Hii dunia imejaa mamtu ya hovyo sana na yanafikiri yana mamlaka juu ya kila mtu kisa hayajamwona kwenye chaneli zao....yakiona yameshindwa yanakuona wewe ndo mwanga kumbe hata hujui kinachoendelea, yanapigana vita na mamlaka za juu kabisa.Big up. Chuma ulete wapo wengi tu. Mimi nilisumbuliwa nao ila kwa nguvu nilimalizana nao. Yaani ilikuwa nikishika pesa tu lazima matatizo ya kishenzi yajitokeze. Mara magonjwa ya ajabu. Nilipomalizana nao kila kitu kiko shwari kabisa. Mijusi ndiyo nimejua leo na nitapambana nao. Nyumba Safi kabisa yaani mpaka umatamani ukae humo tu usitoke eti unakutana na mjusi ukutani na kimende. Mimi mpaka tandu na majongoo nililetewa. Mpaka chura na nikafafanuliwa kuwa jongoo na chura maana yake ni kama kukufunga usiweze kusogea kimaisha. Uchawi upo na vitabu vya dini vimebainisha. Muhimu omba Mungu na ikishindikana shirikisha wataalam. Maisha ni kujipambania.