Ukiona panya, popo, mende, mijusi wanazoea ndani mwako usipuuze. Huenda ni uchawi na chuma ulete umewekewa ndani

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
6,745
2,000
Kuna sehemu nimesema kuwa wadudu wengine huja kuishi kwenye makazi ya mtu kwakuwa mazingira kuwa rafiki kwao.
Mimi nyumba yangu mpya full tiles, gypsum rangi nzuri. Eti mjusi anakaa ukutani bila aibu. Huo sio uchawi kweli?
Inategemeana na aina ya ukuta na aina ya mjusi pia.

Kwa mfao wale mijusi jafiri wenye rangi maridhawa sana shingoni mwao, hupenda kuishi kwenye mawe ama nyumba zenye kuta za upele(chiping).

Sasa kuna hawa wanaitwa 'vigoni' na 'nole'.

Hawa hawakwepeki kwenye mazingira aishiyo binadamu, hapo kwako nao ni kwao pia, ukihama nao watahama kukufuata ama kujitokeza ulipohamia na hawana madhara isipokuwa faida, maana chakula chao ni inzi, tandabui, mbu na mende.
 
sysafiri

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
1,033
2,000
Sijamaanisha kuwa Uchawi hauko! Lakini siamini katika Uchawi hata kama upo.
Kama huamini kuwa kuna uchawi basi hufai kuwa mkristo, mwislamu na hata Mbudha.
Vitabu vya imani hizo zimeandika neno uchawi mara nyingi, sasa wewe inaonyesha huna imani.
Huwezi kuushinda uchawi kwa kuamini kuwa haupo, never.
 
Miguel Alvarez

JF-Expert Member
May 28, 2019
545
1,000
Uko sahihi mkuu hao mijusi ugomvi wangu na wao ni vile wanavyokunya ovyo mavi yao yananuka haswa
Inategemeana na aina ya ukuta na aina ya mjusi pia.

Kwa mfao wale mijusi jafiri wenye rangi maridhawa sana shingoni mwao, hupenda kuishi kwenye mawe ama nyumba zenye kuta za upele(chiping).

Sasa kuna hawa wanaitwa 'vigoni' na 'nole'.

Hawa hawakwepeki kwenye mazingira aishiyo binadamu, hapo kwako nao ni kwao pia, ukihama nao watahama kukufuata ama kujitokeza ulipohamia na hawana madhara isipokuwa faida, maana chakula chao ni inzi, tandabui, mbu na mende.
 
Donkey

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
1,076
2,000
Kuna sehemu nimesema kuwa wadudu wengine huja kuishi kwenye makazi ya mtu kwakuwa mazingira kuwa rafiki kwao.
Mimi nyumba yangu mpya full tiles, gypsum rangi nzuri. Eti mjusi anakaa ukutani bila aibu. Huo sio uchawi kweli?
Una kiwango gani cha elimu ndugu
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
7,585
2,000
Mambo ya waswahilina hayo, kuna mzee mmoja mswahilina ni jirani yangu tulishapigizana sana kelele kuhusu maswala ya mpaka hadi kwa mtendaji. Ikawa kipindi hicho sijisikii amani moyoni na pia niliugua sana, nilivyomwambia Mungu amani ya moyo ikarudi. Nilichoamua na wife ni kwamba hatuna salamu wala story yoyote tena na wao, mambo mengine nimeacha yaende kisheria, ila panya, mara vindege vinaruka kuingia ndani, wale mijusi wa ndani, njiwa wake alfajiri tu wamesharukia kwenye paa la nyumba yangu sioni sana ila nitaendelea kuwa makini zaidi. Nilichogundua baada ya kupigizana naye kelele mbele ya mjumbe kuhusu njiwa wake kuruka kwenye paa langu kila alfajiri na kuniletea usumbufu, wale njiwa walipunguza sana kurukia kwenye paa langu jambo ambalo linaashiria anazo nguvu za kuwa direct waruke kwenda mahali......kwa kuwa imani yangu kwa Mungu Mwenyezi inanipa uhakika wa kujua na kufahamu kuwa hakuna uchawi wala uganga wowote ule unaoweza kupenya kwa namna yoyote ile ule ukingo wa moto ambao Mungu kaniwekea mimi na familia yangu. Kama ilivyoandikwa 'hakuna uchawi wala uganga juu ya Yakobo' na kama ilivyoandikwa 'mwenye haki ataishi kwa imani'.....huwa nabaki tu nawatafakari hawa watu wanaoitwa wachawi, walozi, washirikina na takataka nyingine kama hizo.....
 
