Ukifanya Mapenzi mara kwa mara unakuwa hatarini kupata UTI

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Screenshot_2024-01-15-08-14-59-933_com.instagram.android-edit.jpg

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke Dkt. Ikrah Abdallah ametoa wito kwa Jamii kutofanya tendo la ndoa mara kwa mara badala yake tendo hilo linaweza kufanyika angalau mara Tatu (3) au Nne (4) kwa wiki ili kuondokana na hatari ya kupata UTI

Dkt. Ikrah ametoa ushauri huo wa kitaalamu leo, Jumatatu Januari 15.2024 wakati akifanya mahojiano maalumu Clouds FM kupitia Kipindi cha Power Breakfast

"Tendo la ndoa likifanyika mara kwa mara na lenyewe linamfanya mtu kuwa katika hali hatarishi ya kupata UTI, kwa Wanawake vile vijidudu kutoka pale nje na kuingia ndani vinakuwa katika hali ya haraka zaidi" -Dkt. Ikrah

"Angalau Watu wafanye tendo la ndoa mara Tatu (3) au Nne (4) kwa wiki na mara baada ya kufanya tendo la ndoa tabia ya kutoa haraka kwenye kukojoa au kutoa haja ndogo ni tabia nzuri sana ya kukufanya usipate UTI mara kwa mara" -Dkt. Ikrah
 
Madaktari wanatuvuruga sana wenyewe kila siku wako vinenani huku wanataka ndoa zetu ziteketee!! Yani mimi dude limenisimama nifatishe hizo mara nne kwa wiki, thubutu!!!
 
Why? Mi nilidhani ni kutokufanya ngono kwa watu tofautitofauti kumbe ni kwa mwenzangu? Hapa hakuna cha mara tatu au nne kwa wiki, ni kila siku shoo inapigwa labda tuwe hatuko pamoja kitandani au kuna udhaifu wa mwili. Show ni kama chakula tu hamu huja kila muda mwili ukihitaji napiga hata mara tatu kwa siku
 
Kikubwa usafi, na unywaji maji vizuri, matunda na mlo kamili

Sehemu tuendako jisaidia - baadhi ya maeneo yanachangamoto, waweza bana mkojo kutoka mbezi kibanda cha mkaaa hadi posta ... lengo lako ni kwenda kutumia choo kisafi ukiaminichoo

Kutotumia dawa kwa usahihi (kukatisha dozi) nako ni tatizo
 
Back
Top Bottom