Ukiwa maskini sana hata mbwa wako anaweza kukung'ata!!

Mganguzi

JF-Expert Member
Aug 3, 2022
1,032
2,769
Umaskini ni tafsida !

Unaweza kuitumia kwa ujumla au kwa mtu Mmoja Mmoja ! Tukiwa kama nchi mbele ya mataifa mengine nchi yetu inaitwa maskini.

Hata viongozi wetu wengi wanapotoa hotuba zao mbele ya mataifa yaliyoendelea wanajitambulisha kama nchi maskini ' ukisema hivyo unajumlisha wote ,sisi na ardhi yote ya jamhuri ya muuungano inakuwa maskini ,humo ndani Kuna akina wao na akina sisi, wote tunaitwa maskini ,anaekaa ikulu mpaka Bakhresa na matajiri wote mbele ya mataifa yaliyoendelea nchi yetu inaitwa maskini! Pamoja na mbuga na madini ,vivutio vya utalii ,maziwa na bahari vyote vinaitwa maskini.

Mwenye mbwa ni maskini na mbwa pia ni maskini .si ajabu kuona mbwa anabweka Kila dakika haachi kupiga kelele ,kuna wakati harufu ya minofu kutoka kwa nyumba ya tajiri inamfanya mbwa wako akuchukie na akuone mzembe sana!

Mbwa anaelazimishwa kula mifupa ya ng'ombe aliyekufa miaka minne iliyopita hawezi kutulia muda wote atapiga kelele na kutoa povu mdomoni, siku mbwa atakapo choka kabisa atakung'ata hata wewe mwenyewe uliyemfuga

Usichukie mbwa anapopiga kelele tafuta ufumbuzi ni kwa Nini anapiga kelele ! Kama nchi awamu hii kipindi hiki Cha utawala huu kelele zinazohusu ufisadi zimekuwa nyingi sana. Watawala msitufungie mabandani mkapuuza kelele zetu. Kumbukeni hata mbwa huhisi njaa!
 
Yaani kuna watu kiswahili cha tafsida bado hawakifahamu na wanaforce waandike maneno yenye tafsida.
Mara UKIWA MASKINI SANA MBWA WAKO ANAKUNG’ATA.
(Hii haina ukweli wowote)

Mbwa anaelazimishwa kula mifupa ya ng'ombe aliyekufa miaka minne iliyopita hawezi kutulia muda wote atapiga kelele na kutoa povu mdomoni, siku mbwa atakapo choka kabisa atakung'ata hata wewe mwenyewe uliyemfuga

Nini kimeandikwa hapa?.
Yaani hamna mashiko kabisa na swala la mbwa . Miaka minne mifupa inatoaje harufu mpaka mbwa atoke mate. Labda awe chizi.
Ungetumia mifano mingine au kwenda direct kwenye point. Kutumia Mbwa kupersonalize story yako. Umekua kama unaandika huku unakimbia.
Rekebisha thread boss
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom