Biblia ni kitabu pekee cha kidini kilichojaribu kugusa vitu vingi, na hata kujaribu kutengeneza kitu kinaitwa unabii!
Hebu tuangalie unabii mchache wa biblia kuhusiana na dunia ya leo, nitatumia zaidi
mathew 24
1. Kutakuwa na
MANABII WA UONGO
Kwa mtu aliyebwia opium ya dini, sentensi hii ina maana ya manabii walio kinyume na huyo mungu. Lakini hebu tuitazame kwa umakini, Kwa mujibu wa biblia, nabii wa uongo ni yeyote aendaye kinyumee na mafundisho ya biblia.
picha halisi
Waandishi wa biblia walijua hawajatimiza kila kitu katika kufika lengo halisi la uandishi wa kitabu kile, Hivyo wakajua kabisa watakuja watu wenye
akili na fikra sahihi na kuitangazia dunia madhumuni halisi ya dini, hao watu wakawekwa pamoja na yeyote aongozaye kundi la watu huku akiruka hata kifungu kimoja, na wote wakaitwa manabii wa uongo.
Je fundi gani asingeweza kutabiri ajali ya gari kama anajua breki hakuzitengeneza imara?
2. Kuutakuwa na matetemeko ya ardhi.
Matetemeko ya ardhi yalianza hata kabla ya kuwapo kwa biblia, Biblia haijawahi kutaja kitu chochote ambacho enzi hizo hakikuwa kimevumbuliwa, mfano, badala ya kudeal na matetemeko ya ardi, kwa nini isitabiri na kutaja kutokea kwa
super computers, cha ajabu inacombine vyote na kusema kutakuwa na maendeleo makubwa,
Je mjinga yupi asiyejua kwamba mwanadamu ni kiumbe
aliye na nguvu ndani yake, ambazo anapozidi kuzoea mazingira (duniani) anazidi kuvumbua na kukuza maendeleo yake? Inahitaji utabiri?
3 Kutakuwa na njaa
Sijui hata mwandishi alifikiria nini, jambo la
kawaida kama hili halihitaji unabii ili litokee, Old tale stories (old testament) inasema kulikuwa na njaa hadi wanawake wa ufalme wa suleimani waliwachinja watoto wao wachanga, Njaa ya Wanaisrael ilihitaji msaada tu wa mana toka mbinguni (real?)
Sasa mpuuzi gani aliyeyashuhudia au kuyasikia mabaa haya ya njaa atabiri kutakuwa na njaa duniani?
Wastage of time and energy.
4.Watu watajipenda wao wenyewe
Naomba niseme kwa ufupi, Wanaisrael wanapoua wakaazi wa nchi za Kanaan, Yeriko, Wafilist, Waashuru, walikuwa wanawakilisha tabia ipi ya mwanadamu, kupenda wote sawa na unavyojipenda, au walionyesha maana halisi ya kujipenda tu wao wenyewe?
Hakuna unabii hapo.
Ni kitabu pekee kinachosema
hakuna jipya chini ya jua (Mhubiri) na hapohapo kinatabiri
mapya yatayotokea wakati wa siku za mwisho (mathew) huku kimesahau kwamba yote
yalitokea kabla hata huyo yesu hawajamtengenezea script.
Kutabiri mvua itanyesha baada ya kuona mawingu mazito ni
kutuibia.
waandishi wa biblia
kajipangeni upya.
Ntarudi na Quran! ....
cc
Ishmael FaizaFoxy Eiyer Mashaxizo
Njoni na Tusemezane!