UKAWA kumpata mgombea Urais Jumamosi

UKAWA kumpata mgombea Urais Jumamosi

Kila la heri viongozi wetu wa UKAWA tunawategemea mtoke mkiwa wamoja .
 
Wadau ni kweli kwamba UKAWA na kujisifu kote kushinda uchaguzi asubuhi wanasubiri kushangiliwa kukatwa kwa Lowassa?
 
TEKNOLOJIA, Tatizo hampendi kuambiwa ukweli. Kila kitu alichokisema Msaka Gamba ni Kweli Tupu
 
Last edited by a moderator:
Mpaka akatwe ndo tunalala.
kama tumeweza kulinda kura hadi usiku, tutashindwaje kusubiria kuona mtu anakatwa kidizaini Fulani vile. Kiufupi hatulali mpaka wakate
 
kwa namna mazungumo yanavyo endelea ni dhahiri kwa namna yoyote ile mgombea wa urais kupitia ukawa atatoka chadema.

Vigezo

1. Chadema ndio chama chenye mtandao mkubwa uliopenya mpaka vijijini kwenye ngazi ya msingi miongoni mwa vyama vyote vilivyo katika ukawa. Hakuna ubishi kwamba baada ya ccm chadema ndio chama kinachofuata kwa mtandao.

2. Kama matokeo ya serikali za mitaa ni kigezo cha kutoa mgombea urais, chadema ndio chama kinacho ongozwa kwenye matokeo ya serikali za mitaa miongoni mwa vyama vinavyo unda ukawa. Pekee kimeshinda 30% kabla ya kuchanganya na matokeo ya vyama vingine vya ukawa.

3. Chadema kina mtaji wa kura za urais wa 2010 kwa kushika nafasi ya pili, ndio chama kilichotoa mgombea bora aliyepata kura nyingi miongoni mwa vyama vya upinzani. Dr slaa alishika nafasi ya pili nyuma ya jk tena kwa kuchakachukiwa.

4. Cuf wamesha weka mgombea urais zanzibar ambaye ni maalim seif. Kwa dhana ya ushirikiano na mashirikiano ya ukawa cuf watakuwa wenye dhamira mbaya naya hovyo kama watang'ang'ania kusimamisha mgombea bara kama ambavyo prof lipumba alivyo anza harakati za misikitini naza udini kuwa yeye ndio anafaa kuwa mgombea.

Kama cuf watang'ang'ania na kutaka kusimamisha mgombea maana yake ni kwamba hawana dhamira na kitu kinachoitwa ukawa bali watakuwa wabinafsi wasiotaka kuona watanzania wana ondokana na dude liitwalo ccm.

Nani kikwazo mpaka sasa.

Ukawa wanaweza kuwa wamechelewa kutaja mgombea urais wao mpaka sasa kwa sababu zifuatazo.

1. Undumila kuwili wa prof lipumba, mpaka sasa amekosa busara za kiungozi kwa ku fight na kujiona yeye au chama chake kina sifa ya kutoa mgombea bara.

2. Hofu ya kijinga ya cuf kutokukubali kwamba chadema ni chama chenye nguvu na mvuto kuliko chama chao.

3. Ziara anazo fanya prof lipumba mikoani ni ushahidi kuwa anafanya maandalizi ya kampeni za urais wa cuf lakini sio wa ukawa

4. Hatua ya cuf kutangaza mgombea urais wao bila kukubaliana na wenzao wa ukawa kuna ibua mashaka ya dhamira zao juu ya ukawa.

Kwa hatua ya sasa mchawi wa ukawa ni nani?!

Jibu ni rahisi sana! Mchawi ni prof lipumba wa chama cha wananchi cuf

ukweli mchungu.
 
Hakuna kikao leo wakuu,vikao vyote kasoro mkutano mkuu ni kesho.
Ni stratergy ya mwaka huu
 
Heee kumbe ni wewe uliyepita juu ya paa la nyumba yetu, asubuhi tunaamka na wewe..tumechoka sasa...
 
Siku ukawa wakimtangaza mgombe mmoja wa nafasi ya urais watu watakufa kwa furaha na furaha hiyo hiyo ilisababisha kifo itakuwa ni chanzo cha kuondoka ccm madarakani
 
Leteni up date.wana jf siku hizi ufukunyuku umepungua Sana.mpaka sasa hata tetesi hamna jamani.usingizi umenishika hapa lakini silali mpaka nipate majibu.amekatwa au badoo..? Na Kama bado wanangoja nini?
 
Back
Top Bottom