Donkey

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
1,076
2,000
Kama huamini kuwa kuna uchawi basi hufai kuwa mkristo, mwislamu na hata Mbudha.
Vitabu vya imani hizo zimeandika neno uchawi mara nyingi, sasa wewe inaonyesha huna imani.
Huwezi kuushinda uchawi kwa kuamini kuwa haupo, never.
Huoni aibu kwa kuabudu Imani za kitumwa na kuacha dini za mababu zako, utumwa bado tu, jitambue
 
Donkey

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
1,076
2,000
Kama huamini basi sio vibaya pia, ila kama unaamini nguvu za mungu basi fahamu na uchawi upo.
Hakuna uchawi, huo ni ufinyu wa uelewa wa mambo ya kidunia na kufuata maandiko ambayo ni simulizi zisizo kuwa na ushahidi
 
Donkey

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
1,076
2,000
Mambo ya waswahilina hayo, kuna mzee mmoja mswahilina ni jirani yangu tulishapigizana sana kelele kuhusu maswala ya mpaka hadi kwa mtendaji. Ikawa kipindi hicho sijisikii amani moyoni na pia niliugua sana, nilivyomwambia Mungu amani ya moyo ikarudi. Nilichoamua na wife ni kwamba hatuna salamu wala story yoyote tena na wao, mambo mengine nimeacha yaende kisheria, ila panya, mara vindege vinaruka kuingia ndani, wale mijusi wa ndani, njiwa wake alfajiri tu wamesharukia kwenye paa la nyumba yangu sioni sana ila nitaendelea kuwa makini zaidi. Nilichogundua baada ya kupigizana naye kelele mbele ya mjumbe kuhusu njiwa wake kuruka kwenye paa langu kila alfajiri na kuniletea usumbufu, wale njiwa walipunguza sana kurukia kwenye paa langu jambo ambalo linaashiria anazo nguvu za kuwa direct waruke kwenda mahali......kwa kuwa imani yangu kwa Mungu Mwenyezi inanipa uhakika wa kujua na kufahamu kuwa hakuna uchawi wala uganga wowote ule unaoweza kupenya kwa namna yoyote ile ule ukingo wa moto ambao Mungu kaniwekea mimi na familia yangu. Kama ilivyoandikwa 'hakuna uchawi wala uganga juu ya Yakobo' na kama ilivyoandikwa 'mwenye haki ataishi kwa imani'.....huwa nabaki tu nawatafakari hawa watu wanaoitwa wachawi, walozi, washirikina na takataka nyingine kama hizo.....
Huna hata shule ya kutambua tabia na asili ya viumbe Hai. Jaribu kusoma hata kidogo upunguze Imani za kishirikina
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
7,585
2,000
Huna hata shule ya kutambua tabia na asili ya viumbe Hai. Jaribu kusoma hata kidogo upunguze Imani za kishirikina
Ahaa, elimu ipi hiyo labda.....maana kama ni elimu ya duniani hakuna degree niliyobakiza huko juu....yaani nipo kwenye level za kina mwakyembe, mzee wa degree nne. Sheria ya kumiliki mifugo mijini inakutaka wewe mwenye mifugo ufanye nini ili kuondoa usumbufu kwa wengine, au changamoto za hiyo mifugo yako zinatakiwa zishughulishe kila mtu.
 
Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,523

Big up. Chuma ulete wapo wengi tu. Mimi nilisumbuliwa nao ila kwa nguvu nilimalizana nao. Yaani ilikuwa nikishika pesa tu lazima matatizo ya kishenzi yajitokeze. Mara magonjwa ya ajabu. Nilipomalizana nao kila kitu kiko shwari kabisa. Mijusi ndiyo nimejua leo na nitapambana nao. Nyumba Safi kabisa yaani mpaka umatamani ukae humo tu usitoke eti unakutana na mjusi ukutani na kimende. Mimi mpaka tandu na majongoo nililetewa. Mpaka chura na nikafafanuliwa kuwa jongoo na chura maana yake ni kama kukufunga usiweze kusogea kimaisha. Uchawi upo na vitabu vya dini vimebainisha. Muhimu omba Mungu na ikishindikana shirikisha wataalam. Maisha ni kujipambania.
 
CREOLE

JF-Expert Member
Mar 21, 2015
564
500
Ukiona wanaonekana na wanapotea kwa ajabu jua ndio wenyewe.
Ukiwaona wana aibu ukiwatazama jua ndio wenyewe
Kama sijui tabasamu la panya sijui nitaelewaje wanavyoona aibu. Hata hivyo asante kwa taarifa Kamanda.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom