KWELI UKIMWI uliingia Tanzania kupitia mkoa wa Kagera

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Nianze kwa ku-declare interest kuwa mimi ni mzaliwa wa Mkoa wa Kagera Wilaya ya Missenyi. Katika makuzi yangu hasa baada ya kutoka nje ya mipaka ya mkoa wa Kagera, nimekuwa nikishambuliwa na kutaniwa sana kuhusu UKIMWI kuanzia mkoa wa Kagera.

Hayati Rais Magufuli kwa nyakati tofauti amewahi kunukuliwa akiusema mkoa huko kwamba kila janga baya huanzia mkoa huo. Rais Magufuli awashangaa Kagera kila jambo baya kuanzia mkoa huo

Pia watu mbalimbali katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakiuponda mkoa huo kuhusu kuwa chanzo cha kuleta UKIMWI Tanzania.

IMG_8059.jpeg

Je, ukweli ni upi kuhusu historia ya UKIMWI nchini?
 
Tunachokijua
UKIMWI ni ufupisho wa maneno Upungufu wa Kinga Mwilini, ugonjwa unaosababishwa na virusi.

Virusi vya UKIMWI (VVU) husababisha Upungufu wa Kinga Mwililini (UKIMWI) kwa kushambulia seli nyeupe za damu aina ya CD4 ambazo ni muhimu katika kujilinda dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Kwa sababu kitendo cha kupungua kwa kinga ya mwili hutokea polepole sana, watu wengi wanaweza kuishi na virusi hivi kwa muda mrefu unaoweza kufikia hadi miaka 8-10 kabla wajaugua UKIMWI.

Dalili muhimu zinazoonesha mtu ameshaanza kuugua UKIMWI ni pamoja na kupata magonjwa nyemelezi na kushuka kwa kiwango cha idadi ya CD4 mwilini hadi kufikia 200 au chini ya hapo.

Hivyo, UKIMWI ni matokeo ya mwisho ya mashambulizi ya VVU na sio kila mwenye VVU huwa na UKIMWI hasa kwa watu wenye afya bora, wanaojali afya zao na wanaoanza kutumia dawa za kufubaza virusi mapema.

Takwimu za Ugonjwa huu
Kwa mujibu wa taasisi ya Kimataifa ya UNAIDS, hadi kufikia mwaka 2022, takriban watu milioni 39 duniani walikuwa ni waathirika wa ugonjwa huu ambapo kati yao, watu milioni 1.3 walipata maambukizi mapya.

Aidha, tangu kuibuka kwa ugonjwa huu duniani, takriban watu milioni 85.6 wameathirika huku milioni 40.4 wakipoteza maisha.

Kwa Tanzania, taarifa Rasmi za Serikali zimeonesha uwepo wa maendeleo chanya katika kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa huu.

Imeelezwa kuwa, Tanzania imepunguza maambukizi ya UKIMWI kwa asilimia themanini na nane (88%) kutokana na vifo vitokanavyo na UKIMWI kupungua kwa asilimia hamsini (50%) kutoka vifo 64,000 mwaka 2010 hadi 32,000 mwaka 2020.

Kwa mujibu wa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Tanzania itautokomeza kabisa ugonjwa huu ifikapo mwaka 2023 ambapo hadi sasa 96% ya Watanzania wanaoishi na VVU wanajua kuwa wana maambukizi, 98% ya wanaoishi na VVU wanatumia dawa ARVs, 97% ya wanaotumia dawa wamefubaza makali ya UKIMWI.

Aidha, Julai 13, 2023, Shirika la BBC lilichapisha makala yenye taarifa zinazokazia maneno ya Waziri Ummy. Makala hayo yalisema Tanzania miongoni mwa nchi 5 kutokomeza UKIMWI ifikapo 2030.

Madai ya UKIMWI kuanzia mkoa wa Kagera
Historia ya ugonjwa huu imesimuliwa mara kadhaa na watu wengi ikiwemo Rais Mstaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi alyesema kuwa mgonjwa wa kwanza nchini alipatikana Lukuyu huko Kagera.

Eneo hilo walikuwepo Makahaba waliokuwa wanaletewa Mashati na Madereva wa Malori toka Uganda. Mashati hayo yalikuwa laini na yaliitwa “Juliana” basi na UKIMWI ukapewa jina hilo.

Akifungua semina kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI April 14, 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Leonard Maboko alitoa historia fupi kuhusu chimbuko la ugonjwa wa UKIMWI na kusema uligundulika duniani mwaka 1981 mpaka kufika barani Afrika hatimaye Tanzania ambapo uliingia mnamo mwaka 1983 ambapo mgonjwa wa kwanza aligundulika kutoka mkoa wa Kagera.

Maelezo haya hayatofautiani na yale yaliyotolewa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Ali Hassan Mwinyi.

Tafiti zinasemaje?
Tafiti mbalimbali za afya zimethibitisha pia kuwa mgonjwa wa kwanza aligunduliwa Mkoani Kagera mwaka 1983.

Aidha, andiko maarufu la kiuchuguzi la "War as a social trap: The case of Tanzania" la Francis, Joyce L Ph.D lililochapishwa na The American University mwaka 1994 linathibitisha pia kuwa ugonjwa huu uligunduliwa Mkoani Kagera.

Pia, maoni ya watu wa miaka ile kuhusu asili ya ugonjwa wa UKIMWI nchini yaliyochapishwa kwenye andiko hilo yanaamini UKIMWI uliingia nchini wakati wa vita vya Tanzania na Uganda vilivyopiganwa kuanzia Oktoba 9, 1978 hadi Juni 3, 1979.

Kwa mujibu wa andiko hilo, 31% ya vijana wenye umri kati ya miaka 24-35 Mkoani humo walikuwa na maambukizi ya VVU.

Takwimu hizi hazitofautiani na zile zilizotolewa pia na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi ambaye alisema mwaka 1987, takriban 32% ya wakazi wa Bukoba walikuwa ni waathirika wa UKIMWI.

Hadi kufikia mwaka 1986, ugonjwa wa UKIMWI ulikuwa umeenea katika mikoa mingine nchini.

Kupitia maelezo haya, JamiiForums imejiridhisha kuwa taarifa zinazodai UKIMWI ulianzia Mkoani Kagera zina ukweli
Bila kupima damu kubwa mara tatu kwa kweli sisex na mtu .naogopa sana Hiv.kwanza nimetoboa hadi utu uzima.huu namshukuru MUngu.kosa sio kosa kosa kurudia kosa
 
Ila huko miaka ya mbele nadhani waathirika wataongezeka maana vijana hawaogopi kabisa virusi.wanawaza mimba tu
 
Vijana wanagegedana kavu kavu .hawapimi wala nini.bora wazee tuliosalimika tunajali ila vijana huwaambii kitu
 
Ule mkoa umelaaniwa Ukimwi Kagera Tetemeko Kagera ndege kudondoka Kagera...
Hili nalo mkalitizame
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom