Ukimya wake unaniweka njia panda, naomba ushauri

Ukimya wake unaniweka njia panda, naomba ushauri

Kuolewa ni bahati dada yangu.. Siyo lazima kama zamani.. Hizi bahati unazo zipiga teke sasa hivi utakuja kuzikumbuka baadae na utazitafuta na tochi... Jiongeze akili kichwani mwako..
 
Last Activity: Apr 13, 2016 at 4:10 PM
Joined: Monday
Messages: 2
Likes Received: 1
Trophy Points: 3
Gender: Female
Birthday: October 11
Hivi ulisema wewe ni msomaji mzuri wa JF?
May be alikuwa guest
 
33 f**king years wewe ni bibi ndio maana jamaa kakuachia manyoya..
Maarufu asioe vitu vibichi vidogo vitamu under 25 years
Oh yeah! Age aint nothing but a number dude. My babe is yet to be bor. Ya feel me? Pita hivii. Bibi demu wako
 
Kuolewa ni bahati dada yangu.. Siyo lazima kama zamani.. Hizi bahati unazo zipiga teke sasa hivi utakuja kuzikumbuka baadae na utazitafuta na tochi... Jiongeze akili kichwani mwako..
Sure rasta got soul. Pamoja na bahati, ndoa ni mkataba wa maisha. Kuingia mkataba huu na mtu usiyempenda hata kidogo ni dhambi kwa kweli. Hio itakua ndoano tena!
 
Habari wapendwa wa mmu,

Mimi ni msomaji mzuri sana wa JF majukwaa yote. Nimeonelea nijisajili ili nami niweze kutoa yangu ya moyoni. Kwa kifupi tu mimi ni mwanamke, mwaka huu natimiza miaka 33, ni mfanya biashara kwa hio kwa kiasi kikubwa najitegemea kwa gharama ndogo ndogo. Nachoenda kuelezea ni hali halisi nnayopitia na ninaomba msinihukumu bali mnipe ushauri.

Tokea nivunje ungo, nimeshapitia mahusiano kadhaa, sitopenda kutaja idadi lakini nimewahi kupenda kwa dhati mara 2 tu. Mara ya kwanza ni kwa x wangu ambaye ndio alikuwa bf wangu wa kwanza kabisa. Baada ya kuumizwa sana na huyu x sikuwahi kupenda tena, niliingia kwenye mahusiano ili tu nisiwe mpweke ila sikuwapenda kwa dhati kabisa waliofuata. Huyo x mpenzi wangu wa dhati, ameoa mwaka jana na alinijulisha nami niliridhia kwa kuwa mapenzi yale ya dhati yalishaisha.

Sikuwahi kufikiria kuolewa kabisa baada ya kuumizwa na x mpenzi wangu huyo niliyempenda kwa dhati kwa hiyo niliamua kujisomea na kujipanga kutokuwa tegemezi hata kwa maboyfriend waliofuata. Nimekuja kupenda tena na kwa sasa nataka niolewe nianzishe familia.

Mwaka juzi nikiwa msibani nilikutana na kijana mmoja maarufu mjini akanitongoza na kutaka nikalale naye siku hio hio mi kwa kujiheshimu nikampotezea. Kusema kweli jamaa yuko vizuri, sio tu maarufu ila mpunga anao pia. Kwa upande mwingine huyu jamaa anafahamiana au niseme familia yake na familia ya ndugu zangu wameoleana kwa hiyo kuna kufahamiana zaidi ya kimjini mjini. Yeye alichukua namba yangu ya simu ila mimi sikuchukua.

Kesho yake alinipigia simu na sikupokea kwa kuwa siku hiyo niliuwa safarini na nikaamua kwamba sitopokea namba yeyote mpya. Ikapita kama miezi 3 hivi, nikiwa na dada na rafiki yangu katika story tukajikuta tunamzungumzia huyu mtu maarufu. Kwenye mazungumzo nikawaambia kuwa huyu jamaa aliwahi kunitokea ila mimi sikutilia maanani. Basi ndugu zangu wale wakanisema kweli, "Oooh, unapoteza nafasi, wenzio wanaitafuta, mpigie simu na nini na nini". Kwa kuwa sikua na namba yake, dada yangu akanipa. Nikamwambia dada hata nikimpigia simu nitamuambia nini? Dada yangu akasema hilo niachie. Nitampigia na kuongea nae mimi. Basi nikamuachia hio ligi. Dada akapiga simu, akaongea na mshkaji wakapanga appointment.

