira kama mtu yuko hotelini,hata wanaojifungulia Aghakhan watasubiri sana compare na wanaojifungulia hospitali za serikalini ughaibuni.

Tokea nimeishi ughaibuni sijawahi shuhudia umeme ukikatika wala maji.Huwa wanayafunga tu kwa masaa au kuukata umeme kwa masaa na hapo mnapewa taarifa kuwa saa fulani mpaka saa fulani maji au umeme utazimwa.Sijawahi kuona watoto wanaotembea peku na kaptura zimechanika kwenye masaburi.Sijawahi ona mtoto akishindwa kusoma kwa sababu mzazi hana pesa,sijawahi ona mtu anakufa kwa kukosa elfu mbili ya kununua dawa,sijawahi ona watoto wenye utapiamlo,sijawahi ona watu wakitembea pekupeku,sijawahi ona ambulance za vibajaji LOL,sijawahi ona wakulima masikini kama hawa wa Tanzania.

Scandinavia maji huchemshi,unafungua bombani unakunywa,ukitaka ya baridi au ya moto kila wakati yapo.

Wkati naishi ughaibuni nilikua sina gari binafsi,japo magari ni bei chee sana kila mtu anaweza kuwa nalo cha muhimu tu uwe na vibali vya kukuwezesha kupata driving licence.Sikuhitaji gari binafsi kwa sababu usafiri wa public ni wa starehe.Baada ya kurudi bongo imenibidi tu niwe na usafiri sababu daladala kusema ukweli ni hiyo shida tu lakini ni mateso.

Wabongo walioko ughaibuni wanabezwa kwa kazi wanazofanywa,fine,hata mimi huko kwenye kampuni ya magari sikuwa nafanya kazi niliyosomea,ila ukweli ni kwamba nilikuwa nalipwa vizuri,wakati naanza nilikua nalipwa kama milioni sita za madafu kwa mwezi.Baadae waliniongeza,sasa kwa mtoto wa maskini kama mimi ukiniambia nilivokua ughaibuni nilikua nateseka nakuona unaongea kichini maana mdingi wangu angekua nazo hizo nisingeshindwa kwenda chuo bongo wakati kichwani kuko vizuri.

Hata wanaosafisha wazee hakuna anayepokea chini ya milioni nne za madafu kwa mwezi.Hapo nimetaja kima cha chini.

Kitu ambacho ambacho kwangu kilikua kinanipa stress enzi naishi ughaibuni ni kwamba sijawahi kufeel at home.Hii hali ndiyo ilinifanya kusave na kufanya kazi kwa bidii hadi nikatimiza malengo yangu nikarudi home.Kwa kifupi social life ya ughaibuni sucks(,huu ni mtizamo wangu).

Inshort kwa upande wangu mimi hata wale watanzania wanaoishi ughaibuni bila vibali mateso yao hayafikii hata theluthi ya mateso ya watanzania masikini walioko Tanzania.

Ughaibuni ni kweli kuna maisha ya ghali,ila ukiishi kwa malengo yako hakuna asiyefanikiwa.Pia ukiamua kuwa mtu wa bata ughaibuni utakula bata za maana kuliko wala bata wa bongo.

Ni kweli wahamiaji wengi(sio wabongo tu) wanafanya kazi za wazee,kusafisha na nyingine kama hizo ila ni ukweli pia kuwa wapo wapo wengi tu wenye kazi zao za maana.
Pia wewe secretary au mfanyakazi kwenye kampuni ya simu bongo na nyingine kama hizo hebu jiulize unapata shilingi ngapi kwa mwezi hadi umcheke mwenzio anayesafisha wazee na kupata milioni zake nne kwa mwezi?

Kitu ambacho wabongo wamewazidi walioko ughaibuni ni good social life tu.

Umeongea ukweli mtupu. Yeyote atakayekubeza au kukukashifu ni ana wivu tu wa maendeleo yako. Hata mimi wakati nasoma kuna mahala nilihisi kama unajivuna hivi au una majigambo lakini hapana ukisoma vizuri you have stated the simple truth according to you. Hongera sana kwa hatua ulizopiga ndugu ni haki yako.
Wengine wameenda huko wakarudi na raba tu. Keep it up. Utafute mke na watoto sasa. Hahahaa!
 
Wakiyasikia hayo mahasira yanapanda na kutema nyongo tu ha ha ha ha

Watajiua jamani

Hhhhhaaaaahhhhhaaaa uwiiiiiii kama majini makata, wabongo kwa umbea hatujamboo yaan sie banaaaa bora nihameeee kabisaaaa bongoo
 
Walioko nje ya nchi kama professional migrants hao wana kitu cha kusema, wanafanya kazi za maana zenye ujira mzuri na wako kwenye position ya kuwekeza nyumbani, ila wale wa vibarua kwakweli wana hustle kusogeza siku.
Sio sio kweli,binadamu wa aina yeyote awe msomi au sio msomi akishafanikiwa kukanyaga ughaibuni anayo nafasi ya kufanikiwa,cha muhimu kama kwa Scandinavia ni kujua lugha yao then unaenda kusomea kajikoz ka kazi unayotaka kufanya then unaajiriwa,hata wanaosaidia wazee wanasomea,kuuza madukan unasomea,hata kusafisha wanasomea vikoz vya miez mitatu hivi jspo sometimes unaweza kupata bila kusomea hasa usafi na nyingine,ila wazee lazima usomee.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom