Ukimya wake unaniweka njia panda, naomba ushauri

Pole for the everything... What I can say huyo si wako.. As hard as it is I'm sorry you have to let him Go... I can see you truly love him but he doesn't belong to you... Huyo jamaa knew your weaknesses and hana msimamo na sidhani kama alitaka kukuowa from the beginning... Just for you to track him because of your sister and friend it was the biggest mistake you did... Common now let a man to track you down first and ask you the first date and not you , beautiful... In the beggining you were not suppose to listen your sister or friend , ilitakiwa ujisikilize wewe na maamuzi yako na usimamie maamuzi yako ... Okay hayo yalishatokea tuyaache ... For now move on with your life how? Praying and fasting if you can , do your hobbies, go to the gym , work extra hours , volunteer ili tuu mawazo ya huyo celebrity yasiwepo... Delete all his contacts , block him everywhere .... So you dont get confusion ... About the new guy mama take it slow . if you can ask him to wait if he truly loves you , he will waiting for you ..... Nafikiri as you keep praying and fasting you will get a clear direction., Good luck.. Thanks..
Thank you loveissweet... I really shouldn't have traced him down. Well, can't blame my sister & friends too. They all wished for a better life for me. Watoto wa mjini think money is over everything so i can't blame them either.
 
It is well.. Now you know it .. Make a quick decision.. Good luck.. Thanks..
 
Habari wapendwa wa mmu,

Mimi ni msomaji mzuri sana wa JF majukwaa yote. Nimeonelea nijisajili ili nami niweze kutoa yangu ya moyoni. Kwa kifupi tu mimi ni mwanamke, mwaka huu natimiza miaka 33, ni mfanya biashara kwa hio kwa kiasi kikubwa najitegemea kwa gharama ndogo ndogo. Nachoenda kuelezea ni hali halisi nnayopitia na ninaomba msinihukumu bali mnipe ushauri.

Tokea nivunje ungo, nimeshapitia mahusiano kadhaa, sitopenda kutaja idadi lakini nimewahi kupenda kwa dhati mara 2 tu. Mara ya kwanza ni kwa x wangu ambaye ndio alikuwa bf wangu wa kwanza kabisa. Baada ya kuumizwa sana na huyu x sikuwahi kupenda tena, niliingia kwenye mahusiano ili tu nisiwe mpweke ila sikuwapenda kwa dhati kabisa waliofuata. Huyo x mpenzi wangu wa dhati, ameoa mwaka jana na alinijulisha nami niliridhia kwa kuwa mapenzi yale ya dhati yalishaisha.

Sikuwahi kufikiria kuolewa kabisa baada ya kuumizwa na x mpenzi wangu huyo niliyempenda kwa dhati kwa hiyo niliamua kujisomea na kujipanga kutokuwa tegemezi hata kwa maboyfriend waliofuata. Nimekuja kupenda tena na kwa sasa nataka niolewe nianzishe familia.

Mwaka juzi nikiwa msibani nilikutana na kijana mmoja maarufu mjini akanitongoza na kutaka nikalale naye siku hio hio mi kwa kujiheshimu nikampotezea. Kusema kweli jamaa yuko vizuri, sio tu maarufu ila mpunga anao pia. Kwa upande mwingine huyu jamaa anafahamiana au niseme familia yake na familia ya ndugu zangu wameoleana kwa hiyo kuna kufahamiana zaidi ya kimjini mjini. Yeye alichukua namba yangu ya simu ila mimi sikuchukua.

Kesho yake alinipigia simu na sikupokea kwa kuwa siku hiyo niliuwa safarini na nikaamua kwamba sitopokea namba yeyote mpya. Ikapita kama miezi 3 hivi, nikiwa na dada na rafiki yangu katika story tukajikuta tunamzungumzia huyu mtu maarufu. Kwenye mazungumzo nikawaambia kuwa huyu jamaa aliwahi kunitokea ila mimi sikutilia maanani. Basi ndugu zangu wale wakanisema kweli, "Oooh, unapoteza nafasi, wenzio wanaitafuta, mpigie simu na nini na nini". Kwa kuwa sikua na namba yake, dada yangu akanipa. Nikamwambia dada hata nikimpigia simu nitamuambia nini? Dada yangu akasema hilo niachie. Nitampigia na kuongea nae mimi. Basi nikamuachia hio ligi. Dada akapiga simu, akaongea na mshkaji wakapanga appointment.

