Kijukuu cha Tanzania
Member
- Dec 6, 2025
- 6
- 3
Wakati risasi zilipolia mtaani wananchi walikimbia kuokoa maisha yao na maandamano yakikabiliwa na nguvu ya Dola, vyombo vya habari nchini Tanzania vilikaa kimya.
Kwa wananchi kama Ismail Issa, mkazi wa Dar es salaam huu haukuwa uzembe wa kawaida wa vyombo vya habari, bali ni usalitiwa wazi wa wajibu wa kihabari wa jamii kama anavyoeleza.
"Wananchi tulisalitiwa, kiukweli kile kipindi cha kufungiwa ndio nilijua sisi hatuna vyombo vya habari kabisa, na mpaka sasa siviamini tena. Haiwezekani nchi iilpitia mambo mazito kiasi kile lakini hakuna chombo kilichotipoti, sasa najiuliza niangalie taarifa ya habari ya nini? Wanahabari walituacha peke yetu kwenye kipindi kigumu," alisema Ismail.
Ikumbukwe kuwa kuanzia siku ya uchaguzi mkuu wa TanzaniaOktoba 29, 2025 hadi Novemba 3, 2025, kumeshuhudiwa namna ambavyo tasnia ya habari nchini ilivyoonyesha kudhoofika na kushindwa kutimiza wajibu wake wa msingi wa kusimama na kutetea maslahi ya wananchi.
Hata hivyo, licha ya kuwepo kwa matukio yauchaguzi mkuu na maanamano, tukio la maandamano halikupata nafasi yoyote kwenye vyombo vya habari, kuanzia mitandao ya kijamii hadi vyombo vikuu vya habari (mainstream media).
Taarifa kutoka ndani ya vyombo vya habari zinaonyesha kuwa hapakuwa na amri ya wazi ya iliyotolewa kupiga marufuku kuripoti maandamano, badala yake kulikuwepo na kile wanahabari wanakiita “hofu iliyoelekezwa’ mazingira ambayo yanawakwamisha wahariri kujidhibiti kabla ya kudhibitiwa hali iliyosababisha tahadhari kupindukia na hatimaye ukimya kamili.
Kutokana na hilo watu wengi mitaani na mitandaoni wamekuwa wakihoji na kuvilaumu vyombo vya habari kwa kushindwa kuripoti ukweli kuhusu maandamano hayo, ambayo yameambatana na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwemo mauaji ya raia.
Sababu za ukimya:
Kumekuwa na maswali ya sababu za ukimya huo, hata hivyo, taarifa zinaonyesha kuwa intaneti ilikatwa kuanzia saa 6 mchana na hivyo kusababisha vyombo vya habari kushindwa kuendelea kufanya kazi.
Baada ya kufungwa kwa intaneti, waandihi wa habari walishindwa kutuma na kupokea habari na hivyo baadhi ya vyumba vya habari vilifungwa kwa sku tano, hadi intaneti ilipofunguliwa Novemba 3, 2025.
Hata hivyo, baadhi ya vituo vya televisheni na redio vikiwemo vya Serikali (TBC), televisheni binafsi kama ITV, Star TV waliendelea na matangazo, wakidai kupewa maelekezo na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Meneja wa Utangazaji wa TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kilichozimwa ni mitandao ya jamii tu, lakini njia nyingine za intaneti ziliendelea.
Kuhusu kudhibiti maudhuo yaliyokuwa yakirushwa na vyombo vya habari, Kisaka alisema, TCRA hufuatilia maudhui yanayorushwa na vituo vya utangazaji (content monitoring) ili kuhakikisha yanazingatia sheria na kanuni zinazosimamia sekta.
Kutokana na udhibiti huo, vyombo vya habari na wanahabari wenyewe wlaikosa uhuru wa kufanya kazi yao isipokuwa kwa maelekezo ya Serikali.
Manyanyaso:
Ripoti mbalimbali ikiwamo ya Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (Jowuta) zimeonyesha kuwepo kwa manyanyaso vikiwemo vifo, majeruhi na kunyang’anywa kwa vifaa kwa waandishi wa habari.
Baadhi ya waandishi waliouawa wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, ni pamoja na aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania Maneno Selanyika, aliyepigwa risasi karibu na nyumbani kwake jijini Dar es Salaam siku ya uchaguzi.
Mwingine ni mwandishi wa habari za michezo wa Clouds Media Group, Master Tindwa Mtopa aliyepigwa risasi na kuuawa nyumbani kwake Temeke, Dar es Salaam.
Mwingine ni Mwandishi wa habari wa Baraka FM,Kelvin Lameck aliyeuawa alipokuwa kazini akifuatilia vurugu.
Mbali na mauaji, baadhi ya waandishi wa habari walikamatwa akiwamo Godfrey Thomas (Ayo TV) aliyekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uhaini.
Naye Alphonce Kusaga (Sunrise Radio) alikamatwa lakini baadaye aliachiliwa huru.
Ripoti hiyo pia inabainisha kuwa waandishi saba wa Azam Media na mmoja wa Star TV walijeruhiwa katika vurugu hizo.
Manyanyaso yote hayo yalisababisha waandishi wa habari washindwe kufanya kazi zao ipasavyo.
Wapo walioendelea na kazi pamoja na madhila hayo, baadhi ya waandishi wa habari waliendelea na kazi.
Kuna video moja ambayo mwandishi mmoja alifanikiwa kurekodi video akiwahoji wananchi kuhusu hali halisi mitaani. Wakati mahojiano yakiendelea, milio ya risasi ilisika waziwazi, na hata aliyehojiwa alishindwa kuendelea kuzungumza kwa hofu. Lakini video hiyo haikuonekana kwenye taarifa ya habari iliyorushwa kupitia chombo hicho.
