Ofisi ya Mbunge Mbogwe yakabidhi Kompyuta Shule ya Sekondari Iponya

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,155
1,023
Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Mbogwe, Mkoani Geita, Mhe. Nicodemas Henry Maganga imekabidhi Kompyuta yenye thamani ya Shilingi 1,500,000 katika Shule ya Sekondari Iponya.

Kwa niaba ya Mbunge, Kompyuta zimekabidhiwa na Makatibu wa Mbunge ambaye ni Ndugu Method Nehemia na Ndugu Juma Mohamed walioambatana na Katibu wa Mtandao wa Waraghbishi Wilaya ya Mbogwe, Ndugu Leonard D. Mbigule.

Kompyuta zimekabidhiwa kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Iponya, Mwal. Stephano Kusana ambaye amemshukuru sana Mbunge wa Jimbo la Mbogwe, Mhe. Nicodemas Henry Maganga kwa maono ya kuleta Kompyuta ambapo itasaidia kurahisisha na kuongeza utendaji kazi unahitaji vitendea kazi vya kisasa katika elimu.

"Tunatamani kila Idara iwe na Kompyuta, Tunamshukuru sana Mbunge wetu, Nicodemas Henry Maganga. Tumepitia changamoto hasa wakati wa kuandaa matokeo ya wanafunzi, kumbukumbu ya vitu vya kiofisi ya Mkuu wa Shule na Ofisi ya Taaluma" - Mwalimu Shule ya Sekondari Iponya

"Kimsingi tuna mahitaji ya Kompyuta hapa Iponya, zikipatikana Kompyuta zingine mkatuongezea Ofisi kubwa tano; Ofisi ya Mkuu wa Shule, Ofisi ya Taaluma, Ofisi ya Makamu, Ofisi ya Uhasibu zitasaidia sana. Tunamshukuru sana Mbunge, Mungu ambariki" - Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Iponya, Stephano Kusana.


WhatsApp Image 2024-03-13 at 15.25.35.jpeg

WhatsApp Image 2024-03-13 at 15.25.36.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-13 at 15.25.37.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-13 at 15.25.35(1).jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-03-13 at 15.25.36(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-13 at 15.25.36(1).jpeg
    62.4 KB · Views: 1
Back
Top Bottom