Siku ya siku ikafika nikajiweka sawa nikaenda kukutana na jamaa kwa mara ya pili baada ya miezi 3. Kuanzia siku hio tukawa na mawasiliano mara kwa mara. Nilijikuta napata hisia za kumpenda kwa dhati huyu jamaa. Si kwa uzuri, umaarufu au pesa aliyo nayo, la hasha! Akaniomba nimpe nafasi ili anioe, nikamkubalia. Ila alinitahadharisha kwamba ana girlfriend. Nampenda kweli na wala sikumficha, nilimuambia. Nimewahi kulala nae mara moja tu na kwa hakika alifurahia tendo. Sijawahi ktk pita pita zangu kuona mwanaume amefurahia tendo kama huyo. Mwaka jana alikuwa busy sana na kampeni kwa kuwa alihusika kwa ukaribu sana na mgombea wa urais wa chama kimojawapo. Nilimpa nafasi amalizane na mikiki mikiki ya kampeni ila nikaanza kupata wasi wasi na uhusiano wetu kwa kuwa, kama nisipomtafuta mimi basi yeye hanitafuti ng'o! nilijipa moyo kwamba labda yuko busy akitulia atanitafuta lakini wapi. Kwa kuwa nilipenda kweli sikuacha kumtafuta na kumjulia hali.

Katika kipindi hicho, nilitokewa pia na wanaume 3 waliotangaza nia ya kunioa. Kati yao, 2 nilishakuwa na mahusiano nao 1 ni mpya kabisa. Sikuwapa jibu kwa kuwa yupo nnayempenda kwa dhati na ndio nilikuwa namsikilizia. Mwaka huu ikabidi nianze kuuliza kwa uhakika kama nia ilikuwepo au la! Nikaanza na wale 2 niliokuwa na mahusiano nao. Wote walinijibu kwamba niendelee tu na maisha yangu wao wamebadilisha mawazo. Nikashukuru, nikabaki na yule 1 ambae sijawahi kuhusiana nae mpaka sasa na anasubiri nimpe nafasi ila mi nimeogopa, huenda nae anataka anifunue tu chupi kisha asepe kwaio nimemuweka pending. Nikaja kumuuliza huyu mtu maarufu niliempenda kwa dhati msimamo wake majibu yake ni kwamba "ndio nilitaka kukuoa ila maisha yana changamoto na kwa sasa napitia wakati mgumu siwezi kukuelezea".

Nimejaribu kumsisitiza anipe msimamo wake kama pamoja na changamoto anazopitia kama amebadilisha mawazo au la, ili mi nifanye maamuzi, amekaa kimya. Nimemjulisha pia kwamba yupo anayetaka kuleta posa nyumbani kwaio anipe msimamo wake lakini jamaa bado hajibu, amekaa kimya tuu. Nimemtafuta sanaaa... jamaa response yake kwa kweli ni zero. Namuandikia msgs kwenye whatsapp, naona anasoma lakini hajibu. Nampigia simu hapokei..

Hitimisho!
Jamani, mimi nampenda sana huyu jamaa... huyo mwengine sina kabisa hisia za kumpenda. Natongozwa kila ya leo lakini kila nikitongozwa namuwaza tu huyu mpenzi wangu maarufu. Nikipenda napenda kweli. Ningependa kuishi na mtu nnayempenda kwa dhati na sio tu kwasababu ya umri nikimbilie kuolewa na mtu nisiyempenda. Ndoa itanishinda. Kinachoniuma ni kwamba yeye hataki kuwa muwazi kwangu. Aniambie tu msimamo wake, mie nitaridhika na jibu lolote, hata ikiwa kumkosa kabisa mie nipo radhi. Nisaidieni nipo njia panda.

