Ukimpata Kiongozi Mwaminifu Maendeleo ni Kazi Rahisi Sana: Mbunge wa Mbogwe, Maganga

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

UKIMPATA KIONGOZI AMBAYE NI MWAMINIFU KATIKA MAJUKUMU YAKE MAENDELEO NI KAZI RAHISI SANA: MHE. NICODEMAS HENRY MAGANGA, MBUNGE WA JIMBO LA MBOGWE MKOANI GEITA

"Mwanzoni kulikuwa na watu siyo waaminifu, wakipewa leseni za uchimbaji Madini walikuwa wanawafukuza kama wanyama. Mimi nilikuwa na upeo wa mambo, ndiyo maana hata Bungeni nilikuwa mwiba kuhakikisha watu wanatendewa haki. Jimboni kwangu wapo watu wamefanikiwa kupitia kupaza kwangu sauti Bungeni" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Chunya na Mbeya kuna watu huwa wananipongeza sana pale ninaposimama Bungeni kuwasemea kwasababu wachimbaji ni Jamii yangu ninayoishi nayo. Jimbo langu ukitoa Kilimo, cha pili ni dhahabu. Mkoa wa Geita ni wa pili kitaifa kuongeza pato la Serikali" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Bunge limekuwepo miaka mingi, walikuwepo wabunge waliokuwa wanapaza sauti kama mimi lakini kuna vitu vilikuwa havifanyiwi kazi. Huwa najitahidi kuhakikisha ninachomueleza Waziri aweze kuelewa kwamba ninaongea kwa kumaanisha" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Nilipokuwa nakuja Bungeni, Jimbo langu lilikuwa halina barabara ya lami, baada ya kumlilipa Mama Samia Suluhu Hassan akanipa KM 5, kwanini nisimpongeze mtu wa namna hiyo. Wilaya yangu ipo katikati ilikuwa haina lami, japokuwa bado nina uhitaji" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Muungwana hushukuru kile anachokiomba kinapofanikiwa. Lazima utoe shukurani, siyo unakuwa mtu wa kulalamika na kuponda tu. Bungeni nilitumia dakika saba kuishukuru Serikali. Sikuwa na vituo vya afya vizuri, Sikuwa na maji. Nilipoingia Bungeni na ukorofi wangu visima vikawa vimejengwa" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Tumepokea mabilioni kwenye Mkoa wetu kwaajili ya kukamilisha maboma ya majengo mbalimbali ya huduma za kijamii. Vitu kama hivi ambavyo vimewasumbua wananchi kwa muda mrefu lazima ushukuru. Tunashukuru wakati tunaendelea kuomba kwasababu shida bado hazijaisha" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Kwenye ripoti ya CAG wakati mwingine kunaonekana madudu. Tunaenda kutengeneza Serikali nyingine, kuanzia Serikali za mitaa. Niwaombe sana Wachungaji na Mashehe wachague watu ambao wanadhani watakuwa wakweli. Ukimpata Kiongozi mwaminifu anayweza kusimamia majukumu yake kama alivyochaguliwa na wananchi maendeleo ni kazi rahisi sana" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Tuliahidi lami, Mjini Masumbwe tumepewa KM 5.6 zimeshajengwa. Tuliahidi Maji kupitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, leo hii visima vinaendelea kujengwa maana kuna gari niliomba bungeni" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Niwaambie Jamii ya watanzania wote tuache tabia ya kulalamika. Kulalamika sana na Mungu unaweza kumchanganya kwaajili ya malalamiko yako mwenyewe. Mwaka 2021 na mwaka 2022 Serikali ilinipanga kwenda nchi za nje, India kwenda kujifunza kwamba wengine waliofanikiwa wanaishije" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"India wanafanya kazi masaa 24/7. Sisi watanzania tuwe na uzalendo wa kufanya kazi, dereva wa Bodaboda endesha na hakikisha unaweka vizuri faida unazozipata, kama mkulima unapofika msimu hakikisha unalima shamba lako ikiwezekana unaazima kwa jirani, kama ni msomi hakikisha unaweka vizuri bajeti yako" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Kinachotutesa sisi Tanzania ni starehe na kuwa na mawazo ya kuhisi tunaonewa kila wakati. Watu wengi wanailaumu Serikali lakini hata kama wangelikuwa ni wao au yeye anaiongoza Serikali yule anayelalamika usingeweza watu kuwakamilishia mahitaji yao yote" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-01-19 at 19.58.11.mp4
    12.4 MB
  • WhatsApp Video 2024-01-19 at 19.58.10(1).mp4
    20.1 MB
  • WhatsApp Video 2024-01-19 at 19.58.10.mp4
    18.1 MB
  • WhatsApp Video 2024-01-19 at 19.58.09.mp4
    17.1 MB
  • WhatsApp Video 2024-01-19 at 19.58.08.mp4
    32.8 MB
NDANI YA CCM HAKUNA MTU wa AINA HIYO WAMEJAA MAFISADI WATUPU
huyu MBUNGE hebu Muuliza kwanini Mbunge analipwa Mshahara wa Mil.16 kwa mwezi ili hali watumishi wengine wanalipwa Laki 350?

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom