Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,635
- 8,955
Wanajamvi,
Hili suala la kubaki vituoni baada ya kupiga kura linaanza leta ukakasi sasa, leo Mh. Raisi kaliongelea na kusisitiza watakaobaki vituoni watashughulikiwa. Nimemsikia mhe. Kinana na IGP pia wakiliongelea na mbaya zaidi kwenye magroup yote wana CCM wamefurahia sana tamko la leo la mh. Raisi ambae pia ni Amiri jeshi mkuu katika nchi ambayo Tume ya Uchaguzi haiko huru, tumeona wakurugenzi wa tume wakibadilishwa chini ya mwezi mmoja kabla ya uchaguzi kwa sababu za kikatiba/kisheria maana mhe. Raisi ana uwezo huo.
Lakini pia tuna kumbukumbu za chaguzi zilizo pita ambapo bila wananchi kuwepo eneo la tukio, sina uhakika kama mh. Wenje angepata ushindi zaidi ya mh. Masha aliye kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.
Hii yote inaleta Sintofahamu na kuonyesha kama ule usemi wa Nape unatimizwa kwa njia hii.
Pia nimemuona Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC akiiweka kama issue ya kubaki kwenye vituo haiko kisheria.
Je, kama suala la kubaki vituoni kwa umbali usiopungua mita 100 liko kisheria, ni kwa nini UKAWA wasiende mahakamani kesho kwa hati ya dharula kuweza pata ufafanuzi na order ya mahakama kwenye jambo hili?
Nia ni kuepusha damu za Watanzania kumwagika maana ninavyoona, tunakoelekea sio kuzuri ifikapo tarehe 25 Oktoba.
Nawakilisha.
Mimi naona CCM imeshaona hawashindi uchaguzi na mbinu za magoli ya mikono zimekuwa ni ngumu , iliyobaki watumie goli la hockey , wazushe vurugu hii ndio turufu yao .
Wanataka kulitoboa jahazi tuzame sote