Ukisikia neno siri unaelewa nini?

Ukisikia neno siri unaelewa nini?

Leo nawapa siri vijana wenzangu njia ya kupata mishangazi....
"" Kwanza ni moto.. peleka moto as if hutokuja kumpata tena, moto moto moto mikunjo motoooo moto moto moto... Kuwa mbunifu katika bed, kuwa na ujanja ujanja mwingi.."""
 
Leo nawapa siri vijana wenzangu njia ya kupata mishangazi....
"" Kwanza ni moto.. peleka moto as if hutokuja kumpata tena, moto moto moto mikunjo motoooo moto moto moto... Kuwa mbunifu katika bed, kuwa na ujanja ujanja mwingi.."""
Nilidhani umepona ona sasa too late 😢
 
Leo nawapa siri vijana wenzangu njia ya kupata mishangazi....
"" Kwanza ni moto.. peleka moto as if hutokuja kumpata tena, moto moto moto mikunjo motoooo moto moto moto... Kuwa mbunifu katika bed, kuwa na ujanja ujanja mwingi.."""
Mkuu si uliachika shida ilikua nini? 😂
 
Leo nawapa siri vijana wenzangu njia ya kupata mishangazi....
"" Kwanza ni moto.. peleka moto as if hutokuja kumpata tena, moto moto moto mikunjo motoooo moto moto moto... Kuwa mbunifu katika bed, kuwa na ujanja ujanja mwingi.."""
😄 mimi mshangazi hapana bwashee , kuna mshangazi wa kizungu unayo pesa za kutisha ulidai umenielewa nikauonya ila akaniomba nimtafitie kijana wa nchi yangu , upo tayari niupe namba zako bwashee?
 
SIRI🤐

Ukisikia neno siri unaelewa nini?, Kila mtu ana siri zake asizopenda zifahamike hadharani. Zinaweza kuwa siri nzuri au siri mbaya, Utasikia mtu akisema, Mimi siri zangu nitakufa nazo.

Mara nyingi hii humaanisha kuna mambo aliyoyafanya au anayoyajua ambayo hataki yawekwe wazi kwa sababu yanaweza kuleta aibu, fedheha au madhara kwake. Ndiyo maana anaamua kuzilinda kwa namna yoyote ile zisifahamike.

Umewahi kusikia neno siri za serikali? Au mtu akisema, Mimi nina siri za mtu fulan. Mimi naamini siri zinatofautiana kwa uzito, Ukisikia mtu anakuambia,
Nakueleza ila iwe siri yako, ujue ni siri, lakini sio siri yenye uzito mkubwa sana japo kuna watu husema siri zao nzito na ni mara chache sana


Lakini siri nzito huwa hazitoki kirahisi, Hivi unadhani ni rahisi mtu afanye mauaji halafu aje akuambie waziwazi kwamba ameua!? Au mtu afanye jambo ambalo jamii inaliona la aibu halafu aje alitangaze mwenyewe?..... Si rahisi, kwa sababu anaogopa matokeo na fedheha ambazo zinaweza kutokea siri zake zikiwekwa hadharani

Kuna watu wamefanya mambo mengi maishani mwao, mazuri na mabaya, lakini yanabaki kuwa siri zao mpaka mwisho wa maisha

Sasa tuje kwa wale wanaopenda kufukunyua siri za watu (wambeya)
Unakuta mtu amekaa anapanga namna ya kugundua siri za watu ambazo kimsingi hazimhusu...Akishazigundua, anaanza kushangaa, Heh, kumbe huyu mtu yupo hivi!...Kumbe kuna hiki!( ulitumwa😏)
Baadaye anaenda mbali zaidi na kuanza kuzitangaza


Kitendo cha kufunua siri za watu walizoficha pengine kwa miaka mingi ni hatari. Unaweza kujikuta umejiweka kwenye matatizo yasiyokuhusu(kiranga)..Mara nyingi tabia hii huwa kwa watu ambao badala ya kushughulika na maisha yao, wanatumia muda mwingi kuchunguza maisha ya wengine
Utasikia mtu akisema
..Mimi nina siri zake

Lakini swali ni moja hata kama kweli unazijua, zinakuhusu nini mpaka uanze kuzitangaza?( Unoko)

1. Je umetumwa?
Una uhakika hiyo kazi ya kusambaza siri za watu itakuletea faida au itakuletea hasara.? Kuna watu wakisikia jambo wanawashwa sana kulisema, Hawapati amani mpaka walitoe. Lakini unajua madhara ya kutokuwa msiri hata kwa siri zako mwenye ukiacha mbali siri za wengine?
Watu watakujua kupita kiasi
Ukiwa unaeleza kila jambo kuhusu maisha yako, unawapa watu ramani kamili ya maisha yako(wanakujua njee ndani). Na wakati mwingine hiyo inaweza kutumiwa dhidi yako kukugandamiza maana watu watajua weakness zako

2. Hutakuwa wa kuaminika
Hata wale unaowapelekea siri za wengine watakuona kama mbeya Watajiuliza
Kama ananiletea siri za watu, kesho atapeleka zangu kwa wengine(kamdomo🤐)

3. Unaweza kuingia kwenye matatizo usiyoyatarajia
Wapo watu ambao hawana cha kupoteza. Ukianza kuanika siri zao unaweza kujikuta umeanzisha ugomvi au matatizo ambayo yangeweza kuepukika wakikutia kweny 18 utatii

Dunia ya leo si wanaume wala wanawake wote, lakini baadhi yao wamekuwa watu wa maneno mengi sana...Utakuta wameunda makundi ya kuchambua watu na siri zao
Yule namjua...Huyu namfahamu...Lakini swali ni unamjua kweli, au unamfukunyua?????

Cha kushangaza zaidi, kuna wengine huja kwako kwa gia ya kukueleza siri zao za uongo ili tu wakuaminishe
Baadaye wanakusubiri ufunguke na kuwaeleza yako
Ukishajieleza, umeingia mtegoni hapo tayali umeishaa watu washakumaliza

Sasa swali langu nyie wana JF 🤗

Umewahi kuona mtu ambaye akiambiwa jambo hawezi kukaa nalo?
Hata kama siri hiyo inaweza kuleta maafa, yeye anaropoka tu ?
Je, wewe unaweza kuona au kusikia jambo la mtu na ukatulia bila kulisambaza?

Na siri zako binafsi, unaweza kuzitunza au hupati amani mpaka uzimwage kwa wengine?
Ulijisikiaje ulipogundua siri yako uliyodhani hakuna wanaoijua imeanikwa?
Ukisikia neno siri unaelewa nini? Karibu✍️

ShesRise_1 🤚
Sabato day👌
Thank you D'V 😊 🙏
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom