Ukweli kuhusu ATCL Boeing 787-8

Ukweli kuhusu ATCL Boeing 787-8

Embu nifupishie kuwa nani ameitumia hiyo ndege na ilitumika kwa muda gani? Na pia hizo tarehe zote vipengele kwa kifupi vinaashiria nini hadi Dec 2016. macho yananiuma nimeshindwa kusoma yote vizuri.
Kisebengo haya mambo mazito wewe subiria hoja za Bashite huku hakukufai
 
Nanukuu

Buyers would probably pay less than half the current $211.8 million list price of the 787-8 version, Kelly said. The 787 teens have a market value of $115 million each for a single-unit or small lot sale, according to Avitas estimates. Airlines will probably demand 10 percent to 15 percent discounts, bringing the price closer to $100 million, Kelly said.
 
Acha upuuzi wewe mtoto huyo rais wako ndiye aliyepiga dili hili. Kisha anawaita wenzie wapiga deal. Huyu mtu tumefanyajazi nae tunamjua kinoma. Si msafi hivyo mnavyodhani.

Embu elezea hayo unayodai eti kapiga dili, shuka kama hata unakidunchu cha maelezo zaidi ya kufata mkumbo bila kufikiria.

Jisikitikie
 
Kisebengo haya mambo mazito wewe subiria hoja za Bashite huku hakukufai

Eeeeeeeh kawaambie visebengo wenzako. Mimi hapa nimejaa tele nawapa yao hawa wadaku na wafata mikumbo wanaotutia aibu watanzania wengine sie.
 
Shalom watanzania wenzangu!

Disemba 12, 2016 ilikuwa siku ya furaha kwa baadhi yetu tuliomchagua JPM na Tutamchagu tena 2020 Mungu akitujaalia na wengine mlinuna baada ya taarifa kutoka serikali imeweka oda Boeing, ili kununua ndege ya kisasa kabisa 787-8.

Na yakwamba serikali itatoa $224.6Millioni ili kupata ndege hiyo.

Kumekuwa na taarifa mbali mbali, kwamba manunuzi haya yana chembe chembe za ufisadi. Na kwakuwa sipendi kuamini vitu bila kufanya utafiti nami nimeona nizame kwenye websites mbali mbali kutafuta ukweli.

Kwa ufupi kama wengine wasemavyo ni kweli hata Mimi nimeshaamini "SERIKALI IMEPIGWA"
lakini hadi kufikia hii Conclusion kuna mambo ya msingi unatakiwa kuyajua.

1. SERIAL NUMBER(SN) NA LINE NUMBER.
-Kila ndege huwa na serial number yake kama yalivyo magari. Ndege tulioagiza serial number yake ni 35508
-Line number ni ndege ya ngapi kutengenezwa. Kwa mfano kama zimetengenezwa ndege 10. Ndege ya kwanza itakuwa LN1, ya pili LN2 nakuendelea.

2. TERRIBLE TEENS NI NINI?
Terrible teens ni zile ndege za mwanzo kutengenezwa za Boeing 787-8. Hizi ndege zilikuwa 20. Kwahiyo hiyo ni Line number 1-20 (Kuwa makini hapa). Na hizi ndege zilifanyiwa majaribio mengi na matengenezo mengi mapya ili kupata ndege bora zaidi.

Kwa kifupi tunaweza sema zilikuwa sample ya kutengenezea ndege zingine. Kutokana na kufanyiwa modification za mara kwa mara hizi ndege zilipitiliza uzito uliotakiwa. Kutokana na kuongezeka uzito ndege hizi hata uwezo wake wa Masafa ukawa Umepungua kwa Maili 1000 au KM 1609.344

Kutokana na hili makampuni yaliotaka order za mwanzo kama All Nippon, Maroc etc. yaligoma kuchukua hizi ndege bali yalichukua ndege zilizotengenezwa baada ya zile 20 za mwanzo yaani Line number 21 na kuendelea.

