Ukiweka milioni 200 kwenye fixed deposit unapata mrejesho wa 1.5m kwa mwezi

Ndio maana nikasema kama kuishi kwa kujibana basi hata laki moja kwa mwezi inatosha kuendesha familia ila ukitaka kuishi kistandard hata 1.5m hamna kitu ndio ilikuwa logic yangu.
Sasa Mkuu kuishi ki standard kilamtu anapata hiyo nafasi maana wote tungepata hiyo nafasi 1.5M tungefanyia Shopping Mlimani kwa siku tu ila 90% hawafikii standard ndio maana 1.5 itabaki kuwa nyingi..
 
Option nyingine ni kuwekeza kwenye real estate. Ukipata kiwanja location inayoeleweka unaweka. Kwa milioni 200 unasimamisha apartments za kueleweka. Hata kwa US$500 kwa mwezi kama ziko 20 utaiona faida.
Sehem inayoeleweka yenye kupangishika ya kuweka hzo apartments kadhaa huwez pata kwa mtaj huo wa 200m.....sehem inayoeleweka square metres price znaanzia Tsh 30,000...kwa maana kiwanja cha sqm 1000 ni 30m...sasa kwa apartments utaweka ngap?...kiwanja tu hyo hela unaikata nusu nzima..kama unataka kiwanja kikubwa.
 
Sure Mkuu 1.5m kwa mwezi labda uwe unaishi kisela,waulize wanaolipwa labda mili 3 au nne kwa mwezi....Kama kipato chako ni laki 3 au nne kwa mwezi utaona 1.5m ni nyingi sana.

-Kodi ya nyumba
-Ada ya watoto efemu akademia
-Chakula
-Utilities bills
-Transport/Usafiri
-Support kwa extended family.
-Vocha/Bundles

Kama kuishi kwa kujibana basi hata laki kwa mwezi inatosha kwa matumizi maana utakuwa unakunywa uji na usiku ugali na tembele chukuchuku,watoto wanasoma kayumba.
Porojo
 
Usicheze na hii kitu, jaribu kufatilia hatma ya walioweka hela yao Bank M ndo utajua.

Ilipita memorandum ya BOT kwamba depositors wote wapewe maximum TZS 1,500,000, balance inayobaki mtalipwa on preferential basis.

Ikitokea kwenye preference ukawa wa mwisho maana yake unategemea kitakachobaki.

Mpaka leo kuna watu kibao hawajalipwa. Na hiyo ni practice kwa mabenki yote yaliyochukuliwa na BOT kwa sababu za kufirisika.

Ogopa sana unapoona benki inatoa rates kubwa, hapo wanakutwa wanalazimisha liquidity.
Duh kumbe hawa akina FINCA na Yetu Bank siyo wa kuwakimbilia aisee
 
Wewe nyumba zetu za kishkaji unapata nne hapo
Sio nne...mi ukinipa 32m nakutolea kitu hcho huwez amin...tena cha vyumba vi3...ila ustake mbwembwe sjui tiles kubwa zile mara bat migongo mipana mara utake weather guard rang za gharama ndoo 130k..hapana.kawaida tu.raman open kitchen tena...yaan wabongo wanatishanaga kwenye ujenz had mtu unasema hiv hawa wanajengaje...kwahyo hyo 200m nakutolea nyumba 6 na inabak chenji hapo 20m ya kiwanja..ila sasa kiwanja hko cha 20m kukipata labda uende kigambon mbele ya dege project kule porin.au uende misugusugu huko au kivule mbele hukoooo mbwinde.hahaha
 
Tatizo ni benki ikifilisika hutaipata fedha yako.

Ukitaka kuiweka fedha yako kwa usalama, iwekeze serikalini. Nunua treasury bond au bill. Kwa kufanya hivyo fedha yako inakuwa safe. Labda tu nchi ibadilike iwe kama Somalia.

Apa uwa sielew bank ikifilisika sipat pesa yangu ?? Kwa iyo bank uwa haina bond bank kuu?
 
