Siri za Chumbani
New Member
- Aug 2, 2026
- 3
- 3
Wana JF, salamu!
Tunafurahi kujiunga rasmi na familia ya JamiiForums.
Sisi ni Siri za Chumbani, jukwaa la anonymous confessions linalowapa watu nafasi ya kushiriki siri, changamoto, maumivu na mambo mazito yanayowasumbua moyoni bila kufichua utambulisho wao.
Kila siku tunapokea simulizi halisi kutoka kwa watu wa makundi mbalimbali ya jamii. Baadhi ni za mahusiano, ndoa, familia, urafiki, usaliti, changamoto za kifedha, makosa ya maisha na matukio mengine ambayo mara nyingi huwa magumu kuyazungumza hadharani.
Kuanzia leo tutakuwa tukishiriki baadhi ya anonymous confessions hapa JamiiForums ili kujenga mijadala yenye maana, kubadilishana mawazo, kujifunza kupitia uzoefu wa wengine na kutoa ushauri unaoweza kubadili maisha ya mtu.
Ikiwa una mkasa, siri au jambo zito linalokusumbua moyoni na ungependa ulifikishe kwa jamii bila kujulikana, unaweza kulituma kupitia mfumo wetu wa anonymous unaopatikana kwenye link iliyopo kwenye Bio ya ukurasa rasmi wa Instagram wa Siri za Chumbani. Mfumo huo umeundwa kulinda faragha ya mtumaji ili aweze kushiriki simulizi lake kwa usalama bila kufichua utambulisho wake.
Kwa sasa huo ndiyo mfumo rasmi wa kupokea mikasa. Wakati huohuo, tunafanyia kazi njia rahisi zaidi itakayowawezesha wanajamii wa JamiiForums kutuma mikasa yao moja kwa moja kupitia jukwaa hili.
Tunafurahi kuwa sehemu ya jamii hii kubwa. Karibuni tushirikiane kujenga mijadala yenye heshima, busara na msaada kwa kila anayehitaji kusikilizwa.
Karibu Siri za Chumbani ndani ya JamiiForums.
Kila mtu ana siri. Kila siri inastahili kusikika.