UKAWA nendeni Mahakamani kesho 15/10/2015

UKAWA nendeni Mahakamani kesho 15/10/2015

Akivunjwa miguu atakuwa na bahati sana, wengine hutolewa upepo halafu viongozi wa vyama vyao hutunza familia zao!

Tumeona Arusha &Moro familia za marehemu (watu waliouawa kwenye maandamano) zinavyo saidiwa na Mbowe!
hatudanganyiki tunapiga kura na kwenda kulala nyumbani
 
Umeshaambiwa piga kura sepa unalinda kura kwani wewe ni wakara sasa mjifanye wabishi upige kura ukae kituoni uone kitakacho kutokea unavunjwa miguu unasekwa ndani tii sheria bila shuruti vinginevyo utaona vyombo vyadola vinavyo fanya kazi yake
Sheria inaniambia nisubiri matokeo mita zisizopungua 100 toka kituoni. Ni Sheria ipi inakataza hilo?
 
Hebu jiulizeni kwanini Wana ccm Wana furaha sana na kauli hizi za kupiga kura na kuondoka? Jua kua wanajua tume na polis vyote vipo chini yao. Mfano mwaka 2010 majimbo mengi hujuma zikifanywa na viongozi wa serikali na ccm mf sumbawanga, Shinyanga na Ulanga mashariki na hii yote ulinzi hakua mkari. Mwaka huu hatukubali hatukubali hatukubali! Mbona wanaintarahamwe wote wa nafurahi a kauli hizi? Kuna nini mpaka wao wasiwe na hofu kuibiwa. Jibu kila mmoja analo. Hatutakubali vitisho hivi.
 
Hivi nyie mnaowaza kuibiwa kura, mawakala wenu wanafanya kazi gan ndan ya kituo

Hili suala liko kwenye sheria, ukimkamata MTU aliyeko umbali unaokubalika na sheria kutoka kituoni utamshitaki kwa kifungu kipi?
Hakuna haja ya kwenda mahakamani, ni kupoteza muda!
Mimi nitakaa umbali unaokubalika kisheria ie at most 200m. Sina haja ya kufundishwa na yeyote kuhusu jambo hili lililo wazi kwenye sheria. Wakibandika tu matokeo naenda kituoni kusoma matokeo, vinginevyo waseme hawatabandika! Wakibandika ni kwa sababu ya kutoa taarifa kwa wananchi!! Na hakuna namna nyingine ya watu kuipokea taarifa wanayopewa zaidi ya kwenda kituoni kusoma tangazo hili la matokeo kwa kituo husika! Vinginevyo katika siku zilizobaki wapeleke muswaada bungeni waifanyie marekebisho hiyo sheria ya uchaguzi!!!!!
 
Wanajamvi,

Hili suala la kubaki vituoni baada ya kupiga kura linaanza leta ukakasi sasa, leo Mh. Raisi kaliongelea na kusisitiza watakaobaki vituoni watashughulikiwa. Nimemsikia mhe. Kinana na IGP pia wakiliongelea na mbaya zaidi kwenye magroup yote wana CCM wamefurahia sana tamko la leo la mh. Raisi ambae pia ni Amiri jeshi mkuu katika nchi ambayo Tume ya Uchaguzi haiko huru, tumeona wakurugenzi wa tume wakibadilishwa chini ya mwezi mmoja kabla ya uchaguzi kwa sababu za kikatiba/kisheria maana mhe. Raisi ana uwezo huo.

Lakini pia tuna kumbukumbu za chaguzi zilizo pita ambapo bila wananchi kuwepo eneo la tukio, sina uhakika kama mh. Wenje angepata ushindi zaidi ya mh. Masha aliye kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Hii yote inaleta Sintofahamu na kuonyesha kama ule usemi wa Nape unatimizwa kwa njia hii.

Pia nimemuona Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC akiiweka kama issue ya kubaki kwenye vituo haiko kisheria.

Je, kama suala la kubaki vituoni kwa umbali usiopungua mita 100 liko kisheria, ni kwa nini UKAWA wasiende mahakamani kesho kwa hati ya dharula kuweza pata ufafanuzi na order ya mahakama kwenye jambo hili?

Nia ni kuepusha damu za Watanzania kumwagika maana ninavyoona, tunakoelekea sio kuzuri ifikapo tarehe 25 Oktoba.

