UKAWA nendeni Mahakamani kesho 15/10/2015

UKAWA nendeni Mahakamani kesho 15/10/2015

Raisi amesema MAWAKALA tu ndio wanatakiwa kubaki na wawe ndani ya chumba cha kura. sasa ina maana HUWAAMINI mawakala wako?

Sio suala la kumwamini wakala au kutomwamini, sheria ya uchaguzi inasemaje baada ya kupiga kura, kama inaruhusu watu kukaa umbali usiopungua mita 100, hao wanaozuia wanatumia kigezo gani?
 
Hakuna sheria inayowataka wanaosubiri matokeo kuwa umbali huo, bali inaruhusu meetings kuwepo kuanzia umbali huo, sasa mkitaka kufanya meetings ni lazima muwe na kibali toka polisi cha kukusanyika, hivyo watu hao wanaotaka kukaa mita 200 waombe kabisa kibali polisi,wasiporuhusiwa maana yake sheria haipo upande wao.

Nani kasema watafanya mkutano/kikao hadi waombe kibali polisi? Mara ngapi tumeshuhudia mikutano/maandamano ikiahirishwa na polisi licha ya wahusika kua na vibali halali?
 
Kamanda tunauzoefu na mahakama zetu. Wengi was majaji ni wana was system wanaweza wakatumika kutoa tafsiri mbovu na ya ajabu. Au wakachelewesha huo uamuzi.Duniani kote including Nigeria inaruhusiwa. Na raisi hana mamlaka ya kuzungumzia mambo ya uchaguzi. Ni tume tu ndiyo yenye mamlaka hayo. Dawa yake ni watu kujipanga na kukaa nje ya vituo kwa mita hizo. Kama ni kosa watupe vifungu vya sheria otherwise tusubiri matokea. Wasije wakataka kuwalazimisha mawakala. ICC is waiting.

Sasa mbona mgombea wenu anadai tumpeleke mahakamani kuhusu Richmond? Leo hii hamna imani na mahakama? Dah mna short memory!
 
asipelekwe mgombea wenu kwa kesi za ufisadi apelekwe mkuu wa nchi!! maajabu ya dunia
 
Kinacho wafanya mtake kug'ang'ania kubaki vituoni ni kitu gani?

Je mawakala wenu wajibu wao ni nini? Mbinu za viongozi wenu za kutaka kuhamasisha wafuasi wao ili walete vurugu kwenye vituo vya kupigia kura kutokana na imani zenu potofu za kuibiwa kura - viongozi wenu wasipo chunga kauli zao wanapokuwa majukwaani,basi wachukuliwe hatua stahiki kabla hawaja tuletea balaa kwenye Taifa letu - hatutaki chokochoko na tactics za KIMUNGIKI nchini,kama wanajidanganya kwamba Serikali yetu Tukufu itaogopa lawama na kuwachia watu wachache wawe chanzo cha kuvuruga amani ili Nchi hisitawalike basi wataishia kwenye slammer na hakuna ataye wasikitikia.

Wakati upigaji kura unaendelea kwa nini wabaki vituoni? Mwaka 2010 ilikuwa hivi: tulipiga kura tukarudi nyumbani. Saa 10 au saa 11 tukarudi vituoni na tukakesha hata siku 3 ilipotakiwa. Hawa viongozi wanaotaka hata wakati wa upigaji kura wabaki wanafanya VOTER INTIMIDATION na hakuna panapokubalika hilo duniani. Ukimaliza kupiga kura nenda nyumbani na urudi kupata matokeo.
 
Wanajamvi,

Hili suala la kubaki vituoni baada ya kupiga kura linaanza leta ukakasi sasa, leo Mh. Raisi kaliongelea na kusisitiza watakaobaki vituoni watashughulikiwa. Nimemsikia mhe. Kinana na IGP pia wakiliongelea na mbaya zaidi kwenye magroup yote wana CCM wamefurahia sana tamko la leo la mh. Raisi ambae pia ni Amiri jeshi mkuu katika nchi ambayo Tume ya Uchaguzi haiko huru, tumeona wakurugenzi wa tume wakibadilishwa chini ya mwezi mmoja kabla ya uchaguzi kwa sababu za kikatiba/kisheria maana mhe. Raisi ana uwezo huo.

