Ukikutana na mazingira haya unafanyaje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukikutana na mazingira haya unafanyaje

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Aine, Jul 12, 2011.

 1. A

  Aine JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mteja anakuja ofisini kwako, nawe unamkaribisha vizuri sana, una concentrate kumsikiliza shida yake mara ghafla simu yake inaita kwa sauti ya juu, anapokea tena bila kuomba msamaha, anaongea kwa sauti ya juu sana kiasi ofisi inakuwa kama genge. Akimaliza kupokea simu unaanza tena kwa mara nyingine kumsikiliza simu yake inaita tena kwa sauti na anaongea kwa sauti kuubwa tena anacheka na huyo anayeongea naye. Sasa unapoteza mood ya kumsikiliza lakini huna jinsi unaendelea kumpa nafasi aeleze shida yake, mara simu yake nyingine inaita anaongea tena this time anatoka nje, wewe unaendelea na kazi yako, anaingia tena, unampa nafasi unamsikiliza. Ila kama mood imepungua kidogo na suala lake anataka umshughulikie haraka.

  Hebu tusaidiane ni serious imenitokea, katika mazingira haya wewe unafanyaje?

  TUSAIDIANE KWA FAIDA YA WOTE WANA JF
   
 2. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,700
  Likes Received: 8,238
  Trophy Points: 280
  Du yani nimemaliza tu kusoma hii thread afu kaingia kwa bahati mbaya huku kwangu na akiwa anaongea na simu...ana bahati baada ya kukata ameapologize!
  Huyo wa kwako unamkalisha chini (ikiwezekana mtengenezee na chai), unamfundisha etiquette kwanza..bonge la lecture afu ndo unampa huduma anayoihitaji!!!
   
 3. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Customer Care!
  Mhudumie mteja bila kumuonesha kwamba umekerwa na zaidi ya yote mpatie simu ili aweze kumalizia maongezi na wateja wake!
  Huwezi jua upeo wa ustaarabu wa wateja wako unaowahudumia, kila mmoja ana yake! si wote wanajua kuheshimu kazi za wenzao, bali wengi wetu tunajua thamani za mahala petu pa kazi.
  Na kama huamini hili nawe nenda ofisini/kwenye biashara yake na ufanye alichokifanya kwako na umtazame usoni uone atakuchukulia vipi...
  Lakini pia wako watu hawajali na wana-'KIHEREHERE" sitoshangaa utakapokuwa unaongea na simu kwa sauti ofisini kwake akawa akikuuliza "NANI HUYO..EHE ANASEMAJE??!!!"
  Tunatfautiana ndio maana tunapaswa kuvumiliana! mkuu saa zingine inabidi kujifunza kuvumilia na kuchukuliana!!!
   
 4. A

  Aine JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Yaani Mentor!! unenichekesha sana umenifanya hasira ziniishe kwa kweli, ahsante sana mkuu
   
 5. A

  Aine JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ahsante sana, najitahidi sana ila kuna wengine kweli kabisa wanaboa sana inabidi uchukuliane nao tu kama unavyosema upeo wa kufikiria unatofautiana ni kweli kabisa
   
 6. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Kabisa mkuu ni heri kusema kuliko kunyamaza! kuelimishwa na kuelewa ni jambo moja. na kuelimishwa na utoelewa ni jambo jingine!
  Ningelipenda amuelimishe baada ya kwenda kwake na utenda kama alivyotenda ofisini kwa mwenzake ili apate mfano hai maana sisi watanzania duh! unaweza ueleweshwa ukatoka hapo na kuanza "jamaa nimeenda ofisini kwake anajifanya muchknow sana yule.. mara ooh usiongee na simu ofisini nasi tuna dili kwenye simu....."
   
 7. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  nashukuru pia mkuu karibu tena. Yaani inabidi hakuna njia, katika kutoa huduma inabidi ushuke, ndio maana inatupasa kuwa na maji ya kunywa ofisini ili kupunguza majoto na mapresha ya watu aina hizo! saa zingine afadhali ya huyo wa simu anaeongea tu na saa zingine kutoka nje... je yule anaekuja akaongea na simu ofisini kwako akanyanyuka kitini na kukaa kwenye meza yako ya ofisi huku akifoka na kugonga meza???
  Ila ndio sisi hao!! Kama ilivyo hakuna adabu majumbani na maofisini na kwenye jamii tuko hivyohivyo!
   
 8. A

  Aine JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hiyo ishanitokea mkuu, mteja kaongea na simu mara anasimama, mara anabadilisha kiti anakaa kingine, na kutukana juu hadi unahisi atakurukia, yaani inabidi uwe mpole tu, yaani kazi kweli kweli
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  Jul 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Mteja ni mfalme....
   