Nawakilisha.

Mbaya zaidi watu wakibaki kituoni wataanza kuongelea siasa kitu ambacho ni hatari kwa siku iyo bora tu kila moja arudi kwake
 
mkuu unadhani siwez weka tusi hapa la kukukera? Kuwa muungwana tu.... cha msingi je sheria inasemaje? Mbona nchi nyingine wapiga kura wanabaki ..... sio lazima kulinda kura lakini kusubiri matokeo na ndo maana yanabandikwa vituoni.... sasa mnayabandika ya nn kama watu hawatakuwepo?

Na hata Kabla ya kubandikwa, yanasomwa kwanza.
 
Mawakala huwa wanatishwa ndani ya vituo wanahitaji support kutoka nje presence ya wanachama huwa inawatoa hofu.
 
Kazi ya kulinda kura lowasa aliambiwa aachiwe hiyo kazi nyie mmpigie tuuu kura kihere here cha nini subilini mtakiona cha mtema kuni pumbavu sana nyie sijui hamjielewi
 
Kinacho wafanya mtake kug'ang'ania kubaki vituoni ni kitu gani?

Je mawakala wenu wajibu wao ni nini? Mbinu za viongozi wenu za kutaka kuhamasisha wafuasi wao ili walete vurugu kwenye vituo vya kupigia kura kutokana na imani zenu potofu za kuibiwa kura - viongozi wenu wasipo chunga kauli zao wanapokuwa majukwaani,basi wachukuliwe hatua stahiki kabla hawaja tuletea balaa kwenye Taifa letu - hatutaki chokochoko na tactics za KIMUNGIKI nchini,kama wanajidanganya kwamba Serikali yetu Tukufu itaogopa lawama na kuwachia watu wachache wawe chanzo cha kuvuruga amani ili Nchi hisitawalike basi wataishia kwenye slammer na hakuna ataye wasikitikia.

Waliosema wataingia msituni walikuwa wanahubiri injili ya amani siyo?
 
Kamanda tunauzoefu na mahakama zetu. Wengi was majaji ni wana was system wanaweza wakatumika kutoa tafsiri mbovu na ya ajabu. Au wakachelewesha huo uamuzi.Duniani kote including Nigeria inaruhusiwa. Na raisi hana mamlaka ya kuzungumzia mambo ya uchaguzi. Ni tume tu ndiyo yenye mamlaka hayo. Dawa yake ni watu kujipanga na kukaa nje ya vituo kwa mita hizo. Kama ni kosa watupe vifungu vya sheria otherwise tusubiri matokea. Wasije wakataka kuwalazimisha mawakala. ICC is waiting.

Who is ICC toa ujinga wako, mahakama hazikuwekwa kwa ajili ya wanyama au miti. Serikali haiwezi kuacha wajinga wachache walithiri taifa kisa kuogopa ICC. Kupigwa mtapigwa na kuvunjwa vyunjwa na ICC kama kuna wa kwenda ataenda lkn nyie mtabaki walemavu maisha yenu yote, maana hakuna namna tena, tumechoka na kutishiwa na nyau wa ICC.
 
Raisi amesema MAWAKALA tu ndio wanatakiwa kubaki na wawe ndani ya chumba cha kura. sasa ina maana HUWAAMINI mawakala wako?

Kuna nguchiro huwa wanapiga kura maofisini Kisha wanazileta zihesabiwe. Hao ndio wanatakiwa kuzuiliwa kuingia chumba cha kura. Mawakala wanaweza kununuliwa au hata kutishwa na wakati mwingine kusingiziwa wanaleta fujo pindu wanapo protest hujuma. Wanaitiwa Polisi, wanakuwa detained na hii inampa nafasi msimamizi wa uchaguzi ambaya ni kada tu wa CCM kuandaa matokeo anayotaka. Pia wakati mwingine kuwepo Watu nje ya kituo kunawakumbusha mawakala kuwa kununuliwa ni hatari kwao na pia kuwa kuna support nje in case maharamia wakitaka kuanzisha udhalimu wao. Purely simple.
 
