Ukisikia neno siri unaelewa nini?

Ukisikia neno siri unaelewa nini?

😄 mimi mshangazi hapana bwashee , kuna mshangazi wa kizungu unayo pesa za kutisha ulidai umenielewa nikauonya ila akaniomba nimtafitie kijana wa nchi yangu , upo tayari niupe namba zako bwashee?
Mpe nipo tayari..
Hili jambo sifanyi kama ni mazoea hapana ila ni kipawa na kipaji ambacho Mungu amenipa hivo mpe nipo tayari kumkamia mpaka anipw uraia wa marekani
 
Mungu wangu😂🙌
 
SIRI🤐

Ukisikia neno siri unaelewa nini?

Kila mtu ana siri zake asizopenda zifahamike hadharani

Zinaweza kuwa siri nzuri au siri mbaya

Utasikia mtu akisema, Mimi siri zangu nitakufa nazo.

Mara nyingi hii humaanisha kuna mambo aliyoyafanya au anayoyajua ambayo hataki yawekwe wazi kwa sababu yanaweza kuleta aibu, fedheha au madhara kwake

Ndiyo maana anaamua kuzilinda kwa namna yoyote ile zisifahamike.

Umewahi kusikia neno siri za serikali? Au mtu akisema, Mimi nina siri za mtu fulani

Mimi naamini siri zinatofautiana kwa uzito
Ukisikia mtu anakuambia,
Nakueleza ila iwe siri yako, ujue ni siri, lakini sio siri yenye uzito mkubwa sana japo kuna watu husema siri zao nzito na ni mara chache sana

Lakini siri nzito huwa hazitoki kirahisi

Hivi unadhani ni rahisi mtu afanye mauaji halafu aje akuambie waziwazi kwamba ameua?

Au mtu afanye jambo ambalo jamii inaliona la aibu halafu aje alitangaze mwenyewe?

Si rahisi, kwa sababu anaogopa matokeo na fedheha ambazo zinaweza kutokea siri zake zikiwekwa hadharani

Kuna watu wamefanya mambo mengi maishani mwao, mazuri na mabaya, lakini yanabaki kuwa siri zao mpaka mwisho wa maisha

Sasa tuje kwa wale wanaopenda kufukunyua siri za watu (wambeya)

Unakuta mtu amekaa anapanga namna ya kugundua siri za watu ambazo kimsingi hazimhusu

Akishazigundua, anaanza kushangaa
Heh, kumbe huyu mtu yupo hivi!
Kumbe kuna hiki!( ulitumwa😏)

Baadaye anaenda mbali zaidi na kuanza kuzitangaza

Kitendo cha kufunua siri za watu walizoficha pengine kwa miaka mingi ni hatari

Unaweza kujikuta umejiweka kwenye matatizo yasiyokuhusu(kiranga)

Mara nyingi tabia hii huwa kwa watu ambao badala ya kushughulika na maisha yao, wanatumia muda mwingi kuchunguza maisha ya wengine

Utasikia mtu akisema
Mimi nina siri zake

Lakini swali ni moja hata kama kweli unazijua, zinakuhusu nini mpaka uanze kuzitangaza?( Unoko)

Je umetumwa?
Una uhakika hiyo kazi ya kusambaza siri za watu itakuletea faida au itakuletea hasara?

Kuna watu wakisikia jambo wanawashwa sana kulisema

Hawapati amani mpaka walitoe
Lakini unajua madhara ya kutokuwa msiri hata kwa siri zako mwenye ukiacha mbali siri za wengine?

Watu watakujua kupita kiasi
Ukiwa unaeleza kila jambo kuhusu maisha yako, unawapa watu ramani kamili ya maisha yako(wanakujua njee ndani)

Na wakati mwingine hiyo inaweza kutumiwa dhidi yako kukugandamiza maana watu watajua weakness zako

2. Hutakuwa wa kuaminika
Hata wale unaowapelekea siri za wengine watakuona kama mbeya Watajiuliza
Kama ananiletea siri za watu, kesho atapeleka zangu kwa wengine(kamdomo🤐)

3. Unaweza kuingia kwenye matatizo usiyoyatarajia
Wapo watu ambao hawana cha kupoteza
Ukianza kuanika siri zao unaweza kujikuta umeanzisha ugomvi au matatizo ambayo yangeweza kuepukika wakikutia kweny 18 utatii

Dunia ya leo si wanaume wala wanawake wote, lakini baadhi yao wamekuwa watu wa maneno mengi sana
Utakuta wameunda makundi ya kuchambua watu na siri zao
Yule namjua...
Huyu namfahamu...
Lakini swali ni unamjua kweli, au unamfukunyua?????

Cha kushangaza zaidi, kuna wengine huja kwako kwa gia ya kukueleza siri zao za uongo ili tu wakuaminishe

Baadaye wanakusubiri ufunguke na kuwaeleza yako
Ukishajieleza, umeingia mtegoni hapo tayali umeishaa watu washakumaliza

Sasa swali langu nyie wana JF 🤗

Umewahi kuona mtu ambaye akiambiwa jambo hawezi kukaa nalo?

Hata kama siri hiyo inaweza kuleta maafa, yeye anaropoka tu ?

Je, wewe unaweza kuona au kusikia jambo la mtu na ukatulia bila kulisambaza?

Na siri zako binafsi, unaweza kuzitunza au hupati amani mpaka uzimwage kwa wengine?

Ulijisikiaje ulipogundua siri yako uliyodhani hakuna wanaoijua imeanikwa?

Ukisikia neno siri unaelewa nini? Karibu✍️

ShesRise_1 🤚
Sabato day👌
Usiombe ukawa unafanya Kazi ya kutunza Siri kwenye nchi yenye viongozi wezi ,ujue unaweza Kufa Mda wowote ili Siri zao zisivuje
 
Neno siri linamaanisha taarifa, jambo, au maarifa yoyote yanayotunzwa kwa makusudi ili yasijulikane na watu wote, isipokuwa tu na mtu mmoja au kikundi kidogo cha watu walioidhinishwa.

Katika muktadha wa maisha ya kila siku, siri hujidhihirisha kama mambo ya kibinafsi ya mtu—kama vile afya au maisha ya familia—ambayo analinda kwa ajili ya faragha yake. Kijamii na kitaalamu, siri ni nguzo kuu ya uaminifu ambapo madaktari, wanasheria, na mabenki wanawajibika kisheria kutofichua taarifa za wateja wao, huku makampuni yakilinda mifumo na fomula za bidhaa zao ili kuhimili ushindani wa kibiashara.

Kiwango cha juu zaidi cha siri kinahusisha usalama wa nchi, ambapo taarifa za kijeshi na kidiplomasia hulindwa vikali ili kuzuia hatari yoyote dhidi ya taifa, ulinzi ambao siku hizi unajumuisha pia usalama wa kidijitali kupitia usimbaji wa nywila na data za mtandaoni ili kuzuia uhalifu wa kimtandao.
 
Nadhani hapa duniani 99% hakuna siri, mana siri n ya mtu mmoja
Mkishakuwa wawili, hy sio siri.
 
Asante kwa ufafanuzi mzuri🙏🙏
 
Nadhani hapa duniani 99% hakuna siri, mana siri n ya mtu mmoja
Mkishakuwa wawili, hy sio siri.
Siri zipo na ndio hizo ambazo huzijui
Siri hutofautiana uzito
Hizo unazozijua ni siri nyepesi
Siri nzito huwezi kuzijua watu hufa nazo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom