UKAWA nendeni Mahakamani kesho 15/10/2015

UKAWA nendeni Mahakamani kesho 15/10/2015

Mkuu mawakala wanaweza tishwa.... wanaweza nunuliwa.... tumeyaona haya na kuyasikia wafuasi mahili wa upinzania kununuliwa.....
Hasa vijijini ambapo watu hawajazoea kuona polisi wenye silaha. Mfumo mzima wa NEC umetengenezwa kuibeba CCM. Kwa kweli Chadema (UKAWA) wana udhaifu mkubwa wa kutishia kwa mdomo bila kutumia mahakama na vyombo vingine vilivyopo kisheria. Si kazi ya tume, Rais au polisi kutafsiri sheria. Hiyo ni kazi ya mahakama.
 
Strategically bado wako na shida. . . .
 
Kikwete alishawahi kumletea nani kiroba cha sembe...labda ile sembe nyingine inayozungumzwa kuwa mwanae ni supplier, importer na exporter mkubwa wa mazao ya 'nafaka'.

Kila mtu anayajua maisha yake, kwani siku zote wewe ndio unawalisha?
Tatizo ni kwamba wengi wanadhani kwa kufanya hivi itasaidi 'goli la mkono' huku wakisahau kuwa wizi wa kura umefanyika karibia chaguzi zote zilizotangulia na mambo yalikuwa yakiwaendea vizuri waibaji wa kura. Kufanikiwa kwao kuiba kura ilikuwa ni kwa sababu walikuwa na watu 'smart' na wenye IQ za juu lakini katika kuvutana mikono na kuingizana wajomba, mama wadogo nk kwenye system safari hii walio nje nao wanaonekana kuwa even smarter kuzidi waliomo ndani na ndio maana hata wengine wakaropoka kabla uchaguzi hata haujafanyika.
Issue ya kuaminiana sio kwa cdm au UKAWA pekee bali ni asili yetu binadamu na ndio maana ukidondosha wallet yako yenye laki mbili alafu mtu akakuletea mita 500 kutoka ulipoidodosha bila kuchukua hizo pesa unamuona kama 'malaika'. Na hii ndio inapelekea kuwepo hata sheria ili zitubane sote! Kwani wewe unadhani huko Uswisi au Amerika mabenki hayawekewi ulinzi, ofisi za umma hazina code of conduct au unadhani mbali na Dr. Slaa wakina Blatter wa FIFA walikuwa hawalipwi mishahara na kuaminiwa!?

Kama mwanzoni wamesema vituo 70,000 na baada ya Duni kuliweka mezani wakavipunguza, kama JK anasema kuna wapiga kura 28 million huku tume ikisema 22 naturally kwa mwenye IQ ya kuanzia 18 kwenda juu lazima ashituke. Wasioshituka ni wenye below IQ 10 labda!

Mgombea urais wa TLP japo kuwa yuko na watu dizaini ya Mrema lakini yuko vizuri na nilimsikia akisema kuwa kosa kubwa kwa wasiosoma alama za nyakati safari hii ni kujaribu kumweka mshindi kwa nguvu. Alisema itakuwa very temporal na wakija kugundua hilo kosa basi Tanzania tunayoijua itakuwa sio yenyewe tena!

Hii nchi mambo yke mengi yanakatisha tamaa sana ni aibu kuona wasomi wetu wengi wanakosa maarifa na mbinu za kusaidia mambo kma hya yaweze kukaa sawa.Naweza kusema wapinzani wengi ndo wanaoonesha kua na uchungu na nchi hii.Wasom wengi waliomo ndani ya mfumo wa ccm akili zao zimefifishwa
 
The National Election Act Cap 343, inasema ni ndani ya mita 200, kuanzia mita 201+ ni ruksa!
 
Wanajamvi,

Hili suala la kubaki vituoni baada ya kupiga kura linaanza leta ukakasi sasa, leo Mh. Raisi kaliongelea na kusisitiza watakaobaki vituoni watashughulikiwa. Nimemsikia mhe. Kinana na IGP pia wakiliongelea na mbaya zaidi kwenye magroup yote wana CCM wamefurahia sana tamko la leo la mh. Raisi ambae pia ni Amiri jeshi mkuu katika nchi ambayo Tume ya Uchaguzi haiko huru, tumeona wakurugenzi wa tume wakibadilishwa chini ya mwezi mmoja kabla ya uchaguzi kwa sababu za kikatiba/kisheria maana mhe. Raisi ana uwezo huo.