Lakini pia tuna kumbukumbu za chaguzi zilizo pita ambapo bila wananchi kuwepo eneo la tukio, sina uhakika kama mh. Wenje angepata ushindi zaidi ya mh. Masha aliye kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Hii yote inaleta Sintofahamu na kuonyesha kama ule usemi wa Nape unatimizwa kwa njia hii.

Pia nimemuona Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC akiiweka kama issue ya kubaki kwenye vituo haiko kisheria.

Je, kama suala la kubaki vituoni kwa umbali usiopungua mita 100 liko kisheria, ni kwa nini UKAWA wasiende mahakamani kesho kwa hati ya dharula kuweza pata ufafanuzi na order ya mahakama kwenye jambo hili?

Nia ni kuepusha damu za Watanzania kumwagika maana ninavyoona, tunakoelekea sio kuzuri ifikapo tarehe 25 Oktoba.

Nawakilisha.

Mahakama si mnasema za ccm leo limekuwa kimbilio lenu
 
kikwete atajichafulia cv yk yt aliyopata kimataifa,,,, muach aendelee kuchez n kur zetu
 
Bwana mdogo linapokuja jambo la kisheria huwa hakuna uhuni...

Kama sheria imefafanua jambo hili kwa nini uogope wahusika wakienda mahakamani kupewa muongozo?

Acheni uhuni wenu.kila mtu akibaki kituoni itakuwa fujo.wewe huelewi nini!
 
Wanajamvi,

Hili suala la kubaki vituoni baada ya kupiga kura linaanza leta ukakasi sasa, leo Mh. Raisi kaliongelea na kusisitiza watakaobaki vituoni watashughulikiwa. Nimemsikia mhe. Kinana na IGP pia wakiliongelea na mbaya zaidi kwenye magroup yote wana CCM wamefurahia sana tamko la leo la mh. Raisi ambae pia ni Amiri jeshi mkuu katika nchi ambayo Tume ya Uchaguzi haiko huru, tumeona wakurugenzi wa tume wakibadilishwa chini ya mwezi mmoja kabla ya uchaguzi kwa sababu za kikatiba/kisheria maana mhe. Raisi ana uwezo huo.

Lakini pia tuna kumbukumbu za chaguzi zilizo pita ambapo bila wananchi kuwepo eneo la tukio, sina uhakika kama mh. Wenje angepata ushindi zaidi ya mh. Masha aliye kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Hii yote inaleta Sintofahamu na kuonyesha kama ule usemi wa Nape unatimizwa kwa njia hii.

Pia nimemuona Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC akiiweka kama issue ya kubaki kwenye vituo haiko kisheria.

Je, kama suala la kubaki vituoni kwa umbali usiopungua mita 100 liko kisheria, ni kwa nini UKAWA wasiende mahakamani kesho kwa hati ya dharula kuweza pata ufafanuzi na order ya mahakama kwenye jambo hili?

Nia ni kuepusha damu za Watanzania kumwagika maana ninavyoona, tunakoelekea sio kuzuri ifikapo tarehe 25 Oktoba.

Nawakilisha.

Pia waitishe press conference kuelezea vifungu vinavyo ruhusu uwepo wa watu ndani ya mita mia moja, pamoja na kulaani uvunjaji wa wazi wa sheria unao fanywa na wana ccm wakishirikiana na tume, Polisi.
 
Tatizo ccm mnafurahi ili mpate kuiba kura ndo mana kikinuka wote tutaumia we need fair ground kabisa sasa tegemeeni msaada wa jeshi mwaka uu Mpaka kieleweke tu.

