Ukweli kuhusu "Kaskazini kuendelezwa na Wanakaskazini"

Ukweli kuhusu "Kaskazini kuendelezwa na Wanakaskazini"

Wacheni ubaguzi Tanzania ni yetu sote hata wasio wa kaskazini wamechangia maendeleo.
 
1.)...

Kaskazini ni maeneo ya mwanzo ambayo Wamisionari wa Ukristo walijenga MAKANISA na SHULE. ...

Nahisi maeneo ya mwanzo ni Peramiho na Ndanda. Nisahihishe kama una data tofauti. Nimeupenda mchango wako.

Niongezee tu kuwa waKaska wawashukuru zaidi waarabu waliowaimarisha kibiashara na kuleta bunduki.

Wakija waarabu Kaska ilikua na vita vingi sn vya kienyeji na alliances za machifu/Mangi kadhaa dhidi ya wengine. Na hapo uchawi na teknolojia ulitamalaki. Mangi flani angenunua uchawi Tanga na Chuma Upare ili amzidi mwingine kushikilia biashara ya Northern corridor.

So uarabu na uislamu usiwekwe kando.

Kuthibitisha hilo, Mangi wa Marangu walishasilimu kitambo sana mfn. Hassan Mareale na walioana na waarabu (huenda ndo sababu waMarangu wana weupe sana wa sura na nywele msokoto).

Figisu za kiungozi na kukosa mtoto wa kiume nadhani ndo ziliondoa utawala wa Mangi muislamu.

Msikiti wa kwanza kabisa klm ulijengwa marangu maeneo ya waMangi. Na upo hadi leo (walau location) kwa wenye taarifa zaidi.

Elimu credit iende kwa wakristo biashara credit kwa waarabu.
 
Na sasa kibosho ipo pia mkuu njoo uone,mimi nkipanda gari ubungo nakanyaga lami mpaka mgombani kwetu kule kibosho,nikiingia msikitini napiga rakaaa ktk zulia na huo pia upo mgombani huko kibosho
Mkuu kibosho unasalia kombo, nkomongo au unaenda lyamungo?
 
Nimekubali uchambuzi wako lakn hapo ulipowashambulia watu kwa dini yao ndio umeonyesha kua ni mpuuzi wa kiwango cha lami maana hao wanaolalamika Kaskazini kupendelewa sio waislam tu bali wapo wanadini nyingine wengi kutoka mikoa mbalimbali wanaolialia na sio waislam
Amesahau pia kwamba waarabu na uislam ndo ulileta hamasa kubwa sana ya biashara Klm na kaska kwa ujumla
 
Hayo maendeleo yako wapi??

Mbona mwanza imepata hadhi ya kuwa jijji mwaka 2000 lakini Kilimanjaro mpaka leo ni manispaa??
Mwanza ni jiji kwa sababu watu wanaoishi mjini (katikati ya mji-kulala vibarazani wanazidi milioni moja )

Moshi watu wanaenda kufanya biashara mjini, jioni wanarudi kwao vijijini ambako kuna huduma zote za kijamii
 
Mwanza ni jiji kwa sababu watu wanaoishi mjini (katikati ya mji-kulala vibarazani wanazidi milioni moja )

Moshi watu wanaenda kufanya biashara mjini, jioni wanarudi kwao vijijini ambako kuna huduma zote za kijamii
Hivyo unalinganisha Mwanza na Arusha au Moshi. Hahaha kwa taarifa yako in jiji la Arusha tu ndo kunanyumba za miti na matope. Nenda kata ya ungalimited
 
Mkuu Kaskazini ni Tanzania ama ni nchi gani? Kama iko ndani ya mipaka ya Tanzania ni maendeleo yetu sote.
Hivyo ni kusema wakati Mikoa MINGINE IKIKUMBUKWA kimaendeleo basi watu wa Kaskazini MSIPIGE kelele maana MLITANGULIA!
Hata hivyo usimdharau aliye chini SIKU MOJA atafanikiwa.
Maana Kiburi huja kabla ya mwanguko/PRIDE comes before a FALL!!
Kaska hawana majivuno kamwe. As a people. Humility yao ndo imefanya wapenye misukosuko mingi sana tangubawamu ya kwanza. Msome Gervas Tatah Mlola katika "Ways of a Tribe"
 
Nadhani ukilinganisha kanda hizi mbili utaona ni ipi inaendelea kwa kasi. Pia utaona mabadiliko makubwa hasa kwenye sekta ya elimu umeme na makazi.

Pia ukiongelea hizi kanda uwe specific unaongelea mji au eneo gani.

