Kukopesha bila kuwa na leseni adhabu faini milioni 20, jela miaka miwili

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imepiga marufuku kwa taasisi, kampuni na watu binafsi kufanya biashara ya kukopesha fedha bila kuwa na leseni ya BoT au taasisi zilizokasimishwa majukumu hayo.

Wasiotii sheria inayowataka kuwa na leseni watakabiliwa na kifungo jela kisichozidi miaka miwili au kulipa faini.
Imesema ni makosa kisheria kujihusisha na biashara ndogo ya huduma za fedha bila kuwa na leseni ya benki hiyo au taasisi zilizokasimishwa majukumu hayo.

Kupitia taarifa yake kwa umma, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba alisema benki hiyo imebaini kuwepo kwa baadhi ya taasisi, kampuni na watu binafsi kujihusisha na biashara ya kutoa mikopo bila kuwa na leseni.

Alisema jambo hilo ni kinyume na Kifungu cha 16(1) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018.
Tutuba alisema taasisi, kampuni na mtu binafsi wa-sio na leseni hawaruhusiwi kufanya biashara ya kukopesha.
"Kutokana na kifungu cha 16(2)(a) cha Sheria ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2018, hatua zitakazochukuliwa kwa ukiukaji wa sheria hivo ni pamoja na faini isiyopungua shilingi milioni 20 au kifungo cha muda usiopungua miaka miwili," alisema.

Kutokana na hilo, alisema wanawakumbusha watoa huduma ndogo za fedha waliokwishapata leseni kuzingatia sheria, kanuni na miongozo inayotolewa na BoT ikiwemo kuwapa wakopaji mikataba, kuonesha riba ya mkopo kama ilivyopitishwa kwenye sera ya mkopo, gharama nyingine zote wanazotoza na riba kukokotolewa kwa mwezi na sio kwa siku.

Tutuba alibainisha kuwa orodha ya taasisi, kampuni na watu binafsi wenye leseni za biashara ya kukopesha zilizotolewa na BoT inapatikana kwenye tovuti ya benki hiyo ambayo www.bot.go.tz na kwenye matawi yake yote.

Screenshot 2023-06-23 at 14.15.34.png
 
Kausha damu ni noma. Marejesho ni kila siku. Ukichelewa, unachimbwa mkwara wa kufa mtu. Cha kushangaza kuna wadau wengine wanatoa mikopo kwa wanawake tu.
 
Yaani mtu anifate kuniomba nimkopeshe nimwambie hapana sina leseni
 
Back
Top Bottom