Kwanini mnapenda kuujumu mkoa wa Kagera?

Morning_star

JF-Expert Member
Apr 21, 2018
4,167
11,491
Katika takwimu zote za miaka yote ya makusanyo ya TRA, mkoa wa kagera ni miongoni mwa mikoa iliyojuu katika kuchangia pato la taifa. Kwa report ya hivi karibuni ya TRA, mkoa wa Kagera katika uchangiaji wa pato la taifa imeshika nafasi ya 9. Sasa linapokuja suala la kugawanya pato la taifa kwa kila mwananchi wa Kagera (per capital, GDP), wanauhujumu mkoa wa kagera na kuufanya mkoa miongoni mwa mikoa fukara. Sijui wanapata faida gani kwa uongo huu wa mchana kweupe?

Kwanza kwa wale waliobahatika kukaa au kutembelea mkoa wa kagera, hali ya maisha ya wananchi wake ni bora zaidi saana kuliko mikoa mingi. Hapa tunaongelea malazi, chakula, elimu, barabara, umeme, kiwango cha wasomi, njia bora za mawasiliano ya ardhi na anga, n.k.
Sasa nawaambia nyie nyote mnaotumwa kuuchafua mkoa wa Kagera mshike adabu zenu!!!

Hata mikoa mingine wee nenda, huwezi kukuta mzawa wa kagera amekaa kihasarahasara! Utamkuta yuko vizuri. Sasa huo umasikini mnaotaka kuaminisha umma wa watanzania, mnafanya hivyo kwa faida gani? Wahaya kwanza ni wasomi na wachapakazi wanaotumia brain (akili zao) kupambana na kutoboa! Huwezi kukuta mhaya mtaani akilialia maisha magumu! Pamoja na kutopata mkono wa shirika kutoka serikalini kwa miaka mingi, lakini wananchi wa kagera wameendelea kupambana na kujikwamua huku wakimtegemea Mungu. Mungu ubariki mkoa wa Kagera na watu wake! Mungu ibariki Tanzania kwa ujumla! Amina
 
Kagera tatizo lenu ni kutokukubali ukweli kuhusu hali yenu mbaya kiuchumi. Mtabaki katika nafasi ya mwisho kwa miaka mingi na ni aibu kubwa.
 
Ukweli upi sasa? Tanzania ina mikoa zaidi ya 25+. Katika makusanyo ya TRA mkoa wa kagera ni miongoni mwa mikoa bora 10. Sasa utasemaje mkoa fukara?
 
Katika takwimu zote za miaka yote ya makusanyo ya TRA, mkoa wa kagera ni miongoni mwa mikoa iliyojuu katika kuchangia pato la taifa. Kwa report ya hivi karibuni ya TRA, mkoa wa Kagera katika uchangiaji wa pato la taifa imeshika nafasi ya 9. Sasa linapokuja suala la kugawanya pato la taifa kwa kila mwananchi wa Kagera (per capital, GDP), wanauhujumu mkoa wa kagera na kuufanya mkoa miongoni mwa mikoa fukara. Sijui wanapata faida gani kwa uongo huu wa mchana kweupe?

Kwanza kwa wale waliobahatika kukaa au kutembelea mkoa wa kagera, hali ya maisha ya wananchi wake ni bora zaidi saana kuliko mikoa mingi. Hapa tunaongelea malazi, chakula, elimu, barabara, umeme, kiwango cha wasomi, njia bora za mawasiliano ya ardhi na anga, n.k.
Sasa nawaambia nyie nyote mnaotumwa kuuchafua mkoa wa Kagera mshike adabu zenu!!!

Hata mikoa mingine wee nenda, huwezi kukuta mzawa wa kagera amekaa kihasarahasara! Utamkuta yuko vizuri. Sasa huo umasikini mnaotaka kuaminisha umma wa watanzania, mnafanya hivyo kwa faida gani? Wahaya kwanza ni wasomi na wachapakazi wanaotumia brain (akili zao) kupambana na kutoboa! Huwezi kukuta mhaya mtaani akilialia maisha magumu! Pamoja na kutopata mkono wa shirika kutoka serikalini kwa miaka mingi, lakini wananchi wa kagera wameendelea kupambana na kujikwamua huku wakimtegemea Mungu. Mungu ubariki mkoa wa Kagera na watu wake! Mungu ibariki Tanzania kwa ujumla! Amina
Nimekaa kagera kwa miaka karibia 12

Unachosema mleta mada ni uongo mtupu

Kagera ni miongoni mwa mikoa masikini tanzania lakini pia kuelimu uko nyuma mnoo

Wadada wengi toka huu mkoa ndo wanaongoza kukimbia shule na kukimbilia biashara ya kujiuza mijini hii ndo jadi yao

Vijana wa kiume hovyo sana wengi ni wavivu na sio wachapakazi utapeli na uongo ndo jadi yao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom