Mbunge Nicodemas Maganga: Mbogwe Tumejipanga, Mtumishi Mwizi Hatatoka Salama, Tumejipanga Kuzuia Uhalifu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,901
944

Mbunge Nicodemas Maganga: Mbogwe Tumejipanga, Mtumishi Mwizi Hatatoka Salama, Tumejipanga Kuzuia Uhalifu

Mbunge wa Jimbo la Mbogwe, Mhe. Nicodemas Henry Maganga wakati akichangia Mpango wa Bajeti 2024-2025 ya Shilingi Trilioni 47.4 amesema kuwa Mbogwe wamejipanga kuzuia uhalifu fedha za Serikali.

"Mpango wa Bajeti 2024-2025 unaelezea Shilingi Trilioni 47.4 ambao utakwenda kubadilisha maisha ya watanzania hasa waishio maeneo ya Vijijini" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Katika Jimbo la Mbogwe walikoniamini vipo vitongoji ambavyo havina umeme kabisa, Vijiji 87 wananchi wana matumaini makubwa sana kwamba tutakwenda kufungua Vijiji vyao. Kuna baadhi ya maeneo wananchi hawana vituo vya afya na leo ni miaka 60 ya Uhuru" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Naomba Serikali iweze kuliangalia Jimbo langu la Mbogwe ili iweze kuwasaidia wananchi wangu. Wilaya imekuwa na miaka mingi ikikiamini Chama Cha Mapinduzi lakini ni kweli kuna mahitaji mengi sana bado hayajawafikia" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Nawapa pole wananchi wa Kata ya Isebya kwa kufiwa na Diwani. Napenda kuwatoa wasiwasi wananchi wa Isebya, endeleeni kuamini Chama Cha Mapinduzi kiko kazini na hakuna jambo litabadirika, msimamizi Mkuu wa Jimbo niko Makini kuliko jana kuhakikisha maendeleo yanawafikia" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Waziri wa Mipango na Uwekezaji unasema Umekusudia kwenda kukopa mikopo ya bei nafuu. Mikopo wakati tunakopa inakuwa haina tija. Mfano, unakopa unaenda kujenga Shule, shule itazalisha lini na kuingiza nini" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Ni vyema tufikirie, tunapochukua mikopo tunao wafanyabiashara wa ndani ambapo ukichukua watu waliomaliza elimu ya juu kiwango cha Shahada ukawakopesha kama Serikali kama Milioni 100 akafanya biashara kuiingizia Serikali faida tunaweza kurejesha mikopo vizuri" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Sasa hivi tunadaiwa mikopo mingi ya bei nafuu. Sisi kama Tanzania tuna vyanzo vingi vya Mapato. Tuna Maziwa mengi yanazalisha Dagaa, Samaki. Tuna migodi ina dhahabu. Ni vyema tuangalie. Hii Mipango inafanana na ya nyuma, changamoto ni usimamizi tu" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Tumejadili ripoti ya CAG tumeona kabisa watu wanatuibia. Ni vyema kwenye mpango tuelezee tumejipangaje kudhibiti wezi wanaotubia kwenye Mapato tunayotarajia kuyakusanya. Siyo tu kuongeza vyanzo vya Mapato wakati kwenye usimamizi tunashindwa" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Kwenye mifumo ya Kielektroniki tunaibiwa sana mara zaidi ya tulivyokuwa hatutumi Kielektroniki. Naipenda nchi yangu, Natamani tupige hatua kufikia mwaka 2025 ikiwezekana kila Mbunge awe anatoa ushuhuda kwa kile alichokifanya kwenye Jimbo lake" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Tukiruhusu wizi unaofanyika kwenye POS hata hizi Trilioni 47 hatutazifikisha kwasababu mpango ni kitu kingine na utekelezaji ni kitu kingine kabisa" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Wafanyabiashara wa Mafuta wanakabiriwa na changamoto nyingi. Anakutana na TRA (TIN) , Cheti za Mazingira, Cheti cha OSHA, Tozo, Cheti cha Zimamoto, Leseni ya EWURA, Leseni za Halmashauri, NSSF. Serikali ifikirie inaendaje kumsaidia mfanyabiashara" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Jambo la vikokotoo kwa watumishi ni kilio kikubwa. Watumishi hawajakubaliana kabisa na suala la kikokotoo. Serikali iwasikilize wananchi na kufanya mabadiliko kwenye hili eneo ili watu waishi vizuri kwenye maeneo yao" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Tupo kwenye wakati wa mvua, wakulima wanategemea kupata Mbolea na Mbegu lakini Wizara ya Kilimo ni kama Mipango haijakaa vizuri. Nikuombe Waziri wa Kilimo huu ni wakati wa msimu, wakulima wetu wanahitaji Mbegu, Mbogwe wanahitaji Mbegu na Mbolea" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Nikuombe Waziri wa TAMISEMI aweze kunip watumishi kwenye Halmashauri ya Mbogwe. Wakuu wa Idara wazuri wanaoipenda kazi yao, waaminifu, wenye hofu ya Mungu" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Mtumishi mwizi hatatoka salama Mbogwe, tumejipanga vizuri kuhakikisha tunazuia uhalifu. Watoto wetu wakija kuchungulia makaburi yetu waone kweli kuna watu walikuwa wanaisimamia Serikali. Nitaendelea kusimamia kuhakikisha siikwamishi Serikali ili niweze kufanya kama walivyonituma wananchi" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe
 

Attachments

  • mbogwe 2.jpg
    mbogwe 2.jpg
    33.4 KB · Views: 4
Back
Top Bottom