Ukomo wa Urais Kikatiba na usawa wa wagombea, napendekeza Katiba itamke ukomo wa Urais pale tunapoingia katika kampeni

Konseli Mkuu Andrew

JF-Expert Member
May 10, 2013
740
855
Salaam Wakuu.

Napenda kushare nanyi wakuu wa jukwaa hili kuhusu Ibara moja wapo ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanania ya mwaka 1977.

Ukisoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 42(3)(a) inasomeka hivi-

(3) Mtu aliyechaguliwa kuwa Rais atashika kiti cha Rais hadi-
(a)siku ambapo mtu atakayemfuatia katika kushika kiti hicho atakula kiapo cha Rais; au.

Hii maana yake ni kuwa wakati huu wa kampeniza Uchaguzi mkuu bado Mgombea wa Urais kupitia CCM bado ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivo anapoenda kwenye kampeni anakuwa na makoti mawili anaenda kama mgombea hapo hapo anaenda kama Rais wa Jamhuri na ata ulinzi wake unakuwa vivyo hivy ambapo ni tofauti na wagombea wengine na tulisoma kwenye somo la uraia kuwa kiashiria kimoja wapo cha uchaguzi wa huru na haki ni usawa kwa wagombea.

Ninapendekeza kufanyiwa marekebisho katika ibara hiyo ya 42(3)(a) na itamke kuwa Ukomo wa Urais ni pale tunapoingia katika kampeni na madaraka ya Rais yata kaimiwa na Jaji Mkuu au mtu mwingine ambae ataonekana kufaa.

Wapinzani mlishindwa kweli kuliona ili? halihitaji tume huru..
 
Mnapenda kujizonga tu... Watetezi wa mfumo wa demokrasia ikifika kampeni rais anaendelea kuwa rais tu.

USA sasa ivi wanapiga kampeni na rais wao ni Trump
 
Hivi kuna Nchi yoyote duniani yenye utaratibu huu unaopendekezwa?

Hata kwa wale wanaodaiwa kuwa vinara wa demokrasia, Trump mpaka sasa kavaa koti la Urais huku akipiga kampeni za kuchaguliwa tena
 
unajua hasara na faida za kaimu Rais?
Hata marekani hawafuati mapendekezo yako
Hao wapinzani walipewa fursa ya kubadili katiba wakaichezea,badala ya kutunga sheria wakawa wanashindana kujionesha nani mkali wa sheria
 
Wapinzani wanaangalia ulaji tu, vitu vya msingi kama hivi viko visogoni.
 
Mnapenda kujizonga tu... Watetezi wa mfumo wa demokrasia ikifika kampeni rais anaendelea kuwa rais tu.

USA sasa ivi wanapiga kampeni na rais wao ni Trump
Tanzania sio Marekani chief, ndio maana kule mifumo ya kumpata Rais ni tofauti na huku
 
unajua hasara na faida za kaimu Rais?
Hata marekani hawafuati mapendekezo yako
Hao wapinzani walipewa fursa ya kubadili katiba wakaichezea,badala ya kutunga sheria wakawa wanashindana kujionesha nani mkali wa sheria
Nalo ni tatizo asee
 
Hivi kuna Nchi yoyote duniani yenye utaratibu huu unaopendekezwa?

Hata kwa wale wanaodaiwa kuwa vinara wa demokrasia, Trump mpaka sasa kavaa koti la Urais huku akipiga kampeni za kuchaguliwa tena
Tusiige mifumo ya utawala ya Afrika na hizo nchi mkuu.Tutengeneze yetu Ila tuwe mifano ya kuigwa
 
Mnapenda kujizonga tu... Watetezi wa mfumo wa demokrasia ikifika kampeni rais anaendelea kuwa rais tu.

USA sasa ivi wanapiga kampeni na rais wao ni Trump
USA ni USA mkuu na Tanzania ni Tanzania hiivyo kujilinganisha na hao ni kudumaza akili zetu ni sawa na kusuburi mzungu afumbue teknolojia alafu wewe uigilize.
 
kuigiza teknoloji ya mtu ni jambo jema, ndani yake unajifunza.

Anyways, naunganisha na reply yako nyengine ulosema kuwa Tanzania sio USA. Kumbuka, system ya governance iliopo haipo Tanzania. Watanzania tulikuwa na ma chief na sio rais.
 
Okay ila haya yalikuwa ni maoni yangu binafsi
 
Salaam Wakuu.

Napenda kushare nanyi wakuu wa jukwaa hili kuhusu Ibara moja wapo ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanania ya mwaka 1977.

Ukisoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 42(3)(a) inasomeka hivi-

(3) Mtu aliyechaguliwa kuwa Rais atashika kiti cha Rais hadi-
(a)siku ambapo mtu atakayemfuatia katika kushika kiti hicho atakula kiapo cha Rais; au.

Hii maana yake ni kuwa wakati huu wa kampeniza Uchaguzi mkuu bado Mgombea wa Urais kupitia CCM bado ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivo anapoenda kwenye kampeni anakuwa na makoti mawili anaenda kama mgombea hapo hapo anaenda kama Rais wa Jamhuri na ata ulinzi wake unakuwa vivyo hivy ambapo ni tofauti na wagombea wengine na tulisoma kwenye somo la uraia kuwa kiashiria kimoja wapo cha uchaguzi wa huru na haki ni usawa kwa wagombea.

Ninapendekeza kufanyiwa marekebisho katika ibara hiyo ya 42(3)(a) na itamke kuwa Ukomo wa Urais ni pale tunapoingia katika kampeni na madaraka ya Rais yata kaimiwa na Jaji Mkuu au mtu mwingine ambae ataonekana kufaa.

Wapinzani mlishindwa kweli kuliona ili? halihitaji tume huru..
Sure 💯
 
Back
Top Bottom