Ukikutana na kikwete, utamshauri nini?

Ukikutana na kikwete, utamshauri nini?

1. "akili zake achanganye na za viongozi waadilifu walioko chini yake, aachane na za mbayuwayu".

2. Achukue ushauri wowote mzuri aufanyie kazi hata kama unatoka kwa wapinzani wake

3. Akiona moshi ajue kuna moto na dalili ya mvua ni mawingu, ajipange sawa sawa, asome alama za nyakati.
 
Naona hali ya utawala wa JK inazidi kuwa mbaya, mambo haendi, mfumuko wa bei uko juu, viongozi wanalipuka, askari wanaua, wanafunzi wanafeli masomo, mishahara inachelewa. wafanyakazi hawajitumi, rushwa inazidi kuota mizizi, viongozi ni waongo,

Ikitokea ukapata nafasi ya kuonana na JK katika hali hii utamshauri nini.

Atuombe radhi kwa kutudanganya na kauli mbiu zake za kutongozea!

----Maisha bora kwa kila Mtanzania.....
----Ari mpya Nguvu mpya na Kasi mpya...
----Ari zaidi, Nguvu zaidi na Kasi zaidi.....
nk. nk. nk.
 
Aachie ngazi haraka sana yeye na viongozi wake wakuu wote. Turudi kwenye drawing board tufanye uchaguzi mpya!!!

Na hapo ndipo kwenye tatizo anawekuwa anataka kuachia ngazi ila tatizo ni kwamba serikali yake haina pesa za kufanya uchaguzi kwa sasa, pili mtamshitaki..labda mmhakikishe kama hamta mshitaki kwa wezi wake pamoja na washirika wake..
 
Aache ngono
unajua kuna dhambi zingine zinazalisha dhambi hata haya yanayotokea yana chanzo chake sasa nashauri akiweka hili sawa hope mengine yatafutika
 
Naona hali ya utawala wa JK inazidi kuwa mbaya, mambo haendi, mfumuko wa bei uko juu, viongozi wanalipuka, askari wanaua, wanafunzi wanafeli masomo, mishahara inachelewa. wafanyakazi hawajitumi, rushwa inazidi kuota mizizi, viongozi ni waongo,

Ikitokea ukapata nafasi ya kuonana na JK katika hali hii utamshauri nini.

Sababu za watanzania kuwa maskini ni nini
Umuhimu wa kutumia raslimali tulizo nazo kuwaletea maendeleo watanzania
Umuhimu wa kuwa na dhana ya kuwajibika miongoni mwa viongozi wake maana wanaboronga na bado wanaendelea na madaraka
Umuhimu wa kuwa wakweli kwenye kupambana na rushwa kwa vitendo na sio maneno
Umuhimu wa kuhakikisha ufisadi unatoomezwa kwa vitendo na sio maneno
Atekeleze ahadi zake basi hata kama ni kwa asilimia tano sio kutuacha mwaka unakatika hakuna hata harufu ya utekelezaji wa kile alichoahidi
 
Naona hali ya utawala wa JK inazidi kuwa mbaya, mambo haendi, mfumuko wa bei uko juu, viongozi wanalipuka, askari wanaua, wanafunzi wanafeli masomo, mishahara inachelewa. wafanyakazi hawajitumi, rushwa inazidi kuota mizizi, viongozi ni waongo,

Ikitokea ukapata nafasi ya kuonana na JK katika hali hii utamshauri nini.
Ningemshauri atengeneze baraza jingine la mawaziri umri kati ya 35-55 halafu serikali itekeleze yote kadri ya uwezo utakavyopatikana yale yote yatakayotolewa na wataalamu wetu wa vyuo vyetu vikuu. Asifanye jambo bila wao kumhakikishia linawezekana na litakuwa na tija. Wataalam wetu watutengenzee sera zitakazolipeleka taifa letu mbele! Ni hayo ndiyo ningemshauri afanye. Nawasilisha.
 
Aache longolongo, U-Rais si jambo la kukimbilia!
 
hii mbona kawaida mzee....kama unabisha nenda kawaulize the same question wazazi wa wale walio uwawa pale tarime utagundua hasira walizonazo.
 