Apa uwa sielew bank ikifilisika sipat pesa yangu ?? Kwa iyo bank uwa haina bond bank kuu?
Na paste kutokana na andiko la Ndeyanka Mushi nililolitoa mtandaon


BOToverview.jpg

Majengo Pacha ya Benki Kuu ya Tanzania, Wizara ya Fedha na Mipango (Hazina), Dar es Salaam
Benki ni sehemu salama zaidi ya kutunza fedha zako. Hata hivyo zipo nyakati ambazo benki hufilisika. Benki inapofilisika, fedha zako kuna uwezekano mkubwa kwamba ziko salama. Nchini Tanzania benki na taasisi zote za fedha zinatakiwa kisheria chini ya Benki Kuu ya Tanzania, kuwa wanachama wa Bodi ya Bima za Amana (Deposit Insurance Board), kwa hiyo kwa kuwa benki na taasisi zote za fedha lazima kisheria ziwe wanachama wa bodi hii, benki au taasisi inapofeli basi huna haja ya kupata wasiwasi.

Benki hufeli na kufilisika pale zinaposhindwa kutimiza majukumu yake ya kibenki. Mfano wakati Benki Kuu ya Tanzania ilipotangaza kuzifuta baadhi ya benki mapema mwezi Januari 2018 kama Efatha, iliweka bayana kwamba benki hizi zimeshindwa, pamoja na mambo mengine, kulipa madeni yake na kuishiwa na mtaji.

Benki haziweki fedha zako katika sefu, bali inazifanyia biashara kupitia uwekezaji kwa riba. Benki zinaweza kupoteza fedha nyingi kupitia uwekezaji, au zinaweza kushindwa kukupa fedha pale unapokwenda benki kutoa. Kadiri benki zinavyopata hasara katika ukopeshaji wake ndiyo uwezekano wa kufilisika unavyoongezeka.

Nani analinda fedha zako iwapo benki inafilisika?
Benki Kuu ya Tanzania kwa niaba ya serikali, ina jukumu la kulinda fedha za wateja iwapo benki inaingia matatizoni. Sheria ya Fedha ya mwaka 2006 imeipa jukumu Benki Kuu ya Tanzania kuwa na Bodi ya Bima ya Amana ambayo ndiyo yenye jukumu hilo.
Katika hili, majukumu ya bodi hiyo katika fedha iliyopo benki ni:

a) Kufanya malipo ya shilingi 1,500,000 baada ya kutoa madeni ambayo mteja anadaiwa na benki au taasisi ya kifedha iliyofilisika. Awali kiwangi hiki kilikuwa shilingi 500,000.

b) Kupokea malalamiko. Inapotokea benki ikafilisika mteja anapaswa kupeleka lalamiko katika bodi hii kabla ya kulipwa.
c) Kuitisha na kuhakiki vielelezo. Kabla ya kulipwa, mteja anapaswa kuwa na vielelezo vyote ambavyo bodi itahitaji ili kujiridhisha ustahiki wake wa malipo husika.

Soma zaidi kuhusu Bodi hiyo ya Benki Kuu katika tovuti ya BoT hapa.
Ziada:
Ukiwa na fedha nyingi zaidi ya shilingi milioni 1.5, unapewa kwanza malipo ya awali ya shilingi milioni 1.5, kisha unasubiri malipo mengine baada ya hatua ya “Liquidation”. Hatua hii hufanyika kwa kufuata makundi, wanaanza kulipwa wenye ubia wa mtaji wa benki na makundi mengine ambayo yanaidai benki. Mfano benki itapiga mnada majengo yake, vitu vya thamani na kadhalika na kulipa wanaoidai, ikiwemo wewe mteja mwenye fedha ya ziada. Zoezi zote hili wakati huo linakuwa chini ya serikali.

Kwenye utaratibu wa kulipa madeni, wateja wenye amana kama wewe huwa ni wa awali kabisa, wenye ubia benki (shares) huwa ni wa mwisho, na kama ni hasara wabia hugawana hiyo hasara kama ambavyo hugawana faida.

Jambo muhimu zaidi ni wateja kusoma taarifa za fedha za benki zao kila kota, kwani ni jukumu lao ili kufahamu mwenendo wa benki mara kwa mara.
Ndeyanka Mushi
Follow me on Twitter & DM.
 
Back
Top Bottom