Mkiambiwa watu Wana uzoefu hamuelewi, mnapiga kelele... Ni kwamba mawakala wengi si WAZALENDO sana, wanahongwa pesa ndefu aka wananunuliwa, na ndio maana Tume wamekataa UKAWA wa we na mawakala wa vyama vyao, stuka toroka uje

Sasa mkuu mawakala kuhongwa kirahisi ni organizational problem kwa nini mnataka kuleta vurugu?
Narudia wakati wa upigaji wa kura rudini nyumbani. Jioni upigaji kura ukimalizika rudini kusikiliza matokeo. Mkiweka kibaraza mnaleta Voters' intimidation yaani mnatishia wapiga kura wengine.
Mbona kinaeleweka?
 
Hapa kuna hatari ya kutokea vita hata kabla ya matokeo kutangazwa, waache ubabe hao ccm hii nchi ni yetu sote, kama hupendwi kubali ushindwe kihalali. tume ya uchaguzi haiaminiki.

Labda vita vya kwenye keyboard. Acha kupotosha watu. Piga kura yako, rudi nyumbani kwako au kwenu. Subiri matokeo kutangazwa. Vinginevyo kama hamuiamini tume ya uchaguzi wapo waangalizi wa kimataifa
 
Si kila mtu atabaki kituoni lakini wanaotaka kubaki waachwe wabaki kwa mujibu wa Sheria. By the way, wapiga kura wote wakiondoka vituoni, msimamizi wa uchaguzi atamtangazia nani matokeo? Au watapiga kengele kuita Watu? Kama suala la kusubiri matokeo lipo kisheria, kwa nini. NEC, IGP na hata Rais wanaliongelea kama ni jambo linalofanywa kinyume cha Sheria? Sheria hiyo kwa nini hawakuifuta 'kisheria' kama wanaona hawaipendi. Nami nashauri wanasheria wa CHADEMA/UKAWA wakatafute ufafanuzi mahakamani.

Utangazaji wa kura ni BAADA YA upigaji kura. Ila wakati kura zinapigwa hakuna kubaki. Mbona mwaka 2010 hamkubaki? Mbona sheria iko wazi?
 
Wakati upigaji kura unaendelea kwa nini wabaki vituoni? Mwaka 2010 ilikuwa hivi: tulipiga kura tukarudi nyumbani. Saa 10 au saa 11 tukarudi vituoni na tukakesha hata siku 3 ilipotakiwa. Hawa viongozi wanaotaka hata wakati wa upigaji kura wabaki wanafanya VOTER INTIMIDATION na hakuna panapokubalika hilo duniani. Ukimaliza kupiga kura nenda nyumbani na urudi kupata matokeo.

Acha uzushi. Watu walioko mita 200 na ambao hawana utambulisho wa kundi lolote la siasa watamtishaje mpiga kura aliyeko ndani?

Pili, Unaweza kuniambia kwa nini 2010 ilichukua siku 3 kwa baadhi ya majimbo kutangazwa mshindi?
 
Who is ICC toa ujinga wako, mahakama hazikuwekwa kwa ajili ya wanyama au miti. Serikali haiwezi kuacha wajinga wachache walithiri taifa kisa kuogopa ICC. Kupigwa mtapigwa na kuvunjwa vyunjwa na ICC kama kuna wa kwenda ataenda lkn nyie mtabaki walemavu maisha yenu yote, maana hakuna namna tena, tumechoka na kutishiwa na nyau wa ICC.

kumbuka hata wapigaji wamechoka na system na kupiga watu ,

utapiga more than 15 000000 si wazimu ni kitu gani


Mnaishi dunia ipi nyinyi ???
 
Unalinda nini nje ya kituo cha kura?

Huamini mawakala wa ukawa waliopo ndani ya vituo? Huamini wasimamizi wa Kimataifa? Huwaamini NEC waliopo ndani ya vituo?

Hawa watu wanataka kuleta fujo tu, washughulikiwe ipasavyo.
 
inakuwaje mnatumia chopa za kumwaga halafu mnashindwa kuwalipa vizuri mawakala wenu ili kuondoa wasiwasi.
hii ni ajabu sana ikiwa hata wakala humuamini sasa utanuamini nani?

Mkuu, nasubiri wanijibu hili. Yaani matatizo yao ya ndani wanataka kuleta vurugu maana vyama vyote vikiamua kulinda kura kwa kubaki kituoni ni uendawazimu!
 
Back
Top Bottom