 10. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,700
  Likes Received: 8,238
  Trophy Points: 280
  Haha..nadhani itategemea na jinsi utakavyoitoa hiyo lecture! Unaeza iweka kama joke pia..lakini ujumbe ukamfikia.
  Ama na wewe ujifanye unapokea simu...
  Tafuta njia yoyote ile ujumbe umfikie, ahta kama itamuuma- ili iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia kama zake!
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Hiyo mimi imenitokea saana

  nilichofanya ni kuweka tangazo mlangoni

  huruhusiwi kuongea na simu while upu ndani ya ofisi yangu...

  Mtu akijaribu tu,,
  namkunjia uso huku namuonyesha tangazo au namuonesha mlango.....

  Siipendi hii tabia,
  mwingine simu ina mchiriku au taarabu,na anaongea kama yuko mnadani....
  Mimi huwa nawaonesha mlango kwa ishara tu,huku nimekunja uso...
   
 12. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Simu yako haina "option" ya ku-fake call?

  Maana mimi binafsi ninge "activate 6 fake calls" na ile anaingia na mimi naanza kupokea na kuongea mpaka angeamua kuondoka!
   
 13. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,700
  Likes Received: 8,238
  Trophy Points: 280
  Hata Mfalme **** alikuwa Mfalme...
  cha maana hapo kama umemshtukia ni mfalme **** type then na wewe unamtreat ki-****, kama yule fundi wake na kanzu ya ajabu!lol
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  sio wote ni wateja
  wengine yeye ndo ana shida..
  Sijui ndugu yangu hana kazi,au amekuja kukopa
  na kero juu
   
 15. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Wakuu!
  hii inategemea na aina ya ajira/biashara mlizonazo! Kama hamuwahitaji wateja ni rahisi kufanya hivyo msemavyo (na hili linafanywa sana na maafisa wa serikali) lakini kwa wale wanaojua kwamba mteja huyo/hao ndio wanaosababisha mwisho wa mwezi aonane na mlipafedha sidhani kama ni rahisi kumuonesha mteja mlango alioingilia. Na ikitokea hivyo, ukapatikana unamuonesha mteja mlango alioingilia nadhani ni wakati sahihi kabisa wa kuwajibishwa.
  Na katika hili ndipo wachagga na wahindi wanapotuzidi mbali katika kazi na biashara. kwani wanajali na kumthamini mteja kwa kadri ya uwezo wao.
   
 16. A

  Aine JF-Expert Member

  #16
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Issue itakujaje, boss wako akiliona hilo tangazo na wakati yeye ofisini kwake hajaweka tangazo kama hilo!!
   
 17. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Wafalme wengine wanaturudisha tuliko toka kwenye utumwa.
   
 18. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #18
  Jul 12, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  zungumza na bosi wako
  huo utaratibu wa kawaida mtu kutoruhusiwa kuongea na simu ofisi za watu

  mbona hospitali za private tunalipa mahela mengi
  na matangazo hayo yapo?????????

  Hapa ni ustaarabu tu,sio kupoteza wateja
   
 19. Baby msangi

  Baby msangi Member

  #19
  Jul 12, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ungemwambia atoke nje amalizane na simu zote then ndo muanze maongez.kama ataona maongezi yenu ni muhimu basi atazima simu then mtaendelea na maongez.
   
 20. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #20
  Jul 12, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  kanuni za CUSTOMER CARE Kuu mbili.CUSTOMER IS A KINGCUSTOMER IS ALWAYS RIGHT. KM wewe ni mtu wa customer care ukizitambua hizi kanuni utaenjoy kazi yako na wala hutasononeka. mteja ni mfalme lazima abembelezwe asikilizwe kwa namna yeyote ile. ktk dunia ya ushindani wa kibiashara wa kwelikweli you cant afford to loose a customer! hii kibongobongo ni ngumu sana kutekelezeka has kwenye institutions na maofisi ya serikali ambako customer care ni almost negligible hakuuuuna kabisa Mteja kila wakati yupo sahihi, yeye hajui kuhusu huduma zenu, anachokijua juu yenu ndicho sahihi kwake, hapaswi kuambiwa mwongo au hapana au nani kakuambia. atleast siku hizi ukiingia kwenye ma bank binafsi utachangamkiwa na smile lkn si nmb na crdb sijajua nbc. kuna dizaini mbaimbali za wateja vilevile na jinsi ya kuwa handle.
   
Loading...