nyeti za kuku
Member
- Aug 13, 2015
- 49
- 10
Kila wanachoongela ccm jamani mkipime mara2 sio akili zao jamani wamepagawa
Kwan nchi nzima imesongamana kama dar?? Kuna maeneo mengi sana ya wazi maeneo mengineyo ya Tanzania mkuu wangu. Hata mkisema suala la sheria za serikali za mitaa....zimeshindwa kuua vijiwe vya bangi leo ndo mtazuia watu kukaa tena wakisubir matokeo ya uchaguz?? Hapana.
Ujue Vitu Vingine Inabidi Tuwe Tunafikiria Kidogo,mkuu Wewe Unapiga Kura Saa Ngapi Na Matokeo Yanatangazwa Saa Ngap?
Kura zitalindwa bila shaka yoyote .Acheni uhuni wenu.kila mtu akibaki kituoni itakuwa fujo.wewe huelewi nini!
Bavicha wakibaki vituoni kulinda kura, nao UVCCM watakuwa na haki kubaki vituoni kulinda kura.Acheni uhuni wenu.kila mtu akibaki kituoni itakuwa fujo.wewe huelewi nini!
Sasa mkuu mawakala kuhongwa kirahisi ni organizational problem kwa nini mnataka kuleta vurugu?
Narudia wakati wa upigaji wa kura rudini nyumbani. Jioni upigaji kura ukimalizika rudini kusikiliza matokeo. Mkiweka kibaraza mnaleta Voters' intimidation yaani mnatishia wapiga kura wengine.
Mbona kinaeleweka?
Wanajamvi,
Hili suala la kubaki vituoni baada ya kupiga kura linaanza leta ukakasi sasa, leo Mh. Raisi kaliongelea na kusisitiza watakaobaki vituoni watashughulikiwa. Nimemsikia mhe. Kinana na IGP pia wakiliongelea na mbaya zaidi kwenye magroup yote wana CCM wamefurahia sana tamko la leo la mh. Raisi ambae pia ni Amiri jeshi mkuu katika nchi ambayo Tume ya Uchaguzi haiko huru, tumeona wakurugenzi wa tume wakibadilishwa chini ya mwezi mmoja kabla ya uchaguzi kwa sababu za kikatiba/kisheria maana mhe. Raisi ana uwezo huo.
Lakini pia tuna kumbukumbu za chaguzi zilizo pita ambapo bila wananchi kuwepo eneo la tukio, sina uhakika kama mh. Wenje angepata ushindi zaidi ya mh. Masha aliye kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.
Hii yote inaleta Sintofahamu na kuonyesha kama ule usemi wa Nape unatimizwa kwa njia hii.
Pia nimemuona Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC akiiweka kama issue ya kubaki kwenye vituo haiko kisheria.
Je, kama suala la kubaki vituoni kwa umbali usiopungua mita 100 liko kisheria, ni kwa nini UKAWA wasiende mahakamani kesho kwa hati ya dharula kuweza pata ufafanuzi na order ya mahakama kwenye jambo hili?
Nia ni kuepusha damu za Watanzania kumwagika maana ninavyoona, tunakoelekea sio kuzuri ifikapo tarehe 25 Oktoba.
Nawakilisha.
Tutasubiri matokeo ya kituo husika na sio ya nchi nzima mkuu....kwan watahesabu wiki nzima kituo kimoja??
haya bana nendeni kulala vituoni kulinda kura kila la kheri.Kwan wakati wa kupiga kura wanaccm watatengwa na waupinzani? "Think twice "
Patatosha. And by the way, hatutakuwa tumevaa jezi za vyama vyetu maana ni kosa kisheria. Na naturally, si kila mtu atabaki. lakini ni lazima wabaki watu wa kutosha kuhakikisha vituo vinakuwa free of intrusion by "caterers" wanaoleta kura kwenye "hot-pots" za "chakula" na chupa za chai!Well, sasa wewe mtu wa UKAWA ukitaka kubaki kulinda kura yako (presumably haumwamini mtu yeyote au unaona wakala wako hana nguvu), na CCM nao na ACT nao wabaki unadhani hapo nje ya kituo PATATOSHA?
Acheni uhuni wenu.kila mtu akibaki kituoni itakuwa fujo.wewe huelewi nini!
Hivi nyie mnaowaza kuibiwa kura, mawakala wenu wanafanya kazi gan ndan ya kituo