Hakuna dini ambayo haijawahi kupingwa na wenyeji wake.
Kuanzia Uyahudi, Ibrahim alipingwa na Jamii yake ndio akakimbia kutoka Ukaldayo mpaka Canaan(Palestine)
Ukristo ulipingwa na Warumi mpaka mfalme wa Kirumi constanino aliposilimu na kuingiza mila za Kirumi kwenye Ukristo ndio ukawa ukristo unaouoma hivi leo.
Muhamad alipingwa na Makuresh nusura wamuue lakini baadaye uislamu ukàkubalika hapo mashariki ya kati.
Dini kwa zamani ilikuwa inahusisha siasa na utawala.
Uislamu ungetumika kuunganisha jamii zote za mashariki ya kati ikiwemo Waarabu kwa sababu ndio imebeba utambulisho wa jamii hizo.
Ndio maana nikakuambia bila kutawaliwa (ukoloni) hizo dini ni tamaduni za jamii zingine. Hazina uhusiano na mila, desturi, tamaduni na miungu ya waafrika.
Kila jamii ina dini yake.