Ningemshauri atengeneze baraza jingine la mawaziri umri kati ya 35-55 halafu serikali itekeleze yote kadri ya uwezo utakavyopatikana yale yote yatakayotolewa na wataalamu wetu wa vyuo vyetu vikuu. Asifanye jambo bila wao kumhakikishia linawezekana na litakuwa na tija. Wataalam wetu watutengenzee sera zitakazolipeleka taifa letu mbele! Ni hayo ndiyo ningemshauri afanye. Nawasilisha.

Kwani mkuu unafikiri hazipo
Zipo ila zinakosa wa kuzifuatilia kila mtu yuko mbio kutayarisha maisha yake ya baadae ya kustaafu na kujilimbikizia mali kwa sana
 
Ningemshauri atengeneze baraza jingine la mawaziri umri kati ya 35-55 halafu serikali itekeleze yote kadri ya uwezo utakavyopatikana yale yote yatakayotolewa na wataalamu wetu wa vyuo vyetu vikuu. Asifanye jambo bila wao kumhakikishia linawezekana na litakuwa na tija. Wataalam wetu watutengenzee sera zitakazolipeleka taifa letu mbele! Ni hayo ndiyo ningemshauri afanye. Nawasilisha.
kwani kuna wmaziri wangapi ambao hawako kwenye hiyo miaka, CCM ni CCM hata ukiteua mawaziri walio zaliwa leo ukiwa na maana ya damu changa bado ngoma ni ile ile...Mwangalie Masha alivyo kuwa,Mwangalie Ngereja, Mwangalie Nape.....
 
Aache longolongo, U-Rais si jambo la kukimbilia!
kweli mkuu umeongea unajua Kikwete aliutaka uraisi kwa udi na uvumba matokeo yake ndiyo haya kila kitu kime halibika alikuta hazina inapesa za kutosha leo hii hoi......
 
Na sijui akiondoka kutakuwaje maana jamaa kabla ya mwaka wa bajeti kuisha yeye fungu lake la safari za nje lishaisha
 
Lakini si alishamuomba Dr Slaa amuachie kipindi chake amalizie,ili wasijepinduanapinduana.
Maana leo kwake kesho kwa Dr Slaa
Mimi nitamshauri atekeleze angalau ahadi moja ya nguvu kama Daraja la Kigamboni.
 
1. "akili zake achanganye na za viongozi waadilifu walioko chini yake, aachane na za mbayuwayu".

2. Achukue ushauri wowote mzuri aufanyie kazi hata kama unatoka kwa wapinzani wake

3. Akiona moshi ajue kuna moto na dalili ya mvua ni mawingu, ajipange sawa sawa, asome alama za nyakati.
-Kikwete alisha sema ni mbishi sana huwa hakubali ushauri uwe wa daktari, Mlizi wake nk hivyo la rangi ya blue kwa kikwete sahau
-Rangi nyekundu naona unamfumbia sana kifupi ni kwamba achie ngazi amepwaya sana tena sana...
 
Lakini si alishamuomba Dr Slaa amuachie kipindi chake amalizie,ili wasijepinduanapinduana.
Maana leo kwake kesho kwa Dr Slaa
Mimi nitamshauri atekeleze angalau ahadi moja ya nguvu kama Daraja la Kigamboni.

Mkuu mstari wa umaskini unazidi kushuka kw awatanzania hata kupata mlo mmoja ni issue kwa sasa
Akitekeleza hilo yaani inakuwa kama kumwaga chumvi kwenye kidonda
 
Na sijui akiondoka kutakuwaje maana jamaa kabla ya mwaka wa bajeti kuisha yeye fungu lake la safari za nje lishaisha
Sipati picha raisi ajae maana atakuta hazina kweupe na madeni juu...
 
Merytina 02:12 PM Today
aamishie ikulu msikitini kwa mtoro Reply Report Post Thanks
Merytina hapo umeua mtu wangu duh!
 
Back
Top Bottom