Paul Makonda: Usimbeze mtu maana kesho anaweza kuwa Bosi wako

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,343
9,770
Ndugu zangu Watanzania,

Mheshimiwa Paul Makonda Mwamba na katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa ameendelea kuwa mfano wa kuigwa na kuwa kiongozi anayeteka hisia za watu wengi sana pamoja na mijadala mingi sana hapa nchini kila afunguapo kinywa chake kuzungumza maneno. kutokana na kuzungumza kwake kwa hekima, busara ,staha na maneno yenye mafunzo makubwa sana ndani yake.

Sasa leo tena katika muendelezo huo huo wa kuzungumza kinabii na kuwa mbele ya muda kimaono na kimawazo amezungumza juu ya kuheshimiana, kupendana,uvumilivu,subira wakati unapokuwa huna uongozi na unapokuwa kiongozi katika nafasi fulani.

Amesema unapokuwa kiongozi hupaswi kuwadharau wale ambao hawana uongozi au hawapo uongozini maana hujuwi kesho itakuwaje maana huyu unayemuona leo siyo kitu na ukamdharau , kesho anaweza kuwa ndio Bossi wako. Akizungumza kwa uchungu na hisia kali sana zilizogusa waandishi wa habari na kusambaa kwa kasi ya mwanga katika mitandao mbalimbali ya kijamii maneno hayo yameonekana kugusa hisia za wengi na kuungwa mkono na wengi sana.

Wengi wakisema kuwa Mh Paul Makonda yupo sahihi maana uongozi ni dhamana. Mheshimiwa Makonda amejitolea mfano yeye mwenyewe kuwa nani alitegemea kuwa atakuwa na kukalia kiti alichopo kwa sasa? Wengi wameonekana kuguswa sana na kauli hiyo na mfano huo na kuonyesha kupata somo lililowakaa akilini mwao na kuelewa kuwa inahitaji upendo kuishi na watu na kumheshimu kila mtu hata kama hana cheo chochote kile maana aijuaye kesho ya mtu ni Mungu Pekee.

Mheshimiwa Makonda amezungumza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya ziara ya Mheshimiwa Rais na mwenyekiti wa CCM Taifa Mh Dkt Mama Samia Suluhu Hasssan atakayoifanya unguja katika mikoa minne ndani ya siku mbili Tarehe 17-18 januari 2024.

Nami Mwashambwa namuunga mkono na kuiunga mkono kauli ya Mheshimiwa Paul Makonda kuwa Mheshimu kila mtu,usimdharau mtu kwa maisha aliyo nayo leo maana hujuwi kesho yake itakuwaje .Mungu humuinua mtu yeyote yule bila kujali historia yake. Hii ndio maana Mungu alimuinua Daudi aliyekuwa anachunga kondoo porini na kumpa ufalme na kuwaacha watu kama akina Eliabu. Hii ndio maana Mungu aliwainua watu kama akina yefta.

Kikubwa ni kuwa mnyenyekevu na mwenye upendo na tabia njema kwa watu wote.waheshimu watu wote maana Mungu hupitishia baraka zake kupitia watu,huinua watu kupitia watu.tabia yako mbaya inaweza kuchelewesha baraka zako hasa pale kila mtu atakapokuwa anasita kuweka mkono wake na baraka zake juu yako kwa kibuli chako,dharau zako, ujivuni wako na manyanyaso yako kwa watu.

Lakini pia ukiwa sehemu usitake kuwazimia taa watu .penda kuwawashia taa watu ya kusonga mbele maana hujuwi ni nani atakaye kuja kukushika mkono mbele ya safari utakapokuwa umeanguka na unahitaji msaada wa kushikwa mkono na kuinuliwa .usifurahie anguko la mtu wala maumivu ya mtu .furahi unapoona kupitia wewe wengi wameinuka na kusonga mbele na kila wakikupigia simu waseme Mungu Akubariki sana na kukujalia maisha marefu yenye heri na baraka tele hapa Duniani.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Anajisema mwenyewe enzi zile za chongola makonda anamwambia awe na adabu...
Mheshimiwa Makonda ni mtu mnyenyekevu na mwenye huruma sana na ndio maana ulikuwa ukiona namna alivyokuwa akisaidia watu mbalimbali, wakiwemo wajane, yatima, watu wenye ulemavu,wagonjwa n.k. lakini pia kutofautiana katika uongozi ni jambo la kawaida.kikubwa mnatofatiana katika mambo ya msingi na juu ya njia za utekelezaji wa jambo fulani .na siyo masuala ya visasi na chuki binafsi .

Ndio maana kwa moyo wake huo wa upendo, unyenyekevu,subira,utulivu na uvumilivu tumeona na Taifa zima limeshuhudia Mheshimiwa Makonda akiinuka na kuinuliwa tena mbele ya macho ya maadui zake waliokuwa wamefurahi na wamemtangazia mwisho wa kisiasa lakini Mungu wa Mbinguni aliye hai akautangaza Mwanzo wenye kishindo kama cha wakoma waliolikimbiza jeshi la maadui.
 
Uungwana siku hizi ni kutomwambia kiongozi ukweli?
Akikosea mfano akaiba umwambia umehamisha bahati mbaya?
Afrika tuna unafiki mwingi sana.
Wanafiki ni wapinzani kama CHADEMA ambao wao kila kitu ni kibaya na kwa wao kwa akili zao na upeo wao kwamba hakuna kitu chochote kile cha maana kilichofanyika tangia tupate uhuru katika Taifa letu, jambo ambalo ni la uongo mkubwa sana maana kila mtu na mtanzania anaona namna maendeleo makubwa yalivyopatikana tangia tumepata uhuru kutoka kwa wakoloni.
 
Mheshimiwa Makonda ni mtu mnyenyekevu na mwenye huruma sana na ndio maana ulikuwa ukiona namna alivyokuwa akisaidia watu mbalimbali, wakiwemo wajane, yatima..
Mimi nimesema hivi,

Alikuwa anajisema mwenyewe alivyomwambia chongolo kipiñdi kile awe na adabu pasipo kujua anaweza kuwa bosi wake siku moja hata kwa mwezi mmoja.

Risala yote haikuwa na haja labda kama unapinga kuwa hakuwahi mwambia awe na adabu..
 
Akina Mheshimiwa Mbowe wanajishusha wenyewe kwa matendo yao na kauli zao zilizokosa uungwana.
Lucas...hao waheshimiwa sikuhizi hawahangaiki na mitandao ya kijamii, huku wala hawatembelei.
Mambo yao safi.
Nakushauri nenda kwenye ofisi zao moja kwa moja, huku wamejaa chawa tu.
 
Lucas...hao waheshimiwa sikuhizi hawahangaiki na mitandao ya kijamii, huku wala hawatembelei.
Mambo yao safi.
Nakushauri nenda kwenye ofisi zao moja kwa moja, huku wamejaa chawa tu.
Niende kwenye ofisi zao kufanya nini na kutafuta nini.
 
Hata kama uchawa jamani ila kwa Bashite umezidi khaaaa. Yaani kwa kutuonaje yaani. Kwamba sisi woooooote hatuna macho ila wewe tu ndio unaona mambo kisha utusimulie?
Wewe kama una chuki binafsi basi kaa nayo tu kifuani pako mpaka upasuke mwenyewe. Chuki na uzushi pasipo ushahidi ni ubabaishaji na porojo tu kama ilivyo kwa porojo na blaa blaa zingine.
 
Back
Top Bottom