Ki mkoa hakuna mkoa wa kaskazini unaoikaribia Mwanza kama mkoa kwa kila kitu. Labda barabara.

Kwa ufupi. Ukiondoa MOSHI ambayo wana lami hadi milimani huko machame. Hakuna maendeleo ya zaidi yaliyopo kanda ya kaskazini ambayo kanda ya ziwa hawana KWA UJUMLA WAKE.

Iwe ni elimu maji ujenzi wa nyumba za kuishi na za biashara. kipato yaani utajiri wa mmoja mmoja au hata umeme na afya.

Tukubali kwamba wasukuma wanajenga kwao kwa kasi ya ajabu na miji ya usukumani inakua kwa kasi sana.
 
HAWA WATU WA KASKAZ NI WAJIVUNI TU MAENDELEO WALIYOPATA SIO YA KUJIVUNIA SANA KWANI BADO KUNA KUNDI KUBWA LA WASIOSOMA NA MASIKINI WALIONDELEA NI WACHACHE YAPO MAKABILA WATU WANA PESA LAKINI KIMYA KAMA WAPEMBA NA WAKINGA.HUKO HUKO KASKAZ NDO KUNA WATU WANAVAA NGOZI NA WANALALA NYUMBA MOJA NA NGOMBE
Unajua lawama za mapigano ya wafugaji na wakulima lawama zinaenda kwa watu wa wapi? Japo si kweli. So walianza kulala na ng'ombe na sasa wanalalamikiwa kuvamia nchi nzima.
 
Wewe sijui wa wapi?

Wasonjo wapo manyara sio Arusha.

Arusha ina waarusha,/wamasai wachaga na wameru

Nenda kaangalie maisha yao, kaangalie nyumba zao, kaangalie miundo mbinu halafu ulinganishe na huko kwenu.
Miundombinu ipi ya wamasai zaidi ya nyumba za msimu pale Enguikument
 
Mkuu leo hii ujue kwamba:

Hakuna mkoa uliopaswa kuendelea sana hapa Tanzania kama Tabora. Na sababu ni hizi zifuaeazo:-

1) The Nyamwezi / wanyamwezi ni kabila la kwanza kufanya biashara Tanzania bara kama ilivyo Wakamba kwa Kenya. Mliwatangulia kabisa wachaga ktk trade activities ila leo ni zerooo.

2) Utawala mzuri wa machief wenu kuanzia Mirambo-> Fundikira

3) Uwepo wa Tabora Boys na Tabora Girls kwenu.

Ila mkalalaa....leo mnalalamikia UKASKAZINI.
Chanzo cha wao kufanya biashara sana ilikua ruti ya waarabu kina tipu tipu
 
Mtoa thread ana inculcate spirit ya ukanda na Ukabila bila kujitambua. Mpishano wa kimaendeleo ni mlundikano wa factors nyingi sana! Mtoa mada anamawazo ya Kikoloni Tena yanauono wa Kibaguzi sana! Hana tofauti na wale wanaoamini ktk Hamitic Myth kuwa watu wa race fulani ni superior na ndio wenye fikra za kimaendeleo kuliko wengine! My friend, Kaskazini na Wanakaskazini ni Watanzania na they have nothing unique except favour due to colonial regionalism which favoured that part of the country basing on their own colonial reasons and marginalising other areas. Nani alichagua kuzaliwa mahali au Kabila hilo hata apate courage ya kujinasibu mbele za watu Timamu? Stop being mkoloni ktk fikra zako za kiafrika! North is nothing out of JMT

Nadhani hafanyu uchochezi. Ni mmoja kati ya wengi wannayoishuhudia dhambi ya ubaguzi na ya wazi na ya kihistoria kwa kabila hizi ambazo hazijamkosea yeyote zaidi ya kifanya kazi kwa bidii na kujibana pia kujitesa
 
Miundombinu ipi ya wamasai zaidi ya nyumba za msimu pale Enguikument
Ukitafuta tu sehemu chache zenye mapungufu haitaleta maana kwasababu hata USA kuna mahali tu kuna gheto za ajabu

Hara Mwanza na kuendelea kote kuna sehemu tu yenye nyumba za hovyo.

Umeenda meru na uarushani huko migombani?
 
Kaskazini. Haha hii ni Mada mbaya lakini kwa uzoefu wangu sijaona tofauti muhimu ya kikanda nchi hii. Sasa Arusha ukiondoa jiji wilaya zake in maskini tu kama maneo mengine Tz. Jamani hivi munazugumzia Moduli nmafahamu Irkisale au vipi.. Unaweza hisi uko pre history.
Irkisale ndio wapi mkuu?
 
Back
Top Bottom