Lakini pia tuna kumbukumbu za chaguzi zilizo pita ambapo bila wananchi kuwepo eneo la tukio, sina uhakika kama mh. Wenje angepata ushindi zaidi ya mh. Masha aliye kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Hii yote inaleta Sintofahamu na kuonyesha kama ule usemi wa Nape unatimizwa kwa njia hii.

Pia nimemuona Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC akiiweka kama issue ya kubaki kwenye vituo haiko kisheria.

Je, kama suala la kubaki vituoni kwa umbali usiopungua mita 100 liko kisheria, ni kwa nini UKAWA wasiende mahakamani kesho kwa hati ya dharula kuweza pata ufafanuzi na order ya mahakama kwenye jambo hili?

Nia ni kuepusha damu za Watanzania kumwagika maana ninavyoona, tunakoelekea sio kuzuri ifikapo tarehe 25 Oktoba.

Nawakilisha.

Mkuu ushauri mzuri sana huu, UKAWA wasipouzingatia nitawashangaa
 
Acheni uhuni wenu.kila mtu akibaki kituoni itakuwa fujo.wewe huelewi nini!

Watu 450!

Fujo itatoka wapi?

Hakuna umeme, radio/tv zitatupaje taarifa?

Kuna haja gani ya kubandika matokeo kama hadhira haipo?
 
Mmezoea kubembelezwa Watanzania. . . .Kama una hakika na sheria isemavyo fine be there. . . . . Hili lilihitaji mjadala??!!
High IQ unajenga premises tu conclusion inakuja automatically. . . . . .

Kama una uhakika be there. . . .
section 4(1) of The National election.Act Cap343, imesema ndani ya mita 200 ambapo huruhusiwi kukusanyika ,kuvaa nembo ya chama au sare za Chama, huu unaosemwa na Tume ni uongo
 
Watu 450!

Fujo itatoka wapi?

Hakuna umeme, radio/tv zitatupaje taarifa?

Kuna haja gani ya kubandika matokeo kama hadhira haipo?

Mkuu Kura Zinahesabiwa Na Vituo Vinafungwa Saa Ngapi Na Nyie Mnataka Kukaa Kuanzia Saa Ngapi?
Kama Tatizo Ni Kujua Matokeo Kwanini Msiende Kuanzia Saa 10 Wakati Vituo Vikiwa Vinafungwa?
 
Wanajamvi,

Hili suala la kubaki vituoni baada ya kupiga kura linaanza leta ukakasi sasa, leo Mh. Raisi kaliongelea na kusisitiza watakaobaki vituoni watashughulikiwa. Nimemsikia mhe. Kinana na IGP pia wakiliongelea na mbaya zaidi kwenye magroup yote wana CCM wamefurahia sana tamko la leo la mh. Raisi ambae pia ni Amiri jeshi mkuu katika nchi ambayo Tume ya Uchaguzi haiko huru, tumeona wakurugenzi wa tume wakibadilishwa chini ya mwezi mmoja kabla ya uchaguzi kwa sababu za kikatiba/kisheria maana mhe. Raisi ana uwezo huo.

Lakini pia tuna kumbukumbu za chaguzi zilizo pita ambapo bila wananchi kuwepo eneo la tukio, sina uhakika kama mh. Wenje angepata ushindi zaidi ya mh. Masha aliye kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Hii yote inaleta Sintofahamu na kuonyesha kama ule usemi wa Nape unatimizwa kwa njia hii.

Pia nimemuona Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC akiiweka kama issue ya kubaki kwenye vituo haiko kisheria.

Je, kama suala la kubaki vituoni kwa umbali usiopungua mita 100 liko kisheria, ni kwa nini UKAWA wasiende mahakamani kesho kwa hati ya dharula kuweza pata ufafanuzi na order ya mahakama kwenye jambo hili?

Nia ni kuepusha damu za Watanzania kumwagika maana ninavyoona, tunakoelekea sio kuzuri ifikapo tarehe 25 Oktoba.

