geraldkowero1
JF-Expert Member
- Jul 5, 2014
- 1,838
- 647
Uko sahihi kabisa Mkuu. Ni vema UKAWA wachukue hatua sasa kabla hawajachelewa.
Mimi nakuunga mkono ila ninavyowaelewa ukawa wanaweza kuzembea jambo hilo hadi mwisho na likaleta maafa hiyo tarehe 25/10/'15. Jambo la kupuuzia mambo kwa viongozi wa ukawa niliuona wakati wa uteuzi wa wagombea ubunge na udiwani uliohusisha kuachiana majimbo kwa vyama washirika . Kwa uzembe tu lilipojitokeza tatizo la wagombea wawili wawili kujitokeza kwenye baadhi ya majimbo na kata viongozi wa juu walingangana tu makao makuu badala ya kwenda kutatua migogoro hiyo kuepusha kugawa kura na kuruhusu ccm kushinda. Hakika hili litawagharimu sana ukawa kwa kukosa majimbo.Maovu yanayoweza kufanywa na ccm wakiachwa wenyewe ni mengi na haitakuwa mara yao ya kwanza kufanya mbinu chafu kwa lengo la kukibakiza chama na serikali yake madarakani.Chaguzi za nyuma zote zilizohusisha upinzani zinaonyesha hivyo. Vinginevyo huo ushindi utapokonywa wazi wazi.