Terrible teens zingine ziliwekwa kwenye majumba ya kumbukumbu na baadhi ya kampuni walizichukua. Zikabaki 12 uwanjani miaka mitano bila mnunuzi toka 2009 zilipoanza tengenezwa.

Kutokana na aibu iliyokuwa inaipata Boeing ya kukaa na mindege isiyo uzika. Ikaamua yafuatayo

(a) Kutafuta Wateja ambao hawatajali issues ya kikomo cha masafa ya ndege

(b) Kuziuza hizi ndege kwa bei rahisi ( karibu nusu bei kutoka $224M hadi $99M)

CONCLUSION
Kutoka katika websites ya Boeing na na web zingine za usafiri wa anga zimeweka wazi Ndege tulio iwekea order ni Boeing 787-8, serial number 35508, Line number 19.

Sasa kwa maelezo niliyotoa Line number 19 IPO ndani ya Line number 1-20. Kwa kifupi ndege tuliogiza ndio zile ndege za mwanzo 20 zilizopachikwa jina la Terrible Teens.

Swali lingine la kujiuliza kwanini tumeuziwa ndege iliyo doda ,iliyoshushwa bei hadi kufikia $99M kwa bei ya ndege mpya yaani $224.6M?

Bila kupepesa macho hapa tumepigwa $124M na ushee ambazo tungeweza nunua Boeing 737-800 Next Generation mpyaaaa ya 2016.

Kama nilivyokwisha sema Nina imani na Rais Magufuli ni mtu makini anayeipenda Tanzania. Na imani hili litatolewa maelekezo na kufanyiwa kazi.

Nimewawekea link na picha mbali mbali kusappoti uzi.

66cbe3973d2476f0afd0ef4b23f5d581.jpg


5ffe88270490cadedd65af84f1f2a940.jpg
32a59f2db3a1932ae85e9b8bfd8d26fd.jpg


Boeing 787 Register - Welcome

www.airliners.net/forum/viewtopic.php?t=1335649

www.airportspotting.com/boeing-finding-homes-terrible-teen-787s/

www.boeing.com/commercial/customers/air-tanzania/air-tanzania-787-order.page

Haya nakupa tu vionjo ili ujue serikali ipo makini na inachokifanya na jiaandae ukipenda utajumuika na Timu ya Wataalam watakaoenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa ndege yetu!
 

Attachments

Ninavyojua ndege hazitengenezwi kama magari kisha kutafutiwa mteja, utaratibu unatoa order kisha wanakutengenezea, hiyo uliyotengeneza kwa excel mtu yoyote anaweza kutengeneza.
Kama Rwandair waliinunua kwanini baada ya miezi miwili hawajaichukua ikarudishwa sokoni (kwa majibu ya draft ya excel yako) kwanini sisi tumeambiwa mpaka 2018 ndiyo itafika hapa?
Punguzeni chuki hazisaidii chochote acheni rais apige kazi kama mnachuki nae hamieni hata Burundi au Congo, akija siku yoyote akichukua madaraka mnaemtaka mtarudi, mtakufa kwa chuki zenu.

Boeing's most turbulent saga of the past decade is finally over

Soma vizuri Article hiyo kama wasiwasi wako ni kwa nini two years ndio delivery ifanywe. Boeing waliweka wazi hapo itachukua miaka miwili (tangu Juni 2016) kukamilisha mchakato wa kuwafikishia waliozinunua kwa ndege zote za terrible teens. Watanzania hampendi kuumiza akili lakini msingeshindwa kujua kwamba Boeng na Airbus kwa sasa wamezidiwa kutokana na order nyingi zilizotolewa na mashirika ya ndege. Hivyo ni kituko kuamini Tanzania ingeweza kupata Brand new in two years.
 
Hiyo clip ya Aljazira, hata wafanyakazi pamoja na Engineers waliotengeneza hii ndege wanaogopa kupanda. Yaani ukiitazama hii clip ina mambo ya ya ajabu sana kuhusu hii ndege na inatia mashaka.
 
