Inaweza kuwa utoto. Inaweza kuwa hajui maana ya maisha. Nimeona dalili za ww kumuacha, lkn km umedhamiria kuoa usifanye hivyo. Hata unaowaona wanafuraha mbele yako na wamekaa kwa muda mrefu ktk ndoa kuna majaribu mengi nyuma yao. Moja ya njia sahihi ni kumtembeza kwa marafiki wako wenye ndoa zenye upendo na furaha ili ajifunze. Huko anaweza kupata hadithi za shida walizopitia. Pia ataambiwa kuwa hata walipo bado kuna karaha ktk baadhi ya nyakati ila huzivumilia zipite. Kuona na kusikia ni njia nzuri ya kijifunza. Usimwache maana utamkumbuka utakapoyaona ya firauni huko mbele. Hayo unayoyaona ni ya Musa tu kwa sasa.