Asanteni na karibuni kwa michango.
Kwani kila anayekutongoza lazima umvulie chupi inaonyesha wewe beki hazikabi kbsaaaa pole kwa atakayekuoa
 
Loooooooh!!!...... Baada ya kurudiana nae aliomba utamu baada ya mda gani?(i normally study behaviour of human beings so as to understand their mind-objectives and aims)
Mkuu hakurudi tena... Ilaa, kuna wakati alinivuruga kidogo. Aliandaa party nikaenda kumpa support kama watu wengine tu. Huko nlimkuta na huyo girlfriend wake but akawa na wasiwasi sana. Hakutulia kabisa siku ile. Alidhani nitaenda kumchafulia party yake but mi sikua na mpango huo. Alipoona najichanganya na wala sileti vurugu akaanza yeye kuzingua. Akaninyima nisicheze na guys wengine kisa anaona wivu. Na ali-admit kabisa kwangu. Mi nikavunga. Since that day....
 
Teh...pole mwaya haya mambo yanachanganya si kidogo...nani ni nani Mungu ndio anajua wewe tulia tu kwa sasa
 
Hapa mi naona kama we ndo ulimpenda na kumtongoza huyu jamaa coz umesema baada ya kuchukua no yako alikupigia mara moja tu na hukupokea sim yake lakin baada ya miezi mitatu ukaunganishwa kwake na rafki yako sasa hapo si unaona kuwa ulitongozewa na rafki yako coz jamaa mwenyewe hakukuambia hata kwa text kuwa ana nia na ww.
Halafu umemwambia kuna mtu anataka kuleta posa kwenu yeye kakaa kimya .....ni sawa coz hata kimya ni jibu.
Hata mimi nikitaka kuacha mtu sipokei cm yake wala cjibu text zake.
 
Kwani kila anayekutongoza lazima umvulie chupi inaonyesha wewe beki hazikabi kbsaaaa pole kwa atakayekuoa
Hapana mkuu... Hata nami nachagua nimpe nani. Sio wote wanaonitongoza nalala nao. Mimi ni binadamu sio umbwa. Tuheshimiane. Nna maamuzi na mwili wangu
 
Hapa mi naona kama we ndo ulimpenda na kumtongoza huyu jamaa coz umesema baada ya kuchukua no yako alikupigia mara moja tu na hukupokea sim yake lakin baada ya miezi mitatu ukaunganishwa kwake na rafki yako sasa hapo si unaona kuwa ulitongozewa na rafki yako coz jamaa mwenyewe hakukuambia hata kwa text kuwa ana nia na ww.
Halafu umemwambia kuna mtu anataka kuleta posa kwenu yeye kakaa kimya .....ni sawa coz hata kimya ni jibu.
Hata mimi nikitaka kuacha mtu sipokei cm yake wala cjibu text zake.
Kwa kweli sikumtongoza. Yeye ndio aliyenitongoza. Thanks!
 
Last Activity: Apr 13, 2016 at 4:10 PM
Joined: Monday
Messages: 2
Likes Received: 1
Trophy Points: 3
Gender: Female
Birthday: October 11
Hivi ulisema wewe ni msomaj mzuri wa JF?
Kwani huezi kua msomaji bila kua na Id? Mfano mm nimekua Niki ingia jf fr ages lkn nakuja kma guest acha kukurupuka na kujiona unajua to a ushauri huezi tambaa na biti. Nakerwa na wajuaji kama nyinyi
 
Hapana mkuu... Hata nami nachagua nimpe nani. Sio wote wanaonitongoza nalala nao. Mimi ni binadamu sio umbwa. Tuheshimiane. Nna maamuzi na mwili wangu
Sawa Dada una maamuzi na mwili wako lkn sidhani kama una maamuzi na akili yako? Samahani kwa kauli Kali lkn naomba kuuliza kichwani zipo timam kweli? Hakupendi Huyo mwanaume acha kujitia upofu
 
Habari wapendwa wa mmu,

Mimi ni msomaji mzuri sana wa JF majukwaa yote. Nimeonelea nijisajili ili nami niweze kutoa yangu ya moyoni. Kwa kifupi tu mimi ni mwanamke, mwaka huu natimiza miaka 33, ni mfanya biashara kwa hio kwa kiasi kikubwa najitegemea kwa gharama ndogo ndogo. Nachoenda kuelezea ni hali halisi nnayopitia na ninaomba msinihukumu bali mnipe ushauri.

