Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 35,826
- 47,147
Ukristo wa huko Marekani umechukua mkondo wa siasa za Kiliberali.Ingawa wakristu wanajieneza kwa kupinga sana uislamu, ni wazi kwa nini uislamu umekuwa unasambaa sana Marekani siku za hivi karibuni huku ukiristo ukisinyaa.
Mim ni nilikuwa nasali kanisa la kikatoliki kwa muda mrefu sana kwani ndilo nililoona lilikuwa karibu na nyumbani kwani na ibada zake zianendeshwa kama zile za Kiluteri nilikotokea. Isipokuwa niliacha tena kwenda kanisani kwani kila mara sehemu kubwa ya mahubiri yao ni kuhimiza watu kuchagua republican tu.
Baada ya kuhudhuria kwa muda mrefu kanisa hilo, niliggundua kuwa hata mapadri walikuwa na ubaguzi fulani dhidi ya watu weusi. Sasa ukienda kwenye hao Evangelicals, ndiko utakuta wanalofahamu ni kuwa Marekani ni nchi ya weupe tu, wengine wote ni haramu.
Jana nimekutana na website hii ndipo nikagundua kweli imani yangu kuhusu ukristo kukosa mweleko ni ya kweli kabisa.
![]()
God Bless The USA - Official Store
Welcome to the official God Bless The USA store. GodBlessTheUSA.com is proudly endorsed by Lee Greenwood and is your home for all things America.godblesstheusabible.com
Haishangazi hata kuona namna hao Engavelicals wanavyosapoti Vita vya Israel huko Gaza kwa kisingizio cha kiimani bila kutambua hata Wapalestina Wakristo wanateseka sana na hiyo Vita.
Hayo ni matokeo ya mapokeo ya kidini ya kibinadamu , ila ' Ukristo ' kwa mujibu wa Biblia haupo hivyo.
zitto junior Mathanzua
DR Mambo Jambo