[COLOR=]Muulizeni Lowassa,Kingunge na Sumaye Kura zinaibwaje maana wameshiriki kuiba pia Tangu 1995!![/COLOR]
 
Kamanda tunauzoefu na mahakama zetu. Wengi was majaji ni wana was system wanaweza wakatumika kutoa tafsiri mbovu na ya ajabu. Au wakachelewesha huo uamuzi.Duniani kote including Nigeria inaruhusiwa. Na raisi hana mamlaka ya kuzungumzia mambo ya uchaguzi. Ni tume tu ndiyo yenye mamlaka hayo. Dawa yake ni watu kujipanga na kukaa nje ya vituo kwa mita hizo. Kama ni kosa watupe vifungu vya sheria otherwise tusubiri matokea. Wasije wakataka kuwalazimisha mawakala. ICC is waiting.
Lowassa atatimkia nyumbani kwake Uingereza,Mbowe Dubai.Wengine watakapokuwa wanapelekwa ICC wewe utakuwa KABURINI MUDA HUO.Wazazi na wako watakuwa wanahangaika ukimbizini.
 
Acheni uhuni wenu.kila mtu akibaki kituoni itakuwa fujo.wewe huelewi nini!

Nani ataleta fujo zaidi ya wale wenye mazoea na nia ya kuvunja sheria?

Lini watanzania walipokusanyika walifanyiana fujo kama si ccm wanaojiweka juu ya sheria?

Mipirani, misibani, makazini, nyumba za ibada, masokoni, kwenye vyombo vya usafiri n.k Watanzania wamkuwa wakikutana na kuhitimisha shughuli zao kwa amani bila fujo pamoja na tofauti zao za kivyama. Inakuwaje kwenye ushindi na upatikanaji wa viongozi wao watakaoshinda kwa wingi wakura wakatazwe kukutanika kwamba watafanyiana fujo?

Hiyo amri ya watu kutokukusanyika paomja itaendlea hadi miaka mitano ya utawala huo itakapokwisha? Kwa nini muone hatari ipo tu siku ya uchaguzi?

Ninashauri nguvu ambayo Kinana, Lubuva na Kikwete wamepanga kuitumia kuua wapinzani, (kama wanaamini kwamba vita haina macho na wao ni marehemu wtarajiwa), itumike kuwalinda hao wanaokaa mita 200 ili wakae kwa amani pasiwe na fujo. Na hao waliopangwa kutuua, wahakikishe tunasubiri matokeo na kushangilia kwa amani baada ya matangazo.

Kifo ni mara moa na watu wote nao watakufa ila huwa tunatangulizana. Ninaamini nikiuawa na kikwete, kinana na lubuva kwa sababu ya kusimamia shsria za nchi ambazo wao wamekuwa wakitamani nchi hii isiwe na sheria kabisa, nitakufa kifo cha kishujaa. Lakini hao kina kikwete, kinana, lubuva na mangu, nao watakufa siku moja. Watakufa kifo cha aina gani, Mungu anajua. Acha watuuwe kwakuwa wameamua sasa kutuua hadharani.

Labda watatuua kwa mabomu ama silaha sumu. Ninadhani gas ya sumu itawarahishia kwa kuwa tuko wengi.
 
kikwete atajichafulia cv yk yt aliyopata kimataifa,,,, muach aendelee kuchez n kur zetu

Hayo mataifa anayowahadaa kwa unafiki kiasi wamuone mtu ya maana, watamjua uhalisia wake baada ya 25 October, 2015. Ninahisi kam awengine watanyofoa hata degree walizompa kwa majuto.
 
Biti zinapigwa hatari? Safari wawe makin tu wakizingua kutaharibika naona raia wameamua any way ngoja tusubiri tuone kama kwel watu wakipiga kura watarud nyumbani? Kweny kura wanajifanya wanaijua amani? Ila mafisad wakipiga pesa no tamko lolote tunamwona anakwea pipa kwenda kupata u dktar

mkuu umemaliza kabsa.
teh!
 
RadioOneStereo
Serikali imeonya kuwa itawachukulia hatua za kisheria watakaobaki katika vituo vya kupigia kura kwa madai ya kulindakura kwa kuwa ni kinyume cha sheria.
1-Tutashinda hata kwa bao la mkono
2-CCM haitong'oka kirahisi kama jino
3-Hatutofanya kosa kukabidhi Ikulu kwa wapinzani
?????????????!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom