CCM: Azimio La Zanzibar Lina Faida Gani?

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
Kama mwanachama hai wa CCM, natambua Mwongozo Wa mwaka 1981 katika sehemu ya (57) ibara ya (5) unatamka kwamba: "Kujikosoa na kukosoana ni silaha ya Mapinduzi". Katika sehemu ya (59), Mwongozo unazidi kuhimiza kwamba:"Suala la kukosoa, kujikosoa na kukosoana lina sura kadhaa. Kwanza linataka wanachama na viongozi kuwa tayari kusema kweli katika vitendo vyao na kukubali kuambizana ukweli. Pili, linataka wanachama na hasa viongozi wawe tayari kukosolewa bila kuhamaki na inapobidi kukubali kujirekebisha. Tatu ni kuwa Chama chenyewe katika vikao vyake vya ngazi mbalimbali kuwa na utaratibu wa kujikosoa." Hivyo mwongozo wa CCM unanipa haki zote, kama mwanachama, kukikosoa chama changu cha CCM kila inapobidi.

CCM ni mwasisi wa Azimio La Arusha na pia ni mwasisi wa Azimio la Zanzibar. Baada ya miaka 50 ya uhuru, maazimio haya yanawajibika moja kwa moja juu ya hali za maisha ya watanzania kiuchumi na kijamii. Wakati Azimio la Arusha lilidumu kwa miaka 18 (1967 – 1985), Azimio La Zanzibar limedumu kwa miaka 20 (1992 – 2012). Pia, tofauti na Azimio La Arusha ambalo liliungwa mkono na wananchi wengi vijijini na wasomi Chuo Kikuu, Azimio La Zanzibar lilipitishwa kimya kimya na CCM-NEC Zanzibar, jambo ambalo hata Mwalimu Nyerere lilimkuta kwa mshangao. Ni kama vile CCM ilikuwa inasubiri Nyerere ang'atuke Uenyekiti CCM Taifa Mwaka 1990; Vinginevyo nini ilikuwa ni sababu ya msingi ya kuendelea na Azimio La Arusha kwa miaka 7 zaidi (1985-1992)?

Azimio La Zanzibar la mwaka 1992, liliwezesha CCM na serikali yake kuanza rasmi kuitumikia ITIKADI YA ULIBERALI KIVITENDO, INGAWA KINADHARIA, ITIKADI YA CCM KWA MUJIBU WA KATIBA YAKE YA SASA BADO NI YA UJAMAA. Mbali na hiki KIGEUGEGU, mabadiliko muhimu kwa mujibu wa Azimio La Zanzibar ni kwamba, tofauti na Azimio la Arusha, VIONGOZI WENYE DHAMANA YA UMMA sasa wamepewa rukra rasmi ya kupokea mshahara zaidi ya mmoja, kumiliki nyumba za kupanga, na kuwa na hisa katika makampuni binafsi. Azimio La Zanzibar halikufanya jitihada yoyote kurekebisha masharti haya ya uongozi wa umma pamoja na umuhimu wake. Badala yake iliyafuta kama yalivyo. Hii ina maana kwamba kuanzia mwaka 1992, ikawa ni ruksa kwa viongozi kutumia nafasi zao za uongozi kwa maslahi binafsi. Nadiriki kusema hivi kwa sababu Azimio La Zanzibar halina masharti yoyote ya uongozi, pamoja na kwamba uongozi bado unaendelea kuwa ni ‘dhamana'. Hii ni ajabu kwa sababu katika mazingira yoyote yale, hakuna dhamana isiyokuwa na masharti.

Maazimio ya Arusha na Zanzibar yamegawanya watanzania kimtazamo katika makundi mawili. Kundi la kwanza linahimiza haja ya CCM kurudia baadhi ya mambo muhimu ndani ya Azimio La Arusha kama njia ya kurudisha uadilifu wa uongozi, hasa katika kusimamia maslahi ya taifa. Hoja nyingine ya kundi hili ni kwamba, Azimio La Arusha lilisaidia Watanzania Kujitambua, liliwapatia Nia kama taifa, na Ushupavu, na haya ndio yaliyochochea ongezeko la juhudi miongoni mwa watanzania, katika ujenzi na ulinzi wa taifa lao, kwa manufaa yao na ya vizazi vijavyo.

Kundi la pili ni lile linalounga mkono Azimio La Zanzibar huku likipinga lile la Arusha. Kundi hili lina hoja kadhaa lakini hoja ya msingi ni kwamba Azimio la Arusha halikuwatendea haki watanzania na ndio chanzo kikuu cha umaskini wao leo. Msisitizo wao ni kwamba Azimio la Arusha liliwanyima watanzania uhuru wa kushiriki katika shughuli za kiuchumi kwa kutumia uwezo na vipaji vyao walivyojaliwa ili kujitafutia rizki bila ya kuingiliwa na nguvu yoyote nje ya nguvu ya soko. Pia kuna hoja muhimu kwamba, haikuwa sahihi kwa TANU/CCM kuwanyima watanzania haki ya msingi kabisa ya ‘umiliki binafsi wa mali'.

Nia ya kuleta mjadala huu ni kubadilishana mawazo juu ya masuala haya muhimu, huku nikilenga zaidi katika kuchokoza mada. Mwalimu alipokuwa anan'gatuka uenyekiti wa CCM mwaka 1990 alitoa wosia ufuatao: "Mimi Nang'atuka Lakini Naendelea Kuamini Kuwa Bila CCM Madhubuti, Nchi itayumba."

Swali la ujumla la mada hii ni je:

  • Utabiri wa Mwalimu kuhusu CCM kuyumba una uhusiano gani na utekelezaji wa Azimio La Zanzibar?
Lakini maswali mahususi ni haya yafuatayo:

1. Iwapo Azimio La Zanzibar lina manufaa kwa watanzania walio wengi, kwanini mchakato wake ulifanyika kimya kimya bila ya kuwashirikisha wanachama wengi?

2. Iwapo Azimio La Zanzibar lina manufaa Kwa watanzania walio wengi, kwanini CCM bado haipo wazi kuhusiana na utekelezaji wa Azimio hili kwa mujibu wa Katiba ya sasa ya chama ambayo bado inatamka itikadi yake kuwa ni ya Kijamaa?

3. Ikilinganishwa na Azimio La Arusha lililoishi kwa miaka 18 (1967 – 1985), Je, miaka 20 ya Azimio La Zanzibar imewaletea watanzania ‘walio wengi' manufaa gani?

4. Je, kwa kuzingatia mahitaji ya sasa ya watanzania ‘walio wengi', Azimio La Zanzibar lina mazuri na mabaya gani?

5. Je, kuna mambo gani ndani ya Azimio la Arusha ambayo bado yana manufaa kwa watanzania ‘walio wengi' katika nyakati za sasa?

Kama nilivyosema awali, nia yangu kuu ni kuchokoza mada. Ningependa nianze na majibu aliyoyatoa Rais Benjamin Mkapa mwaka 2005, kwa mwandishi mmoja wa Uingereza aitwaye Jonathan Power. Mwandishi huyu alimuuliza Mh. Mkapa swali lifuatalo:

"Mh. Rais, iwapo Mwalimu Nyerere anafufuka Leo, Kwa mtazamo wako, angezungumziaje hali ya sasa ya Tanzania?"

Mh. Mkapa alimjibu hivi:

"Mwalimu angesema nimegawa rasilimali nyingi sana ambazo awali zilikuwa chini ya umma. Lakini pia Mwalimu angekasirika sana kwamba nimejenga tabaka kubwa la kibepari lenye mafanikio na linalozidi kustawi."
Mh. Mkapa alikuwa mkweli katika hili kwani hiyo ndiyo hali halisi chini ya soko huria na Azimio La Zanzibar. Kama itakumbukwa vizuri, moja ya hoja kubwa za kulizika azimio la Arusha mwaka 1992 ilikuwa ni pamoja na kwamba, miaka 18 ya azimio la Arusha ilipelekea hali za watanzania wengi kiuchumi na kijamii kuzorota, hivyo kulikuwa na muhimu wa kurekebisha udhaifu huo. Ndipo Azimio la Zanzibar likabuniwa kama tiba, baada ya Azimio la Arusha kuonekana halikuwa tiba bali ugonjwa uliokuwa umeenezwa kwenye jamii kwaa miaka 18. Watanzania wamekuwa chini ya tiba ya ‘Azimio la Zanzibar' kwa muda wa miaka 20 sasa.
Je, kwanini Mwalimu aliona Azimio La Arusha ndio dawa ya Umaskini?

Dawa ilikuwa katika neno ‘mapinduzi' chini ya TANU/CCM, mapinduzi ambayo yalilenga kuwakomboa watanzania walio wengi kutoka kwenye minyororo ya unyonyaji uliotokana na miaka zaidi ya 50 ya kuwa chini ubeberu na ukoloni. Ndio maana dhamira kuu ya Azimio la Arusha ikawa ni kumtokomeza ‘bwanyenye' ili kuisafishia njia jamii mpya iliyotarajiwa kushamiri na kustawi katika mazingira ya usawa - kichumi na kijamii. Ni dhahiri kwamba, bila ya Mwalimu kuanzisha mapinduzi yale, basi angekumbana na mapinduzi ya umma, kwani umma ulikuwa na kiu ya ahadi nyingi zilizotolewa na TANU wakati wa harakati za uhuru.

Mwalimu alikuwa na wakati mgumu katika hili kwani hata baada ya uhuru, ardhi iliendelea kuwa ndiyo njia kuu ya uzalishaji, hivyo uchumi. Mwaka 1961, jumla ya wahindi na wazungu Tanganyika ilikuwa karibia 2% ya idadi ya watu wote, huku wahindi na wazungu wakimiliki karibia 50% ya jumla ya ardhi yenye rutuba Tanganyika. Kwa upande mwingine, Watanganyika weusi idadi yao ilikuwa ni 98% ya watu wote, na wao walimiliki karibia 50% ya ardhi yenye rutuba. Hivyo, mantiki na uhalali wa Azimio La Arusha vilichangiwa na uhalisia huu.