Nawakilisha.

Mkuu naomba tu nikwambie ukweli kuwa hujui unachokisema. Hivi hata ukitumia akili yako ya kawaida unaona inawezekana watu wa vyama vyote wakalinde kura kweli? Mbona mnataka kuletea hii nchi vurugu zisizo na maana? Ni kweli wewe hujui binadamu huwa hawawazi the same?

Ukikusanya watu elfu moja au hata billion moja hakuna hata mmoja kati yao atafanana mawazo na mwingine. Hao watu unaotaka wakalinde kura umehakikisha kuwa watakuwa wanawaza kama wewe yaani kulinda tu kura na wasifanye fujo?

Nyie wengine humu nishagundua ni kati ya wale wasiokuwa na huruma na nchi na familia zenu. Sasa hivi nyie mnahifadhi wakimbizi wengi wa burundi. Jaribu kuangalia wewe utakimbilia wapi halafu ndiyo uanze kushabikia huo upuuzi wako. Nakutakia uchaguzi mwema.
 
Tutalinda kura. Mimi ntakuwa mstari wa mbele kati ya watakao kaa kituoni

Mkuu utazilindaje? utalazimisha kubaki ndani kuhesabu? sioni jinsi gani utakavyozilinda kwa kukaa nje ya mita 100
 
Mkuu naomba tu nikwambie ukweli kuwa hujui unachokisema. Hivi hata ukitumia akili yako ya kawaida unaona inawezekana watu wa vyama vyote wakalinde kura kweli? Mbona mnataka kuletea hii nchi vurugu zisizo na maana? Ni kweli wewe hujui binadamu huwa hawawazi the same?

Ukikusanya watu elfu moja au hata billion moja hakuna hata mmoja kati yao atafanana mawazo na mwingine. Hao watu unaotaka wakalinde kura umehakikisha kuwa watakuwa wanawaza kama wewe yaani kulinda tu kura na wasifanye fujo?

Nyie wengine humu nishagundua ni kati ya wale wasiokuwa na huruma na nchi na familia zenu. Sasa hivi nyie mnahifadhi wakimbizi wengi wa burundi. Jaribu kuangalia wewe utakimbilia wapi halafu ndiyo uanze kushabikia huo upuuzi wako. Nakutakia uchaguzi mwema.
Mkuu sheria inasemaje? Mbona huongelei experience ya Wenje na je watu 450 kweli wanaweza fanya fujo?
 
Sikatai "i may still be young" but a minded developed sane guy.Watch out brother,Your mind is in Mbowe's trouser pocket.
Not young..I said small....kichwani. Talk about Mbowe, that's your opinion and one guy once said "opinions are like 'as...holes', everybody's got one"
 
Sio suala la kumwamini wakala au kutomwamini, sheria ya uchaguzi inasemaje baada ya kupiga kura, kama inaruhusu watu kukaa umbali usiopungua mita 100, hao wanaozuia wanatumia kigezo gani?

SIO KWELI, Kukaa mita 100, au 200 au 350 ni UVUNJAJI WA SHERIA! tafuta ukweli na ukweli utakuweka huru.
 
Kuna nguchiro huwa wanapiga kura maofisini Kisha wanazileta zihesabiwe. Hao ndio wanatakiwa kuzuiliwa kuingia chumba cha kura. Mawakala wanaweza kununuliwa au hata kutishwa na wakati mwingine kusingiziwa wanaleta fujo pindu wanapo protest hujuma. Wanaitiwa Polisi, wanakuwa detained na hii inampa nafasi msimamizi wa uchaguzi ambaya ni kada tu wa CCM kuandaa matokeo anayotaka. Pia wakati mwingine kuwepo Watu nje ya kituo kunawakumbusha mawakala kuwa kununuliwa ni hatari kwao na pia kuwa kuna support nje in case maharamia wakitaka kuanzisha udhalimu wao. Purely simple.

Well, sasa wewe mtu wa UKAWA ukitaka kubaki kulinda kura yako (presumably haumwamini mtu yeyote au unaona wakala wako hana nguvu), na CCM nao na ACT nao wabaki unadhani hapo nje ya kituo PATATOSHA?

Back
Top Bottom