Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,473
- 13,629
MkuuTravic, umegusa mule mule. JPM alikuwa anamaanisha kitu ambacho wazungu wanakiita guts, uwezo wa kuthubutu kufanya kitu bila ya kusikiliza maoni yatakuwa vipi.Nilisikiliza neno kwa neno hotuba ya Rais JPM huko Ukerewe.
Pamoja na mambo mengi aliyoyahutubia, naona habari ya mjini ni ishu ya kusema alimchagua Waziri Mpina kwa sababu naye ni kichaa kichaa kama yeye.
Kwanza, kiu ya siasa nchini ni dhahiri ipo juu sana. Watu wanatamani kufanya siasa za kejeli na propaganda kwa namna ile ile iliyozoeleka miaka ya nyuma. Hii kiu haitaisha, mpaka pale Rais atakapoamua kuruhusu mikutano ya kisiasa iendelee kwa mtindo uliozoeleka.
Pili, kauli ya ukichaa imechukuliwa out of context. Na ndivyo propaganda zilivyo. Kwa ambaye hakutazama hotuba nzima, ni rahisi kuchotwa na maneno yanayoendelea mtandaoni kwamba Rais 'amekiri' kuwa yeye ni kichaa na anaowateua nao ni vichaa.
Hata hivyo, Usahihi upo kwenye context, kwamba Rais alizungumzia ukichaa kumaanisha kiongozi mwenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu kwa maslahi mapana ya taifa, akirejea uamuzi wake wa kukamata meli yenye samaki waliovuliwa kiharamu kipindi akiwa waziri wa Uvuvi.
Kama watu wanafanya utani, sawa. Lakini kama kuna wanaoipa uzito hiyo propaganda kwa kuiamini, nayo ni sawa tu. La muhimu, ieleweke kuwa ni propaganda.
Naamini Rais hawezi kupaniki kwenye hilo!
Kuvunja nyumba zote ambazo zimeshavunjwa tangu awe waziri sio jambo ambalo linahitaji akili ya upole, hata kidogo.
Maamuzi magumu yanahitaji mtu ambaye muda wowote anakunja uso, ukicheka na wabongo ukisikiliza siasa zao za demokrasia na uhuru wa maoni, utajikuta hufanyi kitu.
Nchi zetu za kiafrika kwa uzoefu wa tangu zipate uhuru, hazihitaji mtu wa kuremba, hazihitaji mtu wa kumsikiliza kila mtu.
Ni lazima kichwa kiwe na chembe ya ukichaa ili unachotaka kifanyike kiweze kwenda kwa wakati unaotakiwa.
Muda haumsubiri mtu, muafrika kwa bahati mbaya sana haujui huo ukweli.