Pamoja na hayo, wapo waliopinga Azimio hili, wengi ikiwa ni wenzake na Mwalimu ambao walikuwa na matarajio tofauti juu ya matunda ya uhuru. Historia inaelezea jinsi gani baadhi ya viongozi hawa walivyoanza kujijenga zaidi na wahindi na wazungu kupitia nafasi zao za uongozi, badala ya kujijenga kwa wananchi. Mwalimu hakusita kulisemea hilo katika kitabu chake cha TANU NA RAIA mwaka 1962, mwaka mmoja tu baada ya uhuru:

[…kilichokuwa kikituuma ni kwamba ubwana na ufahari wa wazungu waligawana wenyewe tu, bila kutugawia sisi pia; baadhi yetu hatukuwa tunadai uhuru ili uwapunguzie watu wetu mzigo huu wa ubwana na ufahari, bali tamaa yetu ilikuwa ni kukalia viti vile vya ubwana na ufahari. Tamaa yetu haikuwa kushika vyeo tu, vilivyokuwa vimeshikiliwa na wazungu hapo zamani, tulitaka na mishahara pia iliyokuwa ikifuatana na vyeo hivyo, bila kujali kama watu wetu wanaweza kulipa mishahara hiyo, bila kujali maisha ya watu wetu…"].

Pia, ni muhimu tukakumbuka kwamba, wakoloni hawakumwendeleza mtu mweusi. Kabla ya uhuru, watu weusi walikuwa ni vibarua mashambani, huku wachache wakiwa na ajira za ngazi ya chini katika serikali ya mkoloni. Vinginevyo mkoloni alitumia muda wake mwingi kujenga wahindi kibiashara na kijasiriamali kwa kuwapatia fursa nyingi kama vile uwakala wa biashara n.k. Ndio maana mwaka 1961 wakati Tanganyika inapata uhuru, hapakuwa na idadi kubwa ya watu weusi waliokuwa na uzoefu au shughuli yoyote ya kijasiriamali. Wengi ilikuwa ni wahindi. Kulikuwepo na baadhi ya viongozi serikalini waliotamani kutumia nafasi zao za uongozi kushirikiana na wafanyabiashara waliokuwepo, lakini Azimio la Arusha lilikuja kuwabana katika hili. Na hapa ndipo ‘safari ya uadui' baina ya Mwalimu na baadhi ya wanasiasa na wafanyabiashara wa ndani na nje, ilipoanzia rasmi.

Zipo tafiti kadhaa (mfano Issa Shivji, Horace Campbell, Howard Stein n.k) zinazoelezea jinsi gani baadhi ya wanasiasa waliendelea kushirikiana na wafanyabiashara kulihujumu Azimio la Arusha, kwa mfano kwa kuanzisha vitu kama ‘black markets' n.k. Njia hizi za panya pia zilitumiwa na wafanyabiashara na wanasiasa wasio waaminifu kutorosha fedha nyingi za umma nje ya nchi. Lakini ‘ironically', uchumi ulipofikia hatua mbaya, hasa ile hali ya uhaba wa bidhaa madukani, CCM iliwageukia wahujumu wale wale, aidha kwa kujua au kutokujua, ili watumie fedha zao kuliokoa taifa kwa kuagiza bidhaa kutoka nje kwani serikali iliishiwa fedha. Walichokifanya wahujumu hawa ni kutumia fedha zile zile walizowaibia walipa kodi, kujinufaisha na fursa iliyotolewa na serikali ya kuagiza na kujaza bidhaa madukani. Matokeo yake ni kwamba – maadui wa Azimio La Arusha wakageuka kuwa marafiki wakubwa wa CCM, na urafiki huu ukaja kuboreshwa na kuhalalishwa zaidi chini ya Azimio La Zanzibar kuanzia mwaka 1992.

Moja ya hatua za awali za kulizika azimio la Arusha ilikuwa ni pamoja na kuuza mashirika ya umma kuanzia miaka ya tisini. Ni muhimu tukatambua kuwa pamoja na ukweli kwamba mashirika mengi ya umma yalikosa ‘ufanisi', hivyo kupelekea kuwa mzigo kwa walipa kodi, kuna tafiti mbalimbali zinazoelezea uwepo wa hujuma za makusudi zilizolenga kuyaua mashirika haya kama njia ya kumkomoa Nyerere. Lakini pamoja na haya yote, ilifikia hatua kwamba suala la kubinaifisisha mashirika mengi ya umma lisingeweza kukwepeka. Ndio maana leo, malalamiko mengi juu ubinaifishaji hayapingi ‘ubinaifishaji Per Se', bali yanapinga ‘utaratibu mbovu uliotumika'.

Kwa mtazamo wangu, zipo njia nyingi ambazo iwapo zingefuatwa, wananchi wengi wangebariki zoezi la ubinaifishaji wa mali zao bila ya kinyongo wala manung'uniko mengi. Kwa mfano:

Moja, mashirika yote ambayo yalikuwa na maslahi kwa taifa pamoja na yale yaliyokuwa yanaendeshwa kwa faida yangebakishwa chini ya umma, au angalau, serikali ingeendelea kumiliki hisa nyingi kwa niaba ya wenye mali yani umma.

Mbili, serikali ingetoa fursa kwa wazawa weusi wenye uwezo na Uzalendo kwa nchi yao, pia kwa wananchi kupitia vyama vyao vya ushirika, kununua hisa kwenye mashirika haya.

Tatu, kwa vile mashirika haya yalijengwa na fedha za walipa kodi, ilibidi mchakato wote wa ubinaifishwaji uwashirikishe wenye mali hiyo (umma), kwa namna moja au nyingine, badala ya maamuzi kufanyika kwenye ‘board rooms' mawizarani.

Nne, pamoja na umuhimu wa zoezi zima, umma ungepewa taarifa za mapato yaliyopatikana na pia kushirikishwa katika maamuzi jinsi gani mapato yale yatumike. Badala yake, umma haukupewa taarifa zozote. Mbaya zaidi ni uwepo wa taarifa kwamba nyingi ya fedha hizi, WorldBank na IMF waliamrisha ziende kulipa riba ya madeni yetu kwao, huku pia tukiamrishwa kutumia baadhi ya fedha hizo kuwekeza katika maeneo ambayo wao WorldBank na IMF wanaamini yana umuhimu katika kusaidia kasi ya kukua kwa uchumi (GDP Growth Rate). Matokeo yake ni nini? Tumeshuhudia kasi kubwa ya kukua kwa uchumi wa nchi (on macro level) kufikia wastani wa 7% kwa miaka 12 mfululizo, huku uchumi wa wananchi walio wengi (on micro level) ukizidi kudidimia kwa zaidi ya hiyo 7% katika kipindi chote cha miaka 12.

Pia fedha nyingi sana za walipa kodi zimekuwa zikitoroshwa nje ya nchi i.e. "Capital Flight". Kwa mfano, ripoti moja ya NORAD (2011), inaonyesha mwaka 2002 pekee yake, capital flight ilifikia US Dollars Millioni 600. Pia takwimu zinaonyesha kwamba katika kipindi cha 2000 – 2008 pekee, capital flight ilifikia kiasi cha US Dollars Billion 2.8. Je watanzania wameibiwa fedha zaidi chini ya mfumo upi: wa Azimio La Arusha au Zanzibar? Katika miaka nane tu (2000-2008), kiasi cha US dollar billioni 2.8 kilichotoroshwa nje wakati kwa mujibu wa ripoti ya UNCTAD (2005), katika kipindi cha miaak 26 (1970 – 1996), fedha hizo zilikuwa ni Dollar Bilioni 1.7, huku nyingi ya hizi zikitoroshwa katika kipindi cha 1992 – 1995. Kwahiyo jibu ni kwamba Azimio la Zanzibar limehujumu fedha nyingi za walipa kodi kuliko Azimio la Arusha.

Huu ni ushahidi tosha kwamba wanasiasa waliokuwa wanapinga maadili ya uongozi chini ya azimio la Arusha, walifanya hivyo kwa maslahi yao binafsi, sio maslahi ya taifa.

Inawezekana Azimio La Zanzibar lilikuwa na nia nzuri ya kujenga mazingira ya tabaka la ubepari kushamiri na kustawi, kwani ubepari ndio uti wa mgongo wa sekta binafsi, na hakuna uchumi wowote duniani unaoweza kushamiri bila ya uwepo wa sekta binafsi. Lakini je:

  • Ubepari unaojengwa chini ya Azimio la Zanzibar ni ubepari wa asili? Ubepari huu unafanana vipi na ubepari uliopo katika mataifa yaliyofanikiwa kiuchumi?
  • Nini ni asili ya mabepari wazawa Tanzania? Je asili yao ni Ujasiriamali, Ubunifu, Uzalendo wa nchi yao, kama ilivyo kwenye mataifa yaliyo fanikiwa kiuchumu?
​
Kwa kiasi fulani, watanzania ni wa kujilaumu wenyewe kwa matatizo yalipo kwani tumekuwa tunawaunga mkono hata mabepari uchwara miongoni mwetu bila kutambua kwamba hawa ni sumu kwa Maendeleo yetu. Tumekuwa na jadi ya kuamini kwamba kila mfanyabishara mwenye

Mafanikio ni ‘mjasiriamali', bila ya kujiuliza, je katika nchi za wenzetu tunazowaiga juu ya soko huria, ubepari, na ujasiriamali, wao wanatambuaje ‘mjasiriamali'. Nchi za wenzetu, ufisadi sio sehemu ya ujasiriamali. Na kanuni za soko huria, uliberali na ubepari zinapinga mafisadi kwa sababu shughuli zao huwa ni sumu katika ustawi wa uchumi na jamii. Ndio maana ni kawaida kwa wenzetu kuwa na sheria kali dhidi ya mafisadi, hasa wanaotokana na siasa. Kuna tofauti kubwa kati ya mjasiriamali asili na yule atokanae na ufisadi:

1. Kwanza, wanatofautiana na vyanzo vya mitaji yao au ulimbikizaji wao – halali/sio halali.
2. Pili wanatofautiana katika motisha zao na tabia zao za uwekezaji - Kusafisha fedha chafu/kujenga uchumi.
3. Tatu wanatofautiana kwa athari zao katika uchumi - kwa mfano ulipaji kodi n.k.