Ushauri wangu ni huu tu
Si vibaya serikali kununua hiyo ndege lakini kwa bei ya soko kwa maaana around 100m na itakuwa vizuri kwa shirika la ndege kupata ndege kubwa kwa half price kwa shirika changa kama shirika letu la tz. Lakini kama watakua wamepiga hela kwa bei ya ndege mpya around 211m basi litakuwa ni boonge la scandal.

Peace Tz.
 
Hivi huyu cocochanel ni mtanzania kweli au mhamiaji tu. Maana uandishi wake wa Kiswahili unatia shaka.
 
Halafu ndege yenyewe ya masafa marefu ni moja, ikibuma ndio imebuma. Hawa watu wanawajua lakini wazungu au? Yaani aache kupata raha za dunia Emirates na Qatar akapande Air Tanzania????? Hizi pesa tungezitia kwenye kuboresha miundombinu ya kilimo na utalii tungepata much kuliko huko.
Usemayo ni kweli mkubwa
 
Hivi huyu cocochanel ni mtanzania kweli au mhamiaji tu. Maana uandishi wake wa Kiswahili unatia shaka.

Ha ha haaaaaa

Unasahau kuwa wengine akina mimi tulizaliwa tunaongea kilugha cha makabila yetu, na sasa tunajifunza kiswahili chenu.

Usijali mdau mimi mutanzania mnono haswa.
 
  • Thanks
Reactions: mij
Jamani tuacheni hizi maneno tutakosa ndege ,jamaa hachelewi ata wapa wajeda subirin!! =
 
Alinunua meli mbovu baada ya kusakamwa sana akaipeleka JW ili tusioji. Sasa kauziwa kituko kingine,sijui hiki atakipeleka wapi ili tusioji.
 
Wewe kweli halinzuli ulisikia wapi inaanza kwenye ndege kwanza kwa wananchi wako then uko lakini ndege upumba tu MTU tuna uana mitaan hali mbaya kweli iyo ni seri nzuri au upumbavu jitambueni kidogo mtakufa namtaani watu kam nyie tuna wala nyuma
 
Kweli kabisa. Tulisema tunanunua ndege tangu 2016. Ndege iliyoko tayari inasubiri miaka miwili kufika. Hapo ndio shida. Hapo bado inaonekana kama iko "on order". Wakati wa Q400 Bombardier walisema inachukua masaa matatu -Dar-Moshi. haikuwa hivyo.

Kwenye mikataba hakuna anaye disclose details. Kampuni ya Canada imeigomea Marekani kudisclose details. Itajulikana tumenunua bei gani tu haijifichi-si mkaguzi mkuu si yupo

Ila hizi kelele si jambo baya. Airline safety and security ni kitu sensitive sana. Kwenye hii industry hakuna nafasi ya kufanya makosa.

Niulize tu. Kwa hiyo na Japan wanayo hizo terrible teens; kulingana na mleta mada.
Hii comment yako hawataijibu watakuwa wanairuka tu kwa kuwa wakiijibu Nyumbu watawashutukia
 
wanasema hiyo ndege kama vile iko ghalani. kinachoshangaza kama ndege ipo kwa nini delivery iwe 2018 na sio sasa wakati serikali imesema hela zipo? nadhani serikali inafuatilia hizi taarifa za mitandaoni. tumeona hila za kila aina mitandaoni kuichafua awamu ya 5.
hizi taarifa kama zina ukweli serikali kuingizwa mjini bado ipo nafasi kurekebisha makosa ila natia shaka kwani wanaoshikia bango ndio wale walisema bombadier ni mitumba.
Kwani Bombadia ni mpya? Ndege gani mpya zinafunguka milango angani? Au kwanini haziashirii uko wazi kabla haijapaa?

Hiyo boingi wamepigwa kwenye bei au wametudanganya bei halisi. Boingi wenyewe walishazishusha bei. Imekuaje Magu kanunua kwa bei ya hizi za sasa zisizo na mawaa ya za mwanzo?
 
Back
Top Bottom