Siku ya siku ikafika nikajiweka sawa nikaenda kukutana na jamaa kwa mara ya pili baada ya miezi 3. Kuanzia siku hio tukawa na mawasiliano mara kwa mara. Nilijikuta napata hisia za kumpenda kwa dhati huyu jamaa. Si kwa uzuri, umaarufu au pesa aliyo nayo, la hasha! Akaniomba nimpe nafasi ili anioe, nikamkubalia. Ila alinitahadharisha kwamba ana girlfriend. Nampenda kweli na wala sikumficha, nilimuambia. Nimewahi kulala nae mara moja tu na kwa hakika alifurahia tendo. Sijawahi ktk pita pita zangu kuona mwanaume amefurahia tendo kama huyo. Mwaka jana alikuwa busy sana na kampeni kwa kuwa alihusika kwa ukaribu sana na mgombea wa urais wa chama kimojawapo. Nilimpa nafasi amalizane na mikiki mikiki ya kampeni ila nikaanza kupata wasi wasi na uhusiano wetu kwa kuwa, kama nisipomtafuta mimi basi yeye hanitafuti ng'o! nilijipa moyo kwamba labda yuko busy akitulia atanitafuta lakini wapi. Kwa kuwa nilipenda kweli sikuacha kumtafuta na kumjulia hali.

Katika kipindi hicho, nilitokewa pia na wanaume 3 waliotangaza nia ya kunioa. Kati yao, 2 nilishakuwa na mahusiano nao 1 ni mpya kabisa. Sikuwapa jibu kwa kuwa yupo nnayempenda kwa dhati na ndio nilikuwa namsikilizia. Mwaka huu ikabidi nianze kuuliza kwa uhakika kama nia ilikuwepo au la! Nikaanza na wale 2 niliokuwa na mahusiano nao. Wote walinijibu kwamba niendelee tu na maisha yangu wao wamebadilisha mawazo. Nikashukuru, nikabaki na yule 1 ambae sijawahi kuhusiana nae mpaka sasa na anasubiri nimpe nafasi ila mi nimeogopa, huenda nae anataka anifunue tu chupi kisha asepe kwaio nimemuweka pending. Nikaja kumuuliza huyu mtu maarufu niliempenda kwa dhati msimamo wake majibu yake ni kwamba "ndio nilitaka kukuoa ila maisha yana changamoto na kwa sasa napitia wakati mgumu siwezi kukuelezea".

Nimejaribu kumsisitiza anipe msimamo wake kama pamoja na changamoto anazopitia kama amebadilisha mawazo au la, ili mi nifanye maamuzi, amekaa kimya. Nimemjulisha pia kwamba yupo anayetaka kuleta posa nyumbani kwaio anipe msimamo wake lakini jamaa bado hajibu, amekaa kimya tuu. Nimemtafuta sanaaa... jamaa response yake kwa kweli ni zero. Namuandikia msgs kwenye whatsapp, naona anasoma lakini hajibu. Nampigia simu hapokei..

Hitimisho!
Jamani, mimi nampenda sana huyu jamaa... huyo mwengine sina kabisa hisia za kumpenda. Natongozwa kila ya leo lakini kila nikitongozwa namuwaza tu huyu mpenzi wangu maarufu. Nikipenda napenda kweli. Ningependa kuishi na mtu nnayempenda kwa dhati na sio tu kwasababu ya umri nikimbilie kuolewa na mtu nisiyempenda. Ndoa itanishinda. Kinachoniuma ni kwamba yeye hataki kuwa muwazi kwangu. Aniambie tu msimamo wake, mie nitaridhika na jibu lolote, hata ikiwa kumkosa kabisa mie nipo radhi. Nisaidieni nipo njia panda.

Asanteni na karibuni kwa michango.





Una fanana na ex girlfriend aiseee hila ngoja nipite mbio tu
 
Murete aay...pole bana.oree ta tesupaarato mo olndung'ani likiamaa ilo.toomon Engai pikinjo olino kake miigil agurane kewon tiloo tung'ani.talama ndung'anaka loo mbesai au ngoshola .supai nganashe
 
Duh.....Mkuu kwa maelezo yako wanne walikuwa tayari kuleta posa home...Mimi cha kukushauri ndoa uwa zinakuja tu automatically halafu ukiona mtu anakufata kwa gia ya kuoa basi huyo anataka tamu then anasepa kama usain bolt penda maisha yako kwa sasa kula vizuri fanya mazoezi utapata mume bora kutoka kwa Mungu aiseee
 
Dash kweli mwanamke dalali wa mwanamke,,"eti wenzako nafasi wanaililia"
Endelea tu kuililia,,,,,ila huo umri wako ninamashaka nayo maana utu zima dawa,,,ila wewe kijana chizi,,sorry kama umekwazika
 
Dada achana na tamaa za moyo.ukitaka mwanaume unayependa tangu moyoni ujue utaumizwa kila siku.kumbuka wanawake wameumbwa kupendwa.ukipendwa utakuwa na thamani.mpende akupendaye.
Pia una miaka 33 Dada hiyo miaka ni mingi na utakuwa umekomaa hivo Dada angu utachina kitaa ukitafuta chemistry. Unachopaswa ni kuwa na mwanaume mwenye malengo.