Pengine ni muhimu kutazama uhusiano baina ya ubepari na ujasiriamali. Chini ya mfumo wa kiliberali, uhusiano kati ya ubepari na ujasiriamali ni ule wa ‘kutegemeana'. Chini ya mfumo huu, bila ya ujasiriamali, ubepari hauwezi kushamiri au kustawi na bila ubepari, ujasiriamali hauwezi kushamiri.

Je tuna Wazawa wajasiriamali wa aina gani? ili mtu aitwe mjasiriamali, ni lazima awe na uthubutu, ujasiri na kujiamini (risk taker) katika malengo yake ya kibiashara kwa mujibu wa nguvu za soko (bila ya mkono wa kisiasa). Ni lazima awe tayari kutumia mtaji wake alioupata kwa njia halali (e.g., sio wizi serikalini, TRA, BOT n.k), awe tayari kutumia ‘nguvu kazi yake' au ili ya kuajiri, na achanganye haya na ubunifu wake, lengo ikiwa ni kujitengeneza faida. Katika hali ya kawaida, lazima akabiliwe na hali ya kutokuwa na uhakika (uncertainity) juu ya matokeo ya shughuli zake, hivyo ulazimika pia kuwekeza katika mikakati/mbinu mbalimbali za kibiashara, kwa nia ya kuhakikisha kwamba malengo yake ya kutengeneza faida yanafanikiwa kwa kadri inavyowezekana. Msisitizo juu ya mtaji: Kwa kawaida, iwapo mtu huyu anaendesha shughuli na wenzake katika mazingira ya kampuni iliyo halali, vyanzo vikuu vya mtaji huwa ni ‘Debt' na ‘Equity', kwa njia ya uwazi (transparent), inayotokana na nguvu za soko, na bila ya uvunjifu wa kanuni za soko na sheria za nchi zilizopo.

Vinginevyo kama ufisadi ungekuwa unakubalika kama njia halali ya kujipatia mitaji, basi ufisadi ungekuwa na soko lake la mitaji, linaloendeshwa na riba zake. Na kama ungekuwa unakubalika kwa mujibu wa kanuni za soko huria, uliberali na ubepari, basi katika nchi kubwa kiuchumi (e.g. Ujerumani, China, USA, UK, Japan n.k), kila mwaka zingezaa wajasiriamali wengi wakubwa. Lakini tofauti na hali hii, mtumishi yoyote wa umma anayebainika kujihushisha na ufisadi huchukuliwa hatua mara moja. Tujiulize: Kwanini China wanawanyonga? Ni kwa sababu, nchi hizi zimefanikiwa chini ya kanuni za ubepari, uliberali, soko huria na ujasiriamali, baada ya kuelewa kwamba, ‘ufisadi' sio kiambato (ingredient) kizuri katika uchumi bali sumu ya Maendeleo ya uchumi na jamii.

Hivi karibuni, suala la ujasiriamali uchwara liliibuka katika mjadala kuhusu sheria ya uthibiti wa fedha chafu bungeni. Umma ulielezwa bayana na Mh. Lissu, Zitto n.k, jinsi gani wahujumu uchumi wanatumia mbinu mbali mbali kusafisha fedha zao chafu, huku nyingine nyingi zikitoroshwa nje ya nchi. Kwa bahati mbaya, hii ndio aina ya ubepari ambao tumekuwa tunaukumbatia chini ya Azimio la Zanzibar. Kuna mabepari wazawa wachache sana ambao ni mabepari wa ‘asili' na wanaowekeza waziwazi katika sekta zenye manufaa kwa watanzania walio wengi. KWa mfano, ni nadra kwa mabepari wazawa kuwekeza kwenye sekta muhimu kama viwanda na kilimo, ingawa wengi ndio walinunua viwanda vya umma na kuvitelekeza bila ya kuchukuliwa hatua, na wengi wanahodhi ardhi nyingi bila ya kuzitumia ipasavyo. Na wengi kwenye kilimo hawana Uzalendo na taifa lao kwani hujishughulisha zaidi kunufaisha masoko ya nje pamoja na ukweli kwamba hata soko la nyumbani lina mahitaji makubwa. Walio hodhi maelfu ya heka za ardhi yenye rutuba wanasubiria wawekezaji toka nje waje kushirikiana nao kuzalisha mazao kwa ajili ya soko la nje, kwa mfumo ule ule wa kikoloni. Sekta ya madini hali ndiyo mbaya zaidi kwani imejaa ufisadi na uhujumu uchumi 'unaolindwa' kwa nguvu zote za ndani na nje.

Ubepari wa namna hii chini ya Azimio La Zanzibar hauna manufaa kwa watanzania walio wengi. Ubepari huu ungekuwa na manufaa iwapo ungeongeza ajira na vipato kwa watanzania, ungetoa fursa za biashara kwa wakulima na wafugaji ya kuuza malighafi za viwandani n.k. Wanachohitaji watanzania walio wengi (hasa vijana), ni ubepari wa viwanda. Kwani, mbali na kutoa fursa za ajira na soko la malighafi viwandani, pia viwanda hivi vitatusaidia kama taifa, kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje, utegemezi mwingine ambao sio wa ulazima, ambao unatumalizia akiba yetu ya fedha za kigeni. Matokeo ya utegemezi wa aina hii ni kuzidi kupanuka kwa pengo la biashara baina ya Tanzania na nchi nyingine, na kupelekea kuzidi kuporomoka kwa shillingi yetu kutokana na kutegemea sarafu ya dollar kuagiza hata dawa za kichwa (panadol), siagi ya mkate (blueband) n.k., badala ya kuzalisha bidhaa za msingi kama hizi ndani ya nchi ili wafanyabiashara wasilazimike kuachana na shillingi na badala yake kutafuta dollar ili kutuletea bidhaa hizi madukani, hivyo kuipa sarafu yetu nguvu. Wenzetu Kenya hawahitaji kutumia dollar kuagiza bidhaa za msingi kwani wana viwanda vingi kutosheleza mahitaji hayo muhimu na ya msingi, hivyo kupelekea mahitaji na matumizi makubwa ya shillingi ya Kenya ndani ya uchumi wao, na kuzidi kuifanya shillingi ya Kenya kuwa imara dhidi ya dollar.

Kwa kumalizia, niseme tu kwamba: Mabepari wengi Tanzania sio mabepari wa asili bali wa ‘kuchakachua'. Pamoja na kumsumbua Mwalimu kwa miaka mingi kulipinga Azimio la Arusha, tumeona kwamba baada ya kufunguliwa milango na Azimio La Zanzibar, wengi wao hawajawa na faida yoyote kwa watanzania walio wengi, zaidi ya kuwa mzigo mkubwa kwa taifa letu. Ni kutokana na asili yao, ndio maana wengi hawana uhalali, hivyo nguvu na uwezo wa kuleta faida kwa katika uchumi wetu, kama inavyotarajiwa chini ya kanuni za ubepari, uliberali na soko huria.

Lakini ni muhimu kwa watanzania kuelewa kwamba miaka 50 baada ya uhuru, ubepari bado ndio njia pakee ya kuwakomboa, ilimradi ubepari huu usiwe wa kifisadi na pia serikali yetu (kama ilivyo kwenye nchi nyingine zenye mafanikio na soko huria), iwe na uwezo wa kuukemea kila mara ubepari huu unapokwenda kinyume na kanuni za soko na pia sheria husika. Kutokana na kukosekana kwa haya yote, watanzania wengi wameshindwa kuelewa maana halisi ya ubepari na faida zake, na badala yake wengi waanashindwa kuutofautisha na ufisadi, wakidhania kwamba ubepari unaishi juu ya sheria. Hali hii hujitokeza zaidi pale CCM na serikali yake inapojisahau na kusafisha ufisadi badala ya kusafisha ubepari ambao umechafuliwa na ufisadi.

Watanzania wanahitaji mabepari wa asili (sio wa kuchakachua) na wenye hadhi ya kuwa magnates wa 'finance' na industrialization'. Watanzania wanahitaji mabepari wabunifu (innovators) kama nchi za wenzetu, sio imitators. Watanzania wanahitaji mabepari wenye ‘inward orientation' na ‘Global view with local interest', sio mabepari wenye ‘outward orientation na ‘Global view' and ‘Global interest'. Kwa kufanya hivyo, tutapata mabepari wenye Uzalendo badala ya mabepari wanaowajengea daraja wawekezaji ‘wa ovyo', ili kwa pamoja wahamishe rasilimali za watanzania kwenda nje. Watanzania hawahitaji mabepari ambao kazi yao ni kuwa ‘agents' au ‘intermediares' wa makampuni ya nje baada yak u-sign mikataba mibovu na kupewa 10% au hisa kwenye makampuni yanayokuja kuiba rasilimali zetu. Watanzania wanahitaji industrial capitalists ambao watakuwa ni vinara/heroes wa uchumi wetu, na ambao shughuli zao zitakuwa na manufaa kwa watanzania walio wengi, hasa wa vijijini.

CCM inashindwa kuelewa kwamba Vyama Vya Siasa imara duniani hulindwa na uchumi imara [sio uchumi imara pekee on macro level (GDP growth rate ya 7%), bali uchumi imara pia on micro level – ongezeko la vipato vya wananchi walio wengi]. CCM inabidi itambue kwamba uchumi imara ni ule unaotokana na mfumo imara wa ndani unaojenga mabepari wazawa na wazalendo, sio ule unaopendelea mabepari wa kigeni. Ndio Mwalimu alitamka kwamba, "bila CCM madhubuti, nchi itayumba", nah ii chelewa ya CCM itaingiza nchi katika machafuko na pia kukitoa CCM madarakani.

