Ukikutana na mazingira haya unafanyaje

Mteja anakuja ofisini kwako, nawe unamkaribisha vizuri sana, una concentrate kumsikiliza shida yake mara ghafla simu yake inaita kwa sauti ya juu, anapokea tena bila kuomba msamaha, anaongea kwa sauti ya juu sana kiasi ofisi inakuwa kama genge. Akimaliza kupokea simu unaanza tena kwa mara nyingine kumsikiliza simu yake inaita tena kwa sauti na anaongea kwa sauti kuubwa tena anacheka na huyo anayeongea naye. Sasa unapoteza mood ya kumsikiliza lakini huna jinsi unaendelea kumpa nafasi aeleze shida yake, mara simu yake nyingine inaita anaongea tena this time anatoka nje, wewe unaendelea na kazi yako, anaingia tena, unampa nafasi unamsikiliza. Ila kama mood imepungua kidogo na suala lake anataka umshughulikie haraka.

Hebu tusaidiane ni serious imenitokea, katika mazingira haya wewe unafanyaje?

TUSAIDIANE KWA FAIDA YA WOTE WANA JF

ushukuru Mungu karudi na umempa huduma, je angekwambia kaja kukusalimia tu? ungechukua hatua gani?
 
Back
Top Bottom