Wanawake watu Wa ajabu sana utakuta waoaji ndiyo wanaotoswa lakini wapigaji wanajilia papuchi na kuwaumiza na kuja kushitukia wale waoaji wote wameoa na wewe unaoza.

Mwisho mapenzi yakiamliwa na moyo utateseka siku zote.
Angalia Mzee mengi na klyn maisha yanasonga.
Shauri yako tafuta hiyo chemistry yako ya moyo wako ikiongozwa na hisia.
Utaendelea Julia.
 
Dada Murete siezi ku add comment sababu kuna jibu zuri saaana kutoka kwa Paulo Sergio De Souz
 
Au sio... Ila ngumuu! It took me 15yrs to fall in love again. Dunno how long this gonna take again[emoji134] !
Sasa ukisubiri 15 yrs again ushakuwa bibi, kama huna mtoto fanya upate kabla ya 35yrs maana baada ya hapo ni shideer
 
Last Activity: Apr 13, 2016 at 4:10 PM
Joined: Monday
Messages: 2
Likes Received: 1
Trophy Points: 3
Gender: Female
Birthday: October 11
Hivi ulisema wewe ni msomaji mzuri wa JF?
Kasema amejiunga recently ,kwani haujui unaweza kusoma vitu vinavyoandikwa jf bila ya kua na account ? Sema kucoment kulike au kupost ndio hautaweza
 
Umri umeenda dada yangu ,huyo hana mpango na ww unajipotezea mda,
ongea na huyo mwingine mkianza mahusiano taratibu utaanza kumpenda
 
Toka moyoni... Ili wawili waeze kuishi, there has to be some chemistry. Ila kupenda kwa sasa sitaki tena.
Sio kama kupenda hutaki swala la kuja kupenda lazima sema unampenda nani? Je na yeye atakupenda kama ulivyompenda hapo ndio tatizo..lakini ukishajenga mentality ya kutaka kuolewa halafu ukawa unakubali kuingia kwenye mahusiano kisa ndoa sababu umri umeenda hiyo hatari utatembea na wanaume wangapi?Je na maradhi nao yatakuwa yanakusubiri...piga moyo konde tengeneza maisha yako fanya kazi kwa bidii mdada..angalizo unapoingia kwenye mahusiano mambo yako acha kushirikisha rafiki au dada yako hiyo ni personal issues maana ata wao mambo yao ya mahusiano sidhani kama wanakushirikisha
 
Asante mwaya. Haya ni majaribu ya shetani tu. Anahakikisha mtu hupati furaha... Ila, wazungu wana kausemi kao kanasemaa KARMA'S A BITCH. Sasa hivi huyo girlfriend wake yuko jela ana kesi isiyokuwa na dhamana. Mungu hachelewi kulipa.
Sio Shose kweli huyo mana naye ana kesi ya money laundering nasikia haina dhamana..!
 
Wewe dada funguka akili mkaka wa kibongo hawez kukwambia uchukue time yako.Kwenye mawasiliana ndo kuna kila kitu huyo jamaa hakutaki.Na alivyokwambia kuhusu girlfriend ulitakiwa ushtuke na ukimbie.Mwanaume kama anakupenda hadi mke atasema hana kama humjui.Huyo ni bonge la hit and run.Unajitaftia matatizo makubwa.Umri wako ushaenda angalia mwanume anayekupenda na kukujali ndo uolewe nae.Watu maarufu mimi huwa nawakimbiaga acha kabisa tena wanasiasa.Uuuwi sijui nitumie kichaga.Ila nielewe tuu dada huo muda unaopoteza kumtafuta hudhuria ibada muombe Mungu akupe ubavu wako.Kuhusu kufurahia tendo usidanganyike wanaume ni wajanja sana hata kama hakufurahia hawez kukwambia atasema amefurahia sanaa.
Cha mwisho usijifanye unajua sana kupenda utaumia sanaa.Subiri mwanaume akupende na mwanaume akikupenda ukikataa kumvulia atakuacha mpaka siku utakayotaka wewe.Umri wako haurudi nyuma mama .Jiongeze
 
Back
Top Bottom