Watanzania walio wengi walitarajia neema baada ya kuuliwa kwa azimio la Arusha ili kulipisha lile la Zanzibar. Lakini baada ya miaka 20 ya uwepo wake, walio wengi bado hawajaona faida na umuhimu wake. Vinginevyo, CCM ikubali kwamba neno ‘Mapinduzi', sio tena sehemu ya madhumini yake. Kuna kila dalili kwamba hali ikiendelea kubakia kama ilivyo, watanzania (umma) watafanya maamuzi magumu ya kujitafutia mapinduzi wenyewe, na wanaelewa wanahitaji mapinduzi ya namna gani, kwani Mwalimu Nyerere aliyaweka bayana kwa wananchi miaka 50 iliyopita. Na uhalali wa watanzania kujitafutia mapinduzi haya wenyewe, unazidi kuongezeka siku hadi siku, hasa kwa kuzingatia kwamba hata Mwalimu Nyerere katika moja ya hotuba zake ambazo hazijawahi kurudiwa tena na vyombo vya habari, Mwalimu Nyerere alisema:

["To be sure, you few Waswahili, do you really expect to rule Tanzanians through coercion, When there is no hope, and then expect that they will sit quiet in peace? Peace is born of hope, when hope is gone, there will be social upheavals. I'd be surprised if these Tanzanians refuse to Rebel, why? When the majorities don't have any hope you are building a volcano. It is bound to erupt one day. Unless these people are fools (wapumbavu). Many in these countries are fools, to accept being ruled just like that. To be oppressed just like that when they have the force in numbers, they are fools (wapumbavu). So Tanzanians would be fools (wapumbavu), ****** (mazuzu), if they continue to accept to be oppressed by minority in their own country. Why?"]. Source: Shivji, Issa: Critical Elements of a New Democratic Consensus in Africa (pp.25-38), in Othman, Haroub Othman (ed.): "Reflections on Leadership in Africa: 40 years of independence.
 
Kama mwanachama hai wa CCM, natambua Mwongozo Wa mwaka 1981 katika sehemu ya (57) ibara ya (5) unatamka kwamba: “Kujikosoa na kukosoana ni silaha ya Mapinduzi”. Katika sehemu ya (59), Mwongozo unazidi kuhimiza kwamba:“Suala la kukosoa, kujikosoa na kukosoana lina sura kadhaa. Kwanza linataka wanachama na viongozi kuwa tayari kusema kweli katika vitendo vyao na kukubali kuambizana ukweli. Pili, linataka wanachama na hasa viongozi wawe tayari kukosolewa bila kuhamaki na inapobidi kukubali kujirekebisha. Tatu ni kuwa Chama chenyewe katika vikao vyake vya ngazi mbalimbali kuwa na utaratibu wa kujikosoa.” Hivyo mwongozo wa CCM unanipa haki zote, kama mwanachama, kukikosoa chama changu cha CCM kila inapobidi.

CCM ni mwasisi wa Azimio La Arusha na pia ni mwasisi wa Azimio la Zanzibar. Baada ya miaka 50 ya uhuru, maazimio haya yanawajibika moja kwa moja juu ya hali za maisha ya watanzania kiuchumi na kijamii. Wakati Azimio la Arusha lilidumu kwa miaka 18 (1967 – 1985), Azimio La Zanzibar limedumu kwa miaka 20 (1992 – 2012). Pia, tofauti na Azimio La Arusha ambalo liliungwa mkono na wananchi wengi vijijini na wasomi Chuo Kikuu, Azimio La Zanzibar lilipitishwa kimya kimya na CCM-NEC Zanzibar, jambo ambalo hata Mwalimu Nyerere lilimkuta kwa mshangao. Ni kama vile CCM ilikuwa inasubiri Nyerere ang’atuke Uenyekiti CCM Taifa Mwaka 1990; Vinginevyo nini ilikuwa ni sababu ya msingi ya kuendelea na Azimio La Arusha kwa miaka 7 zaidi (1985-1992)?

Azimio La Zanzibar la mwaka 1992, liliwezesha CCM na serikali yake kuanza rasmi kuitumikia ITIKADI YA ULIBERALI KIVITENDO, INGAWA KINADHARIA, ITIKADI YA CCM KWA MUJIBU WA KATIBA YAKE YA SASA BADO NI YA UJAMAA. Mbali na hiki KIGEUGEGU, mabadiliko muhimu kwa mujibu wa Azimio La Zanzibar ni kwamba, tofauti na Azimio la Arusha, VIONGOZI WENYE DHAMANA YA UMMA sasa wamepewa rukra rasmi ya kupokea mshahara zaidi ya mmoja, kumiliki nyumba za kupanga, na kuwa na hisa katika makampuni binafsi. Azimio La Zanzibar halikufanya jitihada yoyote kurekebisha masharti haya ya uongozi wa umma pamoja na umuhimu wake. Badala yake iliyafuta kama yalivyo. Hii ina maana kwamba kuanzia mwaka 1992, ikawa ni ruksa kwa viongozi kutumia nafasi zao za uongozi kwa maslahi binafsi. Nadiriki kusema hivi kwa sababu Azimio La Zanzibar halina masharti yoyote ya uongozi, pamoja na kwamba uongozi bado unaendelea kuwa ni ‘dhamana’. Hii ni ajabu kwa sababu katika mazingira yoyote yale, hakuna dhamana isiyokuwa na masharti.

Maazimio ya Arusha na Zanzibar yamegawanya watanzania kimtazamo katika makundi mawili. Kundi la kwanza linahimiza haja ya CCM kurudia baadhi ya mambo muhimu ndani ya Azimio La Arusha kama njia ya kurudisha uadilifu wa uongozi, hasa katika kusimamia maslahi ya taifa. Hoja nyingine ya kundi hili ni kwamba, Azimio La Arusha lilisaidia Watanzania Kujitambua, liliwapatia Nia kama taifa, na Ushupavu, na haya ndio yaliyochochea ongezeko la juhudi miongoni mwa watanzania, katika ujenzi na ulinzi wa taifa lao, kwa manufaa yao na ya vizazi vijavyo.

Kundi la pili ni lile linalounga mkono Azimio La Zanzibar huku likipinga lile la Arusha. Kundi hili lina hoja kadhaa lakini hoja ya msingi ni kwamba Azimio la Arusha halikuwatendea haki watanzania na ndio chanzo kikuu cha umaskini wao leo. Msisitizo wao ni kwamba Azimio la Arusha liliwanyima watanzania uhuru wa kushiriki katika shughuli za kiuchumi kwa kutumia uwezo na vipaji vyao walivyojaliwa ili kujitafutia rizki bila ya kuingiliwa na nguvu yoyote nje ya nguvu ya soko. Pia kuna hoja muhimu kwamba, haikuwa sahihi kwa TANU/CCM kuwanyima watanzania haki ya msingi kabisa ya ‘umiliki binafsi wa mali’.

Nia ya kuleta mjadala huu ni kubadilishana mawazo juu ya masuala haya muhimu, huku nikilenga zaidi katika kuchokoza mada. Mwalimu alipokuwa anan’gatuka uenyekiti wa CCM mwaka 1990 alitoa wosia ufuatao: “Mimi Nang’atuka Lakini Naendelea Kuamini Kuwa Bila CCM Madhubuti, Nchi itayumba.”

Swali la ujumla la mada hii ni je:

  • Utabiri wa Mwalimu kuhusu CCM kuyumba una uhusiano gani na utekelezaji wa Azimio La Zanzibar?

Lakini maswali mahususi ni haya yafuatayo:

1. Iwapo Azimio La Zanzibar lina manufaa kwa watanzania walio wengi, kwanini mchakato wake ulifanyika kimya kimya bila ya kuwashirikisha wanachama wengi?

2. Iwapo Azimio La Zanzibar lina manufaa Kwa watanzania walio wengi, kwanini CCM bado haipo wazi kuhusiana na utekelezaji wa Azimio hili kwa mujibu wa Katiba ya sasa ya chama ambayo bado inatamka itikadi yake kuwa ni ya Kijamaa?

3. Ikilinganishwa na Azimio La Arusha lililoishi kwa miaka 18 (1967 – 1985), Je, miaka 20 ya Azimio La Zanzibar imewaletea watanzania ‘walio wengi’ manufaa gani?

4. Je, kwa kuzingatia mahitaji ya sasa ya watanzania ‘walio wengi’, Azimio La Zanzibar lina mazuri na mabaya gani?

5. Je, kuna mambo gani ndani ya Azimio la Arusha ambayo bado yana manufaa kwa watanzania ‘walio wengi’ katika nyakati za sasa?

Kama nilivyosema awali, nia yangu kuu ni kuchokoza mada. Ningependa nianze na majibu aliyoyatoa Rais Benjamin Mkapa mwaka 2005, kwa mwandishi mmoja wa Uingereza aitwaye Jonathan Power. Mwandishi huyu alimuuliza Mh. Mkapa swali lifuatalo:

“Mh. Rais, iwapo Mwalimu Nyerere anafufuka Leo, Kwa mtazamo wako, angezungumziaje hali ya sasa ya Tanzania?”

Mh. Mkapa alimjibu hivi:

“Mwalimu angesema nimegawa rasilimali nyingi sana ambazo awali zilikuwa chini ya umma. Lakini pia Mwalimu angekasirika sana kwamba nimejenga tabaka kubwa la kibepari lenye mafanikio na linalozidi kustawi.”
Mh. Mkapa alikuwa mkweli katika hili kwani hiyo ndiyo hali halisi chini ya soko huria na Azimio La Zanzibar. Kama itakumbukwa vizuri, moja ya hoja kubwa za kulizika azimio la Arusha mwaka 1992 ilikuwa ni pamoja na kwamba, miaka 18 ya azimio la Arusha ilipelekea hali za watanzania wengi kiuchumi na kijamii kuzorota, hivyo kulikuwa na muhimu wa kurekebisha udhaifu huo. Ndipo Azimio la Zanzibar likabuniwa kama tiba, baada ya Azimio la Arusha kuonekana halikuwa tiba bali ugonjwa uliokuwa umeenezwa kwenye jamii kwaa miaka 18. Watanzania wamekuwa chini ya tiba ya ‘Azimio la Zanzibar’ kwa muda wa miaka 20 sasa.
Je, kwanini Mwalimu aliona Azimio La Arusha ndio dawa ya Umaskini?

