Ukiandika wosia, Je? utamuonyesha jinsi ulivyoigawanya mali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukiandika wosia, Je? utamuonyesha jinsi ulivyoigawanya mali

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Shishi, Aug 6, 2009.

 1. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135


  Interesting...hivi are u supposed to share the details of your will na mkeo? and vice versa? ama kama mke anayo mali iloyoko katika jina lake, mume ana haki gani hapo? ama yatakuwa yale mambo ya surprise za JM na Diana Ross??

  mnapoandika will mnashirikiana ama ni kimya kimya tu? jamani haya mahusiano ya usiri mwigngi tu, kama mumeamua till death do us part kwa nini kuwe na usiri???/ mi nashindwa kabisa kuelewa.
   
 2. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mods nisaidie ku-edit title isomeke Ukiandika!!! mambo ya copy paste haya aahahhahah
   
 3. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...wanasheria na wanazuoni mnasemaje? mnh, kwakweli sijawahi sikia mtu anashirikiana na mkewe kuandika wosia, few nimesikia wanashirikiana na wakili/mwanasheria.

  Bahati mbaya katika maisha ya kileo, kuandika wosia ni kama kumepitwa na wakati, wengi huona kama wanajichuria na kifo. Hata kwenye kuyajadili mambo haya, wachache sana wanaojitokeza kuchangia.

  Binafsi, sijaona vibaya kuandika wosia wangu kabla. Kama kuna mabadiliko, una review na kuifanyia marekebisho. Bila Kumshirikisha Mke ofcourse,... yanini kujitafutia kufunikwa uso na mto, au kuminywa pua (pumzi) nikiwa usingizini bure?
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,522
  Likes Received: 81,906
  Trophy Points: 280
  Hayo ni maamuzi ya mke na mume. Mnaweza kabisa kuandika will ya kila mmoja wenu kwa ushirikiano au kila mtu akaandika kwa siri bila mwenzie kujua kilichoandikwa katika will ya mwenzake.
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kisheria haulazimishwi kuonyesha wosia wako. Inakua kati ya wewe na mwanasheria wako na inatunzwa mpaka hapo itakapo hitajika. Ina wezekana hata watu wengine wasi fahamu kama unao wosia au la. Kumuonyesha mumeo/mkeo wosia wako ni chagua lako mwenyewe kutegemeana una uhusiano gani na mwanandoa mwenzio. Pia ina tegemea na wewe mwenyewe kama hauna kitu cha kuficha.
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  MwanaFalsafa..uko sahihi kabisa mwanzoni ulivyosema...
  1.Wosia kisheria ni hati inayotakiwa kuwa siri kati yako unayeandika na mwanasheria au mashahidi wanaotambulika kisheria kufuatana na utaratibu unaoutumia kuandika wosia wako.Kumbuka kuna wosia wa maandishi na ule wa mdomo.
  2.Kisheria, mnufaika hapaswi kujua kilichomo ndani ya wosia.

  3.Hamuwezi kuandika wosia wa pamoja hata kama ni mke na mume.

  4.Kuna kitu pia watu wengi hawajui.Unaweza kugawa mali zako ukiwa hai kama unaogopa kuandika wosia kwa kuchelea kufa upesi.Hii itaepusha kuleta vurugu na manung'uniko pale utakapoaga dunia huku umeusia mali yako kwa upendeleo japo sheria inaruhusu ugawe upendavyo.
   
Loading...