Tokea nivunje ungo, nimeshapitia mahusiano kadhaa, sitopenda kutaja idadi lakini nimewahi kupenda kwa dhati mara 2 tu. Mara ya kwanza ni kwa x wangu ambaye ndio alikuwa bf wangu wa kwanza kabisa. Baada ya kuumizwa sana na huyu x sikuwahi kupenda tena, niliingia kwenye mahusiano ili tu nisiwe mpweke ila sikuwapenda kwa dhati kabisa waliofuata. Huyo x mpenzi wangu wa dhati, ameoa mwaka jana na alinijulisha nami niliridhia kwa kuwa mapenzi yale ya dhati yalishaisha.

Sikuwahi kufikiria kuolewa kabisa baada ya kuumizwa na x mpenzi wangu huyo niliyempenda kwa dhati kwa hiyo niliamua kujisomea na kujipanga kutokuwa tegemezi hata kwa maboyfriend waliofuata. Nimekuja kupenda tena na kwa sasa nataka niolewe nianzishe familia.

Mwaka juzi nikiwa msibani nilikutana na kijana mmoja maarufu mjini akanitongoza na kutaka nikalale naye siku hio hio mi kwa kujiheshimu nikampotezea. Kusema kweli jamaa yuko vizuri, sio tu maarufu ila mpunga anao pia. Kwa upande mwingine huyu jamaa anafahamiana au niseme familia yake na familia ya ndugu zangu wameoleana kwa hiyo kuna kufahamiana zaidi ya kimjini mjini. Yeye alichukua namba yangu ya simu ila mimi sikuchukua.

Kesho yake alinipigia simu na sikupokea kwa kuwa siku hiyo niliuwa safarini na nikaamua kwamba sitopokea namba yeyote mpya. Ikapita kama miezi 3 hivi, nikiwa na dada na rafiki yangu katika story tukajikuta tunamzungumzia huyu mtu maarufu. Kwenye mazungumzo nikawaambia kuwa huyu jamaa aliwahi kunitokea ila mimi sikutilia maanani. Basi ndugu zangu wale wakanisema kweli, "Oooh, unapoteza nafasi, wenzio wanaitafuta, mpigie simu na nini na nini". Kwa kuwa sikua na namba yake, dada yangu akanipa. Nikamwambia dada hata nikimpigia simu nitamuambia nini? Dada yangu akasema hilo niachie. Nitampigia na kuongea nae mimi. Basi nikamuachia hio ligi. Dada akapiga simu, akaongea na mshkaji wakapanga appointment.

Siku ya siku ikafika nikajiweka sawa nikaenda kukutana na jamaa kwa mara ya pili baada ya miezi 3. Kuanzia siku hio tukawa na mawasiliano mara kwa mara. Nilijikuta napata hisia za kumpenda kwa dhati huyu jamaa. Si kwa uzuri, umaarufu au pesa aliyo nayo, la hasha! Akaniomba nimpe nafasi ili anioe, nikamkubalia. Ila alinitahadharisha kwamba ana girlfriend. Nampenda kweli na wala sikumficha, nilimuambia. Nimewahi kulala nae mara moja tu na kwa hakika alifurahia tendo. Sijawahi ktk pita pita zangu kuona mwanaume amefurahia tendo kama huyo. Mwaka jana alikuwa busy sana na kampeni kwa kuwa alihusika kwa ukaribu sana na mgombea wa urais wa chama kimojawapo. Nilimpa nafasi amalizane na mikiki mikiki ya kampeni ila nikaanza kupata wasi wasi na uhusiano wetu kwa kuwa, kama nisipomtafuta mimi basi yeye hanitafuti ng'o! nilijipa moyo kwamba labda yuko busy akitulia atanitafuta lakini wapi. Kwa kuwa nilipenda kweli sikuacha kumtafuta na kumjulia hali.

Katika kipindi hicho, nilitokewa pia na wanaume 3 waliotangaza nia ya kunioa. Kati yao, 2 nilishakuwa na mahusiano nao 1 ni mpya kabisa. Sikuwapa jibu kwa kuwa yupo nnayempenda kwa dhati na ndio nilikuwa namsikilizia. Mwaka huu ikabidi nianze kuuliza kwa uhakika kama nia ilikuwepo au la! Nikaanza na wale 2 niliokuwa na mahusiano nao. Wote walinijibu kwamba niendelee tu na maisha yangu wao wamebadilisha mawazo. Nikashukuru, nikabaki na yule 1 ambae sijawahi kuhusiana nae mpaka sasa na anasubiri nimpe nafasi ila mi nimeogopa, huenda nae anataka anifunue tu chupi kisha asepe kwaio nimemuweka pending. Nikaja kumuuliza huyu mtu maarufu niliempenda kwa dhati msimamo wake majibu yake ni kwamba "ndio nilitaka kukuoa ila maisha yana changamoto na kwa sasa napitia wakati mgumu siwezi kukuelezea".