Dawa ilikuwa katika neno ‘mapinduzi’ chini ya TANU/CCM, mapinduzi ambayo yalilenga kuwakomboa watanzania walio wengi kutoka kwenye minyororo ya unyonyaji uliotokana na miaka zaidi ya 50 ya kuwa chini ubeberu na ukoloni. Ndio maana dhamira kuu ya Azimio la Arusha ikawa ni kumtokomeza ‘bwanyenye’ ili kuisafishia njia jamii mpya iliyotarajiwa kushamiri na kustawi katika mazingira ya usawa - kichumi na kijamii. Ni dhahiri kwamba, bila ya Mwalimu kuanzisha mapinduzi yale, basi angekumbana na mapinduzi ya umma, kwani umma ulikuwa na kiu ya ahadi nyingi zilizotolewa na TANU wakati wa harakati za uhuru.

Mwalimu alikuwa na wakati mgumu katika hili kwani hata baada ya uhuru, ardhi iliendelea kuwa ndiyo njia kuu ya uzalishaji, hivyo uchumi. Mwaka 1961, jumla ya wahindi na wazungu Tanganyika ilikuwa karibia 2% ya idadi ya watu wote, huku wahindi na wazungu wakimiliki karibia 50% ya jumla ya ardhi yenye rutuba Tanganyika. Kwa upande mwingine, Watanganyika weusi idadi yao ilikuwa ni 98% ya watu wote, na wao walimiliki karibia 50% ya ardhi yenye rutuba. Hivyo, mantiki na uhalali wa Azimio La Arusha vilichangiwa na uhalisia huu.

Pamoja na hayo, wapo waliopinga Azimio hili, wengi ikiwa ni wenzake na Mwalimu ambao walikuwa na matarajio tofauti juu ya matunda ya uhuru. Historia inaelezea jinsi gani baadhi ya viongozi hawa walivyoanza kujijenga zaidi na wahindi na wazungu kupitia nafasi zao za uongozi, badala ya kujijenga kwa wananchi. Mwalimu hakusita kulisemea hilo katika kitabu chake cha TANU NA RAIA mwaka 1962, mwaka mmoja tu baada ya uhuru:

[…kilichokuwa kikituuma ni kwamba ubwana na ufahari wa wazungu waligawana wenyewe tu, bila kutugawia sisi pia; baadhi yetu hatukuwa tunadai uhuru ili uwapunguzie watu wetu mzigo huu wa ubwana na ufahari, bali tamaa yetu ilikuwa ni kukalia viti vile vya ubwana na ufahari. Tamaa yetu haikuwa kushika vyeo tu, vilivyokuwa vimeshikiliwa na wazungu hapo zamani, tulitaka na mishahara pia iliyokuwa ikifuatana na vyeo hivyo, bila kujali kama watu wetu wanaweza kulipa mishahara hiyo, bila kujali maisha ya watu wetu…”].

Pia, ni muhimu tukakumbuka kwamba, wakoloni hawakumwendeleza mtu mweusi. Kabla ya uhuru, watu weusi walikuwa ni vibarua mashambani, huku wachache wakiwa na ajira za ngazi ya chini katika serikali ya mkoloni. Vinginevyo mkoloni alitumia muda wake mwingi kujenga wahindi kibiashara na kijasiriamali kwa kuwapatia fursa nyingi kama vile uwakala wa biashara n.k. Ndio maana mwaka 1961 wakati Tanganyika inapata uhuru, hapakuwa na idadi kubwa ya watu weusi waliokuwa na uzoefu au shughuli yoyote ya kijasiriamali. Wengi ilikuwa ni wahindi. Kulikuwepo na baadhi ya viongozi serikalini waliotamani kutumia nafasi zao za uongozi kushirikiana na wafanyabiashara waliokuwepo, lakini Azimio la Arusha lilikuja kuwabana katika hili. Na hapa ndipo ‘safari ya uadui’ baina ya Mwalimu na baadhi ya wanasiasa na wafanyabiashara wa ndani na nje, ilipoanzia rasmi.

Zipo tafiti kadhaa (mfano Issa Shivji, Horace Campbell, Howard Stein n.k) zinazoelezea jinsi gani baadhi ya wanasiasa waliendelea kushirikiana na wafanyabiashara kulihujumu Azimio la Arusha, kwa mfano kwa kuanzisha vitu kama ‘black markets’ n.k. Njia hizi za panya pia zilitumiwa na wafanyabiashara na wanasiasa wasio waaminifu kutorosha fedha nyingi za umma nje ya nchi. Lakini ‘ironically’, uchumi ulipofikia hatua mbaya, hasa ile hali ya uhaba wa bidhaa madukani, CCM iliwageukia wahujumu wale wale, aidha kwa kujua au kutokujua, ili watumie fedha zao kuliokoa taifa kwa kuagiza bidhaa kutoka nje kwani serikali iliishiwa fedha. Walichokifanya wahujumu hawa ni kutumia fedha zile zile walizowaibia walipa kodi, kujinufaisha na fursa iliyotolewa na serikali ya kuagiza na kujaza bidhaa madukani. Matokeo yake ni kwamba – maadui wa Azimio La Arusha wakageuka kuwa marafiki wakubwa wa CCM, na urafiki huu ukaja kuboreshwa na kuhalalishwa zaidi chini ya Azimio La Zanzibar kuanzia mwaka 1992.

Moja ya hatua za awali za kulizika azimio la Arusha ilikuwa ni pamoja na kuuza mashirika ya umma kuanzia miaka ya tisini. Ni muhimu tukatambua kuwa pamoja na ukweli kwamba mashirika mengi ya umma yalikosa ‘ufanisi’, hivyo kupelekea kuwa mzigo kwa walipa kodi, kuna tafiti mbalimbali zinazoelezea uwepo wa hujuma za makusudi zilizolenga kuyaua mashirika haya kama njia ya kumkomoa Nyerere. Lakini pamoja na haya yote, ilifikia hatua kwamba suala la kubinaifisisha mashirika mengi ya umma lisingeweza kukwepeka. Ndio maana leo, malalamiko mengi juu ubinaifishaji hayapingi ‘ubinaifishaji Per Se’, bali yanapinga ‘utaratibu mbovu uliotumika’.

Kwa mtazamo wangu, zipo njia nyingi ambazo iwapo zingefuatwa, wananchi wengi wangebariki zoezi la ubinaifishaji wa mali zao bila ya kinyongo wala manung’uniko mengi. Kwa mfano:

Moja, mashirika yote ambayo yalikuwa na maslahi kwa taifa pamoja na yale yaliyokuwa yanaendeshwa kwa faida yangebakishwa chini ya umma, au angalau, serikali ingeendelea kumiliki hisa nyingi kwa niaba ya wenye mali yani umma.

Mbili, serikali ingetoa fursa kwa wazawa weusi wenye uwezo na Uzalendo kwa nchi yao, pia kwa wananchi kupitia vyama vyao vya ushirika, kununua hisa kwenye mashirika haya.

Tatu, kwa vile mashirika haya yalijengwa na fedha za walipa kodi, ilibidi mchakato wote wa ubinaifishwaji uwashirikishe wenye mali hiyo (umma), kwa namna moja au nyingine, badala ya maamuzi kufanyika kwenye ‘board rooms’ mawizarani.

Nne, pamoja na umuhimu wa zoezi zima, umma ungepewa taarifa za mapato yaliyopatikana na pia kushirikishwa katika maamuzi jinsi gani mapato yale yatumike. Badala yake, umma haukupewa taarifa zozote. Mbaya zaidi ni uwepo wa taarifa kwamba nyingi ya fedha hizi, WorldBank na IMF waliamrisha ziende kulipa riba ya madeni yetu kwao, huku pia tukiamrishwa kutumia baadhi ya fedha hizo kuwekeza katika maeneo ambayo wao WorldBank na IMF wanaamini yana umuhimu katika kusaidia kasi ya kukua kwa uchumi (GDP Growth Rate). Matokeo yake ni nini? Tumeshuhudia kasi kubwa ya kukua kwa uchumi wa nchi (on macro level) kufikia wastani wa 7% kwa miaka 12 mfululizo, huku uchumi wa wananchi walio wengi (on micro level) ukizidi kudidimia kwa zaidi ya hiyo 7% katika kipindi chote cha miaka 12.

Pia fedha nyingi sana za walipa kodi zimekuwa zikitoroshwa nje ya nchi i.e. “Capital Flight”. Kwa mfano, ripoti moja ya NORAD (2011), inaonyesha mwaka 2002 pekee yake, capital flight ilifikia US Dollars Millioni 600. Pia takwimu zinaonyesha kwamba katika kipindi cha 2000 – 2008 pekee, capital flight ilifikia kiasi cha US Dollars Billion 2.8. Je watanzania wameibiwa fedha zaidi chini ya mfumo upi: wa Azimio La Arusha au Zanzibar? Katika miaka nane tu (2000-2008), kiasi cha US dollar billioni 2.8 kilichotoroshwa nje wakati kwa mujibu wa ripoti ya UNCTAD (2005), katika kipindi cha miaak 26 (1970 – 1996), fedha hizo zilikuwa ni Dollar Bilioni 1.7, huku nyingi ya hizi zikitoroshwa katika kipindi cha 1992 – 1995. Kwahiyo jibu ni kwamba Azimio la Zanzibar limehujumu fedha nyingi za walipa kodi kuliko Azimio la Arusha.

