Kilimanjaro: Aliyekuwa Mhasibu Mapato Same afungwa jela Miaka 20 kwa Ubadhirifu

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,618
Machi 19, 2024 shauri la uhujumu uchumi Na 23/2022 dhidi ya PAULO NGILORITI TEVELI limeamriwa katika Mahakama ya Wilaya ya Same, mbele ya Mhe Hellen Hozza, likiendeshwa na wakili Suzan Kimaro.

Mshtakiwa ambaye alikuwa Mhasibu wa Mapato wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, ametiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 jela bila faini.

Mshtakiwa alikuwa akikabiliwa na makosa mawili:- matumizi mabaya ya mamlaka chini ya kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329 na kosa la ufujaji na ubadhirifu wa shilingi 8,377,000 / ambazo zilikusanywa na watumishi 3 wa Hospitali ya Wilaya ya Same. Fedha hizi ni za makusanyo ya kila siku kutoka kwa wagonjwa ambazo hakuzipeleka benki kwa kipindi cha Mwaka 2020.

Pamoja na adhabu hiyo mshatakiwa ametakiwa kurejesha fedha alizofanyia ubadhirifu ambazo ni mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Same .

Chanzo: TAKUKURU
 
Tunaelekea uchaguzi.
Hawa small fish lazima washushiwe majabali mazito kama mfano.

Wale wanaotrend kwenye ripoti za CAG ndo wanaotoa maelekezo kwa hizi junior courts how to deal na hawa samaki wachanga
 
HAwa wa vihela vidogo ndio wanafungwa ule mtandao aliyoutaja waziri mkuu mbona hatusikii tena au wamesanehewa???
 
Hii nchi ngumu sana nikikumbuka yule mzee balozi aliyekula pesa za ujenzi wa ubalozi kule nchi Gani sijui alifikishwa MAHAKAMANI akafungwa miaka miwili alipotoka akapewa ujumbe katika bunge la katiba
 
Yaani nigungwe miaka 20 na Bado nilipe SI Bora tu waongeze miaka ntakuwa nshapata uzoefu gerezani
 
Tunaelekea uchaguzi.
Hawa small fish lazima washushiwe majabali mazito kama mfano.

Wale wanaotrend kwenye ripoti za CAG ndo wanaotoa maelekezo kwa hizi junior courts how to deal na hawa samaki wachanga
Kidogo kidogo ndo baadae unashangaa ripoti inasema wizara ya afya kuna fedha bilion kadhaa hazijulikani zilipo.

Ila uhasibu ni kazi mbaya mno. Unaweza kuta yeye ni mbuzi wa kafara sababu makaratasi yote yalimpitia na yeye ndo muandaa ripoti.
 
Duh mln 8 na usheh kala miaka 20

Tz ukipiga kuanzia mabilion hufungwi

Ova
Huwa nawaambia watu kama wameamua kuwa wezi basi waachane na ishu za kuiba hizi fedha za karanga. Angekuwa ana kesi ya 500m au bilioni hukumu ingekuwa kumalizana na DPP kisha kulipa kama 50m fidia. Hawa juniors wawe makini sana. Wengi wameishia jela.
 
wanahangaika na vidagaa wakati kina mwigulu wanamiliki mabasi zaidi ya 500 na wanaendelea kukwiba tu na mama yao wala hashituki wala haambiliki anavuta shungi tu, kimsingi nchi yenu ngumu sana hivyo.
 
Hivi Takukuru ilianzishwa ishughulike na WALA RUSHWA au WEZI??!! Mbona kesi zao nyingi ni za wezi wa mali ya umma, wizi unaoitwa ubadhirifu! Kazi nzuri ila sidhani kama ni malengo ya kuanzisha chombo hiki, wezi wa kalamu au wa bunduki washughulikiwe na polisi.
 
Back
Top Bottom