Nimejaribu kumsisitiza anipe msimamo wake kama pamoja na changamoto anazopitia kama amebadilisha mawazo au la, ili mi nifanye maamuzi, amekaa kimya. Nimemjulisha pia kwamba yupo anayetaka kuleta posa nyumbani kwaio anipe msimamo wake lakini jamaa bado hajibu, amekaa kimya tuu. Nimemtafuta sanaaa... jamaa response yake kwa kweli ni zero. Namuandikia msgs kwenye whatsapp, naona anasoma lakini hajibu. Nampigia simu hapokei..

Hitimisho!
Jamani, mimi nampenda sana huyu jamaa... huyo mwengine sina kabisa hisia za kumpenda. Natongozwa kila ya leo lakini kila nikitongozwa namuwaza tu huyu mpenzi wangu maarufu. Nikipenda napenda kweli. Ningependa kuishi na mtu nnayempenda kwa dhati na sio tu kwasababu ya umri nikimbilie kuolewa na mtu nisiyempenda. Ndoa itanishinda. Kinachoniuma ni kwamba yeye hataki kuwa muwazi kwangu. Aniambie tu msimamo wake, mie nitaridhika na jibu lolote, hata ikiwa kumkosa kabisa mie nipo radhi. Nisaidieni nipo njia panda.

Asanteni na karibuni kwa michango.

Stori yako kama yangu sema mimi ni "me"
Mpotezee tu kama mimi nilivyoamua kumpotezea wangu 😀 kiroho safi
 
Natamani sana angeniambia hivo. Ingenipa ahueni sana kwani kwenye maisha binadamu hapati kile anachotaka bali kile anachohitaji. Na mimi napenda kuwa muwazi na ndio maana nilifurahi alipokuwa muwazi kwa kuniambia ukweli kuhusu girlfriend. Basi angeendelea na huo uwazi basi kusema msimamo wake kuliko kuniacha njia panda.
Kwani mtu akikwambia ana g'friend kwa dunia ya sasa ww unaelewa nini? maana yake ana mpenzi kwa hiyo ww lengo lako unataka aachane na huyo g'friend wake akuoe wewe sio? basi endelea kusubiria ukweli mwingine zaidi ya hiyo.
 
Stori yako kama yangu sema mimi ni "me"
Mpotezee tu kama mimi nilivyoamua kumpotezea wangu 😀 kiroho safi
Au sio... Ila ngumuu! It took me 15yrs to fall in love again. Dunno how long this gonna take again[emoji134] !
 
Endelea kusubiri,naoba ushachanganyikwa 33 bado haupo kwenye nahusiano rasmi?menopause inakuhusu
 
Kwani mtu akikwambia ana g'friend kwa dunia ya sasa ww unaelewa nini? maana yake ana mpenzi kwa hiyo ww lengo lako unataka aachane na huyo g'friend wake akuoe wewe sio? basi endelea kusubiria ukweli mwingine zaidi ya hiyo.
Watu wanakuwa na girlfriends but hawaoi hao girlfriends. Hata wengine wanaishi nao miaka na wanaishia kuoa mwingine. Ningejuaje bahati ni yangu au sio kama ningekataa?!
 
Heart, asante!
Siwezi kupinga kwamba jamaa hana tena interest. Ukweli huu niliuona ila as the english say, LOVE IS BLIND. Nimeusikiliza moyo zaidi ya kutumia akili
Eti love is blind Dada angu are you 33 kweli?
Aisee sjui kwann hii kitu nimechukulia personal sana lkn mm naudhikaa mnooo na wanawake vinganganizi daah
Embu jithamini at age 33 bado huja jua kua love is a temporary feelings? Unavo zidi kumganda ndo unazidi kumtibua Huyo jamaa embu kua na staha Dada half jiheshimu. Ole wko unichambe wkt nimekupa ushauri
 
Back
Top Bottom