Huu ni ushahidi tosha kwamba wanasiasa waliokuwa wanapinga maadili ya uongozi chini ya azimio la Arusha, walifanya hivyo kwa maslahi yao binafsi, sio maslahi ya taifa.

Inawezekana Azimio La Zanzibar lilikuwa na nia nzuri ya kujenga mazingira ya tabaka la ubepari kushamiri na kustawi, kwani ubepari ndio uti wa mgongo wa sekta binafsi, na hakuna uchumi wowote duniani unaoweza kushamiri bila ya uwepo wa sekta binafsi. Lakini je:

  • Ubepari unaojengwa chini ya Azimio la Zanzibar ni ubepari wa asili? Ubepari huu unafanana vipi na ubepari uliopo katika mataifa yaliyofanikiwa kiuchumi?
  • Nini ni asili ya mabepari wazawa Tanzania? Je asili yao ni Ujasiriamali, Ubunifu, Uzalendo wa nchi yao, kama ilivyo kwenye mataifa yaliyo fanikiwa kiuchumu?
​
Kwa kiasi fulani, watanzania ni wa kujilaumu wenyewe kwa matatizo yalipo kwani tumekuwa tunawaunga mkono hata mabepari uchwara miongoni mwetu bila kutambua kwamba hawa ni sumu kwa Maendeleo yetu. Tumekuwa na jadi ya kuamini kwamba kila mfanyabishara mwenye

Mafanikio ni ‘mjasiriamali’, bila ya kujiuliza, je katika nchi za wenzetu tunazowaiga juu ya soko huria, ubepari, na ujasiriamali, wao wanatambuaje ‘mjasiriamali’. Nchi za wenzetu, ufisadi sio sehemu ya ujasiriamali. Na kanuni za soko huria, uliberali na ubepari zinapinga mafisadi kwa sababu shughuli zao huwa ni sumu katika ustawi wa uchumi na jamii. Ndio maana ni kawaida kwa wenzetu kuwa na sheria kali dhidi ya mafisadi, hasa wanaotokana na siasa. Kuna tofauti kubwa kati ya mjasiriamali asili na yule atokanae na ufisadi:

1. Kwanza, wanatofautiana na vyanzo vya mitaji yao au ulimbikizaji wao – halali/sio halali.
2. Pili wanatofautiana katika motisha zao na tabia zao za uwekezaji - Kusafisha fedha chafu/kujenga uchumi.
3. Tatu wanatofautiana kwa athari zao katika uchumi - kwa mfano ulipaji kodi n.k.

Pengine ni muhimu kutazama uhusiano baina ya ubepari na ujasiriamali. Chini ya mfumo wa kiliberali, uhusiano kati ya ubepari na ujasiriamali ni ule wa ‘kutegemeana’. Chini ya mfumo huu, bila ya ujasiriamali, ubepari hauwezi kushamiri au kustawi na bila ubepari, ujasiriamali hauwezi kushamiri.

Je tuna Wazawa wajasiriamali wa aina gani? ili mtu aitwe mjasiriamali, ni lazima awe na uthubutu, ujasiri na kujiamini (risk taker) katika malengo yake ya kibiashara kwa mujibu wa nguvu za soko (bila ya mkono wa kisiasa). Ni lazima awe tayari kutumia mtaji wake alioupata kwa njia halali (e.g., sio wizi serikalini, TRA, BOT n.k), awe tayari kutumia ‘nguvu kazi yake’ au ili ya kuajiri, na achanganye haya na ubunifu wake, lengo ikiwa ni kujitengeneza faida. Katika hali ya kawaida, lazima akabiliwe na hali ya kutokuwa na uhakika (uncertainity) juu ya matokeo ya shughuli zake, hivyo ulazimika pia kuwekeza katika mikakati/mbinu mbalimbali za kibiashara, kwa nia ya kuhakikisha kwamba malengo yake ya kutengeneza faida yanafanikiwa kwa kadri inavyowezekana. Msisitizo juu ya mtaji: Kwa kawaida, iwapo mtu huyu anaendesha shughuli na wenzake katika mazingira ya kampuni iliyo halali, vyanzo vikuu vya mtaji huwa ni ‘Debt’ na ‘Equity’, kwa njia ya uwazi (transparent), inayotokana na nguvu za soko, na bila ya uvunjifu wa kanuni za soko na sheria za nchi zilizopo.

Vinginevyo kama ufisadi ungekuwa unakubalika kama njia halali ya kujipatia mitaji, basi ufisadi ungekuwa na soko lake la mitaji, linaloendeshwa na riba zake. Na kama ungekuwa unakubalika kwa mujibu wa kanuni za soko huria, uliberali na ubepari, basi katika nchi kubwa kiuchumi (e.g. Ujerumani, China, USA, UK, Japan n.k), kila mwaka zingezaa wajasiriamali wengi wakubwa. Lakini tofauti na hali hii, mtumishi yoyote wa umma anayebainika kujihushisha na ufisadi huchukuliwa hatua mara moja. Tujiulize: Kwanini China wanawanyonga? Ni kwa sababu, nchi hizi zimefanikiwa chini ya kanuni za ubepari, uliberali, soko huria na ujasiriamali, baada ya kuelewa kwamba, ‘ufisadi’ sio kiambato (ingredient) kizuri katika uchumi bali sumu ya Maendeleo ya uchumi na jamii.

Hivi karibuni, suala la ujasiriamali uchwara liliibuka katika mjadala kuhusu sheria ya uthibiti wa fedha chafu bungeni. Umma ulielezwa bayana na Mh. Lissu, Zitto n.k, jinsi gani wahujumu uchumi wanatumia mbinu mbali mbali kusafisha fedha zao chafu, huku nyingine nyingi zikitoroshwa nje ya nchi. Kwa bahati mbaya, hii ndio aina ya ubepari ambao tumekuwa tunaukumbatia chini ya Azimio la Zanzibar. Kuna mabepari wazawa wachache sana ambao ni mabepari wa ‘asili’ na wanaowekeza waziwazi katika sekta zenye manufaa kwa watanzania walio wengi. KWa mfano, ni nadra kwa mabepari wazawa kuwekeza kwenye sekta muhimu kama viwanda na kilimo, ingawa wengi ndio walinunua viwanda vya umma na kuvitelekeza bila ya kuchukuliwa hatua, na wengi wanahodhi ardhi nyingi bila ya kuzitumia ipasavyo. Na wengi kwenye kilimo hawana Uzalendo na taifa lao kwani hujishughulisha zaidi kunufaisha masoko ya nje pamoja na ukweli kwamba hata soko la nyumbani lina mahitaji makubwa. Walio hodhi maelfu ya heka za ardhi yenye rutuba wanasubiria wawekezaji toka nje waje kushirikiana nao kuzalisha mazao kwa ajili ya soko la nje, kwa mfumo ule ule wa kikoloni. Sekta ya madini hali ndiyo mbaya zaidi kwani imejaa ufisadi na uhujumu uchumi ‘unaolindwa’ kwa nguvu zote za ndani na nje.

Ubepari wa namna hii chini ya Azimio La Zanzibar hauna manufaa kwa watanzania walio wengi. Ubepari huu ungekuwa na manufaa iwapo ungeongeza ajira na vipato kwa watanzania, ungetoa fursa za biashara kwa wakulima na wafugaji ya kuuza malighafi za viwandani n.k. Wanachohitaji watanzania walio wengi (hasa vijana), ni ubepari wa viwanda. Kwani, mbali na kutoa fursa za ajira na soko la malighafi viwandani, pia viwanda hivi vitatusaidia kama taifa, kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje, utegemezi mwingine ambao sio wa ulazima, ambao unatumalizia akiba yetu ya fedha za kigeni. Matokeo ya utegemezi wa aina hii ni kuzidi kupanuka kwa pengo la biashara baina ya Tanzania na nchi nyingine, na kupelekea kuzidi kuporomoka kwa shillingi yetu kutokana na kutegemea sarafu ya dollar kuagiza hata dawa za kichwa (panadol), siagi ya mkate (blueband) n.k., badala ya kuzalisha bidhaa za msingi kama hizi ndani ya nchi ili wafanyabiashara wasilazimike kuachana na shillingi na badala yake kutafuta dollar ili kutuletea bidhaa hizi madukani, hivyo kuipa sarafu yetu nguvu. Wenzetu Kenya hawahitaji kutumia dollar kuagiza bidhaa za msingi kwani wana viwanda vingi kutosheleza mahitaji hayo muhimu na ya msingi, hivyo kupelekea mahitaji na matumizi makubwa ya shillingi ya Kenya ndani ya uchumi wao, na kuzidi kuifanya shillingi ya Kenya kuwa imara dhidi ya dollar.

Kwa kumalizia, niseme tu kwamba: Mabepari wengi Tanzania sio mabepari wa asili bali wa ‘kuchakachua’. Pamoja na kumsumbua Mwalimu kwa miaka mingi kulipinga Azimio la Arusha, tumeona kwamba baada ya kufunguliwa milango na Azimio La Zanzibar, wengi wao hawajawa na faida yoyote kwa watanzania walio wengi, zaidi ya kuwa mzigo mkubwa kwa taifa letu. Ni kutokana na asili yao, ndio maana wengi hawana uhalali, hivyo nguvu na uwezo wa kuleta faida kwa katika uchumi wetu, kama inavyotarajiwa chini ya kanuni za ubepari, uliberali na soko huria.

Lakini ni muhimu kwa watanzania kuelewa kwamba miaka 50 baada ya uhuru, ubepari bado ndio njia pakee ya kuwakomboa, ilimradi ubepari huu usiwe wa kifisadi na pia serikali yetu (kama ilivyo kwenye nchi nyingine zenye mafanikio na soko huria), iwe na uwezo wa kuukemea kila mara ubepari huu unapokwenda kinyume na kanuni za soko na pia sheria husika. Kutokana na kukosekana kwa haya yote, watanzania wengi wameshindwa kuelewa maana halisi ya ubepari na faida zake, na badala yake wengi waanashindwa kuutofautisha na ufisadi, wakidhania kwamba ubepari unaishi juu ya sheria. Hali hii hujitokeza zaidi pale CCM na serikali yake inapojisahau na kusafisha ufisadi badala ya kusafisha ubepari ambao umechafuliwa na ufisadi.