Facebook
www.facebook.com
Mwandishi mwingine, licha ya hatari, alijaribu kufika eneo la tukio kuripoti moja kwa moja, lakini alikamatwa na askari, akaulizwa anapanga kupeleka wapi taarifa hizo. Hatimaye vifaa vyake vya kazi vilinyang’anywa na alidai kupigwa.
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) uliripoti kuwa mwandishi wa Watetezi TV alikamatwa wakati akitekeleza majukumu yake ya kihabari jijini Dar es Salaam, alipigwa na kunyang’anywa vifaa vyake Oktoba 31, 2025, na alipatikana tarehe 1 Novemba 2025 akiwa Kibaha, mkoani Pwani.
Vyombo vya habari vya nje
Awali Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) liliripoti maandamano yalipoanza Dar es Salaam maeneo ya Kimara, lakini ilipofika saa 7 intaneti ilizimwa.
Aljazeera nao waliendelea kuripoti matukio ya vurugu hata baada ya intaneti kufungwa. Baada ya intaneti kurejeshwa, BBC Swahili walitoa ripoti iliyoonyesha mkusanyiko wa matukio ya vurugu yakiwamo ya polisi wakiwafyatulia risasi waandamaji, huku pia wakionyesha maiti zilizodaiwa kukusanywa.
Katika ripoti hiyo, BBC walidai kuthibitisha uhalali wa picha na video kwa kutumia teknolojia ya satelaiti. Walidai kuzitafuta mamlaka za Tanzania kufafanua lakini hawakupata ushirikiano.
Novemba 21, CNN nao walitoa ripoti yao wakionyesha mfululizo wa makabiliano kati ya polisi wenye sare na wasio na sare na waandamanaji. Walidai kuthibitisha picha na video kwa kutumia satelaiti na pia walidai kuzitafuta mamlaka za Serikali lakini hazikujibu.
Ripoti hizo ziliibua mjadala mkali ndani na nje ya nchi, hadi Novemba 23, Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa alipokuja kulalamikia mashirika ya habari ya kimataifa ya BBC, CNN, Aljazeera na DW kwa kutoa habari hizo bila kutafuta upande wa Serikali.
Mwandishi wa televisheni ya CNN Africa, Larry Madowo, akiizungumza kupitia mitandao yake ya kijamii alisema kuwa Tanzania inakabiliwa na ukandamizaji mkubwa wa uhuru wa habari, kiasi cha kuwafanya waandishi wa habari kutoka nje kushindwa kuingia nchini kufanya kazi zao bila vibali maalum.
Waandishi walalamika
Suala la u huru wa vyombo vya habari kudhibitiwa, liliwasilishwa na wahariri wa vyombo vya habari hapa nchini mnamo November 25, 2025 walipokutana na Waziri Mkuu Dk Mwigulu Nchemba, ambapo walidai kuwa tasnia ya habari inaonekana ya hovyo kutokana na vitisho wanavyokutana navyo kutoka kwa taasisi za serikali hasa mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Akiwasilisha changamoto hiyo Mhariri NevilleMeena alihoji, sababu ya TCRA kuvibana vyombo vya habari wakati wa uchaguzi.
Akijibu swali hilo, aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ProfesaPalamagamba Kabudi alisema kuwa serikali ina nia ya kufanya mchakato wa kupitia sera ya vyombo vya habari ya mwaka 2013 ili kuweka mazingira rafiki kwa vyombo vya habari katika kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Kwa upande wake Edwin Soko ambaye ni mwenyekiti wa MISA-TAN, amekiri kwamba licha ya jitihada ambazo zilichukuliwa kabla ya uchaguzi ya kuwajengea uwezo wanahabari juu ya namna ya kufanya kazi wakati wa uchaguzi, lakini jambo lilitokea halikutarajiwa hapa nchini hivyo ilikuwa ni ngumu kukabiliana nalo.
Soko amekiri kuwa, vipo vyombo vya habari ambavyo viliripoti kwao kuwa vilitishiwa na waandamanaji kutokana na itikadi zao hivyo vyombo hivyo vililazimika kufunga vituo hivyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Novemba 3, 2025 Msemaji mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alivipongeza vyombo vya habari vya Tanzania kwa kutoripoti kilichotokea Kuanzia Oktoba 29 huku akisema kuwa huo ni uzalendo na ni uandishi wa habari wa uwajibikaji uandishi wa habari wa uwajibikaji.
Kauli hiyo iliibua mijadala miongoni mwa wadau wa habari nchini wengine kudai kuwa kauli hIyo inadhhirisha kuwa uhuru wa vyombo vya habari umeshikiliwa na serikali na pengine wao ndio wanafuaika wa mfumo huo wa udhibiti.
View: https://www.instagram.com/reel/DSFdwtADFn9/?igsh=MWVjMHJjZ2duMzRkeQ==
View: https://www.facebook.com/share/v/19pQwYoahg/
Nini Kifanyike?
Dk. Richard Mbunda, mhadhiri chuo kikuu cha Dar es Salaam, anasema kuwa, uhuru kamili wa vyombo vya habari hautaimarika bila mabadiliko ya sheria kwani kwa upande wake anaona kuwa matatizo mengi yanayoathiri uhuru wa vyombo vya habari yanatokana na misingi ya kisheria akibainisha kuwa matamko mbalimbali ya wanasiasa hayawezi kuvipatia uhuru vyombo vya habari bila kubadili sheria.