Ukiwa Tanga usiwe na haraka

Ukiwa Tanga usiwe na haraka

massage ya kiswahili wenyewe wanaita kusinga, hahahahaha Tanga kuna raha zake bwana kwa tunaopenda burudani....kilago chawekwa chini wenyewe waita kijamvi kidume unalazwa hahahahahaha lazima usahau kufa...me simo muoe vijana..
so kabila gani wanajua mapenzi hapo tanga?
 
Chief
Mimi nimezaliwa Tanga na kuishi mpaka utu uzima wangu huu
Sijawahi ona sifa hii au kusikia katika Mji wetu
Si mjini wala vijijini

Bali
Naona kwenye mitandao watu wakisema kwa wingi na kutoa sifa chafu hizi kwa wazawa wa Tanga

ila nilichojua, ni jambo moja tu
Wengi wenu, huwa mnajijua na kufahamiana katika upuuzi huu
Unataka kubisha kuwa Tanga hakuna mambo kibao ya Uswazi?
Ebu sema, maduka mengi huwa yanafunguliwa saa ngapi asubuhi?
 
Hili Jambo linanishangaza Sana, maana mtu utakuta sio mzawa wa Tanga Wala hajawahi kufika ila vile amesikia habari za huko basi atazieneza na kutia chumvi zake nyingine nyingi.

Mimi ni mzawa wa Tanga na nimekulia Tanga, Mambo mengine kuhusu Tanga tunayashangaa yanavyovuma mno aisee maana ni tofauti kabisa na uhalisia.

Lakini kiukweli Tanga ni sehemu moja nzuri tulivu na isiyo na tafrani za kubughudhi, na kwa maendeleo watu wanapambana, swala la kupiga kazi watu wanapiga na ndio maana maisha yanaendelea na watu wanakula bata tena Bata mzinga sababu wanakidhi mahitaji yao.
Nimewahi kuishi Tanga miaka ya nyuma.
Haya mambo yaliyoandikwa hapa jukwaani yapo japo mengine machache yameongezewa chumvi kidogo.
Ushirikina, uvivu, uswahili swahili haya mambo yapo.
Nimeishi Nguvumali, ilikuwa ni kawaida kukuta mtu kapasua vifuu vya nazi na mayai viza katikati ya mji hasa pale kwenye mataa - Mwembe mawazo!
 
Nimewahi kuishi Tanga miaka ya nyuma.
Haya mambo yaliyoandikwa hapa jukwaani yapo japo mengine machache yameongezewa chumvi kidogo.
Ushirikina, uvivu, uswahili swahili haya mambo yapo.
Nimeishi Nguvumali, ilikuwa ni kawaida kukuta mtu kapasua vifuu vya nazi na mayai viza katikati ya mji hasa pale kwenye mataa - Mwembe mawazo!
Umesema vyema kua ni miaka ya nyuma, nafikir jaribu kutembelea Tanga Tena........swala la kupasua na Nazi na mayai sio Tanga tu mkuu tembea uone!
 
kiongozi unaweza kubaliana na mimi kwamba Wewe mwenyew huwezi jiona una tatizo mpaka aje mwingine ndo atajua una tatizo.Wewe kukulia tanga mambo unayaona ya kawaida tu akija mgeni ataona kuna tofauti kubwa..Ndo ilivyo hii maada!! Siku zote huwezi kuona Boriti lililopo katika jicho lako mwenyew Ila unaona kibanzi kilichopo kwenye jicho la nduguyo, Maana yake huwezi kuona matatizo yako mwenyew ila ya mwingine ni rahis kuyaona.
Sure!
 
Nilitunukiwa “ustaarabu wa Tanga” nikajikuta naongeza siku za kukaa Tanga japo shughuli iliyonileta niliishaimaliza. Tanga nitarudi aisee
 
Back
Top Bottom