Kwa mara nyingine tena mkoa wa Kagera unaachwa mpweke.
Kwa kujenga mnara wa mashujaa mkoa tofauti na Kagera ambapo ndo mkoa unaobeba historia ya vita na Uganda ni kuunyima mkoa huu fursa. Pale Bunazi kuna uwanja wa mashujaa unaitwa Chakaza, kwa nini hiyo miradi ya mnara wa mita 100 na kadhaa unaoenda kujengwa Dodoma usijengwe pale Chakaza?
Cha kushangaza ule uwanja hauna activity yoyote inayofanyika pale zaidi ya kufyekwa tu!
Vita ilileta athari kubwa sana mkoa wa Kagera hasa maeneo ya Missenyi ila hakuna compasation yoyote iliyofanywa na serikali, na hili la mnara wa mashujaa pamoja na hiyo miradi inayoendana na mnara bado serikali inainyima Kagera?
Ukweli hapa ni kwamba aidha wawakilishi wanaotoka mkoa wa Kagera hawalisemei sana hili la vita ya Kagera na wala hawajui athari zilizotokana na vita. Lakini ukweli ni kwamba ile vita iliharibu uchumi wa raia sana ingawa serikali haijawahi kuchukua hatua za makusudi kuwasaidia wananchi kurudi katika hali zao.
Kwa hili la kupeleka mnara wa mashujaa mkoa mwingine wakati nembo ya vita ya Tanzania na Uganda iko Kagera ni kuukosea tena mkoa wa Kagera.