Watanzania wanahitaji mabepari wa asili (sio wa kuchakachua) na wenye hadhi ya kuwa magnates wa ‘finance’ na industrialization’. Watanzania wanahitaji mabepari wabunifu (innovators) kama nchi za wenzetu, sio imitators. Watanzania wanahitaji mabepari wenye ‘inward orientation’ na ‘Global view with local interest’, sio mabepari wenye ‘outward orientation na ‘Global view’ and ‘Global interest’. Kwa kufanya hivyo, tutapata mabepari wenye Uzalendo badala ya mabepari wanaowajengea daraja wawekezaji ‘wa ovyo’, ili kwa pamoja wahamishe rasilimali za watanzania kwenda nje. Watanzania hawahitaji mabepari ambao kazi yao ni kuwa ‘agents’ au ‘intermediares’ wa makampuni ya nje baada yak u-sign mikataba mibovu na kupewa 10% au hisa kwenye makampuni yanayokuja kuiba rasilimali zetu. Watanzania wanahitaji industrial capitalists ambao watakuwa ni vinara/heroes wa uchumi wetu, na ambao shughuli zao zitakuwa na manufaa kwa watanzania walio wengi, hasa wa vijijini.

CCM inashindwa kuelewa kwamba Vyama Vya Siasa imara duniani hulindwa na uchumi imara [sio uchumi imara pekee on macro level (GDP growth rate ya 7%), bali uchumi imara pia on micro level – ongezeko la vipato vya wananchi walio wengi]. CCM inabidi itambue kwamba uchumi imara ni ule unaotokana na mfumo imara wa ndani unaojenga mabepari wazawa na wazalendo, sio ule unaopendelea mabepari wa kigeni. Ndio Mwalimu alitamka kwamba, “bila CCM madhubuti, nchi itayumba”, nah ii chelewa ya CCM itaingiza nchi katika machafuko na pia kukitoa CCM madarakani.

Watanzania walio wengi walitarajia neema baada ya kuuliwa kwa azimio la Arusha ili kulipisha lile la Zanzibar. Lakini baada ya miaka 20 ya uwepo wake, walio wengi bado hawajaona faida na umuhimu wake. Vinginevyo, CCM ikubali kwamba neno ‘Mapinduzi’, sio tena sehemu ya madhumini yake. Kuna kila dalili kwamba hali ikiendelea kubakia kama ilivyo, watanzania (umma) watafanya maamuzi magumu ya kujitafutia mapinduzi wenyewe, na wanaelewa wanahitaji mapinduzi ya namna gani, kwani Mwalimu Nyerere aliyaweka bayana kwa wananchi miaka 50 iliyopita. Na uhalali wa watanzania kujitafutia mapinduzi haya wenyewe, unazidi kuongezeka siku hadi siku, hasa kwa kuzingatia kwamba hata Mwalimu Nyerere katika moja ya hotuba zake ambazo hazijawahi kurudiwa tena na vyombo vya habari, Mwalimu Nyerere alisema:

[“To be sure, you few Waswahili, do you really expect to rule Tanzanians through coercion, When there is no hope, and then expect that they will sit quiet in peace? Peace is born of hope, when hope is gone, there will be social upheavals. I’d be surprised if these Tanzanians refuse to Rebel, why? When the majorities don’t have any hope you are building a volcano. It is bound to erupt one day. Unless these people are fools (wapumbavu). Many in these countries are fools, to accept being ruled just like that. To be oppressed just like that when they have the force in numbers, they are fools (wapumbavu). So Tanzanians would be fools (wapumbavu), ****** (mazuzu), if they continue to accept to be oppressed by minority in their own country. Why?”]. Source: Shivji, Issa: Critical Elements of a New Democratic Consensus in Africa (pp.25-38), in Othman, Haroub Othman (ed.): “Reflections on Leadership in Africa: 40 years of independence.

Mkuu Mchambuzi, hakika nafikiri tunaelekea kurudi enzi za ma-Great Thinker wa ukweli, wanamtandao wenye uwezo wa kuchambua issue na kuweka bayana matatizo yanayoikabili nchi.

Nimeifurahia hii mada maana imechokoza uwezo wa kufikiri na kuona kwa undani muelekeo wa masuala ya kisiasa na uchumi wake.
Nime-highlight kwenye red, masuala yote ambayo yangeweza kupatiwa majibu-kisiasa -na chama tawala, lakini hakijawahi kuattempt kufanya hivyo.
Kwa jinsi umahiri wa kisiasa ulivyo dorora ndani ya chama tawala, sina uhakika kama wanauwezo wa hata kupata quorum ya kujadili mada hizi.
Ni wazi kuwa dira ya kiuchumi na kisiasa kwa siku za leo zina uhuria unaoedana na uvunjufu wa sheria.
Binafsi nikitazama safu ya uongozi iliyopo sioni kiongozi mwenye ubavu wa kuasisi na kusimamia sera madhubuti za kiuchumi ili kuendana na wakati tuiopo.

Bado nashawishika kufikiri kuwa maendeleo ya nchi hii , kama alivyosema Mwalimu yana misingi ya vitu vinne
  • Watu
  • Ardhi
  • Siasa safi
  • Uongozi bora
Katika vitu hivyo vinne hapo juu, viwili vya kwanza ndio mtaji wa utajiri wetu. Hivyo viwili vya mwisho ndio msingi wa umasikini unaotukabiliwetu.
Ni suala la kusikitisha kwamba dira ya kisiasa na uchumi, nautekelezaji wake nchini hauko dhahiri na unasua sua.
Kwa wengi wetu masuala ya ufisadi unaotisha ni kielelezo kikubwa cha kusua sua huku.
Kwa waliosoma vitabu vya Marx, afikiri sasa hivi ndio kuna the silent class struggle pamoja na primitive accumlation of capital.
Masuala haya yasipodhibitiwa kwa sera zinazoeleweka si ajabu tukaishia kwenye violent class struggle, ambayo kwa uhakika ndio mapinduzi yenyewe.
Thanks Mchambuzi
 
Lole,
Nashukuru kwa mchango wako, hasa kwa kunipa moyo kwamba mada hii inajenga kwani wapo wanaosema inabomoa. Nimependa hoja yako kuhusu Violent Class Struggle Vis-a-Vis ile aliyoifafanua vizuri sana miaka ya sabini Profesa wetu mahiri Issa Shivji. Nadhani Violent Class Struggle imeshaanza kujitokeza, na ni hii volcano ambayo mwalimu aliizungumzia, na kutamka kwamba kwa jinsi hali inavyoendelea, watanzania watakuwa ni majuha na wapumbavu wasipoanza kutafuta mabadiliko kwa nguvu. Watanzania wa leo sio wajinga, kwani wanazidi kuelewa kwamba wanasiasa wanaposema nchi ipo imara kiuchumi, tena bila aibu wanapanda majukwaani na kutamka kwamba uchumi unakuwa kwa asilimia 7 kwa mwaka kwa miaka 12 mfululizo, wananchi wanaanza kujiuliza, uchumi huu unakuwa for who? Pole pole wanaanza kuelewa kwamba lazima kuna kundi la watu linalofaidika na ukuaji huu ambao faida yake haishuki kwa wale walio chini, badala yake faida hii inabakia huko huko juu ambapo wanasiasa na wawekezaji wanagawana kinachopatikana.

Nchi za wenzetu zenye uchumi kubwa kama USA, UK, uchumi ukikua kwa asilimia nne tu, uchumi wa namna hiyo una faida kubwa sana kwa walio wengi. Mara ya mwisho kwa uchumi wa marekani, Japan, UK, Ujerumani kukua kwa asilimai zaidi ya tano labda ni miaka 25 iliyopita. China, India, Brazil, uchumi wao ulikuwa una kua kwa asilimia zaidi ya saba kwa muda mrefu, na matokeo yake ni kwamba nchi hizo sasa haziitwi nchi maskini tena. Brazil ni nchi ya kumi kwa ukubwa kiuchumi duniani. China sasa ni ya pili baada ya Marekani. Nchi hizi za Brazil, China, India, zimefanikiwa kujenga middle class kubwa sana kutokana na kukua kwa uchumi wao kwa muda mrefu wa zaidi ya miaka kumi. Sisi Tanzania je? Kwanini Mwanakijiji ni yule yule kwa miaka 50? Na kwanini wanasiasa wa CCM hali zao zinabadilika kimaisha wakitumikia nafasi zao kwa miaka hata mitano tu?

CCM bado ina nafasi ya kubadilisha haya ingawa jua ndio linazidi kuzama.
 
1. Limemuua J.K Nyerere
2. Kaka zako Walioshiba Wanachukua Ubunge - Raza
3. Kaka wengine ambao hawakupenda jeshini sababu ni pachafu, vyakula vinaua, walipata Ubunge, Lau, Mwinyi, Dewji
4. Baba zetu walianza kuwa na Majumba kama Mahekalu sio moja Mia Lowassa, Mwinyi, Kikwete, na Mawaziri woote - Mkapa
5. Limeruhusu mauzo ya madawa ya kulevya sababu sheria mkononi
6. Sheria ya Uongozi Imevunjwa kwahiyo hakuna Nguzo kuu ya kuwa kiongozi unaweza kuua leo na kesho kuwa Rais wa nchi
 
Mkuu,
Kweli una hasira na Azimio La Zanzibar. Kwa mtazamo wako, ni mambo yepi ndani ya Azimio la Arusha tukiyarejea, yataweza kutatua baadhi ya matatizo uliyoyataja? Na je azimio la arusha linahitaji kufanyiwa marekebisho ya aina gani ili liendane na nyakati hizi?
 
