Ukweli kuhusu ATCL Boeing 787-8

Naona wanatuandalia kifo. Kama mtengenezaji anagoma kupanda ndo sembuse mm kapuku. Siji panda hilo kitu[emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35]
hiyo doc video hakuna kitu kuhusu tween teens na mwisho anakwambia hakunaa ndege hivi sasa duniani inanunukiwa kama dreamliner.
 
Ndege haijawahi kutumika, imekaa muda mrefu bila kutumika na yeyote ikisubiri mteja wa kuinunua
Mkuu ukumbuke hiyo ndege 0019 RwandaAir waliinunua.
Ref soma viambatanishi [emoji115] [emoji115] [emoji115] .
 
Mkuu ukumbuke hiyo ndege 0019 RwandaAir waliinunua.
Ref soma viambatanishi [emoji115] [emoji115] [emoji115] .

Soma vizuri, hiyo ndege haijawahi kutumika. Kununuliwa au kuwekewa oda haimanishi kutumika mkuu!
 
Aisee uko vizuri! Hongera!
 

Asante samurai kwa kusaidia kupanua wigo wa mjadala utata unaoendekea kuhusu ununuzi wa Boeing 787-8 Dreamliner, ati ni moja ya hizo ndege 12 Terrible Teens!

Nikirejea hoja zako hapo juu (nimeziwekea namba):
1) Wanajamvi wanaounga hoja ya mtoa mada, wanapinga ununuzi wa hiyo ndege kwa hoja za kisiasa, kwamba nchi imenunua ndege kati ya zile zikizokataliwa na isiyolingana na thamani yake. Kwa sababu hiyo kuna harufu ya ufisadi. Nawe samurai unahitimisha hisia zako hivyo.

Je, kuna ukweli katika hoja hiyo? Umeijibu kwa hoja zifuatazo:

2) Kiuzalishaji viwandani, ni mara chache kuondoa/kubadilisha line of production yote kwa sababu ya gharama na muda. Muundo wa ndege kama muundo haubadilishwi km Boeing inabaki Boeing tu ikibadilishwa kulingana na matumizi. Vile vile gari hubaki na muundo wake na kubadilishwa baadhi ya vitu, km Benz.

3) Uamuzi wa kununua aina hiyo nina amini umezingatia mahitaji yetu kwa wakati huu. Mimi kama mimi naweza kuhoji uamuzi huo, lakini ni busara kuwaamini waliofanya uamuzi huo.

KUPANGA NI KUCHAGUA - hata ndoa (mwenzi wa maisha) ni kupanga na kuchagua si majaliwa
 
Umefanya vema kutafiti na kutoa maelezo. Huna haja ya kumtetea rais au kujipendekeza. Kama anaamua kila kitu na kukataa ushauri umakini wake unatoka wapi? Usijishushe hadhi mkuu.
 
Ok well said.
Unaponishangaza ni hapo unaposema una imani na JPM.. Utakuwa vipi na imani nae wakati yeye ndie ameshugulikia deal yote ya hii ndege. Kama tumepigwa yeye ndie Mhusika no 1 and not otherwise.
Kumbuka hata negotiations na Boing kafanya yeye maana yule President wa Boing alivyokuja straight alienda kukutana nae Ikulu.
Kama kuna any ufisadi kwenye hili, JPM yumo.
 
Kwenye hili namtetea magu kwa angle moja. Kuna uwezekank JPM hajatapeli ila ametapeliwa.
Lilikuwa kosa takatifu kumexpose raisi na meneja mauzo ambaye kazi yake kuu ni kuvutia wanunuzi kwa raisi asiye na uzoefu halafu impulsive.

Kajiona mjanja kuamua haraka haraka kumbe wajanja wamemuingiza kingi.

So, basically kosa la JPM ni kujifanya mjuaji kumbe kwenye haya maswala mweupe.

Ndio maana tumeuziwa hili dege la showroom kwa bei ya brand new
 
Unakumbuka mchakato ulivokuwa? Na ushapata uhakika ni hzo ndege? Subir hilo dege lije tuone
 
Ndege ni toleo la mwanzo la ndege 20 na sio zinazotengenezwa baada ya hizo 20 nandege ni teyari iko ready na si ya kwamba inatengenezwa from scratch. By the way ndege hiyo ni mpya haijatumiwa na kampuni yeyote lakini ilikaa kiwandani kwa miaka mingi bila kupata mnunuzi ndio bei ikapungua.
 
Unakumbuka mchakato ulivokuwa? Na ushapata uhakika ni hzo ndege? Subir hilo dege lije tuone
Unataka zije nylon covered seats ndio mseme ni brand new?

Unakngelea mchakato,kuna mchakato gani zaidi ya kauli ya jpm kuzinunua?kuna tenda iliyotangazwa?inaweza kutoa majibu hiyo tenda wali-apply makampuni mangapi?

Watu wanatazama airframe na series number.,hilo dide limeundwa toka 2009 hadi leo lilikosa wa kulichukua.

Hii tabia ya kununua vitu vya showroom( showcase) ni tabia turufu ya kanda ile., sio jambo la kushangaza.
 
Unaona sasa? Emu leta tena huo ushahid wa series number ya airtanzania iliyoko huko kiwandan. Afu uje na valid source.
 
Daah kweli raisi wetu yupo makini sanaaa yan mpaka naogopa,vp lakini ilo lidege c litakua linaenda nje ya nchi au ni viwanja vya om tu
 
Afu uje usome na hii. Machakato ulikuwepo au ulitaka ushirkishwe?

Rais Magufuli Atema Cheche Ndege Mpya. | Dunia Leo
 
Kilichotokea kwenye ununuzi wa MV daresalaam naona kina endelea tena kwenye ndege hii sio bahati mbaya ni jambo linalofanywa kwa uzoefu na lengo maalumu, tutoke nje ya box watanzania nchi yetu inaendelea kutafunwa na wale wanaojinadi kuwa waadilifu wanapambana na mafisadi. Mwadilifu alikuwa baba wataifa tu.
 
Basi tutakuwa tuna tatizo kama taifa... hii issue ya kufanya manunuzi halafu baadae tunakuja kugundua tumepigwa huwa inaniumiza sana...
.
Hivi sisi hatuna 'smart people' to make 'quality decisions'..!!!!!??
Nikiwa shule nilifundishwa kitu kinaitwa feasibility study...
ni kheri tukatumia muda kidogo kujiridhisha kabla ya kufanya manunuzi kuliko kuharakisha kufanya manunuzi na mwisho wa siku tunakuja na kitu kilicho chini ya kiwango.
Kwani tulikuwa na haraka gani ya kununua ndege pasipo kujiridhisha kwanza..!! Tumekaa muda gani bila kuwa na ndege za maana ,?Je miezi minne mitano au hata mwaka tuka-research tutakuwa tumepata hasara gani ? tulishindwa nini hata kutumia pesa kidogo kutuma timu ya watu wetu waende huko kutafiti kabla ya kufanya manunuzi??!!
Mara nyingi tujifunze kwa watu 'MAKINI' waliowahi kufanya kile ambacho tunataka kufanya ili tufanye maamuzi yaliyo na tija.

we must accept the fact that, mambo mengi hasa ya teknolojia mpya tunakuwa hatuna uelewa nayo wa kutosha wakati mwingi..
Please let us put much efforts on feasibility study before making our decisions..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…