Kubwa (pamoja na mengine) nilioliona katika Azimio la Arusha, ni ile deliberate attempt ya ku rationalize uchumi wa nchi, na ili kutekeleza hili, Na kwakuwa Viongozi ndio wenye dhamana ya distribution ya uchumi wa nchi, ndio pakawepo na "Maadili ya Viongozi" ambayo yalistipulate miiko ya uongozi, ili kuenforce hili, paliundwa Tume ya Kuchunguza Maadili ya Viongozi, ambayo viongozi waliiheshimu na kuiogopa sana. Ufisadi uliopo hivi sasa, ni matokeo ya Viongozi kukosa maadili, na wala hakuna proper mechanism ya kudhibiti uozo huu zaidi ya Politica rhetorics na token gestures za legal action ya kuwasukasuka mafisadi wachache waliofall out of line au out of touch! Angalia Ndugu Mchambuzi, hata sheria ya fedha haramu ilipopendekezwa na John Mnyika ifanyiwe marekebisho kwa kutoa adhabu Kali zaidi kwa wakosaji, wabunge wengi, hasa wa chama tawala walikataa, kwani ni dhahiri wengi wao wana aspirations za kifisadi. Kuna mahali Nyerere alisema, ingawa sikumbuki vyema ni wapi, kuwa " Ukombozi wa pili wa Taifa hili utakuwa mgumu zaidi, kwani ni afadhali kujikomboa kutoka wakoloni kutoka nje kuliko wakoloni wenzetu wenyewe!" (naweza kuwa nimekosea quote lakini context ni hiyo)
Mwisho napenda kuconclude kuwa, naona ilikuwa ni makosa makubwa kuliAbandon totally Azimio la Arusha, ingekuwa busara zaidi kama lingefanyiwa marekebisho ili liendane na wakati, altrnatively, the so called Azimio la Zanzibar limetuzalishia viongozi mafisadi ambao kwa nguvu zao za fedha hawataachia madaraka, imefikia sasa wameanza kuuana wenyewe kwa wenyewe kuwania kushika madaraka makubwa zaidi, lakini wanasahau ukweli, ma kama alivyosema Nyerere kwenye kitabu cha TUJISAHIHISHE kuwa "ukweli una tabia ya kumwadhibu mwenye kuupuuza" basi wajue wanazidi kuitengeneza ile Volcano ambayo hivi sasa ku Rumble, uroho wao wa madaraka na mali umewatia uziwi hivyo hawasikii sauti za awali za Volcano inayotaka kulipuka, kwani kwa hakika Watanzania siyo Wapumbavu wala Majuha wala Mazuzu, uvumilivu wetu usitafsiriwe hivyo, la hasha, ni suala la muda tu, kwani kama alivosema Abraham Lincoln, "Huwezi kuwafanya Wapumbavu Watu Wote Muda Wote!"
 
Mkuu,
Kweli una hasira na Azimio La Zanzibar. Kwa mtazamo wako, ni mambo yepi ndani ya Azimio la Arusha tukiyarejea, yataweza kutatua baadhi ya matatizo uliyoyataja? Na je azimio la arusha linahitaji kufanyiwa marekebisho ya aina gani ili liendane na nyakati hizi?
Bwana Muchambuzi, mimi nilsema nitarudi kwenye kajamvi kujadili mada hii.
Nimelala wee na kutafauri na nimeona mambo ambayo yanawatatiza watanzania ni yale yale ya siku zote, yaani umasikini na ujinga.
Hali ya Tanzania haiko tofauti sana na ilipokuwa marabaada ya uhuru miaka 50 iliyopita.
Mikakati ya maendeleo kwa ujumla bado haieleweki vyema kwa umma.
Mtu wa Sumbawanga , ili aendelee kwa kupaa, hajui leo kuna mikakati gani kiinchi katika kujikwamua.
Kama tulikuwa na Azimio la Arusha , ambalo lilitakiwa KUBORESHWA na Azimio La Zanzibar, je tunaenda mbele ki-dira au tunarudi nyuma.
Tatizo kubwa ninaloliona mimi ni umasikini, tena umasikini binafsi wa viongozi ambao unafanywa kuwa mbaya zaidi na kuwa na umasikini wa kimawazo.
Je kuna long-term strtegic plans zipi kiitikadi na kiuchumi kwa Taifa letu?
Kila anayeingia madarakani anataka kutatua matatizo ya mpito huku akikodolea macho wafadhili na waChina kwa matatizo ambayo yangeweza kutatuliwa kimkakati na wananchi wenyewe.
Lazima tukubali kwamba Uongozi Kitaifa umewaangusha wananchi-hasa mategemeo yao.
Ubepari, kama ndugu Muchamuzi ulivyodokeza, si tatizo,tatizo ni mikakati ya Kitaifa kudhibiti amendeleo na uchumi wetu ili utumikie wananchi.
Nchi kama Korea, sasa Vietnam zinaendelea kwa kasi, mimi sijui kwa nini hatutaki kusoma hii mifano hai.
 
Umenena mambo ya msingi sana. Tatizo letu ni umaskini na ujinga,lakini ujinga huu sio ule ambao Mwalimu alijaribu kuumaliza miongoni mwa maskini, bali ujinga wa sasa ni wa viongozi waliopo kwenye nafasi za kubadilisha hali mbaya ya umaskini miongoni mwa walio wengi lakini kwa sababu ya ujinga wao, watanzania wanazidi kudidimia katika tope la umaskini.

Azimio la Zanzibar limewafanya watanzania wengi kuwa maskini kuliko azimio la Arusha. Hili ni jambo lisilo na ubishi na takwimu zipo wazi. Lakini cha ajabu ni kwamba hakuna kiongozi anayejali hili, san asana wanajikita kwenye mikorogo mingi na isiyo na mpangilio – mara mkukuta, mara mkurabita, mara malengo ya millennia, mara dira ya 2020…, na hatuoni matokeo zaidi ya nyimbo zao majukwaani eti uchumi upo imara, na unakuwa kwa asilimia 7 kwa miaka 12 mfululizo. Je uchumi huu unakuwa kwa ajili au kwa manufaa ya nani? Hakika sio kwa manufaa ya wananchi walio wengi bali kukua huku kunavutia wawekezaji wengi waje zaidi hivyo kuwapatia viongozi 10% kwenye miradi ya migodi n.k, ambayo ndio sababu hasa ya kukua kwa uchumi wetu, lakini uchumi uchwara kwani madini hayo hayana faida yoyote kwa mtanzania, sio kwa njia ya kuzaa ajira, sio kwa njia ya kodi, si kwa njia yoyote yenye faida kwa wananchi walio wengi. Ukiondoa exports za dhahabu kwenye equation ya GDP yetu, uchumi wetu upo chini sana, pengine chini ya asilimia 5% kwa mwaka (growth).

CCM imeharibu kabisa dhana ya ubepari kwa kuufanya uonekane kama vile upo juu ya sheria. Uongozi umejikita zaidi kusafisha mafisadi badala ya kusafisha ubepari uliochafuliwa na ufisadi.

Na kinachokatisha tamaa walio wengi ni kwamba hakuna anaye hoji kiini cha matatizo haya. Kwa mfano, Mzee Mtei angehojiwa juu ya ujio wa IMF ambao yeye aliona IMF ndio malaika wa taifa hili baada ya kumkimbia Nyerere kwa imani kwamba Ujamaa na Azimio La Arusha lilikuwa ni tatizo la msingi kwanini mtanzania maskini. Matokeo ya IMF ni kwamba "mtanzania wa kawaida" wa sasa ni hoi kuliko mtanzania chini ya ujamaa. Ndio maana nazidi kusisitiza kwamba Chadema chini ya sera za za sasa, hawatakuwa na jipya zaidi ya kwenda ikulu kutekeleza mawazo yale yale ya CCM ambayo ni IMF development alternative kwa kasi zaidi na nguvu zaidi. Anaepingana na kauli hii, namkaribisha kwenye mjadala huo tujadili kwa hoja, takwimu, na ushahidi. Chadema ikiingia ikulu kwa sera zake za sasa, miaka kumi ni mingi kabla wananchi kuichoka na kutaka mbadala mwingine. Chadema haipigani dhidi ya ufisadi unaolelewa na CCM, kwa kulenga mizizi, inalenga matawi, kwani hata wao ruzuku za serikali ambazo wanapokea, zimejaa ufisadi- ruzuku kwa CCM, Chadema, ufisadi mtupu. Hizi fedha zingeenda kwenye maendeleo ya jamii. Mbali ya hilo, hata source ya hizo fedha ni zile zile za kifisadi ambazo ni za wawekezaji majangili ambao ndio wamiliki wa IMF na WorldBank, ambao wanatoa fedha hizo eti kwa kwa nia ya kukuza demokrasia na uchumi, wakati ukweli ni kwamba hii ni kwa ajili ya kufaidisha zaidi mataifa ya nje, sio watanzania waliopo vijijini.

Lakini pia kwanini vyama vikubwa havitaki ruzuku zao ziwe audited? wanaficha nini?

Ndio maana vikijitokeza vyama vipya ambavyo vinakuwa na mtazamo tofauti na ule wa CCM na Chadema, ambayo kimsingi ni sawa, kidogo huwa inafufua matumaini. Kwa mfano ujio wa CCK. Tunasubiri kuona chama hiki kitaziba vipi pengo hili la umaskini ambalo sababu yake kubwa ni sera za kiliberali zisizo na mchujo ambazo CCM imekuwa inazitekeleza tangia mwaka 1986, na Chadema ikiwa ndio muasisi wake chini ya mzee mtei akisaidiwa na IMF. NCCR, CUF nao wana changamoto hizi hizi, wote hawa wajitazame upya. Pia ni muhimu Chadema wakiri kuhusu hili la IMF na wabadilike. Wapo viongozi ndani ya chadema wenye uzalendo na nchi yetu, lakini sidhani kama wanajua kwamba wanacheza ngoma wasioijua.
 
Back
Top Bottom